sensa
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 397
- 22
Mimi ni mwanachama kwa mujibu wa sheria lakini ni chama kinachoongozwa na watu ambao ni UWT au wale wanaonufaika na utawala uliopo. Ndio maana huwa kuna kampeni chafu sana kuhakikisha kuwa wanaogombea na kupata uongozi katika chama hicho ni wale wanaokubalika na serikali. Sijahudhuria mikutano yake kwa zaidi ya miaka 7 kutokana na kupoteza kwake muelekeo. Mwaka 2003 niliiambia kamati ya TLS ilyokuwa inaongozwa na Marehemu Prof. Mwaikusa kutokana na mimi kushikwa na kushtakiwa kwa kesi ya uchochezi wakati nikwatetea watu wa Bulyanhulu kuwa "Pale katika nchi yoyote ile duniani ambapo wanasheria wanalala kitanda kimoja na kula sahani moja na wanasiasa basi nchi hiyo imekufa". Bado ninarudia na kusema hivyo. Tanzania imekufa kwa kuwa wanasheria wengi wanajikomba kwa watawala na wanasahau jukumu lao takatifu la kupigania haki na demokrasia ya nchini.
Umesema vizuri lakini kususia kushiriki ndio unatoa nafasi kubwa ya wao kuendeleza madudu wanayotufanyia,ingekuwa vizuri ukaungana na wenzio ambao wanapenda TLS ifanye kazi kwa matarajio ya uundwaji wake nafikiri matatizo yaliyopo mngeweza kuyaondoa kabisa.