Wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa Rais, Mkaguzi mkuu wa serikali Charles Kichere amesema kuwa serikali inadaiwa kiasi cha shilingi Bilioni 7.90 kama fidia kwa waliopisha miradi ya maendeleo.
Aidha ameshauri pesa hizo kulipwa kwa wakati ili kuepusha riba inayoweza kutokea kutokana na kucheleweshwa kwa malipo hayo.