Steven Cheung, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampeni ya Donald Trump, alisema: "Rais Trump yuko salama baada ya risasi kurushwa karibu naye. Hakuna maelezo zaidi kwa sasa."
Pia, Huduma ya Siri ya Marekani imethibitisha hadharani kuwa Donald Trump yuko salama.
Gazeti la New York Post na ABC News vinaripoti kuwa Rais wa zamani alikuwa katika hoteli hiyo wakati watu wawili walipokuwa wakibadilishana risasi karibu. Vyombo hivyo vinasema kuwa Trump hakuwa mlengwa wa shambulio hilo, vikimnukuu afisa wa usalama ambaye hakutajwa jina.
Silaha aina ya AK-47 mtutu wake ukionekana umechomoza katika kichaka cha uwanja wa golf ulistukiwa na mmoja wa walinzi wa Trump ambaye alikuwa akisongea mbele tundu moja la golf kabla Trump hajamaliza lingine ... ktk uwanja wa golf wa International Golf Course in West Palm Beach Florida ..
Picha maktaba: picha ya siku zilizopita ikimuonesha Donald Trump akicheza mchezo wa golf
Habari hii jaribu lingine dhidi ya Donald Trump inatupa funzo Tanzania kuwa watu wasiojulikana hawawezi kuacha nia yao ovu ya,kuteka, kupoteza pia kuua na hasa ikiwa hatutapaza sauti tarehe 23 September 2024 kwa maandamano Dar es Salaam kuipa mbinyo serikali ya Tanzania ifanye kazi ya kulinda usalama wa raia.