Ripoti: Mitandao ya kijamii ni sumu kwa Wanawake Kisiasa

Ripoti: Mitandao ya kijamii ni sumu kwa Wanawake Kisiasa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Baadhi ya wanawake waliojitosa kuwania uongozi wa kisiasa, wamesema walikumbana na udhalilishaji mtandaoni, wakiitaja mitandao ya kijamii kuwa "sumu kwa wanawake kisiasa"

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Kidemokrasia (NDI), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wanawake waliochaguliwa kwa nafasi za ubunge ni asilimia 9.5, wabunge wa viti maalumu ni asilimia 29, hivyo kufanya jumla ya wabunge wanawake kuwa 142 kati ya 393.

Vilevile, ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya mwaka 2020 inaonesha wanawake waliochaguliwa kwa nafasi za udiwani walikuwa asilimia 6.58 (260 kati ya madiwani 3,953), viti maalum walikuwa 1,374 katika halmashauri 184 sawa na asilimia 24.59. Kwa jumla, wanawake walikuwa asilimia 29.24 ya madiwani wote nchi nzima.

Ripoti ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019 pia inaonesha kuwa kati ya nafasi 11,915 za wenyeviti wa vijiji, wanawake walishinda nafasi 246 sawa na asilimia 2.1, huku wanaume wakishika asilimia 97.9 ya nafasi hizo. Kati ya nafasi 4,171 za wenyeviti wa mitaa, wanawake walishinda nafasi 528 sawa na asilimia 12.6.
xJ5zSnEtBOXA0Yr07z8XiKl0Bh02QLRcKKJiIBF2.png
Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mabunge ya Afrika (APU) mwaka 2021, ukihusisha wabunge wanawake 224 kutoka nchi 50, ikiwamo Tanzania, ulibaini kuwa asilimia 80 ya waliohojiwa walipitia ukatili wa kisaikolojia, huku asilimia 46 wakikumbana na ukatili wa kijinsia mtandaoni.

Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya mwaka 2023, inaonesha kuwapo ongezeko kubwa la udhalilishaji wa kidijitali na ukatili wa kijinsia mtandaoni nchini, wanawake wakiwa walengwa wakuu, kwa asilimia 56.

Katika ripoti yake hiyo, LHRC ina lingine la ziada kwamba licha ya unyanyasaji huo, wanawake hawatafuti msaada wa kisheria. Ripoti yake inaonesha kuwa asilimia 65 ya wateja waliotembelea kituo mwaka huo walikuwa wanaume.

Soma, Pia:

+ Kwa Wanawake: Una mipango ya kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu? Kwanini?

+ Ripoti: Wanawake walioko katika Jicho la Umma wanapitia zaidi Ukatili wa Mtandaoni
 
Back
Top Bottom