JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Uhifadhi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba, 2022, limepoteza askari sita kwa kuuawa baada ya kushambuliwa na wananchi nyakati tofauti, wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya uhifadhi.
Kamishna wa Uhifadhi TFS, Profesa Dos Santos Silayo, alisema hayo Desemba 21,2022 wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, alipotembelea kituo cha hifadhi ya msitu wa Pagale, ambacho kilivamiwa na watu zaidi ya 50 kwa lengo la kutaka kuwadhuru askari wa uhifadhi wa kituo hicho .
Profesa Silayo alisema matukio hayo yametokea kwa nyakati tofauti katika kipindi cha kuanzia Januari 2022 hadi Desemba 2022 katika hifadhi za Kanda ya Magharibi, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Mashariki.
"Tunalaani vikali matukio haya ya uvamizi katika vituo vyetu, ambao umesababisha hasara kubwa kwa serikali, lakini hata kugharimu maisha ya askari wetu sita tangu mwaka huu umeanza pamoja na raia, ambao wamekuwa wakitusaidia katika uhifadhi kusabaishiwa ulemavu wa kudumu," alisema Profesa Silayo.
Chanzo: Habari Leo