SI KWELI Ripoti ya Infotrak imeonesha kuwa Edwin Sifuna anaongoza kwenye orodha ya Maseneta

SI KWELI Ripoti ya Infotrak imeonesha kuwa Edwin Sifuna anaongoza kwenye orodha ya Maseneta

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mchoro unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii unadai kuonyesha “Senators Performance Index 2026”, yaani orodha ya maseneta 47 nchini Kenya kulingana na utendaji wao, inayodaiwa kutolewa na kampuni ya utafiti ya Infotrak Research & Consulting.

Kwenye mchoro huo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ameorodheshwa wa kwanza kwa asilimia 80, akifuatiwa na Seneta wa Kajiado Lenku Sankok kwa asilimia 76 na Seneta wa Kisumu Tom Ojienda kwa asilimia 74.

Mchoro huo pia una jina na nembo ya Infotrak, jambo linaloufanya uonekane kama matokeo rasmi ya utafiti wa kampuni hiyo.
763103833_1394976429254219_6314914143555552551_n.jpg
 
Tunachokijua

Infotrak ni nini?​

Infotrak Research & Consulting ni kampuni ya utafiti inayofanya tafiti za maoni ya umma, masoko na mitazamo ya wananchi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo utendaji wa viongozi waliochaguliwa.

Mwaka 2026, Infotrak ilitoa matokeo ya CountyTrak Elected Leaders Performance Index, utafiti uliohusisha kaunti zote 47, maeneo bunge 290 na wadi 1,450. Utafiti huo ulihusisha washiriki 87,286 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Matokeo halisi ya 2026 yanasemaje?​

Hapa ndipo tofauti kubwa kati ya mchoro unaosambaa na matokeo halisi inapojitokeza.

Matokeo halisi ya Infotrak hayakuonyesha Edwin Sifuna kama seneta bora zaidi nchini kwa asilimia 80.

Katika matokeo rasmi, Seneta wa Kirinyaga Kamau Murango aliongoza kwa asilimia 69, akifuatiwa na Seneta wa Nyandarua John Methu kwa asilimia 68, huku Seneta wa Murang'a Joe Nyutu akiwa wa tatu kwa asilimia 65.

Kwa upande wake, Edwin Sifuna alipata asilimia 61, wala si asilimia 80 kama inavyodaiwa kwenye mchoro unaosambaa.

Hivyo, tofauti zilizopo si makosa madogo ya takwimu. Mchoro huo umebadilisha nafasi na alama za maseneta huku ukitumia jina na nembo ya Infotrak, jambo linaloweza kuwafanya watumiaji wa mitandao kuamini kuwa ni utafiti halisi.

Mchoro unaodai kuonyesha Edwin Sifuna akiongoza orodha ya maseneta bora nchini kwa asilimia 80 ni feki.

Infotrak ilifanya utafiti wa utendaji wa viongozi mwaka 2026, lakini matokeo yake halisi ni tofauti. Kamau Murango ndiye aliyeongoza orodha ya maseneta kwa asilimia 69, huku Edwin Sifuna akipata asilimia 61.

Kwa hivyo, mchoro huo umetumia nembo na utambulisho wa Infotrak kuwasilisha takwimu na viwango visivyo vya kweli.

Attachments

Back
Top Bottom