Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kila mara bila kupata jibu, ni kwanini kila mwaka ripoti ya CAG inabainisha wizi wa mabilioni ya shilingi serikalini, bila ya kuchukuliwa hatua yoyote, je ni mkakati maalum wa Serikali hii ya CCM, kukusanya mapesa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025?
Kwa kuwa haiingii akilini, inakuwaje hawa wateule wachache wa CCM, waachiwe kutafuna mabilioni ya shilingi ya walipa kodi wa nchi hii, wakati sheria za watenda makosa ya jinai zinajuliikana wazi kuwa, kila muhalifu yeyote ndani ya nchi hii, ni lazima mkono wa sheria umkumbe kwa kufikishwa Mahakamani, Ili ajibu tuhuma zake.
Wakati kuna wezi kwa maelfu wa wizi wa kuku, wamehukumiwa na wanatumikia vifungo vyao magerezani, iweje hawa wezi wa mabilioni ya shilingi za walipa kodi wa nchi hii, waachiwe huru bila kuchukuliwa hatua yoyote Kila ripoti ya CAG, inapotoka Kila mwaka?
Tukichukulia pia waliokubuhu kwa wizi huu, ni wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini, ambao ni makada wa CCM, ambao pia ni wateule wa Rais, tukizingatia pia Rais, ametangaza nia ya kugombea u-Rais Katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025, je hii kutochukuliwa hatua yoyote ya kisheria kwa wezi hawa, je ni mkakati wa ukusanyi mapesa kwa chama cha CCM, kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025?
Jibu unalo msomaji wa thread hii.