Ripoti ya Mabomu Mbagala iko wapi?

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,935
Reaction score
3,346
Heshima kwenu wana JF,
Ni muda mrefu sasa umepita tangu majanga ya kulipuka kwa mabomu kule mbagala. Kwa hekma ya Mh. waziri wa wizara husika aliunda tume ya kuchunguza nini ilikuwa sababu hasa ya ile milipuko iliyo sababisha vifo na hasara nyingi kwa ndugu zetu wa mbagala na maeneo jirani, kwa busara za mh waziri alitamka wazi kuwa kama itathibitika kuwa yale matukio yalitokana na uzembe wa watendaji wake basi angejiuzulu wadhifa wake, sasa je mpaka sasa ile tume bado haijawasilisha ripoti au Mh. anaogopa kutimiza azma yake ya kujiuzulu pindi atakapo tangaza yaliyomo kwenye tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha maafa.
 
Da! Joji usinikumbushe machungu.
Swala la kujiuzuru kwa viongozi wa afrika halipo. tusahau.
 
Unataka ripoti ya nini wewe??
Kuna kitu kilifanyika kule ambacho si cha kawaida...
Na lile ghala lilichomwa moto makusudi.
Baada ya silaha nyingi kuuzwa congo kinyemela, na wizi ulipogunduliwa wakaamua kuharibu ushahidi.
 
Tujikumbushe na mengine matukio ya 2009...
Mh. Chenge kugonga na kuua wasichana waliopanda daladala..kesi hiyo imefikia wapi?
 
Tujikumbushe na mengine matukio ya 2009...
Mh. Chenge kugonga na kuua wasichana waliopanda daladala..kesi hiyo imefikia wapi?
Hiyo ya Chenge bado ipo pale Kinondoni, inapigwa kalenda kama haina akili nzuri vile
 
Unataka ripoti ya nini wewe??
Kuna kitu kilifanyika kule ambacho si cha kawaida...
Na lile ghala lilichomwa moto makusudi.
Baada ya silaha nyingi kuuzwa congo kinyemela, na wizi ulipogunduliwa wakaamua kuharibu ushahidi.
Hii imekaa vibaya. tena imekaa vibaya vibaya sana. Ukijiita Kiranja Mkuu manake huwezi kufanya kitu bila kuwa na ushaidi wa kutosha. Hili nalo hakika neno.Unaweza kusema tumefika mahala tunachoma surface to air missile?Surface to surface au air to air missile. We unadhani lile ghala la mbagala ni la kitoto la vijikombora? Hili neno kaka. Tupe za kweli si za kusikia usidhanie pale wanahifadhi SMG au RPG na kama kweli unaweza kuondoa madudu yale pale kirahisi hivyo unavyodhani wewe.Lojistiki kaka au sivyo utuambie inakwendaje vile! Na hapa sizungumzii ripoti, hiyo inaweza kuwafaa wao wenyewe kwa sababu mambo mengine yatatolewa na mengine ni baada ya miaka 30, ni taratibu tu. Lakini Kiranja hili nalo neno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…