ngulukizi
JF-Expert Member
- Oct 10, 2018
- 619
- 1,749
Leo ndugu zangu nitawapa mkasa uliotokea kwenye mapenzi katika kambi moja ya jeshi Mkoa WA pwani.Katika mahusiano ya jamaa mmoja ambaye alikuwa mjeshi jamaa tulizoea kila siku anapigiwa na mkewe sasa siku hiyo akakuta SMS za mapenzi Kwa mkewe ndio kisanga kikaanza hapo jamaa akaanzisha timbwili la kufa mtu baada ya kutembeza kichapo akaaifungia familia yake ndani na kuwambia Leo hakuna kutoka naenda kulewa nikirudi naendelea na nilipoishia kaenda zake huko kulewa kulewa kumbe bahati mbaya funguo aliyoondoka nayo akapoteza kurudi kugonga mlango na makelele juu anamwambia mkewe umeamua kujifungia ndani inamana unaigiza mwanaume kwangu kumbuka huyu Jamaa wanakaa ghorofa za juu kabisa hapo Kota mkewe akamkumbusha kuwa si umetufungia toka mchana na umeondoka na funguo basi mjeshi na pombe akawa haelewi si ndio mwana kuzunguka na kutaka kuruka ili adake kona apite dirishani Bana Ile kuruka akajikuta kapitiliza na pombe zake mpaka chini hapo hapo akafa Kwa kupasuka kichwa,tukumbuke hasira hasara
RIP MJESHI
RIP MJESHI