Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ndio maana kule kwenye thread ya MMKJ nimependekeza majeshi yetu yawafanyie kweli hii mijitu. Kwani hao "wapiganaji" wakiamua kusimama na kupigana kitatokea nini? Si fall-out tu ndani ya chama halafu baada ya hapo watu wanapangana upya? Kama kutakuwa na CCM Original, CCM Extra, CCJ na God-knows-what si viwe tu?
 
Tuseme nini (naogopa kufungiwa). Lakini nimeishiwa na nguvu na maneno pia siamini macho yangu kwa ninayoyasoma siamini hata kidogo lakini nadhani huo ndio ukweli wenyewe. Sasa ukisikia mpambano unaanza ni sasa tumechoka,tumechoshwa na hawa watu wanajiita wabunge wasio na huruma na nchi yao. Ni hivi kama wewe ni mbunge wa kuteuliwa wa kuchaguliwa mwisho wenu ni sasa 2010 ni mwaka wa ukombozi ndiyo nasema ni mwaka wa kujikomboa hata kama tupo mbali na nchi yetu tupo tayari kuliokoa katika hali yoyote. Wote mliokuwa bungeni mmekosa kuwatendea haki Watanzania waliowachagua.
 

hawa wapinzani tunaowajua au wengine??
 


- Baaada ya kufungwa kwa rasmi kwa mjadala wa Richimonduli huko bungeni, Mungu aibariki Tanzania!

Respect.


FMEs!
 

- In the wake ya yaliyojiri leo bungeni ni vyema wananchi wa Tanzania tukajikumbusha tena tumetokea wapi na hii ishu na nini hasa kilichofanyika na nini hakikufanyika na the whole ishu ya Richimonduli kwa kuiangalia upya ripoti ya kamati ya bunge ya Mwakyembe.

Respect.


FMEs!
 
1.2 Hadidu za Rejea


Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Novemba, 2007 uliipa Kamati Teule siku thelathini kukamilisha kazi yake na Hadidu za Rejea zifuatazo kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo ya uchunguzi:


1. Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina nani, na ni kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa gesi wa MW 100;


2. Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni waliyoshinda Richmond ilivyoshughulikiwa kuanzia Kamati ya Zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha kuwa sheria, taratibu, miiko na maadili ya zabuni yanayotawala zabuni za aina hiyo vilifuatwa au vipi;


3. Kutathmini mkataba baina ya Richmond Development Company LLC na TANESCO ili kujiridhisha kuhusu uhalali wa masharti ya mkataba huo ukizingatia gharama na masharti mengine ukilinganisha na masharti yaliyomo katika mikataba ya aina hiyo iliyoafikiwa na TANESCO/Serikali;


4. Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliyopewa Richmond kama vile kufunguliwa Letter of Credit na kupima uhalali wake;


5. Kuziangalia na kuzitolea maoni taarifa za TAKUKURU, PPRA na taarifa zozote nyingine zilizoangalia utaratibu wa zabuni ya Richmond; na


6. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na mchakato mzima wa Richmond ili kutoa mapendekezo ya kuboresha taratibu za zabuni kwa siku zijazo, kwa maslahi ya Taifa letu.
 
Suala hili (la Richmond) ni kama angel in disguise mana hii ndio ilikua/itakua turning point ya ufisadi nchini..! Na mabadiliko yooote yataanzia hapa.!
 

- Now look at this, kamati ilikuwa na nguvu za kisheria kwa sababu summons maana yake iko wazi ukitumiwa ukakataa kujibu au kuja, kamati ilitakiwa kuwa na uwezo wa kukusweka Rumande!



- Sasa tizama wananchi wa Tanzania tunaodai hapa kwamba wamechoshwa na CCM, wanalia pembeni lakini wakiitwa kwenye haki waseme ukweli wanakataa, tena mpaka kwa kulazimishwa na sheria ndio wanakubali kwenda kwenye kamati!

Respect.


FMEs!
 

- Sasa tizama haya madudu yaliyofanyika na hata leo kuambiwa eti mjadala umefungwa bungeni, what a joke!

Respect.


FMEs!
 
I have lost faith na serikali sio siri na watanzania ni waoga mno!!! Tutaendelea kutawaliwa tu hadi tutakapojua madhara ya uoga na unafiki
 
" I dream Edward Lowassa to be the president of this country oneday and Rostam Aziz will be his prime minister"
 
Tarehe 19 Disemba 2007 Katibu Mkuu huyo kwa maneno mengi na ya kuzunguka alithibitisha kuwa alichokifanya Msaidizi wake yalikuwa maelekezo ya Wizara. Kwa kuzingatia uhaba wa muda wa kukamilisha kazi ya Kamati Teule na kwamba suala hilo tayari lilikuwa limechukua siku tatu nzima za Kamati Teule, ugeni wa Katibu Mkuu huyo katika Wizara hiyo na katika masuala ya Bunge na uwezekano uliokuwepo kwa Kamati Teule kupata taarifa za ziada kupitia njia nyingine, Kamati Teule iliamua kusonga mbele na kumuacha Katibu Mkuu huyo na siri kubwa za Wizara yake.


Mheshimiwa Spika, ni kutokana na changamoto hizo Kamati Teule ikaona kuwa ni vyema baadhi ya Wajumbe wake waende Houston, Texas, Marekani ili kupata taarifa za kina na za ziada kuhusu suala hilo. Kamati Teule inakushukuru sana Mhe. Spika kwa kuzielewa changamoto zilizokuwa zinaikabili Kamati Teule na kuwawezesha Wajumbe watatu kwenda Washington DC kukutana na maafisa wa Ubalozi wetu, na Houston Texas kukutana na wamiliki wa Richmond Development Company LLC.
 
Pili, baada ya uchambuzi wa kina wa ushahidi wa maandishi na wa mdomo uliotolewa mbele ya Kamati Teule chini ya kiapo, Kamati Teule iligundua kuwepo kwa mgongano wa ushahidi, hivyo kutia mashaka juu ya dhamira ya baadhi ya mashahidi. Kamati Teule iliona umuhimu wa kuwaita tena baadhi ya mashahidi kuthibitisha kauli zao, na hata kuwachukulia hatua za kisheria baadhi yao ambao wangeendelea kusema uongo chini ya kiapo ili kulinda heshima ya Bunge.
 

sasa mpaka wanaojiita wapinzani ndio wamelala usingizi wa pono, hawa wengine sio ndio wanaanguka vitandani kwa ndoto?
 
Kufuatana na wizi kama huu wa ki-macho macho....Zanzibar na Penba wakitaka kujitenga ...kuna la kushangaza...??
 
KUTOKANA NA YALIYOJIRI HAPO JANA MJENGONI DODOMA, HII KESI ISIYOKUWA NA KICHWA WALA MIGUU NI BORA IFUTWE AU WADAU MNASEMAJE?

" Mshitakiwa Gire anadaiwa kuwasilisha hati za uongo baada ya kudanganya kuwa amepewa idhini na Mohamed Gire ambaye ni Mwenyekiti wa kampuni ya Richmond Development (LLC) ya Texas Marekani ya kuendesha Kampuni Richmond Development (LLC) ya Tanzania."

 
- Now look, sasa huyu Rostam analilia nini hasa na kwenda kusafishwa na majaji, kati ya mashahidi 75 ni wanne tu waliojitokeza bila kulazimishwa na summons, halafu tizama juhudi za kuwarubuni wabunge kuikana ripoti, pamoja na yote haya kuna wanaosema kwamba eti wamesafishwa na ishu imekwisha, hizo ni ndoto za mchana sana! Sasa kama ishu imekwisha kwa nini Rostam analilia kwenda kwa majaji?

Respect.

FMEs!
 
hakuna kesi hapo ni siasa tu..sipati picha EL alivopiga mvinyo jana kusherehekea kushinda hii battle...kweli EL ni mwamba usiotetereka kama mlima sayuni
 
Huu ni uhuni sasa, ni mbinu ya kuwamaliza watu kitaratibu! Wengine hamtanielewa leo. Ni heri liwalo na liwe, mjadala huu ufungwe before 2010!
Niliyasema haya Novemba 10 mwaka jana... Wala hayajachukua muda!

Walau sasa tunaweza kuelewana. This is it...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…