Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Baada ya anguko la klabu za Enyimba, Enugu Rangers na Heartland klabu bora za Nigeria, Ndipo zilipoibuka klabu za Kano Pillars, Plateau United na Rivers United. Ni timu za kiazi kipya kwenye mafanikio.
Ushiriki wao kwenye CAF umeanza hivi karibuni mwaka 2017, Hizi rekodi zao wakiwa nyumbani ambako ndio huwa hatari zaidi.
Michezo kumi na nne ya CAF [14] waliocheza nyumbani wamepoteza Mmoja [1] dhidi ya Far Rabat 1-0, Wameshinda mara kumi na mbili [12] na Sare 1 dhidi ya Disables Noirs.
Miongoni mwa timu ngumu walizowahi kuzifunga nyumbani ni Enyimba, Club Africain, Asec Mimosas, El Merrick, Wydad Casablanca na Bloemfontein.
Credit: Gharib Mzinga