Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza Julai 5, 2025 mbele ya wahariri na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Mratibu wa THRDC Kitaifa, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa wamebaini suala la ushirikishwaji wa wananchi lipo chini kwenye masuala muhimu yanayopitishwa na kuwagusa raia.
Ameongeza"Ni mara chache sana unaweza ukakuta mswaada umeletwa wananchi wemetoa maoni, harafu yale yanayotolewa na wananchi kule bungeni ukayaona yameingizwa"
Ametolea mfano miswaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiletwa kwa ajili ya wadau kutoa maoni, sakata la Ngorongoro ambalo amedai kuwa mpaka sasa kumeendelea kuwepo na malalamiko kwa sababu wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Amedai kuwa kupitishwa kwa masuala muhimu bila kushirikisha wananchi ipasavyo sio suala rafiki kwa ustawi wa jamii inayozingatia misingi ya utawala bora.
Kufuatia changamoto hiyo amesema kuwa wanashauri kuwe na mazingira ya kuruhusu Bunge liwe huru kufanya majukumu yake ya msingi ya kusikiliza maoni ya wananchi .
Ameongeza kuwa ni muhimu Sheria zinapoenda Bungeni, angalau kwa asilimia fulani ionekane kuna mawazo ya wananchi, kuliko wananchi kuanza kuzielewa pale ambapo zinakuwa tayari zimepitishwa na kuanza kutekelezwa.
Itakumbukwa kumekuwepo na malalamiko ya baadhi ya wadau ikiwemo asasi za Kiraia, vyama vya siasa na wadau wengine kudai kwamba mapendekezo yao mengi ambayo walipendekeza kwenye baadhi ya miswaada hayakuzingatiwa ipasavyo.