BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,122
- 4,060
Quote:- Fact
2. However, if some MPs are dissatisfied with any decisions made on this (Richmond saga) issue, we should agree to annul the provisions prohibiting us from deliberating on the matter to allow them to speak their minds.``
Kwakweli ninakuwa guided na huu ukweli hapa juu katika hoja yangu, umesema mengi lakini kwangu it comes down to this, kwamba kuna ambayo hakusema kwa sababu ya kubanwa na sheria za kulinda siri za serikali.
Mengine yote uliyosema ni kweli tupu, lakini integrity ya Mwakyembe abdo iko pale pale kwa sababu ya sheria iliyomzuia asiseme yote, ikivunjwa kama alivyomuomba Spika, na akashindwa basi integrity ya Mwakyembe itakuwa na tatizo, lakini so far bado ni shujaaa wangu na integrity yake iko sawa sana.
Mkuu FMES, heshima yako. hapo ndio unapochanganya mambo na nahisi kwamba ni kwa makusudi tu. Hakuna sheria yoyote iliyomzuia mheshimiwa Mwakyembe asiseme yote yaliyo kwenye ripoti yake zaidi ya muda tu. Kama ipo tutafurahi ukitufahamisha hapa.Sheria/kanuni ambayo mheshimiwa Mwakyembe anataka/anaomba ivunjwe ni ile inayotaka mjadala ambao umeishajadiliwa bungeni usirudiwe kujadiliwa tena bila kuvunjwa kwa sheria/kanuni husika namba 53/54kama sijakosea sana.
Kwa maana hiyo mheshimiwa Mwakyembe anaomba kanuni/sheria hiyo ivunjwe
ili mjadala wa Richmond urudishwe tena bungeni kujadiliwa ili watuhumiwa wajitetee tena na yeye "aseme hata kile alichokuwa ameacha kukisema kwa ajili ya kulinda heshima ya serikali".
kauli hii ina maana kuwa hakuna sheria yoyote inayomzuia kusema kile anachotaka kusema zaidi ya hiyo ya kuwa ni lazima sheria/kanuni husika ivunjwe kwanza ili mjadala urudishwe tena bungeni!
Tunaweza tukazungusha maneno tunavyotaka katika kumtetea mheshimiwa lakini ukweli uko pale pale hata kama tunajitahidi kutouona. Pamoja na kazi yake njema aliyotufanyia ambayo tunamshukuru kwayo, kwa hili la 'kuilindia heshima serikali' ametokota na lazima tumuambie maana ameturudisha kule kule kwa kulindana tunakotaka kutoka!