Ripoti mpya ya Benki ya Dunia yaonesha Tanzania inakabiliwa na ongezeko la mzigo wa kulipa madeni

Tunakopa pesa tunatia kwenye bajeti ya kununulia mashangingi unategemea nini.
Hiyo level ya mtaani tu, huwezi kukopa kwa ajili ya jambo la anasa, utakuwa ni MUFILISI wa akili.
 
Tunayo Exit kwenye hali hii ikiwa tutapush Agenda ya mambo manne kama mkakati wa Kitaifa kwa 2024/2025.
1.Tumalize kwa Haraka sana tatizo la umeme na si hivo tu-Sera za Uwekezaji kwenye Renewable Energies ziwekwe kimkakati kwa namna ambavyo Watu wengi watashiriki kwenye Uwekezaji huo na hivo kupelekea Gharama za Umeme kuwa Rahisi kuliko Nchi nyingine za Ukanda huu.
-Hili likifanyika kwa haraka na kimkakati basi VIWANDA VINGI VITAZALIWA NA HIVO KUONGEZA REVENUE ya Ndani mara dufu!
-Ni Rahisi kunadi sera ya Viwanda ikiwa una competeteve price ya Energies!

2.Mradi wa SGR:Huu ndo umetunyonya damu mpk hapa tulipo sasa hivi!
Mradi huu umekuja pre matured.
Hata hivo tumeshayavulia maji Nguo ni Lazima tuoge!
-Kwanza tukamililishe Miradi yote ya SGR na pili SEKTA BINAFSI ishiriki kikamilifu ktk kutumia Rail kusafirisha Mizigo na hata Abiria.
At least kila baada ya 15Mins au kwa shida sana nusu saa ipite train...Hapa tutaanza kurecover Mkopo kupitia Mradi na siyo Makusanyo mengineyo!
Good thing Serikali imeshatoa mwaliko kwa Sekta Binafsi lakini naona Elimu bado haiko kwa watu waliowengi!
-Financial Institutions pia ziingie huku kuibua MIRADI.

3.Food basket.
-Mkakati wa Kilimo cha Umwagiliaji ni Muhimu sana lakini ni vema attraction ya wakulima wakubwa kutoka ndani na Nje ichukue sura mpya.
-Ngano na Shayiri ni Mazao ya kimkakati kwa kuwa yanaondoa Forex kupeleka nje.
TBL/SERENGETI-walime na wafanye contract farming( sheria).
Siyo option kununua Ngano au Shayiri bali ni Lazima ANUNUE KWA MPANGO WA SERIKALI.
75% Local and 25% perhaps-Imported.

Mafuta ya kupikia the same!

Huu ni Mpango wa muda mfupi sana lakini kimkakati na itasaidia Serikali kubadili kabisa sura ya uchumi wake kwa Sababu ni eneo linalogusa maisha ya watu waliowengi!

-Mifugo-Sekta hii ina potential kubwa sana kwenye Nchi lakini Serikali haipati kitu.
Mifugo ya Tanzania ni Raw materials kwa wenzetu wakati wafugaji wetu wakiwa vibarua tu!
-Hapa kuna Forex za kutosha ikiwa Serikali itaamua kuona potentials kwenye Eneo hili.
-Ufugaji ni Science na Siyo SIASA.
Egypt,Middle East,Far East ni Masoko ya moja kwa moja ya Red meat lakini mpk sasa hakuna biashara yenye tija kwa Nchi na hivo kufanya Wafugaji kufugwa na Mifugo badala ya wao kufuga Mifugo.

Hii ni moja wapo ya Food Basket Complement.


4.Processing of Gold and Deposits of the Same plus Diamond to the Central Bank.

This one has to be a quick activity at which shall stabilise our currency and hence a stable Economy!
At least kila mwaka tudepisit tani 200.


Hayo ni mambo yanayopaswa kufanywa kwa ku gauge kiasi cha fedha kinachopaswa kuvunwa kutokana na mpango huo kwa haraka ukilinganisha na Nchi wenzetu especially kipindi hiki Dunia ikipita kwenye mtikisiko wa KIUCHUMI.

Mwisho ni Kuomba Restructuring ya madeni yetu tukilenga kupata nafuu ya kutekeleza baadhi ya MIRADI ya kimkakati.

We are in a better off position as a country but we should not give a chance for failures!

Politically we are stable and the Current president is Highly Deplomatic so we can attract a lot of projects through DFI.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…