Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Tanzania imeonekana kurudi nyuma kiutawala bora kutokana na vipimo vinavyotolewa na Mpango wa pamoja wa Kujipima Kiutawala Bora (APRM), ikiwa na kuminywa kwa demokrasia, uhuru wa kujieleza na kuendelezwa kwa ndoa za utotoni.
Hayo yamo kwenyue utafiti uliofanywa na (SAIIA) kwa kushirikiana na Tanzania Citizen’s Information Bureau (TCIB), ikiwa imepita miaka minane tangu Tanzania ilipopimwa mwaka 2013 tangu ilipojiunga na mpango huo mwaka 2004.
Utafiti huo uliofanyika mwaka 2024 umegusia mwenendo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, Utawala wa sharia na upatikanaji wa haki, haki za kijamii na ulinzi wake, haki za siasa, uhuru wa kukusanyika na ulinzi wa haki za binadamu.
Mengine yaliyogusiwa ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza, fursa kwa vijana na ushiriki wa wananci katika mchakato wa demokrasia.
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo leo Julai 8, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, amesema kuna kurejea nyuma kwa Serikali katika utekelezaji wa mapendekezo ya utawala bora.
Nuru Maro kutoka Jukwaa la Maendeleo Vijijini (TRDF), amesema ripoti hiyo imezingatia matumizi ya rasilimali zinazopatikana nchini kama ardhi, madini ambazo kama zitazingatiwa zitatoa mchango kwa maendeleo nchini.
Hata hivyo, Mkuu wa Utawala na Diplomasia wa SAIIA, Steven Gruzd amesema APRM haiwezi kutatua changamoto zote kwa siku moja, bali jamii inapaswa kuangalia upungufu ulipo na kuufdanyia kazi.