William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Kwa kawaida kazi ya kamati ya uchunguzi kama ilivyokuwa ile ya Mwakyembe ni kutafuta, kujua na kuanika ukweli na ukweli wote.
Kwa kawaida, meaning kwamba sio kwa kisheria hapo tayari kuna dosari ya hoja mkuu.
Sasa swali linakuja, je Kamati ya Mwakyembe ilitafuta, kujua na kuanika ukweli wote kama tulivyoambiwa awali?
Again tuliambiwa na nani? So far hatukuambiwa na sheria ya jamhuri, ila ni maneno ya kawaida ya kisiasa.
Binafsi nilishatoa maoni yangu tangu awali kwamba kitendo cha kamati ya Mwakyembe kutokumhoji mhusika mkuu wa saga la Richmond Ndugu Edward Lowasa ilikuwa ni mapungufu makubwa yaliyotia dosari ya kutisha credibility ya report. Mpaka hapo kwangu mie report ya Mwakyembe ilikuwa shwari na nzuri sana ukiacha hii methodological fault.
Kamati haikutaka kumuita Lowassa, kwa sababu kama alivyosema Mwakyembe ni kuwa walikuwa na ushaidi wa kutosha against Lowassa, na Mwakyembe alisema wazi kuwa uchunguzi wa kaamti haukuanza under the probable course ya Lowassa, au Lowassa kama kinara wa kuchunguzwa,
hapana wao walikuwa wanatafuta tu ukweli wa kilichotokea, ingawa ni kweli kama Lowassa, leo akiitwa kwenye mikono ya sheria kuhusiana na ile ripoti kutakuwa na good argument toka kwenye defence yake on this ya kutokuitwa kwake na kamati, lakini ninataka kumuamini Mwenyekiti wa kamati Mwakyembe aliposema kuwa kanuni zilizokuwa zikiilinda kamati ziko wazi kwenye hili la kumuita Lowassa au kutomuita zimekuwa fullfilled, lakini mbele ya sheria kunatakiwa kuwa na tatizo.