Ripoti: 37% ya Nchi duniani hazina Uhuru Mtandaoni. Hali mbaya zaidi yaripotiwa China

Ripoti: 37% ya Nchi duniani hazina Uhuru Mtandaoni. Hali mbaya zaidi yaripotiwa China

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Kwa mujibu wa Ripoti ya Freedom House Mwaka 2022, Mazingira ya Haki Za Binadamu Mtandaoni yamezorota katika Nchi 28.

Katika Nchi 70 zilizofanyiwa Tathmini (sawa na 89% ya Watumiaji wa Intaneti Duniani) imebainika 37% Hazipo Huru, 34% zina Uhuru Kiasi na 18% zipo Huru.

Kwa Mwaka wa Nane mfululizo, China imetajwa kuwa Nchi yenye mazingira mabovu zaidi ya Uhuru Mitandaoni.

1673334196858.png


Kwa mujibu wa Ripoti ya Taasisi ya Freedom House ya 'Freedom On The Net 2022' Uhuru kwenye Mitandao umeendelea kuporomoka kwa mwaka wa 12 mfululizo

Hali mbaya zaidi imeripotiwa Urusi, Myanmar, Sudan na Libya. Aidha, katika takriban Nchi 53, Watumiaji walikabiliwa na changamoto za Kisheria kwa Kujieleza Mtandaoni

JITIHADA ZA ASASI ZA KIRAIA ZALETA MATOKEO CHANYA
Licha ya kuwepo mdororo wa Haki za Binadamu Mitandaoni, Ripoti ya Freedom On The Net 2022 imeonesha hali ya Uhuru kwenye Mitandao kuimarika katika Nchi 26 zilizofanyiwa Utafiti

Hatua hiyo imetokana na jitihada za Asasi za Kiraia kuhimiza maboresho ya Sheria, Ustahimilivu wa Vyombo vya Habari na Uwajibikaji katika Kampuni za Teknolojia

1673416556531.png
 
Wale Warusi wa Buza kwa mpalange ngoja wamsome Puttin wao hapa.. [emoji23]
 
Back
Top Bottom