Nilidhani Gatlin wakati anaongoza angeweza kuchomoka lakini wapi bana....hili li Jamaica si binadamu😀
Aisee mie nilidhani Gatlin anachukua Gold, alianza vizuri sana na alikuwa mbele ya Usain lakini jamaa akiamua kuongeza speed hakuna wa kushindana naye. It is sad that this will be his last Olympics.
Gatlin alikuwa na wakati mgumu! Toka kwa watazamaji hadi kwa Bolt! Mbaya zaidi hata yule USA baby wa hapa jamvini leo kamgeuka. ... 😀😀😀!
Wamejaa sana huko Kenya. .. bora hata wangeamia Tz...Sasa wanariadha wa Kenya kuchukua uraia wa nchi za kiarabu maanake ni nini?
Wanariadha wengi wanafanya hivyo kwa ajili ya hela. Uzalendo hauweki ugali mezani wansema. Kwa mfano wanariadha wa marathon wa kiume waliofuzu kuenda Rio toka Kenya walikuwa 44 lakini kila nchi ilipewa nafasi tatu za uwakilishi tu. Ina maana wanariadha 41 waridhike ilhali kuna nchi zinawatongoza kwa dola nyingi tu? Maisha hapa duniani ni mafupi sana kwa binadamu kukimbizana na serikali iweke mambo sawa. Kumbuka pia kuwa familia zao zinabaki nyuma na familia hizo zinapoafaidika tokana na ushindi wa jamaa zao, hawajali hela zitokako.Sasa wanariadha wa Kenya kuchukua uraia wa nchi za kiarabu maanake ni nini?