Ripoti ya Richmond kutojadiliwa

Ripoti ya Richmond kutojadiliwa

  • Thread starter Thread starter GY
  • Start date Start date

GY

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,279
Reaction score
126
wakulu

Nimepata tetesi kuwa repoti ya richmond kutojadiliwa, kwani mh six yupo bize na mambo ya msiba ivo kurudi dodoma wiki ijayo kwa ajili ya kufunga bunge tu...TiaTia maji

Details please
 
Shughuli za bunge zinaweza kusimamishwa kwasababu spika yupo msibani? acha hizo Anne yupo, ila sema JK amempigia magoti 6.
 
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, ndani ya Chadema anaungwa mkono na vijana wajinga. - ABSALOM KIBANDA


Hii nini jamani------------mbona huyu masatu na jina lake simuelewi, anamaanisha nini mbona hayuko straight, nani huyo anayeungwa mkono na vijana wa CHADEMA wajinga?
 
Shughuli za bunge zinaweza kusimamishwa kwasababu spika yupo msibani? acha hizo Anne yupo, ila sema JK amempigia magoti 6.
.
Six can't afford to miss this, amesimamisha mambo yote mpaka awepo yeye in person. labda jumatatu au jumanne.
Hii ndio oportunity ya kukomelea misumari ya mwisho jeneza la Hosea, asiwepo?!
 
bwana masatu,CDM hakuna vijana wajinga, zaidi zaidi kuna vijana intelligent sana, they know what they are doing, na ndo maana tunataka kuwakomboa nyie wote ambao bado mnaonekana mmelala usingizi kama Sungura.
 
any way am not in the country lately lakini nafikiri Generation-Y you are wrong man, bunge haliwezi kusimama, kuna spika yule aliye kunywa maji ya bendera ya CCM hata jina naona siku naanza kumsahau anweza ongoza kikao though najua ataegemea kuinusuru CCM isididimie
 
bwana masatu,CDM hakuna vijana wajinga, zaidi zaidi kuna vijana intelligent sana, they know what they are doing, na ndo maana tunataka kuwakomboa nyie wote ambao bado mnaonekana mmelala usingizi kama Sungura.

Ni kweli lakini hajasema masatu mkuu kuwa CDM kuna wajinga......
 
Ndio unajua leo? pole!

"Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, ndani ya Chadema anaungwa mkono na vijana wajinga" - ABSALOM KIBANDA

Katika mambo mengi ninatofautiana na maandiko ya Kibanda ila katika hili niko naye sambamba.

 
bwana masatu,CDM hakuna vijana wajinga, zaidi zaidi kuna vijana intelligent sana, they know what they are doing, na ndo maana tunataka kuwakomboa nyie wote ambao bado mnaonekana mmelala usingizi kama Sungura.

Uko sahihi lakini usisahau kuwa kwenye msafara wa mamba na....... wamo. Hao ndo wanaomuunga mkono zitto.
 
Serkali na katibu wa bunge wamekubaliana mjadala wa Richmond hauna tija kwa watanzania. Sana sana utaendekeza malumbano. Hivyo hautakuwemo katika mambo yatakayojadiliwa katika kikao cha bunge kinachoendelea. Source TBC habari saa 2.00 jioni. Tarehe 5/11/09
 
Hapo tumeliwa! Live.

TAKUKURU wamefanikiwa kuwa tisha wabunge, seems the now understand kuwa walacho mjengoni si halali ni kaufisadi pia.

now kila mtu afe na lake.

Miss you much BABA WA TAIFA
 
Watu walikuwa na matarajio makubwa sana, na serikali imeshtukia mjadala huu unaweza kuvunja serikali tena!

Nini kitafuata?
 
Watu walikuwa na matarajio makubwa sana, na serikali imeshtukia mjadala huu unaweza kuvunja serikali tena!

Nini kitafuata?

Inasikitisha mno!Na hii ndio inaonyesha wazi kuwa kulindana hakutomalizika katika serikali ya Kikwete.Dawa ya hawa Waungwana ni kutokuwarudisha katika Uongozi 2010.
 
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, ndani ya Chadema anaungwa mkono na vijana wajinga. - ABSALOM KIBANDA


Hii nini jamani------------mbona huyu masatu na jina lake simuelewi, anamaanisha nini mbona hayuko straight, nani huyo anayeungwa mkono na vijana wa CHADEMA wajinga?

Straight = Shoga
 
Inasikitisha mno!Na hii ndio inaonyesha wazi kuwa kulindana hakutomalizika katika serikali ya Kikwete.Dawa ya hawa Waungwana ni kutokuwarudisha katika Uongozi 2010.

Mkuu Mwawado, wote hao ni mafisadi hivyo wanaogopana wao kwa wao maana wanajua madudu yao yote wanayoyafanya dhidi ya nchi yetu.

Kwa nchi nyingine CCM ingeweza kufutika kkatika anga za siasa Tanzania kwa kushindwa vibaya sana kutokana na madudu chungu nzima yaliyojaa ndani ya chama cha mafisadi na Serikali, lakini kwa nchi yetu ambayo ni kichwa cha Mwendawazimu CCM watarudi madarakani tena kwa ushindi mkubwa tu.

Hakuna lolote litakalofanyika dhidi ya EPA, Kiwira, mikataba ya dhahabu, Richmond/Dowans, Rada, Ndege ya Rais, Magari na Helicopters za jeshi, Meremeta n.k. Inasikitisha sana lakini ndiyo ukweli wa mambo
 
Inasikitisha mno!Na hii ndio inaonyesha wazi kuwa kulindana hakutomalizika katika serikali ya Kikwete.Dawa ya hawa Waungwana ni kutokuwarudisha katika Uongozi 2010.
Watarudi "Kwa kishindo" kama hatutaamua kufanya kweli...!
 
Hiyo sio kweli.
According to Mwananchi news paper Mjadala wa richmond ni kesho

Hatima ya kashfa za Richmond, Kiwira yafikia kileleni


Daniel Mjema, Dodoma na Ramadhan Semtawa
SAFARI ndefu ya mjadala mzito wa kashfa ya Richmond iliyotikisa nchi , sasa inakaribia ukingoni baada ya taarifa ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kupangwa kuwasilishwa kesho kwenye chombo hicho.

Kuwasilishwa taarifa hiyo kumekuja wakati kashfa hiyo ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa Richmond Development (LLC), ikiwa imeshasababisha mpasuko mkubwa ndani ya CCM, hasa wabunge tangu sakata hilo lilipoibuka bungeni Februari, 2008.

Wakati Richmond ikitarajiwa kutikisa Bunge kesho, taarifa ya sakata la mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ilikabidhiwa jana kwa Kamati ya Nishati na Madini, kuashiria kuwa wakati wowote itajadiliwa na chombo hicho cha kutunga sheria.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shellukindo, ambaye jana alikuwa jijini Dares Salaam, aliithibitishia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa taarifa hiyo ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge itawasilishwa kesho kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote.

Serikali inatakiwa ieleze hatua ilizochukua katika kutekeleza maazimio hayo, ambayo pia yanahusishwa na kuwajibishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, ambaye inadaiwa kuwa chombo chake kilishindwa kubaini rushwa katika utoaji wa zabuni hiyo kwa Richmond.

Wakati wabunge wakiishinikiza serikali itoe taarifa hiyo baada ya kupewa miezi sita, joto la Richmond limepandishwa zaidi na uamuzi wa Takukuru wa kuwachunguza wabunge kwa tuhuma za kuchukua posho mara mbili wakati wanapotekeleza majukumu ya Bunge, kitu kilichotafsiriwa kuwa kinawalenga wale wanaoshinikiza kutekelezwa kwa maazimio hayo.

Wabunge hao, wakiongozwa na Spika Samuel Sitta wameitaka Takukuru kuachana na mpango huo, baadhi wakidai posho hizo ni haki yao na wengine wakidai taasisi hiyo haikutakiwa ifanye uchunguzi huo katika kipindi ambacho wamekuwa wakishinikiza kuchukuliwa hatua kwa mkuu wa chombo hicho.

Lakini kilio chao kimekumbana na tamko kali kutoka kwa Dk Hoseah ambaye alidai kuwa hatajiuzulu na kuwataka wabunge ambao hawampendi, kupigia kura za kutokuwa na imani naye, kauli iliyotafsiriwa kuwa ya kibabe na iliyozidisha chuki.

Huku wabunge wakiendelea kurushiana maneno makali mbele ya kamati iliyoundwa kuchunguza kiini cha ongezeko la chuki miongoni mwa wanachama na viongozi wa CCM, ikiongozwa na rais wa serikali ya awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kiasi cha baadhi kutaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza upya sakata la Richmond, macho ya wengi sasa yatahamia kwenye mjadala huo kesho.

Akizungumza na Mwananchi hoja hiyo ya baadhi ya wabunge kutaka uchunguzi mpya, Shellukindo alisema hakutakuwepo na kurudi nyuma katika suala la Richmond na kwenda mbali zaidi akisema: "Labda Bunge livunjwe."

Shellukindo alisema Bunge limepanga kulimaliza suala hilo kesho na kuongeza kwamba, halitakubali kuona au kusikia taarifa yoyote ya serikali ambayo itachelewesha tena jambo hilo.

"Maazimio ya Bunge hayarudi nyuma; yanakwenda mbele; hakuna uchunguzi mpya unaoweza kufanyika tena kwa suala kama la Richmond. Hivi sasa tunakwenda kulimaliza jambo hili," alisisitiza Shellukindo.

Mbunge huyo wa Bumbuli alishangaa wanaotaka kujitetea sasa na akahoji: "Siku zote walikuwa wapi... mbona hawakujitetea kamati ilipowapa nafasi iweje waibuke leo."

Aliweka bayana kwamba, suala hilo lingeweza kumalizwa muda mrefu kama serikali isingekuwa na ganzi katika kulishughulikia kama ilivyofanya tangu ilipopewa maazimio hayo na Bunge Februari, 2008.

"Ni basi tu, hata hao wanaosemasema hivi sasa ni kwa sababu serikali yenyewe ilichelewa kutekeleza maazimio ya Bunge, lakini hili lisingekuwepo na tungekuwa tumeshalisahau," alisisitiza.

Kiwira, inayohusisha familia ya rais mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na waziri wa zamani, Daniel Yona, nayo imekuwa suala tete kila Bunge linapofanya mkutano wake na katikati ya mwaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kuwa serikali itautwaa mgodi huo unaodaiwa kuwa ulinunuliwa kwa bei ndogo na baadaye wawekezaji kushindwa kuanza kuzalisha umeme kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Hadi sasa mjadala mzito ni juu ya utekelezaji wa maazimio 23 dhidi ya kashfa ya Richmond, ikiwemo kumwajibisha Dk Hoseah ambaye ameshajitetea kuwa azimio namba 20 la Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini ilishaonyesha kuwa hana kosa.

Lakini, akizungumzia kinga hiyo anayoanza kuitumia Hoseah, Shellukindo alisema hakuna sehemu ambayo kamati imemsafisha bosi huyo wa Takukuru.

Dk Hoseah alitakiwa kujieleza kuhusu sababu za kuisafisha Richmond; kupuuzwa kwa ushauri wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) na kutobaini kasoro kwenye zabuni hiyo kama ilivyofanya kamati. Serikali ilieleza kuwa Dk Hoseaa alikwishajitetea kwa Katibu Mkuu Kiongozi na anasubiri hukumu.
 
mnatuchanganya sana na mambo yenu haya ya Richmond
 
Back
Top Bottom