Ripoti, Kagera: Ndani ya miezi miwili watu 33 wameripotiwa kuuawa

Ripoti, Kagera: Ndani ya miezi miwili watu 33 wameripotiwa kuuawa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Matukio ya watu wawili kuripotiwa kuuliwa kwa vitu vyenye ncha kali hivi karibuni Mtaa wa Kyaya, Kagera yameongeza mazingira ya hofu kwa baadhi ya Wananchi kutokana na mwenendo takwimu za mauaji kuongezeka.

Akizungumzia hali hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kagera, William Mwampaghale amesema “Kati ya Oktoba hadi Novemba 2022 kulikuwa na mauaji 33.

Amesema “Moja ya chanzo kikubwa cha mauaji ni wivu wa mapenzi, wanapendana sana na wanauana, pia kuna migogoro ya mashamba, mfano asubuhi ya leo nimepokea kesi tatu za ugomvi wa mashamba.”

Amewaomba viongozi wa mila na wa vijiji kutatua migogoro kwa wakati kwa kuwa inachangia msongo wa mawazo na mwisho ni kusababisha mauaji

Naye, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Odira Aloyce akitoa takwimu za kesi za mauaji amesema:

“Hadi kufikia Desemba 2021 tulifunga Mwaka tukiwa na kesi 122, Januari hadi Desemba 2022 zilisajiliwa kesi 121, kesi zilizosikilizwa kati ya Januari - Desemba 2021 ni 159, Desemba 2022 tulifunga mwaka tukiwa na kesi 84.

Chanzo: Azam TV
 
Back
Top Bottom