Pole Mkuu Rodelite
Japo unaeleza habari yako nusunsu lakini ni habari yenye kusikitisha sana
Kwa kifupi kitendo cha mwanamke/mwanaume kuvua pete mbele yako na kukwambia, ni kigezo tosha cha hiyo ndoa kuisha, watu wanagombana lakini ikishafika hiyo hatua ni basi tena
Tatizo ninaloliona hapa ni la muda mrefu, namaanisha ulikuwa unatawaliwa (Lugha ya mtaani) na mkeo kwa njia moja ama nyingine, labda kwa kipato, elimu, au ulimpenda kuliko kiasi na yeye alilijua hilo, yaani hukusimama kama mwanaume "(ulienda na wakati zaidi)", kwa maelezo yako huyo mkeo anajiamini kwamba anaweza kusimama mwenyewe na keshaonja hayo maisha kwa kupitia kwa rafiki zake
kwa kifupi hapo huna mke kwa sasa na kiukweli hata wewe unalijua hilo, nadhani tatizo kubwa lipo kwa watoto wako ndilo linalokutisha kufanya divorce, kwa miaka mliyokaa nadhani mna watoto wakubwa na kama ni kweli basi mchezo mzima wameshauona na labda mnawaumiza kisaikolojia,
hakuna releif kubwa utakoyoipata kama kuiweka wazi kwa watoto wenu, waite chini uwaeleze kinachoendelea na kwa mwenendo unaouelezea (mama kulala siku mbili nje) watoto watakuelewa vizuri sana, baada ya hapo anza maisha mapya ya ubachelor, tafuta maid mzuri wa kulea familia na usionyeshe kwa watoto kabisa kuwa una uhusiano na mwanamke yeyote maana wanaweza kujaji kuwa we unaweza kuwa chanzo cha divorce
jiweke free na huru, maisha ni yako usiogope majirani watasema nini, mpe divorce huyo mama na wewe anza maisha mapya kabisa na iweke wazi kwa kila mtu kuwa mmeachana, ukweli na uwazi utakupa uhuru na kujiamini sana
hapo huna mke kaka