Ripoti ya CAG : CHADEMA yapata hati safi

Ripoti ya CAG : CHADEMA yapata hati safi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama cha siasa ambacho kimeshikilia rekodi ya dunia ya kushambuliwa na serikali, kimeonekana na CAG kuwa chama kinachozingatia weledi katika matumizi ya pesa zake, na hivyo kuudhihirishia ulimwengu kuhusu umakini wa viongozi wake, jambo lililopelekea kuiumbua vibaya sana TAKUKURU iliyowahi kutumika kushambulia chama hiki kwa kutumwa na mtu duni aitwaye Lijuakali.

Note : Chadema haijawahi kubebwa.

%22_.jpg


Mungu ibariki Chadema .
 
Sema ubadhirifu upo kama kawaida.
 
CCM ndio kidedea miaka yote imepata Hati Safi!
Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).

Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi.

Wasafi walipewa 140M, TBC 201M na Clouds 629M kutangaza tamasha la Urithi Festival. Lakini hakuna mkataba wala risiti yoyote ya kujustify malipo hayo.

18Bil zilizokusanywa ktk wilaya 135 hazikufika serikalini. Yani zilikusanywa lakini wajanja wakalala nazo mbele.

3.9Bil zilitolewa kukarabati ndege ya ATCL iliyopaki tangu mwaka 2015, lakini hela imeliwa na ndege haijakarabatibwa. Yani watu walitafuna milioni 3,900 halafu hawakupaka hata rangi.Hayo ni baadhi tu ya "madudu" ya serikali takatifu ya mwendazake. Sijaongelea HESLB, TANAPA, TANROADS, SGR, Stligler's gorge, Stand ya Magufuli. Huko kuna madudu ya kutisha.
 
CCM wao hati yao ikoje, nataka kuona ushahidi wa maandishi toka kwenye taarifa ya CAG kama uliowekwa kwa Chadema.
 
Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).

Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi....
Sipati picha stiglers na Sgr
 
Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).

Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi..
Huyu kigwangala anastahili kuwa jela kwa sasa
 
Hela anakula Mbowe kwa akili sana tena kwa maandishi,

Nyie misukule wake hamuwezi kuona lolote
Bilionea Mbowe ndiye kiongozi pekee wa Chama cha siasa nchini Tanzania asiyelipwa na ambaye hutoa hela mfukoni mwake ili kuchangia chama
 
Hati safi

Act wazalendo

Chadema

Ccm

Kwa mujibu wa picha ya mleta mada
 
Back
Top Bottom