Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Ukaguzi wa kiufundi wa ukarabati na ujenzi wa Soko la Kariakoo, Soko Kuu la Mwanza, na Kituo cha Mabasi cha Nyamhongolo umebaini mapungufu katika upangaji wa miradi, usanifu, na usimamizi wa mikataba, hali iliyosababisha ongezeko la gharama na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi.
Kusoma ripoti yote kwa undani ingia hapa: Ripoti ya CAG - Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24
Kutokuwepo kwa tathmini ya kina ya hali ya majengo katika masoko ya Kariakoo na Mwanza kulisababisha kutofafanuliwa kwa wigo wa miradi, hali iliyopelekea mabadiliko yenye thamani ya Shilingi milioni 757.02. Mapungufu katika usanifu wa Soko Kuu la Mwanza yalisababisha kazi za ziada zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.96 kutokana na mahitaji muhimu ya mradi kutokujumuishwa katika hatua za awali.
Pia, malipo ya Shilingi bilioni 9.87 kwa upauaji wa nondo bila kubainisha vipimo vya nondo hizo, hali iliyoongeza hatari ya kupanda kwa gharama zisizo halisi. Aidha, Shilingi milioni 766.90 zililipwa kwa washauri kama gharama za kurejesheka bila nyaraka za uthibitisho, jambo linaloashiria udhaifu katika udhibiti wa fedha.
Ucheleweshaji wa miradi kwa zaidi ya mwaka mmoja (miezi 13) katika Soko la Kariakoo na zaidi ya miaka 3 (miezi 44) katika Soko Kuu la Mwanza ulisababisha madai ya washauri wa Shilingi bilioni 1.35 kwa gharama za usimamizi wa muda uliosongezwa. Ucheleweshaji huu ulitokana na idhini zilizocheleweshwa, malipo yaliyokawia, pamoja na ongezeko la wigo wa miradi.