Ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2025/2026 au 2030/2031 itaonesha ubadhirifu wa awamu ya sita

Ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2025/2026 au 2030/2031 itaonesha ubadhirifu wa awamu ya sita

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Kwa namna siasa zetu zilivyo tutarajie kwamba .

Kama Samia atapita 2025 basi mambo yatabakia hivi hivi nikimaanisha kwamba ripoti ya fedha kwa mwaka 2025/2026 ya CAG itakua safi sana.

Ila kama mambo yakiwa tofauti basi isikilizie kwani lazima itaukandia mno awamu ya sita.

Lakini kwa uhakika sana Mungu akitujalia na sote tuseme Amin basi mwaka 2030/2031 ripoti ya CAG itakua mbaya sana kwa utawala huu.

Na hasa hasa fedha zilizokuwa zinapelekwa Zanzibar , Miradi Taneso na mingineyo tutaambiwa ni ufisadi uliokithiri na watu wale wale wataanza kuikashifu awamu hii kama vile hawakuwepo.

Aina hii ya siasa ni mbaya hailisaidii taifa bali linamsaidia kiongozi anayekua madarakani kwa muda huo.

Tunachohitaji ni maendeleo ya Wananchi na sio mashindano ya viongozi kwamba nani ni bora kuliko mwenzake.

Wananchi tumepata somo , tuna pa kuanzia.
 
Ligasi tuilinde.
Screenshot_20220411-131335.jpg
 
Wanajikinga ili wakiiba wasingizie uongozi uliopita
Hii tabia ya watanganyika kusubiri awamu ni ujinga tupambane tuwaondoe wahuni

Kusubiri ya 2030 ni mambo yasiyofikirika huo mwaka wakijq watoto wa mama tunachetu apo?
 
Itakua imetumia integrals, differental equations, probality, complex numbers wakati mataga wanajua kujumlisha na kutoa tu (refer polepole kwenye wizi wa 1.5 trilioni).
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Kwa kipindi hiki chote watakuwa washajinoa kwenye Pure Mathematics, tutapata uchambuzi murua muda ukifika
 
Yaani tumekuwa kizazi cha very very low IQ, yaani mpaka the country machinery wanabumba ripoti kumchafua kiongozi ambaye walikuwa wanakula.

Meza moja, tena wanasuka mkakati wa kumdhihaki kiongozi aliyewaamini akawateua, inasikitisha sana. Ila nina uhakika 100% Mama Samia atadhalilishwa sana tena dhihaka juu yake itakuwa kubwa mno hata usalama wa familia yake itakuwa shida.

Na hii inatokana na yeye kuandaa mipango ya kumchafua Dkt Magufuli ambaye ni marehemu yaani watanzania wana hasira kubwa sana juu yake.
 
Yaani tumekuwa kizazi cha very very low IQ, yaani mpaka the country machinery wanabumba ripoti kumchafua kiongozi ambaye walikuwa wanakula
Meza moja, tena wanasuka mkakati wa kumdhihaki kiongozi aliyewaamini akawateua, inasikitisha sana. Ila nina uhakika 100% Mama Samia atadhalilishwa sana tena dhihaka juu yake itakuwa kubwa mno hata usalama wa familia yake itakuwa shida. Na hii inatokana na yeye kuandaa mipango ya kumchafua Dkt Magufuli ambaye ni marehemu yaani watanzania wana hasira kubwa sana juu yake.
Dhambi ya usaliti huwa inafuata vizazi na vizazi.
 
Kuipitia historia au sayansi ya siasa ya utawala bora na sera zake siyo kumsema marehemu au uongozi wake .

Historia ni somo zuri kutufahamisha wapi tulifanya vizuri, wapi tulikosea na hivyo sasa tujirekebishe tusirudie makosa.

Kukataa kufanya tathimini ya maamuzi ya utawala uliopita ambao pia uliongozwa na kikundi cha watanzania ni kukataa kutaka kujirekebisha, kuepuka au kufanya vizuri zaidi ya jana .

The study of politics and governance addresses important questions about the nature of power, authority and governance: who gets what, when and how. Yet politics is more than this and concerns notions of freedom and agency in situations of social choice.
 
Kuipitia historia siyo kumsema marehemu au uongozi wake .

Historia ni somo zuri kutufahamisha wapi tulifanya vizuri, wapi tulikosea na hivyo sasa tujirekebishe tusirudie makosa.

Kukataa kufanya tathimini ya maamuzi ya utawala uliopita ambao pia uliongozwa na kikundi cha watanzania ni kukataa kutaka kujirekebisha, kuepuka au kufanya vizuri zaidi ya jana .
bagamoyo kusema marehemu achomwe moto ni tathimini????
 
Yaani tumekuwa kizazi cha very very low IQ, yaani mpaka the country machinery wanabumba ripoti kumchafua kiongozi ambaye walikuwa wanakula....
Hakuna mtanzania mwenye hasira na mama Samia sema nyie waburundi
 
bagamoyo kusema marehemu achomwe moto ni tathimini????

Kupitia sera za mtawala aliyepita, style za uongozi wake, taasisi alizozijenga na maamuzi ya pamoja ya taasisi anazoongoza ni jambo jema sana .

Kuna profesa mmoja alisema kwa mtizamo wake wa kisomi, Yesu Kristo alikuwa mwanaharakati na hivyo kiongozi yoyote dikteta asingeweza kumvumilia Yesu Kristo, lazima angemchapa viboko na kumfunga jela.

Hii haina maana ya kuwa profesa anamkashifu Yesu Kristo kwamba angepata adhabu hiyo, bali anamtazama katika muktadha nje ya imani ya dini na kutoa somo kwetu wanafunzi juu ya msuguano katika upande wa serikali zetu za kidunia kati ya watawala na watawaliwa. Na mfano aliotumia profesa ni rahisi sisi wanafunzi kuuelewa maana stori ya maisha ya Yesu Kristo wengi tunaielewa katika imani mbalimbali.

Hili la kusema marehemu achomwe moto ni maneno matatu labda ya kukazia historia ya maisha ya kisiasa ya marehemu na jinsi alivyokosea.
 
Hii nchi ya kipuuzi sana! Watu wanapelekwa kama upepo!
Hii ripoti niya kubumba tu! Magu alifanya maamuzi kuanzisha na kutekeleza miradi mikubwa yenye tija nchi hii, tafuteni pesa mmalizie miradi!
Kama umeme ukiendelea kusuasua trein la umeme litaendeshwa vipi?
 
Kwa namna siasa zetu zilivyo tutarajie kwamba .

Kama Samia atapita 2025 basi mambo yatabakia hivi hivi nikimaanisha kwamba ripoti ya fedha kwa mwaka 2025/2026 ya CAG itakua safi sana...
Mwakani tu wala huko kwingine ni mbali mno
 
Hapa wapuuzi wanaweza kudhani unawazia mema taifa hili kumbe sababu kubwa ni NJAAAAAAAAAAAA
 
Kuna profesa mmoja alisema kwa mtizamo wake wa kisomi, Yesu Kristo alikuwa mwanaharakati ..

Askofu Dr. Benson Bagonza - "Magufuli alikuwa mwanaharakati ingawa yeye Magufuli alikuwa hapendi wanaharakati"

"Rais wetu amegeuzwa kuwa waziri wa fedha, hii ya kumghasi rais awape fedha inampa pressure kutofuata utawala bora wa miradi kupata fedha kupitia sheria na mgao wa bajeti ulioidhinishwa na Bunge " - Askofu Bagonza

Mfano ninyi waandishi wa habari .....mlikuja kunihoji kwa kupitia vichochoroni msionekane mnakuja kunihoji mimi (askofu), mlikuwa mna mashaka mtaonekana, sasa sura zenu zina furaha mnapitia mlango wa mbele kuja bila kificho ... ili tuongee mambo mbalimbali ....

Ni rahisi vitu vya kushikika kama majengo, viwanja vya ndege n.k kusahaulika hivyo viongozi wawekeze katika mioyo ya watu. Hivi vitu vya kushikika kama majengo, madaraja yanaweza kubomoka angalia mfano wa nchi hii ya Ukraine majengo yamebomoka mara moja ... lakini yaliyopo mioyoni mwao yameifanya nchi hiyo bado ipo pamoja inapitia wakati mgumu.

Hivyo viongozi wa nchi wawekeze sana kwa watu badala ya kusisitiza Maendeleo ya Vitu badala ya Maendeleo ya Watu anakazia baba Askofu Dr. Benson Bagonza ...

Askofu Dr. Bagonza, Kuhusu upande wa Ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ... rushwa kubwa kubwa ilikuwepo sema watu waliogopa kusema ... ni sasa tu ndiyo hali imeruhusu sisi kuona ripoti za ubadhirifu na rushwa kubwa kuanikwa hadharani na kupigwa vita iliyoshamiri katika awamu iliyopita lakini ilifunikwa ...
 
Back
Top Bottom