Ripoti ya CAG: Halmashauri 37 zilikusanya shilingi bilioni 3.45 ambazo hazikuwekwa kwenye akaunti rasmi za serikali

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
"Mheshimiwa Rais ukaguzi wangu pia ulibaini kuwa halmashauri 37 zilikusanya shilingi bilioni 3.45 ambazo hazikuwekwa kwenye akaunti rasmi za serikali. Hali hii inaashiria uwezekano wa ubadhirifu wa fedha za umma na kusababisha ucheleweshaji na utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Napendekeza serikali isimamie kwa ufanisi utekelezaji wa utaratibu wa kisheria unaolazimisha mapato yote yanaokusanywa kuwasilishwa benki ndani ya masaa 24 au 48 baada ya kukusanywa."

"Ukaguzi wangu umebaini mapungufu katika ukusanyaji wa mapato kama ifuatavyo, kwanza kesi za kodi zinazosubiri maamuzi za shilingi trilioni 9.83, Mamlaka ya mapato Tanzania ilikuwa na kesi 1186 za kodi zenye jumla Shilingi trilioni 9.83, zilizokuwa bado hazijatatuliwa katika mahakama za rufaa za kodi kwa Tanzania bara."

"Mheshimiwa Rais kwa upande wa serikali za mitaa, Mamlaka 14 za serikali za mitaa zilitarajiwa kukusanya shilingi bilioni 45.61 kupitia mawakala wa mapato, lakini zilikusanya bilioni 19.49 zikiwa ni upungufu wa bilioni 26.12. Upungufu mkubwa zaidi ulionekana katika halmashauri sita zifuatazo"

"Halmashauri ya jiji la Dar es salaam. ilipaswa kukusanya kutoka kwa mawakala kiasi cha shilingi bilioni 15 lakini ilikusanya bilioni 3.4

Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni ilipaswa kukusanya bilioni 10.25 lakini ilikusanya bilioni 5

Halmashauri ya manispaa ya Ubungo ilipaswa kukusanya shilingi bilioni 3.1, ilikusanya milioni 909.

Halmashauri ya jiji la Mwanza ilipaswa kukusanya bilioni 3.6 lakini ilikusanya bilioni 1.6

Halmashauri ya wilaya ya Kibondo ilipaswa kukusanya shilingi bilioni 2.1 lakini ilikusanya milioni 635.

Halmashauri ya wilaya ya Babati ilipanga kukusanya shilingi bilioni 2.5 lakini ilikusanya bilioni 1.47"

"Mheshimiwa Rais napendekeza menejimenti za mamlaka husika zisimamie kwa karibu utekelezaji wa mikataba na kuhakikisha mikataba inajumuisha kipengele cha dhamana wa fidia pale mawakala wanaposhindwa kutimiza masharti ya mikataba."

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles E. Kichere akiwasilisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Hyo mifumo yenyewe ya kukusanya malipo kwa kutumia Point of sales machine Pos wahasibu Mapato wa halmashauri wanaruhusiwa kuingia kwenye system nakufuta baadhi ya transaction kama zimekosewa ila hyo ruhusa imegeuka fursa kwa wahasibu kufuta transaction kubwa kubwa kwa kushirikiana na wakusanya Mapato kisha hyo pesa wanagawana.
 
The great questions of the day will not be settled by means of speeches and majority decisions but by iron and blood_ chancellor ottoman von Bismarck. Kwenye GERMAN UNIFICATION alipata ku comment hivi na kweli ujerumani ikaungana na kua moja.

Kwa kuanzia tuanze na adui yetu mkuu AMBAE ni CCM huyu adui hataki kutupatia KATIBA MPYA itakayo mpunguzia nguvu rais na ili kutengeneza strong institutions zitakazo wajibisha watu including rais mwenyewe..

Huwa namsikiliza mtu Kama HECHE jicho na sikio langu naona kabisa ana uwezo mkubwa ki uongozi kumzidi majariwa , dotto biteko, na wengine wengi hapo CCM Kama ingekua inawezekana nilitamani nionee akipewa nafasi ya uongozi huko je ataweza ku deliver Kama anavyo upiga mwingi mdomoni.

Ni WAKATI sahihi kwa Sasa iwe "" NO REFORM NO ELECTION"" na sijui kwa Nini CCM wanaogopa Sana wakiambiwa ukweli.
 
NAWATAKIA KILA LA KHERI MKIONA SIPATIKAN SIJHAPENDA NATKA NKAPUMZIKE

AISEE NILIWAHO OMBA HIZI RIPOTI BAKIGI NAZO MSITUWEKEE HADHARANI KUNA SIKU MTASHANGAA MNAONGEZEA ROHO ZA UWASI NA USHETANI TANZANIA

YANAYOTEKEA KONGO NA SIDAN YAKIYANZA HIVIHIVI

HILI LA ILALA BIL 6.8 HAZIONEKAN BANK

MNAFUNDISHA NN WAFANYA BIASHARA

MNAFUNDOSHA NN WATTOTTO WETU WANAOSOMA WAIBE???

JIULIZE KINONDON UBUNGO PWAN HUKO WAMEKULA NGAPI

LAANA YA MUNGU IWASHUKIE

YA MUNGU MENGI

NTASHANGAA SANA KUONA TUNAENDELEA NA WAKUU WA WILAYA NA HALMASHAURI WA HIZI WILAYA

RAHA Y MILELEL UWAANGAXIE WAPUMZIKE KWA AMAN

CYA KIRARACHAAAAAA
 
Mkuu piddy kunywa na pumzika vya kutosha mwanangu
Screenshot_20250328-163613.jpg
 
"Mheshimiwa Rais ukaguzi wangu pia ulibaini kuwa halmashauri 37 zilikusanya shilingi bilioni 3.45 ambazo hazikuwekwa kwenye akaunti rasmi za serikali. Hali hii inaashiria uwezekano wa ubadhirifu wa fedha za umma na kusababisha ucheleweshaji na utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Napendekeza serikali isimamie kwa ufanisi utekelezaji wa utaratibu wa kisheria unaolazimisha mapato yote yanaokusanywa kuwasilishwa benki ndani ya masaa 24 au 48 baada ya kukusanywa."

"Ukaguzi wangu umebaini mapungufu katika ukusanyaji wa mapato kama ifuatavyo, kwanza kesi za kodi zinazosubiri maamuzi za shilingi trilioni 9.83, Mamlaka ya mapato Tanzania ilikuwa na kesi 1186 za kodi zenye jumla Shilingi trilioni 9.83, zilizokuwa bado hazijatatuliwa katika mahakama za rufaa za kodi kwa Tanzania bara."

"Mheshimiwa Rais kwa upande wa serikali za mitaa, Mamlaka 14 za serikali za mitaa zilitarajiwa kukusanya shilingi bilioni 45.61 kupitia mawakala wa mapato, lakini zilikusanya bilioni 19.49 zikiwa ni upungufu wa bilioni 26.12. Upungufu mkubwa zaidi ulionekana katika halmashauri sita zifuatazo"

"Halmashauri ya jiji la Dar es salaam. ilipaswa kukusanya kutoka kwa mawakala kiasi cha shilingi bilioni 15 lakini ilikusanya bilioni 3.4

Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni ilipaswa kukusanya bilioni 10.25 lakini ilikusanya bilioni 5

Halmashauri ya manispaa ya Ubungo ilipaswa kukusanya shilingi bilioni 3.1, ilikusanya milioni 909.

Halmashauri ya jiji la Mwanza ilipaswa kukusanya bilioni 3.6 lakini ilikusanya bilioni 1.6

Halmashauri ya wilaya ya Kibondo ilipaswa kukusanya shilingi bilioni 2.1 lakini ilikusanya milioni 635.

Halmashauri ya wilaya ya Babati ilipanga kukusanya shilingi bilioni 2.5 lakini ilikusanya bilioni 1.47"

"Mheshimiwa Rais napendekeza menejimenti za mamlaka husika zisimamie kwa karibu utekelezaji wa mikataba na kuhakikisha mikataba inajumuisha kipengele cha dhamana wa fidia pale mawakala wanaposhindwa kutimiza masharti ya mikataba."

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles E. Kichere akiwasilisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

View attachment 3284740

Tatizo letu machawa hata mambo ya kiserikali ya marekebisho ya utendaji kama hayamsifii Mama wanakimbia topic kabisa . Lakini kila siku ni Chadema na Lissu wakati kuna mambo muhimu ya kuongelea hapa

ChoiceVariable
Tlaatlaah
 
Kama hauko kwenye mirija basi kimpango wako, sasa hivi wenzako na hii weekend tuko zetu hapa the voice bia moja inauzwa 8,000/= tunatumia hela tu wala hatumbuki hata kuwaomba wahudumu chenji.....

Kama kuna ujinga mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya bssi ni kuwa mzalendo kwenye hili taifa

Nimalize kwa kusema mama mitano mingine...
 
Tatizo letu machawa hata mambo ya kiserikali ya marekebisho ya utendaji kama hayamsifii Mama wanakimbia topic kabisa . Lakini kila siku ni Chadema na Lissu wakati kuna mambo muhimu ya kuongelea hapa

ChoiceVariable
Tlaatlaah
Gentleman,
Changamoto, dosari na kasoro ndogondogo zilizoibuliwa na mkaguzi wa hesabu, ni fursa muhimu ya kujirekebisha, kujisahihisha na kujipanga kufanya vizuri zaidi huko mbeleni,

hata hivyo,
Changamoto hizo nyingi hazikutokea kipindi hiki cha serikali ya awamu ya6 chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan bali ni za vipindi vilivyopita.

Therefore,
hakuna haja na mayowe sanaaaa, yote hayo mkuu wa nchi madhubuti amejipanga kuwashughulikia bila mbambamba za mtu yeyote ili kama taifa, tuendelea kusonga mbele pamoja 🐒
 
Back
Top Bottom