dada white
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 1,228
- 514
Siku hizi maadili yameporomoka kabisa, watoto wako busy na ulimwengu. Ukiangalia familia nyingi nafasi ya mzazi haionekani, kuna watoto wengine wameachiwa jamii iliyowazunguka ndo iwalee. Kwa hiyo mtoto akikutana na watu wenye tabia mbaya na yeye anakua hivyo hivyo.
Kwa ambaye hakupata bahati
ya kuona hii ripoti, imeambatanishwa. Labda itasaidia kujua kwanini
watoto wetu wanafeli, pamoja na ukweli wa hizi ripoti.
Ki ukweli jibu la matokeo mabaya ya hawa watoto ni Wao kutokuwa serious jamani we angalia madudu yaliyoandikwa na hawa watoto.Kama walimu wachache mbona hili tatizo kwa kiasi fulani limepungua kila siku vyuo vya ualimu vinatapika walimu wengi sana.Mi nipo jirani na shule kama nne ila miienendo yao hairidhizishi kabisa.
Sidhani kama umenisoma, mimi nakwambia kabla ya kujudge kuwa mtoto wa form four hatakuwa na analytical skills nenda kwenye muhtasari uone ni competency gani mwanafunzi anapaswa kuwa nazo ndipo uje hapa kuargue kuwa hilo swali limekosewa. Otherwise argument zako ni baseless.
Sijakwambia kuwa kuna swali limekosewa, nakwambia kuwa yale maswali ukiyaangalia yanakwenda kwenye level ya juu ya mwanafunzi wa sekondari. Sasa kama syllabus imeelekeza hivyo basi hiyo silabasi ina kasoro. Huwezi kumpa mtoto wa darasa la kwanza silabasi ya sekondari ukasema utamtahini hivyo. Kwa hiyo kufuata silabasi tu kama kasuku ni ujuha pia. Mtu anayetunga mitihani lazima aangalie anawatungia watu wa level ipi. Na pia awe na uwezo wa kujiuliza hayo maswali anayotunga je kuna mwanafunzi yeyote mwenye uwezi wa kuyajibu?
Unaweza soma hii link uone pia ninachokisema (kwamba utungaji na usahihishaji wa mitihani pia ni issue ya kuangalia kwenye examination performance).
http://www.dailynews.co.tz/index.php/local-news/14850-grading-system-affects-results