AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
RISASI ZA LISSU NA MAJASUSI WA URUSI NCHINI MONTENEGRO.
Na
Augustino Chiwinga
Usiku wa tarehe 16 October 2016 katika Jiji la Podgorica nchini Montenegro kulitokea jaribo la kimapinduzi ambalo pia lililenga kumuua Waziri mkuu wa wakati huo aitwaye Milo Dukanovic.
Kundi la washambuliaj waliojihami kwa silaha kali za kisasa na za kivita walivamia jengo la Bunge la nchi hiyo kwa nia ya kumuua Waziri mkuu ili kusababisha ghasia na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Ikumbukwe ya kwamba siku ya kesho yake yaani tarehe 17 October Serbia ilikua ifanye uchaguzi wake mkuu hivyo washambuliaji walijua kutokana hali ya mambo ilivyokua ni wazi baada ya kumuua Waziri mkuu huyo nchi isingekalika ,pangezuka machafuko ambaye yangepelekea kufanyika mapinduzi ya kijeshi nchin humo.
Lakini kwa bahati nzuri mpango huo uligundulika mapema na makachero na hali ya usalama ilidhibitiwa.
Baadae taarifa za kiintelijensia zikaja kutoka kwamba mipango yote hiyo iliratibiwa ns Serikali ya Urusi .
Urusi ilifanya hivyo ili kuizuia nchi hiyo ya Montenegro kujiunga na umoja wa kujihami wa NATO.
Urusi ilikua inahofia kama Montenegro ingeanikiwa kujiunga na umoja huo na kuwa mwanachama wa 29 wa NATO,basi ingepoteza udhibiti wake katika Bahati ya Adriatic, pia ingeipungizia nguvu na ushawishi katia nchi za Balkans kama vile Serbia.
Hivyo basi Serikali ya Urusi ikawatuma majasusi wake wawili mahiri kabisa Eduard Shishamkov pamoja na Vladimir Popov kwenda mpaka nchini Montenegro kupanga njama za kumuua Waziri mkuu wa Montenegro hali ambayo ingezua taharuki na machafuko ambayo yangepekekea Serikali kupinduliwa na mpango wa Montenegro kujiunga na NATO ungeishia hapo.
Nimeanza story hiyo ili kuwaeleza watanzania kwamba yanapotokea matukio kama yaliyomtokeaTundu haifai kulipuka n kuanza kunyoosheana vidole.
Inahitaji utulivu na kutafakari kwa kina bila ya mihemko au mizuka.
Tukae tukijua kwamba zamani enzi za ukoloni wazungu walitumia mbinu mbalimbali za kututawala na kutuibia mali zetu kama "Divide and Rule."
Lakini sasa hivi wamebadilisha wamekuja na mbinu mpya iitwayo "make them fight and plunder their wealth."
Nani asiyejua kilichotokea Angola ,au kinachotokea Congo.?
Mzungu katia fitna wakapigana wenyewe kwa wenyewe kisha yeye akaanza kukomba madini, mafuta na mali nyinginezo.
Naona kuna kila hali ya kututaka kutufarakanisha watanzania ili waweze kuiba kirahisi mali zetu kirahisi.
Vita ya kiuchumi aliyoianza Mh .Rais Magufuli imezikasirisha nchi za mabepari waliozoea kutuibia kupitia mikata mibovu waliyoingia kwa hila na baadhi ya wenzetu wasiokuwa wazalendo.
Sasa wamekuja na mkakati Mpya wa kutuchonganisha.Shime watanzania tushikamane tuwe kitu kimoja ili zile fitna walizozifanya Libya, Iraq na nchi nyinginezo zisifanikiwe.
Tukikubali kuzifuata fitna zao basi tujue tumekwisha.
Wazungu wanahitaji mafuta yetu gesi yetu Almasi yetu Tanzanite zetu na dhahabu zetu.Watatumia kila mbinu ili wazipate kirahisi , bila shaka wametishika na mwelekeo Mpya wa Serikali ya awamu ya 5 juu ya kulinda na kutetea raslimali hizi kwa maslahi mapana ya Taifa letu .
Narudia tena shambulio la Lissu lenye lengo la kutugombanisha watanzania tuliozoea kuishi kwa amani na udugu.
Tuwe watulivu watanzania , tusikubali kuingia katika mitego ya mabepari na wanyonyaji.
MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI MAGUFULI NA MUNGU MPONYE LISSU KWA HARAKA AREJEE NYUMBA SALAMA SALMIN.
Sent using Jamii Forums mobile app