Ripoti ya CAG: TANESCO kudai madeni makubwa Kwa Taasisi za serikali

Ripoti ya CAG: TANESCO kudai madeni makubwa Kwa Taasisi za serikali

Mhung

Senior Member
Joined
Jun 20, 2025
Posts
165
Reaction score
187
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya mwaka 2025/2026, imeainisha Moja kati ya Madeni wanayodai Tanesco Kwa Taasisi za serikali, madeni hayo ni ya muda mrefu madeni hayo ni kama yafuatavyo.

ZECO: Tsh 292 billion, DAWASA : Tsh 35 billion ,Mamlaka za maji za mikoa : Tsh 21 billion , TPDF: Tsh 14 billion , Hospitali ya Muhimbili : Tsh 10 billion , Wizara ya Maji na Umwagiliaji : Tsh 9 billion, Taasisi ya mifupa ya Muhimbili (Moi): Tsh 4 billion , Polisi: Tsh 4 billion , Magereza : Tsh 3 Billion.

Kutokana na madeni hayo kutolipwa Kwa muda mrefu, utendeji kazi wa Tanesco unadhoofika kwani fedha hizo zingetumika katika usambazaji na uzalishaji umeme, ikifika Juni wakati wa gawio, Tanesco huonekana kutoa gawio dogo kulinganisha na Taasisi nyengine za serikali hali ambayo hupelekea kuonekana Tanesco kama inajiendesha Kwa hasara / faida ndogo.
 
Nawaona kupe wako nafasi ya juu kabisa kwenye madeni. Wanapenda vya bure mpaka basi! I wish ningekuwa Rais wa Tanganyika! Ndani ya siku 100 za uongozi wangu hakika ningewafundisha nini maana halisi ya neno "kujitegemea" .
Shida iyo nyadhifa ya Raisi wa Tanganyika haipo.
 
ZECO ni ndugu zetu katika imani, Mei tunawasamehe deni ila DAWASA and co lazima walipe.
 
Nawaona kupe wako nafasi ya juu kabisa kwenye madeni. Wanapenda vya bure mpaka basi! I wish ningekuwa Rais wa Tanganyika! Ndani ya siku 100 za uongozi wangu hakika ningewafundisha nini maana halisi ya neno "kujitegemea" .
Wangelia sana deni lote hilo linabakia kwa na hawatolipa
 
Anaandika Mh God Godbless J Lema.

Au tutengeneze !!!

TAAKUTA.
Taasisi ya Aibu na Kusuta Tanzania

Kaulimbiu:
Aibu Kwanza, Uwajibikaji Baadaye

Dhamira:
Kuwataja hadharani wale wote wanaosababisha hasara ya fedha za umma ili waone aibu ya taifa.

Majukumu Makuu:
•Kushirikiana na Public Procurement Regulatory Authority na Prevention and Combating of Corruption Bureau kupata orodha ya wahusika
•Kutangaza majina ya “Wasutwe” kila mwaka
•Kuendesha kampeni za VIBE ya AIBU kwenye mitandao ya kijamii

Huduma Maalum:
•Aibu Index: Kipimo cha kitaifa cha nani kaaibisha zaidi
•Wall of Shame: Orodha ya wazi ya waliotajwa
•Badge ya Aibu: Cheti rasmi cha kusutwa kinachoweza kusambazwa online .

Hitimisho:
Kwa sababu wakati mwingine sheria zipo kimya…TAAKUTA inasema kwa sauti kubwa, INATOSHA.
@
1774940728319.jpg
 
hapo hapo serikali ime-transfer >30 million usd kwenda caf afcon kwa ajili ya ku-host mipira kwa mujibu wa makonda, tena wamefanya transfer bila longo longo lolote popote na wao ni wa kwanza kulipia 30 million usd wakati kenya ambao wana uchumi mkubwa karibia mara 2 ya tanzagiza ingawaje wana watu wachache klk tanzagiza mpaka leo hii wanajishauri kama hata its worth it ku-tranfser such a lot money na bado hawaja-tranfser hiyo pesa, hiyo ndiyo tofauti kwenye priorities na muslims wa tanzagiza ...
 
kushinda taasisi zote za Bara baadae utasikia wamesamehewa
Cha kushangaza zaidi, ZNZ wananchi wananunua umeme kama ilivyo Tanzania Bara, Tsh 500 unit 1.4 , je ZECO hizo fedha wanazipeleka wapi badala ya kulipa deni? Hawana Gharama za kuzalisha umeme labda matengenezo na usambazaji maeneo machache.
 
Cha kushangaza zaidi, ZNZ wananchi wananunua umeme kama ilivyo Tanzania Bara, Tsh 500 unit 1.4 , je ZECO hizo fedha wanazipeleka wapi badala ya kulipa deni? Hawana Gharama za kuzalisha umeme labda matengenezo na usambazaji maeneo machache.
wameshaona Tanganyika ni wajinga dawa ni wakatiwe umeme
 
Back
Top Bottom