Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

inji hii sasa haina uelekeo kabisa, ukiangalia kushoto richmonduli, chadema wanatafunana wenyewe kwa wenyewe, ukiangalia nyuma cuf wamewa-disappoint wafuasi/wanachama wake bara + visiwani(muafaka with karume) ukiangalia mbele giza!!!

What next???

ccj
 
Ile dhana tulioanza kujijengea kwamba eti kuna wapiganaji ndani ya CCM ambao wanataka kulinda maslahi ya taifa hili - haipo tena.

Hakuna mpiganaji yoyote ndani ya CCM -mbali na usani usani kama huu na hapo ndiyo tumehakikisha kuwa upinzani kwa kweli utapatikana nje ya CCM.

Hili jambo linatia hudhuni sana - na tusitegemee mengine yoyote yashughulikiwe inavyotakiwa bali utakuwa usanii tu - haya ka KAGODA na EPA yote ni ndanganya toto tu wenzangu.

Pole sana Tanzania na viongozi wako wanaotetea wizi wa mali za watanzania maskini.

Nafikiri hatuna wawakilishi makini (Wabunge) ila tuna makada wa chama wanaoenda kutetea hoja za chama chao ili kuinusuru serikali isiwajibike kwa wananchi wake.

Je sisi wananchi wa ujumla wetu tuna uwezo wa kuichukulia hatua serikali kama kuna maamuzi ambayo tunaona hatujatendewa hakii? - wanasheria plse katiba inasemaje?
 
sasa mpaka wanaojiita wapinzani ndio wamelala usingizi wa pono, hawa wengine sio ndio wanaanguka vitandani kwa ndoto?


Waberoya,

You made my day!!! yani nahasira na jinsi huko bungeni mambo yalivyokwenda but nimecheka sana.
 
Am speechless! Kweli tumeachwa kama watoto yatima. Wkivurunda wao..ooh serikali imejifunza, wengine lazima wapigwe 'kenchi' mpaka lupango!
 
Jamani kuna mabo mengi sana ya kuyajadili zaidi ya hili la richmond liloendelea kwa zaidi ya miaka minne sasa na hakuna lolote zuri la kuwawajibisha hao waliokula pesa zetu walalahoi, mjadala huu wao wameufunga bungeni kibabe, basi kwa sababu hakuna jipya liletwalo na mijadala ihusuyo hii Richmond tuachane nayo na sasa tujadili maswala mbalimbali kwa manufaa na maendeleo ya watanzania waliowengi.

Richmond inagusa maslahi ya waliowengi pia , lakini kuendelea kujadili mambo yaleyale ambayo hata hayafanyiwi kazi ni sawa kabisa na kumpigia mbuzi gitaa ukitarajii atacheza.

Tanzania itajengwa na wazalendo wa kweli tu, ambao leo hawapo wengi madarakani.
 
Wakuu poleni na majukumu.

Naomba msaada kwa yeyote anayeweza kunisaida copy (in form of audio or video CD) ya hotuba ya Dr. Harrison Mwakyembe kuhusu sakata la Richmond aliyoiwasilisha Bungeni Mwezi February 2008. Nimejikuta ghafla naihitaji sasna kwa ajili ya kumbukumbu zangu na za vizazi vijavyo
Nitashukuru sana kwa yeyote atayenisaidia.

Kila la heri
 
Ngoja tukuangalizie, kuta unasoma signature yangu hapa chini.
 
Ngoja tukuangalizie, kuta unasoma signature yangu hapa chini.
Mkuu nitashukuru sana. Du signature yako inatisha. Nayakumbuka sana hayo maneno, natamani kuyarudia tena kwa kusikiliza
 
View attachment 25118View attachment 25118
Soma ripoti bwana. Inawezekana nikawa nimeweka nakala nyingi kwani nilikuwa najifunza jinsi ya kutuma faili.

Ukichukuwa hiyo PDF file na ku-upload kwenye software iitwayo ECHIFWITE v2.6 itabadilisha maandishi hayo na kuwa in form of audio. Wewe jukumu lako kuchagua kama unataka sauti ya kiume au kike kwa ajili ya output audio file.
Kazi kwako.
 
Ukichukuwa hiyo PDF file na ku-upload kwenye software iitwayo ECHIFWITE v2.6 itabadilisha maandishi hayo na kuwa in form of audio. Wewe jukumu lako kuchagua kama unataka sauti ya kiume au kike kwa ajili ya output audio file.
Kazi kwako.
Mkuu thanx. Itabidi niende kwa wataalam si unajua knowledge yangu ni ile ya kusomea mezani kwangu? Thanx alot
 
Hi wanaokumbuka, ripoti ya bunge kuhusu richmond, ilishauri nini kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya dg-pccb?? Wenye kukumbuka wanijuze, wakati tukitafakari kamati ya makani
 
Back
Top Bottom