Risasi zarindima katika eneo la karibu alipokuwepo Donald Trump, Maafisa usalama wanasema yupo salama

Damn! They want him dead so bad!

Ila hili ni doa kubwa sana kwa Secret Service.

Hawa watu wanawezaje kufika karibu hivyo na Rais mstaafu ambaye ni target kubwa?

Au kuna hujuma za makusudi zinazofanywa ili kutoa mianya ya kumdungua?
Mara ya kwanza ulisema ni democrats kwa vile anawashinda kjwenye uchaguzi; baada ya uchunguzi ikaja fahamika kuwa yule kijana aliyemtupia Trump gololi alikuwa ni republican damu damu. Sasa je leo bado unasema huyo pia ni democrat kabla hata uchunguzi haujafanyika?
 
Relax old man! Ukisoma kwa utulivu bila mihemuko, utaelewa na kuona nilichokiabdika.

Hakuna sehemu yoyote niliposema kuwa huyu ni Democrat.

Kama kuna sehemu nimesema/ nimeandika hivyo, onyesha tafadhali.

You are too old kusoma vitu na kuandika kwa mihemuko.
 
andiko lako linaeleweka vizuri sana
 
Angeahirisha tu ugombea
 
andiko lako linaeleweka vizuri sana
Hahahaa 🤣🤣.

Hiyo ni tafsiri yako kwa kutumia mihemuko yako tu.

Ningekuwa nimeandika kama unavyodai, ungenionyesha kwa kuninukuu.

Umeshindwa kuonyesha nilipoandika hivyo unavyodai kwa sababu sijaandika wala kusema hivyo.

Acha uzushi 🤣. Na punguza bias.
 
Majamaa yanamlenga TRUMP bado​

Trump anusurika jaribio jingine la mauaji​

Rais wa zamani Donald Trump yuko salama kufuatia jaribio la mauaji katika uwanja wake wa gofu wa Florida, na "mshukiwa wa tukio hilo " yuko kizuizini, mamlaka ya Marekani imethibitisha.

Maafisa wa usalama waliona mtutu wa bunduki likipenya kwenye vichaka na kumfyatulia risasi, maafisa walisema.

FBI ilisema Trump alikuwa umbali wa yadi 300-500 (m 275 hadi 455) wakati huo. Bunduki ya aina ya AK47 na upeo, pamoja na mikoba miwili na kamera ya GoPro, vilipatikana baadaye kwenye eneo la tukio.

Shahidi aliripoti kumuona mshukiwa akikimbia kutoka kwenye vichaka na kurukia gari nyeusi aina ya Nissan baada ya maafisa hao kumfyatulia risasi mara kadhaa.

Shahidi huyo alipiga picha gari hilo na nambari ya usajili na ilizuiliwa baadaye katika Kaunti ya Martin, kaskazini mwa klabu hiyo.
"Tulikamata Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Martin, tukawajulisha, na wakaona gari na kulivuta na kumzuia mtu huyo," Sheriff Ric Bradshaw wa Kaunti ya Palm Beach alisema.
"Baada ya hapo, tulimchukua shahidi aliyeshuhudia tukio hilo, tukampandisha hadi pale na akajitambulisha kuwa ni mtu ambaye alimuona akikimbia kutoka kwenye kichaka, ambaye aliruka ndani ya gari,"alisema.

Katika barua pepe kwa wafuasi wake, Trump alisema yuko "salama na mzima"." Hakuna kitakachonipunguza kasi," aliandika. "Sitasalimu amri kamwe!"

Tukio hilo linakuja takribani miezi miwili baada ya mtu mwenye silaha kujaribu kumuua Trump katika mkutano wa hadhara huko Butler, Pennsylvania, akimpiga sikioni

Source: BBC Swahili
 
Cha ajabu waliotufundisha Demokrasia hatujasikia wakija na kampeni ya kusema "Biden Must go", ila sisi wanafunzi vilaza wa demokrasia tumekurupuka na viingereza vyetu vya 'kugugo', na kuropoka kuwa "Samia must go".
 
Huyu mtuhumiwa alimpigia kura Trump 2016!
 
Cha ajabu waliotufundisha Demokrasia hatujasikia wakija na kampeni ya kusema "Biden Must go", ila sisi wanafunzi vilaza wa demokrasia tumekurupuka na viingereza vyetu vya 'kugugo', na kuropoka kuwa "Samia must go".
Kwa sababu wote wamejulikana, wamekamatwa au kuuwawa.
 
joto la uchaguzi
 
Rais wa zamani Donald Trump yuko salama kufuatia jaribio la mauaji katika uwanja wake wa gofu wa Florida, na "mshukiwa wa tukio hilo " yuko kizuizini, mamlaka ya Marekani imethibitisha.
Maafisa wa usalama waliona mtutu wa bunduki likipenya kwenye vichaka na kumfyatulia risasi, maafisa walisema.
FBI ilisema Trump alikuwa umbali wa yadi 300-500 (m 275 hadi 455) wakati huo.
Bunduki ya aina ya AK47 na upeo, pamoja na mikoba miwili na kamera ya GoPro, vilipatikana baadaye kwenye eneo la tukio.
Shahidi aliripoti kumuona mshukiwa akikimbia kutoka kwenye vichaka na kurukia gari nyeusi aina ya Nissan baada ya maafisa hao kumfyatulia risasi mara kadhaa.
Shahidi huyo alipiga picha gari hilo na nambari ya usajili na ilizuiliwa baadaye katika Kaunti ya Martin, kaskazini mwa klabu hiyo.
"Tuliwasiliana na Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Martin, tukawajulisha, na wakaona gari na kulivuta na kumzuia mtu huyo," Sheriff Ric Bradshaw wa Kaunti ya Palm Beach alisema.
"Baada ya hapo, tulimchukua shahidi aliyeshuhudia tukio hilo, tukampandisha hadi pale na akajitambulisha kuwa ni mtu ambaye alimuona akikimbia kutoka kwenye kichaka, ambaye aliruka ndani ya gari,"alisema.
Katika barua pepe kwa wafuasi wake, Trump alisema yuko "salama na mzima".
"Hakuna kitakachonipunguza kasi," aliandika. "Sitasalimu amri kamwe!"
Tukio hilo linakuja takribani miezi miwili baada ya mtu mwenye silaha kujaribu kumuua Trump katika mkutano wa hadhara huko Butler, Pennsylvania, akimpiga sikioni
 
Tunatoa kauli ya kupinga udikteta unaofanywa kwa Trump,tunaamrisha uchunguzi huru ufanyike.
 
Nilisoma humu kuna jamaa aliandika baada ya jaribio la kwanza kwamba kabla ya mwaka kuisha litatokea jaribio la pili tena ila hatokufa .
 
Wauaji waipenda sana gari ya Nissan sijui why?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…