Mfumuko wa bei sasa hivi Zimbabwe ni asilimia 800.
Kuna upungufu mkubwa wa chakula. madawa, mafuta na fedha haipo kwenye mzunguko.
Umaskini wa wazimbabwe umekuwa sasa ni asilimia 70 ya idadi ya wazimbabwe.
Miezi miwili yaenda sasa kuna mgomo wa manesi na watumishi wa afya wakitaka wapatiwe PPEs na mshahara wao ulipwe kwa dola.
Bila PPEs wagonjwa wa COVID-19 wataendelea kufa na sasa kuna wagonjwa zaidi ya 5000 na vifo 129.
Isitoshe kuweka zaidi chumvi kwenye kidonda waziri wa afya ni Constatino Chiwenga ambae ni mwanajeshi na hana uzoefu wa masuala ya afya.
Mbali ya hayo serikali ya Mnangagwa imekubali kuwalipa wazungu walowezi dola bilioni 3.5 ambao mashamba yao yalichukuliwa na serikali ya Robert Mugabe, ikiwa ni kutimiza masharti ya kuondolewa vikwazo na nchi za kibeberu.
Sasa Zimbabwe itafanikisha vipi haya yote?
Zimbabwe imeamua kutumia amana zake za kigeni kwa kuuza rasilimali zake kama dhahabu, almasi na ardhi iliyoko katika miji yake maarufu.
Hali ni mbaya sana Zimbabwe kwa sasa na nina watu wa karibu kabisa wapo Harare wananipa updates.
Na siku si nyingi utasikia jeshi limemwondoa Mnangagwa maana anae Chiwenga na yupo mwingine jenerali Sibusiso Moyo yuo pembeni anaangalia ustaarabu.
Kama walimwondoa Mugabe na kumweka Mnangagwa basi hawatashindwa kufanya mabadiliko mengine.
Kama wakumbuka uzuri, ni huyu Chiwenga ndie alietangaza mapinduzi baridi kwenye runinga.
By the way, wafahamu Mnangagwa ana utajiri kiasi gani?
Wewe ni mjuzi wa kutafuta hizi taarifa, basi tafuta nani ni wamiliki wa makampuni ya madini yaitwa Sakunda Holdings na Landela Mining Ventures.
Zimbabwe ipo nyuma sana ya Tanzania kwenye uwekezaji na hizo taarifa ni propaganda za kupindisha ukweli halisi.