PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 969
- 1,055
JItihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukaribisha na kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini unaelezwa kutiwa kigingi na tabia chafu inayozidi kuota mizizi ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kushirikiana na baadhi ya majaji wa mahakama kuu wasio waaminifu kuyatapeli mabenki ya ndani na nje ya nchi kwa na hivyo kuwanyima fursa wafanyabiashara wadogo na wakati kushindwa kuaminiwa na kupata mikopo.
Orodha ya wafanyabiashara wanaotumia mahakama kutapeli na kudhulumu mabenki iliyofanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa na gazeti hili, inaonyesha kuwa wengi kati ya wafanyabiashara hao wanajihusisha na biashara za Mafuta na ushafirishaji ambapo wastani wa shilingi za kitanzania Trilioni 1.3 wamekopa katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani ambako pia wanadaiwa kupata ushindi kwa njia zisizo za kawaida
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wafanyabiashara hao wanaoheshimika nchini wakionekana machoni mwa watu kuwa ni matajiri na wengine wakijionyesha kama wacha Mungu na wenye kumuogopa Mungu huku wengine wakijinasibu kama wana michezo na wawekezaji wakubwa wanaitumia mahakama hasa mahakama ya biashara kama kichaka chao cha kufanyia uhalifu huo wa kimkakati
Mfanyabiashara wakubwa wadaiwa kudhulumu mabenki kutumia mahakama
Wachota mabilioni ya akiba za wateja na kujinufaisha, wagoma kulipa wkimbilia mahakamani mahakama yabariki.
Mmoja akwapua bilioni 40 TADB, akakwapua bilioni 70 Azania, akakwapua bilioni 110 Equity kisha akapiga bilioni 220 ujerumani.
Mwengine kachukua bilioni 15 NMB, akachukua bilioni 80 EQUITY akagoma kulipa akakimbilia mahakamani Jaji akampa ushindi anaendelea kutanua mitaani.
Jaji huyo huyo na kwa staili hiyo hiyo akampa ushindi mfanyabiashara mwingine aliyekwapua dola milioni 15 KCB.
Jitihada za Rais Dkt. Samia kuvutia uwekezaji zinazidi kukwamishwa, BOT, TIC, watakiwa kujipanga upya
Chanzo: Jamvi la Habari
Pia soma: