Yaani serekali inakuaga ni upuuzi upuuzi tu.
Hivi hawa wafanyakazi wa serekali, ndio hawa hawa tunaoishi nao uraiani au?
Mbona uraiani hakuna upuuzi uliopitiliza kama huu.
Ndugu msomaji hebu nisaidie, hapo mtaani kwako, kuna mtu ametelekeza nyumba yake nzima ikiwa na vitu ndani, yaani hata kuipangisha hajataka?
Sasa mbona huko serekalini inaweźekaka? Au ni mimi tu ndio sielewi haya mambo yanavyoendeshwa?
Inawezekana huko serekalini hata u bartazar kwenye maofisi unaendeleaga sana, unakuta jitu muda wote linawaza mapenzi, likipumzisha akili kidogo basi linawaza simba na yanga, yaani upuuzi mtupu.
Pesa za matengenezo ya magari na majenereta ya serekali zikija, mpuuzi huyu, anazitia kwapani, anaenda kuzihonga, na kula chipsi kuku, mara biriyani, unakuta jitu limejinenepea mpaka halijulikani shingo ni ipi kichwa ni kipi kwa wizi wa pesa za serekali.
Mie nikikutana na mtu mnene hata kwenye deals, trust yangu kwako naiweka 50%. ( kama umeshindwa kuwa na discipline kwenye mwili wako, utawezaje kuwa na discipline kwenye mishe nyingine)
Jivunie kuwa mtanzania, fanya jambo kuisaidia nchi yako, jivunie kuwa mchango katika ujenzi wa nchi mzee.
Sio umepewa gari ya serekali basi bizee kuiba mafuta, yaani wewe muda wote unawaza upate safari ili ukaibe mafuta muda wote mawazo yako yanatabirika(wizi, kuhonga, simba na yanga)
Hawa vijana wenzio wasio na ajira unaowaona mtaani, wote walistahili kuwa hiyo nafasi uliyopo, lakini kwa kuwa ni wengi ndio maana wewe umepata bahati ya kuwa hapo, jivunie basi kulihudumia taifa lako.
Ninaombea sana mchina aje hapa Tanzania na kuanzisha kizazi chake.
Kama ilivyo kwa wahindi, tunavyosema ni watanzania wenye asili ya Asia basi tuwe na Mtanzania mwenye asili ya uchina.
Najua mchina sio muoga kama muhindi, mchina ni hustler ataingia mpaka kwenye siasa, na mchina akishaigusa siasa,
utawala wa mkoloni mweusi utakua umefikia mwisho, wanasiasa wataanza kulia kama wanavyolia wafanyabiashara wa kkoo(trust me)
Xi Jinping Penyeza watu wako mpaka kwenye siasa, tena point kubwa ya kuanzia ni huko huko simba na yanga, wala usiwaze kui exploit nchi yetu pendwa, walete wachina tuishi nao kama ndugu zetu, maeneo tunayo mengi tu, Tanzania ni kubwa sana. Bora tuongeze kizazi kipya kwenye nchi yetu ili tumkimbize mkoloni mweusi.