Ripoti ya CAG: Magari 552 yametelekezwa, hayatengenezwi wala kuuzwa

Ripoti ya CAG: Magari 552 yametelekezwa, hayatengenezwi wala kuuzwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imebaini uzembe na ucheleweshaji wa maamuzi katika taasisi mbalimbali za umma, hali iliyosababisha mali za serikali zenye thamani ya mabilioni ya shilingi kutotumika kwa muda mrefu, huku nyingine zikiendelea kuharibika.

1744877907069.png
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, magari 552, pikipiki 98 na mashine 20 hazijatumika kwa muda mrefu katika taasisi 81, bila hatua yoyote ya matengenezo wala kuuzwa, kutokana na ucheleweshaji wa maamuzi na ukosefu wa mipango madhubuti ya matumizi. Aidha, ripoti imebaini majengo na mitambo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 37.07 hayatumiki, yakiwemo jengo la Shirika la IPS lililodumu miaka mitatu bila kutumika, mitambo ya Bohari ya Dawa tangu mwaka wa fedha 2020/2021, na baadhi ya majengo ya utalii katika hifadhi za Taifa.

"Hali hii imesababishwa na ukosefu wa fedha za ukarabati, ucheleweshaji wa manunuzi, na ukosefu wa mpango wa matumizi, hivyo kusababisha hasara na kuathiri huduma kwa wananchi," inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Katika sekta ya afya, ukaguzi umebaini dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.44 vimeharibika kutokana na kuisha muda wa matumizi bila kuondolewa. Ripoti inaeleza kuwa sababu kuu za hali hiyo ni pamoja na ucheleweshaji wa vibali vya kisheria vya kuondoa dawa hizo, ununuzi usiozingatia tathmini ya mahitaji halisi, na kutofuata utaratibu wa FIFO (First In, First Out).

Mbali na hilo, ripoti imebaini kuwa taasisi 269 za umma zinadaiwa jumla ya Shilingi Bilioni 311.98 kwa ajili ya madeni ya watumishi. Kati ya deni hilo, Serikali Kuu inadaiwa Shilingi Bilioni 274.8 (sawa na asilimia 88), Mamlaka za Serikali za Mitaa Shilingi Bilioni 24.54 (asilimia 8), na Mashirika ya Umma Shilingi Bilioni 12.64 (asilimia 4). Madeni hayo yanahusisha mishahara, gharama za usafiri kwa wastaafu na marupurupu mbalimbali.

CAG ameeleza kuwa chanzo kikuu cha madeni haya ni ufinyu wa bajeti, ucheleweshaji wa fedha, pamoja na udhaifu wa usimamizi wa fedha za umma.
 
Halafu hayo magari ni v8GXR ambazo gari Moja ni shilingi Milioni miatano sabibi Hadi miasita.Tufanyae(552*500000000)=bilioni miambili hamsini zimeteketea.halafu hapohapo Kuna wachawi wanasema mitano tena
 
Yaani serekali inakuaga ni upuuzi upuuzi tu.

Hivi hawa wafanyakazi wa serekali, ndio hawa hawa tunaoishi nao uraiani au?

Mbona uraiani hakuna upuuzi uliopitiliza kama huu.

Ndugu msomaji hebu nisaidie, hapo mtaani kwako, kuna mtu ametelekeza nyumba yake nzima ikiwa na vitu ndani, yaani hata kuipangisha hajataka?

Sasa mbona huko serekalini inaweźekaka? Au ni mimi tu ndio sielewi haya mambo yanavyoendeshwa?

Inawezekana huko serekalini hata u bartazar kwenye maofisi unaendeleaga sana, unakuta jitu muda wote linawaza mapenzi, likipumzisha akili kidogo basi linawaza simba na yanga, yaani upuuzi mtupu.

Pesa za matengenezo ya magari na majenereta ya serekali zikija, mpuuzi huyu, anazitia kwapani, anaenda kuzihonga, na kula chipsi kuku, mara biriyani, unakuta jitu limejinenepea mpaka halijulikani shingo ni ipi kichwa ni kipi kwa wizi wa pesa za serekali.

Mie nikikutana na mtu mnene hata kwenye deals, trust yangu kwako naiweka 50%. ( kama umeshindwa kuwa na discipline kwenye mwili wako, utawezaje kuwa na discipline kwenye mishe nyingine)

Jivunie kuwa mtanzania, fanya jambo kuisaidia nchi yako, jivunie kuwa mchango katika ujenzi wa nchi mzee.

Sio umepewa gari ya serekali basi bizee kuiba mafuta, yaani wewe muda wote unawaza upate safari ili ukaibe mafuta muda wote mawazo yako yanatabirika(wizi, kuhonga, simba na yanga)


Hawa vijana wenzio wasio na ajira unaowaona mtaani, wote walistahili kuwa hiyo nafasi uliyopo, lakini kwa kuwa ni wengi ndio maana wewe umepata bahati ya kuwa hapo, jivunie basi kulihudumia taifa lako.


Ninaombea sana mchina aje hapa Tanzania na kuanzisha kizazi chake.

Kama ilivyo kwa wahindi, tunavyosema ni watanzania wenye asili ya Asia basi tuwe na Mtanzania mwenye asili ya uchina.

Najua mchina sio muoga kama muhindi, mchina ni hustler ataingia mpaka kwenye siasa, na mchina akishaigusa siasa, utawala wa mkoloni mweusi utakua umefikia mwisho, wanasiasa wataanza kulia kama wanavyolia wafanyabiashara wa kkoo(trust me)

Xi Jinping Penyeza watu wako mpaka kwenye siasa, tena point kubwa ya kuanzia ni huko huko simba na yanga, wala usiwaze kui exploit nchi yetu pendwa, walete wachina tuishi nao kama ndugu zetu, maeneo tunayo mengi tu, Tanzania ni kubwa sana. Bora tuongeze kizazi kipya kwenye nchi yetu ili tumkimbize mkoloni mweusi.
 
Tulipaswa zaidi kupambana na CCM kuliko tunavyopoteza muda na CDM, CCM wana maswli mengi wanapaswa kutujibu.
 
Halafu hayo magari ni v8GXR ambazo gari Moja ni shilingi Milioni miatano sabibi Hadi miasita.Tufanyae(552*500000000)=bilioni miambili hamsini zimeteketea.halafu hapohapo Kuna wachawi wanasema mitano tena
Inategemeana na taasis, mengi ya hayo magari ni cruiser hardtop and lx, vx v8 ziko chache sana maana si work horse ni za wakurugenzi tu.
 
Back
Top Bottom