WaTanzania wenzangu, ni mawazo tu yanayoingia akilini, wakati tunapofunuliwa yanayofanyika huko ndani ya serikali yetu yanayohusu ufujaji mkubwa wa pesa za wananchi.
Huu ni utaratibu unaojulikana, kwamba kila mwaka CAG anatoa ripoti yake kuonyesha ni namna gani serikali ilivyosimamia matumizi ya pesa za wananchi
Sote tumeshuhudia, karibu kila mwaka ripoti hizi zinapotolewa kunakuwa na kelele nyingi sana, na baada ya kelele hizo hakuna tena linalofanyika hadi hapo ripoti nyingine ya mwaka inapotolewa; tunaanza upya, na wala hatukumbuki yale ya mwaka uliopita, na wala serikali haileti mrejesho wowote kuonyesha marekebisho yoyote ili kuziba palipo na matundu.
Sasa nauliza wanaofahamu haya mambo vizuri waeleze, huko kwenye sekta binafsi, na hasa kule kunakohusisha uwekezaji toka nje, hali huko ipoje?
Kama hii mali kidogo inayoshughulikiwa na serikali inafujwa kiasi hiki, huko kwenye mali, raslimali kubwa zaidi za waTanzania, ambazo tunawakaribisha watu waje hapa kuzitumia raslimali hizo, hali huko ipoje?
Kuna CAG wa huko pia? Mbona hatuoni ripoti zake za kila mwaka?
Watu wanajizolea tu mali zetu bila sisi kujua lolote?
Tumeweka usimamizi kiasi gani huko, ili tusinyang'anywe kizembe?
Ikitokea tukaelezwa kinagaubaga, bila shaka hayatakuwa "majonzi" pekee, huenda tutazimia kabisa.
Mbaya zaidi, kila kukicha viongozi wetu kazi kubwa wanayoijua ni kutafuta hao wanyang'anyi, bila hata ya kujizatiti kuziba mianya ya kutunyang'anya mali zetu kizembe!
Ile gesi tutaambulia kitu kweli? Na hii nickleje?, graphite, Helium....
Hivi Waarabu nao wangelala kama tulivyolala sisi, hiyo Dubai ingekuwepo kule?
Hapa kwetu wanakuja kuzoa tu wakubwa, sisi tunabaki na nyimbo tu!
Kunradhi kama kuna makosa ya kiuandishi.