Ripoti ya CAG - Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24

Ripoti ya CAG - Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Nina furaha kuwasilisha Taarifa yangu ya Jumla ya Mwaka kuhusu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa mujibu wa Ibara ya 143(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, na Kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, Sura ya 418.

Taarifa hii inawasilisha matokeo ya ukaguzi na kupendekeza hatua za kuboresha, ambazo zinalenga kukuza uwajibikaji katika ukusanyaji na matumizi ya rasilimali za umma.

Nawasilisha.

Charles E. Kichere
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Hati za Ukaguzi
Kwa mwaka wa fedha 2023/24, kati ya miradi 332 iliyokaguliwa, miradi 331 (sawa na 99.7%) iilipata hati isiyo na mashaka, ikionesha ufuataji mzuri wa viwango vya utoaji wa taarifa za kifedha.

Hata hivyo, hati yenye shaka ilitolewa kwa mradi wa Mfuko wa Afya unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, kutokana na upungufu wa nyaraka za uthibitisho na malipo yasiyothibitishwa. Hili linaonesha kwamba bado kuna changamoto katika usimamizi wa fedha katika mfuko huu.

Usimamizi wa Fedha na wa Matumizi
Katika mwaka wa fedha uliokaguliwa, jumla ya Shilingi trilioni 8.44 zilikuwepo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kiasi hiki kinajumuisha bakaa ya miaka iliyopita na fedha zilizopokelewa ndani ya mwaka. Kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 5.93 zilitumika, huku Shilingi trilioni 2.50 zilikua hazijatumika hadi kufikia tarehe 30 Juni 2024.

Tathmini ya utendaji wa kifedha ilibaini changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na fedha za mradi kiasi cha Shilingi milioni 635.44 zilizokopwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bila kurejeshwa.

Pia, malipo ya Shilingi milioni 892.92 yalifanywa bila ya kazi iliyokamilika kuthibitishwa na mhandisi mshauri. Katika ukaguzi, nilibaini pia kuwa malipo ya jumla ya Shilingi bilioni 2.01 yalifanyika kwa njia ya fedha taslimu kinyume na taratibu. Vilevile, malipo ya fidia kwa Watu Walioathiriwa na Miradi (PAPs) kiasi cha Shilingi bilioni 24.75 bado hazijalipwa, hali inayosababisha ucheleweshaji wa miradi na ongezeko la gharama za utekelezaji.


Upungufu wa Usanifu - RUWASA ulisababisha ongezeko la gharama Tsh. Bilioni 4.04​
Usambazaji wa Maji Vijijini chini ya RUWASA Ukaguzi wa kiufundi wa Wakala wa Usambazaji wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA) umebaini mapungufu katika upangaji wa miradi, ununuzi, usimamizi wa mikataba, na uhakikisho wa ubora, hali iliyohatarisha ufanisi na uendelevu wa miradi ya maji vijijini.

Katika ukaguzi, nimebaini tathmini ya vyanzo vya maji haikufanyika kwa kina, ambapo ukaguzi wa mara moja tu haukuweza kubaini athari ya mabadiliko ya msimu katika ubora na upatikanaji wa maji. Matokeo yake, miradi ya Morong’anya na Kemondo-Maruku ilitegemea mbinu zisizofaa za uchujaji wa maji, huku miradi ya Kigwa-Uyui na Igogo-Igurubi ikitegemea miundombinu ya mabomba ambayo haikusanifiwa kwa ajili ya upanuzi wa huduma, hali inayosababisha hatari ya muda mrefu kwa upatikanaji wa maji.

Aidha, kujumuisha kipindi cha utekelezaji wa mradi ndani ya miaka 20 ya miradi kulipunguza muda wa matumizi ya miundombinu hiyo kabla ya kuhitaji ukarabati mkubwa.

Aidha, mikataba 14 kati ya 15 iliingiwa bila kufanyika kwa uhakiki wa kina wa makandarasi, jambo lililosababisha ucheleweshaji wa hadi miaka mitano na gharama za ziada za Shilingi bilioni 1.17 kutokana na kuvunjwa kwa mikataba. Pia, ushindani usioridhisha katika zabuni ya mradi wa Morong’anya ulisababisha gharama zisizotarajiwa za Shilingi bilioni 1.26 kutokana na upungufu wa vipengele muhimu katika makadirio ya gharama za ujenzi.

Udhaifu katika usimamizi wa mikataba ulisababisha hasara ya Shilingi milioni 493.08 kutokana na uvunjaji wa mikataba usiozingatia taratibu, pamoja na ongezeko la gharama la Shilingi bilioni 4.04 kutokana na mapungufu katika usanifu wa miradi. Aidha, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi ulisababisha riba ya Shilingi milioni 711.79, jambo lililoongeza mzigo wa kifedha kwenye miradi husika.

Vilevile, matatizo ya usimamizi wa ubora, yakiwemo ufungaji usiofaa wa mabomba, ujazaji udongo usiotosha, na matumizi ya malighafi zisizofaa kwa ajili ya kujaza udongo, yameongeza uwezekano wa kuwa na miundombinu dhaifu ya maji. Hali hii inahitaji maboresho ya haraka katika usimamizi, upangaji, na uzingatiaji wa viwango vya kiufundi ili kuhakikisha ufanisi na uendelevu wa miradi ya maji vijijini.


Ukarabati na Ujenzi wa Masoko na Vituo vya Mabasi​
Ukaguzi wa kiufundi wa ukarabati na ujenzi wa Soko la Kariakoo, Soko Kuu la Mwanza, na Kituo cha Mabasi cha Nyamhongolo umebaini mapungufu katika upangaji wa miradi, usanifu, na usimamizi wa mikataba, hali iliyosababisha ongezeko la gharama na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi.

Kutokuwepo kwa tathmini ya kina ya hali ya majengo katika masoko ya Kariakoo na Mwanza kulisababisha kutofafanuliwa kwa wigo wa miradi, hali iliyopelekea mabadiliko yenye thamani ya Shilingi milioni 757.02.

Mapungufu katika usanifu wa Soko Kuu la Mwanza yalisababisha kazi za ziada zenye thamani ya Shilingi xix bilioni 1.96 kutokana na mahitaji muhimu ya mradi kutokujumuishwa katika hatua za awali.

Pia, malipo ya Shilingi bilioni 9.87 kwa upauaji wa nondo bila kubainisha vipimo vya nondo hizo, hali iliyoongeza hatari ya kupanda kwa gharama zisizo halisi. Aidha, Shilingi milioni 766.90 zililipwa kwa washauri kama gharama za kurejesheka bila nyaraka za uthibitisho, jambo linaloashiria udhaifu katika udhibiti wa fedha.

Ucheleweshaji wa miradi kwa miezi 13 katika Soko la Kariakoo na miezi 44 katika Soko Kuu la Mwanza ulisababisha madai ya washauri wa Shilingi bilioni 1.35 kwa gharama za usimamizi wa muda uliosongezwa. Ucheleweshaji huu ulitokana na idhini zilizocheleweshwa, malipo yaliyokawia, pamoja na ongezeko la wigo wa miradi.


Ukarabati na Ujenzi wa Masoko na Vituo vya Mabasi​
Ukaguzi wa kiufundi wa ukarabati na ujenzi wa Soko la Kariakoo, Soko Kuu la Mwanza, na Kituo cha Mabasi cha Nyamhongolo umebaini mapungufu katika upangaji wa miradi, usanifu, na usimamizi wa mikataba, hali iliyosababisha ongezeko la gharama na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi.

Kutokuwepo kwa tathmini ya kina ya hali ya majengo katika masoko ya Kariakoo na Mwanza kulisababisha kutofafanuliwa kwa wigo wa miradi, hali iliyopelekea mabadiliko yenye thamani ya Shilingi milioni 757.02.

Mapungufu katika usanifu wa Soko Kuu la Mwanza yalisababisha kazi za ziada zenye thamani ya Shilingi xix bilioni 1.96 kutokana na mahitaji muhimu ya mradi kutokujumuishwa katika hatua za awali.

Pia, malipo ya Shilingi bilioni 9.87 kwa upauaji wa nondo bila kubainisha vipimo vya nondo hizo, hali iliyoongeza hatari ya kupanda kwa gharama zisizo halisi.

Aidha, Shilingi milioni 766.90 zililipwa kwa washauri kama gharama za kurejesheka bila nyaraka za uthibitisho, jambo linaloashiria udhaifu katika udhibiti wa fedha.

Ucheleweshaji wa miradi kwa miezi 13 katika Soko la Kariakoo na miezi 44 katika Soko Kuu la Mwanza ulisababisha madai ya washauri wa Shilingi bilioni 1.35 kwa gharama za usimamizi wa muda uliosongezwa. Ucheleweshaji huu ulitokana na idhini zilizocheleweshwa, malipo yaliyokawia, pamoja na ongezeko la wigo wa miradi.


Ununuzi wa Vifaa vya Ujenzi Vyenye Thamani ya Shilingi Bilioni 3.1 kutoka kwa Wazabuni Wasioidhinishwa​
Ukaguzi wa taratibu za ununuzi wa vifaa vya ujenzi vilivyotumiwa katika Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa chini ya Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya ujenzi wa shule mbalimbali katika mkoa wa Mara, ulibaini kuwa ununuzi wa vifaa vyenye thamani ya shilingi 3,100,824,370 ulifanyika kinyume na masharti ya ununuzi ya Vifungu vya 31.4, 31.5 32(2) na 32.3 vya Mwongozo wa Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma wa Utekelezaji wa Kazi za Ujenzi kwa Kutumia Nguvukazi ya Taasisi Nunuzi wa Mei 2020.

Vifaa hivyo vilinunuliwa kutoka kwa wazabuni ambao hawakuwa wameidhinishwa, au katika maduka yasiyokuwa na idhini ndani ya jamii husika, au bila kuwa na makubaliano yoyote ya kimkataba kutoka kwa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA).

Udhaifu huu ulitokana na kushindwa kuhusisha wazabuni waliothibitishwa na kufuata taratibu sahihi za ununuzi kwa kuwashindanisha wazabuni. Matokeo yake, ununuzi ulifanyika kutoka kwa wazabuni wasioidhinishwa, jambo linalodhoofisha kanuni za uwazi, uwajibikaji, na matumizi sahihi ya fedha za umma. Kuvunjwa kwa taratibu za ununuzi kunaonesha wasiwasi kuhusu uadilifu wa mchakato wa ununuzi.

Jedwali Na. 19 linaonesha halmashauri zilizofanya ununuzi wa vifaa vya ujenzi kutoka kwa wazabuni wasioidhinishwa.

Ninapendekeza mamlaka husika za serikali za mitaa zihakikishe ununuzi wote unafanywa kutoka kwa wazabuni walioidhinishwa kama inavyotakiwa na kanuni zilizotajwa hapo juu.

Jedwali Na. 19: Halmashauri Zilizofanya Ununuzi wa Bidhaa za Ujenzi kutoka

kwa Wazabuni Wasioidhinishwa

Mtekelezaji (Halmashauri) Kiasi (Sh.)

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti 274,306,074

Halmashauri ya Mji Mdogo wa Tarime 883,591,555

Halmashauri ya Wilaya ya Rorya 430,993,665

Halmashauri ya Wilaya ya Butiama 464,917,208

Halmashauri ya Wilaya ya Musoma 438,024,996

Halmashauri ya Mji wa Musoma 608,990,881

Jumla 3,100,824,379
 

Attachments

Back
Top Bottom