Ripoti ya CAG 2019/20: Upungufu wa Miundombinu kwenye Shule za Msingi na Sekondari

Ripoti ya CAG 2019/20: Upungufu wa Miundombinu kwenye Shule za Msingi na Sekondari

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kutokana na utelekezaji wa Sera ya Elimu Msingi bila malipo ya mwaka 2015/16, kumekuwa na ongezeko la wanafunzi kila mwaka.

Ongezeko la wanafunzi lilipaswa kwenda sambamba na uboreshwaji wa miundombinu ya shule kama vile vyumba vya madarasa, madawati, matundu ya vyoo nk. Kwa mwaka 2019/20, CAG aliainisha kuwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa 51 zilikuwa na upungufu wa miundombinu ya shule, huku upungufu mkubwa ukiwa kwenye nyumba za walimu na matundu ya vyoo katika shule za msingi na nyumba za walimu, mabweni, maabara na majengo ya utawala katika shule za sekondari

Athari;
Changamoto zilizoainishwa zina athari zifuatazo;

1. Upungufu wa miundombinu ya shule hususani nyumba za walimu na mabweni huathiri ufanisi wa utoaji elimu kwa shule za sekondari haswa kwa wanafunzi wa jinsia ya kike ambao ni wahanga wa vitendo vya ubakaji

2. Upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni huathiri utulivu na usafi wa wanafunzi wakati wa kujisitiri. Tatizo hili linaathiri zaidi wanafunzi wa kike ambao kwa maumbile yao wanahitaji zaidi hali ya usiri na usafi wakati wa kujisitiri.

Ushauri;

Ili kutatua changamoto zilizoibuliwa na CAG, WAJIBU inashauri yafuatayo;

1. Halmashauri za Wilaya kwa kushirikiana na kamati za shule na wananchi kuendelea kuibua na kusimamia miradi ya uboreshwaji wa miundombinu ya elimu nchini (vyoo, mabweni na nyumba za walimu) katika shule za msingi na sekondari

2. Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI zitoe kipaumbele zaidi kwenye upangaji na utoaji wa bajeti ya miundombinu ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa Sera ya Elimu Msingi bila Malipo nchini

WAJIBU INSTITUTE
 
Back
Top Bottom