RIWAYA: Black star

Black Star 2: Astra 33





"Binadamu unadhani una sifa za kuwa bwana wangu" sauti hiyo aliisikia Garaaji peke yake.



"Nani alikwambia mimi nataka niwe bwana wako, tokea siku tulioingia makubaliano mimi na wewe yalikuwa ni makubaliano yenye usawa" alijibu



"Hahaha, unanifurahisha sana. Ila uwezo wako bado uko chini sana. Ili kuingia mkataba na mimi unatakiwa angalau kuwa daraja la Kyodan" alijibu Veremin.



Fahad akasogea mpaka alipo Garaaji na kukaa nyuma yake, "umekidhi vigezo vya kupanda daraja" aliongea na kumgonga sehemu kadhaa mgongoni. Radi yenye rangi ya dhambarau ikashuka kwa kasi na kumpiga Garaaji.



"Mkataba umekamilika" aliongea Veremin na hapo Garaaji akashumtuka, lile yai likapasuka na kutoa moshi mwingi sana wa zambarau. Moshi huwo ukajikusanya sehemu moja na ulipotoweka, mbele ya Garaaji kulikuwa kiumbe mkubwa mwenye rangi ya dhambaray iliyowamba na yenye kumeremeta. Kichwani alikuwa na pembe mbili kubwa kiasi na pembeni ya pande zote mbili za mdomo alikuwa na sharubu ndefu.



Veremin hakuwa nyoka tena bali sasa alikuwa ni dragon, akatembea kwa kasi na kuanza kupaa. Alipofika angani akanguruma kwa nguvu, kila aliesikia mngurumo huwo aliziba masikio.



Gorigo akatoka kwenye mwili wa Fahad na kupaa kwa kasi, "wewe mwehu jua nafasi yako" nae akanguruma. "Wewe unanambia hivyo kama nani" aliongea Veremin akionekana kukerwa na maneno hayo.



"Inaonekana umesahau nafasi yako, na umenisahau mimi si ndio" aliongea Gorigo na kupaa juu zaidi, akatanuwa mbawa zake mpaka mwisho na kuachia ukwenzi mkali sana. Alikuwa akimuonesha Veremin nani ni mwamba kati yao wawili.



"Achana nao, kila mmoja anataka kumtambia mwenzake" aliongea Fahad na kutabasamu. Akaendelea "hongera kwa kufika daraja la Kyodan, atakuja mtu kukuchukuwa akakuoneshe utakapokuwa unaishi. Tumia usiku wa leo kuzoea nguvu mpya ulioipata na kesho tutakwenda kumchukuwa mwanao" aliongea Fahad na kuruka kwa kasi sana. Akatuwa mgongoni kwa Gorigo na kumuamuru waondoke.



Veremin alipomuona Fahad tu, akashusha kichwa. Alielewa kabisa mtu huyo hakuwa kwenye ligi yake. Gorigo akaondoka kwa kasi na kupotelea angani. Veremin akashuka na kuingia katikwa mwili wa Garaaji kwa ajili ya kupumzika.



*********



"Unamuonaje Veremin" aliuliza Fahad wakati Gorigo akiwa angani juu ya mawingu kabisa akielea.



"Pale alipofika sasa ndio kwanza uzao wake wa pili, akifika uzao wa tatu atakuwa na nguvu za huyu mfalme hapa" alijibu Gorigo akimaanisha yeye.



"Hahaha! Ila ukiendelea kuzembea utakutana na mbabe atakae kuweka chini".



"Sidhani" alijibu Gorigo.



"Kwanini unasema hivyo"



"Kabla sijajibu hilo swali, nikuulize jambo kwanza"



"Uliza tu"



"Kwanini unaficha uwezo wako halisi?"



"Oh! Inaonekana umechungulia katika siri zangu".



"Hahaha! Hapana kwasababu ya mkataba tu, kuna mambo huwa nayajua tu kama wewe unavyojua baadhi ya siri zangu".



"Najiandaa na vita hilo ni moja lakini pia mwili kwa ulivyo sasa hauwezi kuhimili uwezo wangu wote. Utavunjika na kifo kitakuwa hakiepukiki"



"Vita, nilijua mapema tu. Jinsi unavyopigana na jinsi unavyochagua watu wako wa karibu. Kwa wengine watadhani unachagua tu kutokana na upendeleo lakini mimi nimeona unachotafuta".



"Hahaha! Ni kipi hicho nitafutacho"



"Hilo nitakuambia siku nyingine lakini jua ukiachilia mimi kuwa mnyama wa kiroho, nina rithi taaluma kutoka kwa mama yangu. Jambo moja ambalo kila nikikuangalia linanijia kichwani ni miezi kumi na mbili. Kwasasa sijapata ufunuo kamili lakini naamini ndani ya muda nitajua" alifafanua Gorigo.



"Una jicho zuri, haya niambie kwanini hakuna myama mwengine atakaekutisha"



"Kwasababu yako, katika mwili wako mpaka sasa kuna nguvu aina nne za asili. Ila mimi pia sijaonesha uwezo wangu wote. Ninaogopa ikiwa nitakuzidi sana, nitakuzuia kufika unapotaka kwa muda. Najua unafahamu uwezo wangu halisi mpaka sasa. Ukifika daraja la uzima wa milele mimi ndio nitaanza kutumia uwezo wangu halisi kwasababu kuanzia hapo tutakuwa katika njia iliyojaa damu na vifo"



"Nipe miaka mitatu nitakuwa katika daraja hilo, mpaka wakati huwo endelea kunilinda" aliongea Fahad na kusimama kisha akajirusha kutoka katika mgongo wa Gorigo na kuanza kushuka chini kwa kasi.



Gorigo akaachia ukwenzi mkali na kufunga mbawa zake, akaanza kushuka kwa kasi. Kwa watu wa mbali walioona tukio jilo walibakiwa na kumbukumbu katika mioyo yao jinsi imani ya kweli ilivyokuwepo kati ya binadamu na mnyama wa kiroho.



Walipokaribia chini, Gorigo akazunguka kwa kasi nankupita chini ya Fahad. Akatua mgongoni na ndege huyo akafungua mbawa zake kubwa. Kasi ikapungua kabla ya kutua kisha akapotea na kurudi mwilini kwa Fahad.



Fahad akaelekea chumbani kwake kwa ajiki ya kupumzika, "nimekusubiri sana mume wangu" sauti laini ya kike ilisikika ikiongea kwa deko.



"Kuna mambo nilikuwa nayaweka sawa" alijibu Fahad akivua nguo na kuzitundika sehemu. Mikono laini ikatarizi kutokea mgongoni kwake na kukutana katika kifua chake. "Mume wangu, nataka mtoto" alinong'oneza na kumpuliza Fahad sikioni.



"Acha nikaoge kwanza, mambo ya watoto tutaongea nikirudi" alijibu Fahad akijitahidi kupotezea mapapai laini yaliokuwa yakijikandamiza mgongoni kwake.



"Nitakuwa nakusubiri" aliongea Nephira na kumuachia Fahad, akarudi kitandani na kujilaza. Ndani ya chumba hicho kulikuwa kunanukia uturi si wa kawaida. Fahad akaelekea nje kwenye bwawa dogo lenye chemchem ya maji ya vugu vugu na kujitumbukiza. Akaegemea jiwe kubwa, na kuacha maji hayo yenye hali ya umoto kuifanya misuli yake ilainike.



**********



Katika pango lenye kiza sana, kelele za mwanamke aliekuwa akilia kwa maumivu zilisikika. Mara kadhaa vilisikika vibao na sauti ya kiume ikifoka.



"Kazi yangu imekamilika, fanyeni mnachotaka na kesho mumlete ngomeni" alitoka mtu mwenye gagulo jeusi lililofunika mpaka kichwani. Akapiga mkofi, mnyama mkubwa mweusi akatuwa kwenye kiza. Akapanda na kuondoka.



"Tumepewa ruhusa tufanye tunachotaka" aliongea mlinzi mmoja akionekana mwenye furaha sana akielekea ndani.



"Ah! Malaya huyu kang'ata ulimi" aliongea kwa nguvu, wenzake wakafika na wote wakaangaliana.



"Oya acha upuuzi, kula hivyo hivyo" aliongea mmoja.



"Ah! Mi siwezi fanya hivyo naogopa hasira za mungu wa kifo" aliongea akiondoka. Kutokana na hilo wote hawakuwa na namna zaidi ya kumfunika mwanamke huyo.



Siku ya pili jioni.



Msafara mkubwa wenye walinzi wengi ulikuwa njiani kuelekea njia ya Lorei. Katika msafara huwo sala na gari iliyokuwa ikivutwa na farasi wawili waliofunikwa kwa vitambaa vya dhahabu.



Wakiwa njiani taratibu mvua ndogo ikaanza kunyesha, "malkia nashauri tusimame kwanza kwa muda mrefu tutaingia katika njia ya milima ambayo itakuwa hatari kama tutaingia na mvua" aliongea mtu mmoja.



"Sawa" sauti laini ikasikika kutoka ndani ya gari hiyo, yule mtu akaiwasilisha amri hiyo kwa wingine na msafara ukasimama. Watu wakatawanyika na kutengeza makazi ya muda mfupi mpaka mvua hiyo itakapopita ili waendelee na safari bila kuwa na shaka ya kupata ajali njiani.



 
Black Star 2: Astra 34

Baada ya muda mvua ikakata lakini wingu halikupotea na lilizidi kuwa jeusi na kuifanya jioni kuwa kama usiku.



"Malkia, malkia" alifika mtu mmoja akihema, alikuwa akitoka jasho.



"Unasemaje, malkia amepumzika kwa sasa" alizuiwa na mlinzi aliekuwa amesimama nje ya tent la malkia.



"Ila ni muhimu sana, hii taarifa ni muhimu naomba nimuone" alisistiza aliefika.



"Muache apite" sauti laini ilisikika ikitokea ndan, yule mlinzi akasogea pembeni na kumruhusu apite.



"Sema kilichokuleta haraka na uondoke" aliongea.



"Nimemuona Marshal Garaaji kilometa kadhaa kutoka hapa" aliongea.



"Unasem nini wewe, Marshal Garaaji! Si nimepokea taarifa ameuwawa".



"Hapana, yuko hai tena anafuatana na mtu mwengine, eh! Yule mwengine sidhani hata kama ni mtu. Hili wingu jeusi linatembea juu yake" aliongea.



"Sawa, unaweza kuenda" aliongea malkia huyo, yule alieleta taarifa akatoka na kuondoka. Akampa maeleke,o mlinzi aliekuwa nje. Mlinzi huyo akaondoka na kuelekea walipokuwa wampumzika wazee fulani hivi wanne.



"Amri imetoka kwa malkia, amesema muandae vikosi na mujiandae kumpokea Marshal Garaaji" alifikisha ujumbe na kuondoka.



"Garaaji! Katika viumbe wenye roho ngumu kufa wewe ni mmoja wapo lakini leo utakufa" aliongea mzee mmoja kati ya wale wanne.



"Sebas, una uadui gani Garaaji" aliongea mwengine na wote wakacheke. Wakaelekea walipo farasi wao na kuvaa mavazi yao ya kivita tayari kwa kumkabili Garaaji.



Baada ya muda kidogo watu wawili wakiwa juu ya wanyama wakaonekana angani wakikaribia eni la makazi hayo ya dharura. Wale wazee wanne wakapaa na kusimama mbele yao.



"Garaaji umekuja kufanya nini?" Aliuliza Sebas.



"Nimekuja kumchuka mwanangu na wala sitaki kumwaga damu" aliongea Garaaji akijitahidi kudhibiti hasira zake. Wale wazee wakaangaliana kisha wakacheka kwa nguvu tena kwa kiburi. Fahad alikuwa kimya akitafuta ni wapi alipo binti huyo kutokana na maelezo ya Garaaji. Ghafla moyo wake ukafa ganzi, alihisi damu ikianza kumchemka.



"Garaaji mwanao yupo kwenye ile gari ya farasi" aliongea akionesha kidole lilipo gari hilo. Garaajai akatikisa kichwa na kutaka kuondoka, "unadhani unakwenda wapi" aliongea Sebas na kutaka kumzuia. Kofi kali sana likatua shavuni, kichwa kikazunguka mara mbili kabla ya kunyofoka shingoni. Mwili wake ukaanguka chini ukiwa hauna uhai tena.



"Niachie mimi hawa nzi, nenda kwa mwanao" aliongea Fahad akifukuta moyoni, alitamani kumwambia jambo Garaaji lakini akasita. Alitaka ashuhudie mwenyewe kisha afanye maamuzi, huwo ulikuwa ni mtihani mgumu kwake kuupita.



"Sawa, Master" aliongea na kuondoka.



"Umemuua Sebas, unamjua ni mkwe wa mfalme huyo" aliongea mzee mwengine.



"Sasa kwani mimi najalo basi" alijibu Fahad na kuwakata jicho kali sana, "inakuwaje binadamu unaweza kufanya ukatili kiasi kile tena kwa binti mdogo" aliwauliza.



"Sasa nani anajali kuhusu binti kama yule, tokea mwanzo maisha yake yalishaamuliwa kuwa awe ni njia ya mfalme kufika mbali zaidi katika martial art yake" alijibu mzee mmoja.



"Kwa hiyo watu wengine hawana thamani mbele ya huyo mfalme wenu?"



"Umewahi kusikia nzi ana thamani, wote wanaishi kutoka na huruma ya mfalme tu. Kama si hivyo wote wangekuwa washakufa na kuwa mbolea kwa mfalme kukuza martial yake" alijibu.



Chini.



Garaaji anatua karibu na gari hiyo lakini mwili wake unaanza kupata wasiwasi na kusita kidogo kabla ya kupiga hatua. Anatoa shuka kubwa iliyokuwa imefunika gari hiyo, ghafla anadondokea magoti. Machozi yakatengeza michirizi mashavuni mwake.



"Laheya wangu, kwanini wamekupa kifo kibaya kiasi hichi. Uliwafanya nini katika uzao wako uliopita mwanagu" aliongea Garaaji akilia. Alikua akiuwangalia mwili wa binti mdogo ukiwa umeharibika vibaya sana. Karibu kila kiungo kilikuwa na kasoro. Mikono na miguu ilikuwa imevunjika, kichwa kilikuwa kimegeuka nyuma.



"Inabidi ukubali tu uhalisia Garaaji, tokea mwanzo Laheya alikuwa akiandalia kukutana na mwisho wa aina hiyo" sauti ya kike ilitokea nyuma yake.



"Feris, wewe ni mama wa aina gani. Unaacha mwanao anakutana na madhila kiasi hichi" aliofoka, mishipa ya kichwa ilikuwa imesimama.



"Hahaha! Masikini Garaaji, unadhani nilikuwa namjali kama mwanangu. Nimjali vipi uchafu kama huwo, watoto wangu wote wanatokana na damu ya mfalme kasoro huyo mjinga" aliongea mwanamke huyo bila kuonesha hata ishara ya kibinadamu.



Kishindo kikasikika baada ya miili mitatu kuanguka, pembeni ya malkia. Fahad akatua pembeni ya Garaaji na kumgusa begani. "Samahani rafiki yangu nimeshindwa kutimiza ahadi yetu" aliongea.



"Sio kosa lako" aliongea Garaaji na kumuangalia Fahad, macho yake yalikuwa na mboni nyembamba yenye rangi ya zambarau, "fanya utakalo, bakisha mtu mmoja ambae atapeleka ujumbe kwa mfalme. Na usijali huyu mbwa nitamzuia hapa, ukishamaliza hao wengine ndio tutamalizana nae" aliongea Fahad.



"Nashukuru" aliitika Garaaji, mapembe yenye ncha kali yakaanza kuchomoza katika kichwa chake. Mwili wake ukaanza kubadilika na kujaa magamba, kucha zake zikarefuka na chini ya mgongo ukatoka mkia. Akanguruma kwa nguvu, mngurumo ambao uliwazibua masikio wengi waliokuwa daraja la chini. Alikuwa ameungana na Veremin.



Akapotea eneo hilo kwa kasi na baada ya sekunde chache vilio vikaanza kusikika.



"Wakati Garaaji akipunguza hasira zake, kwanini mimi na wewe tusiongee" aliongea Fahad na kumuangalia Feris.



"Unaonekana wewe ni mtamu sana" aliongea mwanamke huyo na kuramba midomo yake ya chini.



"Mimi sina ladha mbaya kiasi cha kuvutuwa kikongwe kama wewe, na huko kuchombeza kwako hakuna madhara kwangu. Hivyo kwanini tusiachane na mambo ya kipuuzi na tuongee mambo ya msingi" aliongea Fahad na kumkazia macho.



"Wala siyo raha kucheza na mtu ambae havutiwa na uzuri wangu" aliongea malkia Feris.



"Hahaha, kama wewe ni, hao wazuri wasemeje sasa aliongea Fahad na mzuri" kutambua kwanza leo utakufa, hilo ni moja. La pili unajisikiaje kuzaa na watoto wako mwenyewe".



"Hahaha! Kuzaa na watoto wangu sio kazi yako, na Garaaji hana uwezo wa kiniua" alijitamba malkia Feris.



"Nani alosema kwamba atakaekuua ni Garaaji".



"Hahahah, unataka kusema wewe ndio utaniua. Ikiwa uwezo wako uko chini kuliko Garaaji unategemea kuniuaje kwa mfano"



"Wewe ni mupambavu sana, kukuua sihitaji hata kupiga hatua moja. Kama ungekutana na mimi mwaka mmoja, kweli ningekuwa sina uwezo huo lakini bahati yako mbaya sana Sakyuba" aliongea Fahad na kuita jina laks halisi.



"Umelijuaje jina langu halisi" aliongea Feris akianza kukasirika.



"Kwani hukupokea taarifa za kifo cha Hezoromo"



"We...wewe... usiniambie wewe ndio umemuua kakangu" alifoka Feris (Sakyuba).



"Vita yangu na yeye haikuwa vita kabisa, ilikuwa ni kama kusmhikisha adabu mtoto mdogo. Hatukupigana, nilimponda kisawasawa" aliongea Fahad na kutabasmu.



"Nitakuua, sitapumzika mpaka nichukue roho yako" alifoka.



"Una uhakika unaweza kupiga hata hatua kutoka uliposimama" aliongea Fahad na kukunja ndita. Feris akataka kupiga hatua lakini miguu haikuinuka. Jasho jemba likaanza kumchuruzika, alijaribu tena kuinua miguu ikashindikana.



"Huwo ndio unaitwa uwoga, najua huna uzoefu na hisia hiyo. Hiyo ni hisia inayokuja kabla ya kifo, akili inataka jambo lakini mwili unagoma kutekeleza" aliongea Fahad na kupiga hatua moja tu. Feris akajikuta akipiga goti moja chini kutokana na mkandamizo alokuwa akipata kutoka kwa mwamba huo.
 
Black Star 2: Astra 35







"Nasema niachie" alifoka Feris (Sakyubi), "kama ingekuwa kila mtu akisema aachiwe basi anaachiwa basi magereza yasingekuwa na watu" aliongea Fahad na kutabasamu bila mkunjo wowote usoni. Akakaza macho na magandamizo ukaongezeka. Feris akaanguka chini na kucheuka damu.



Baada ya kama robo saa, harufu kali sana ya damu ikaanza kusikika ikija upande aliokuwa Fahad na Feris. "Hahaha! Inaonekana hatimae mnyama amepoteza akili" aliongea Feris kwa kujikakamua. Aliinua macho yake juu na kumuangalia Fahad. Alitahamaki kumuona akitabasamu, macho yale yalionekana kama yanayong'aa.



"Nguruma Garaaji, nguruma mpaka sonono ndani ya moyo wako liishe" aliongea kwa nguvu na kuinua mikono juu. Misuli yale ikatanuka na mishipa ya damu ikaanza kuvimba. Ilikuwa ilikitweta kama mapigo ya moyo.



"Grrrrr!" Garaaji alinguruma kwangu na kujipinda, mgongo wake ukachanika na kutoka mbawa ndefu. Pingili zake za uti wa mgongo zikaanza kukuwa na kutoka ncha kwa juu. Mgongo ukawa mithili ya mgongo wa mamba.



"Sakyubi, shuhudia uzao makhsusi wa kiumbe kisichobarikiwa mbinguni wala kuzimu, muungano timilifu kati ya viumbe wawili wenye asili tofauti. Maana kamili upendo usio na mipaka" aliongea Fahad. Mgongo wake mkubwa ukatanuka na kusababisha misuli ya mgongo kujichota vilivyo.



"Gorigo nishikir huyu mwanaharamu, radi inakuja" aliongea Fahad na kupepesa macho. Viini vya macho yake vikabadilika. Cha jicho la kulia kikawa cha kijani na jicho la kushoto likajichora alama ya yin na yang.



Mchoro mkubwa wa ajabu ukajichorq chini yake, "nini?" Macho yalimtoka Sakyubi.



"Usifukute, rafiki yangu anataka kuvunja sheria za miungu wenu" aliongea Gorigo na kumkanyaga Sakyubi. "Trigram nane" aliongea Gorigo na kuonesha kufurahia.



"Shuhudia uzao wa Nemesis "adui mkubwa" wa miungu" aliendelea. Duara hilo likatanuka zaidi na kuzungukwa na nguzo kubwa nane na ghafla radi kali sana ikashuka yenye rangi ya dhahabu na kumtandika Fahad aliekuwa amesimama bila dalili ya uoga.



Sekunde chache baada ya radi hiyo kutua, ikasambaratika, Fahad alikuwa amesimama huku mwili wake ukitoa shoti.



"Hakuna binadamu alieweza kuvuka kwa mkupuo mpaka kufika daraja la Selesti" aliongea Sakubi. "Nani aliekupa ruhusa ya kuongea" alijibu Fahad na kumgeukia. Macho yake yalivyokutana na ya Sakyubi, mwili mzima wa mwanamke huyo ukafa ganzi na hatimae moyo ukasimama, alipoteza uhai.



Sekunde chache baada ya tukio hilo, Garaaji akatua mbele ya Fahad na kupiga. "Umetukuka mfalme Asura" aliongea na kupiga goti kisha akainamisha kichwa.



"Inua kichwa Garaaji na uwe upanga wangu wa kusafiaha njia yangu" aliongea Fahad na kutabasamu.



"Ha! Mwili wangu ni ngao yako na mikono yangu panga zako. Tumia kwa vile unavyojisikia" alijibu na minyoro miwili ya nyota ikajichora katika pembe ya hicho lake la kulia.



"Hapa kazi yetu imekwisha, pakia hiyo mizoga kwenye farasi, waache waende zao. Watafika wanapotakiwa kuifika, mkate kichwa huyo mpuuzi na ukitie kwente sanduki iwe zawadi kwa mpumbavu mwenzie" aliongea Fahad akimuangalia Feris aliekuwa amelala chini mwili wake wa baridi.



*******



Wakati huwo huwo, ulimwengu wa Mythril.



Watu wanne walikuwa wamekaa kwenye meza ya duara wakipata chai ya moto. Walionekana ni wazee sana, japo vilivyoonekana vilikuwa ni vivuli vyao.



"Ohooo, inaonekana nemesis amezaliwa tena" aliongea mmoja na kucheka kidogo.



"Safari hii tutamuua nantutahakikisha hazaliwi tena" mwengine alijibu na kusonya.



"Hata ukikasirika, hakuna njia unaweza mpata kwasasa, tuendelee kusubiri huku. Atafika tu, tumesubiri zaidi ya miaka elfu hamsini. Kusubiri michachr mingine haitakuwa shida, ehehehe" sauti ya bibi kizee.



"Karakantha hatimae umefanikiwa kurithisha kisasi chako" aliongea mwengine aliekuwa amekaa kwenye kiti kikubwa. Alikuwa ndio kiongozi wa kikosi cha watu hao waliokuwepo hapa. "Lakini ni masikitiko makubwa kuona ndoto zako zikishindea kutimia tena" akamalizia.



"Lalalala! Indra hujui nini kinakusubiri, huna hata idea ya nini kitakukuta. Anaekujia sio nemesis tu bali achenemesis, kitisho kikubwa sana kwenu. Japo kuwa nasikitika sitakuwepo kushuhudia ukianguka, ila nitakusubiri katika njia ya baada ya maisha" sauti nzito iliyojaa mikwaruzl ilisikika mbali kidogo na meza hiyo kwenye kivuli kisha ikatoweka kabisa.



"Nyie watatu mtasubiri hapa, mimi narudi Yuggdrasil kwa ajili ya kuendelea na mafunzo" aliongea na Indra na kutoweka.



Lorei.



"Taarifa, taarifa" alifika mtu mmoja nje ya ofisi ya waziri mkuu akihema.



"Kuna nini mbona unapiga kelele asubuhi yote hii" alitoka waziri mkuu akifoka.



"Farasi wa malkia wamerudi lakini...., ni bora uende ukaone mwenyewe" alishindwa kuelezea alichoshuhudia, waziri mkuu na mleta taarifa wakafuatana mpaka katika kiwanja maalum anaposimama farasi wa malkia. Walipokaribia tu, walikaribishwa na harufu kali sana ya uoza.



Watu wengu walikuwa wamekusanyika na minong'ono ya hapa na pale ikasikika. "Malkia ameuwawa" alipiga kelele mmoja kati ya waanagaliaji. Ndani ya sekunde mbili tu mfalme akafika eneo hilo kwa kasi ya umeme.



"Lete hicho kisanduku chekundu" alitoa amri, mlinzi mmoja akakiebeba na kumkabidshi waziri mkuu. Waziri mkuu akatembea mpaka karibu na mfalme na kukifungua. Tetemeko kali sana likatokea, nyumba kadhaa zikaangvunjika.



"Nani aliethubutu kufanya hivi" alinguruma kwa hasira mfalme.



"Bwana wangu kuna karatasi yenye ujumbe" aliongea waziri mkuu. Mfalme akamuangalia kwa macho yaliojaa hasira, alikuwa amekunja ndita. Pia alikuwa amekunja ngumi kiasi cha kucha zake kutobia vifanja vyake. Mishipa ilikuwa imesimama pembeni kwenye kichwa, ilikuwa kama ipumuayo. "Isome" alitoa amri.



"Muda wowote utakaokuwa tayari njoo, niko tayari kwa vita. Nitakupa kifo kibaya kuliko cha huyu mjinga mwenzako. Jina langu ni Fahad na kuanzia sasa mimi ni mfalme wa ngome ya Zinga. Kumgusa mwananchi wangu mmoja tu basi mia wako watalipa kwa damu zao. Narudia tena, ukitaka vita muda wowote nipo tayari usipokuja nitakuja mimi. Na nikija mimi hesabu anguko".



Barua iliishia hapo, na maana ilisomea hadharani waliokuwepo hapo wote waliisikia. "Waziri mkuu, wote walioisikia barua hii lazima wafe" alitoa amri mfalme na kugeuka, akaondoka.



Katika mikono ya waziri mkuu ukatoka moshi mweusi na ulipotoweka wote waliokuwa hapo walikuwa chini wamenyauka kama majani makavu. Akaichoma moto barua hiyo na kuondoka. Akalichoma moto gari la farasi pamoja na farasi wake mpaka kubaki majivu. Hiyo iliyakiwa iwe siri kati yake yeye na mfalme.



Akaelekea katika ukumbi wa mfalme, "nimekamilisha" akatoa taarifa.



"Vizuri, miaka mitatu kutoka sasa tutakwenda vitani na Fahad. Tuma ujumbe wa wazee wote, nataka ndani ya muda huu warudi ngomeni. Kushindwa kufanya hivyo kutahesabika kama usaliti, na sitafungia macho usaliti huo. Nitawauwa kwa mikono yangu miwili" aliongea mfalme.



"Maneno yako ni amri, na amri ni wajibu kutekelezwa".



"Vizuri, ndani ya miaka mitatu nitajifungia kwa ajili ya mafunzo. Sitaki kusumbuliwa, mambo yanayohusiana na utawala yatakuwa chini ya mwanagu wa kwanza" alimalizia na kuhudhuria katika mazingira ya kutatanisha.

 
Black Star 2: Nemesis 36





Miaka mitatu baadae.



"Sena! Baba ako amesharudi", anatoka mtoto wa kike na kujirusha mikononi mwa kipande cha mtu "baba, zawadi yangu iko wapi" aliongea akitabasamu.



"Zawadi yako mara hii nitakupa katika siku yako ya kuzaliwa" aliongea Fahad akimshusha. Sena alipokanyaga tu chini akaondoke.



"Inaonekana na leo pia imeshindikana" aliongea Nephira akimgusa Fahad shavuni.



"Ndio ila naamini ipo siku nitafanikiwa" alijibu akishudha pumzi.



"Kama kuna jambo linakutatiza, nishirikishe huenda nikawa na msaada".



"Unajua nahisi kabisa nakaribia kufanikiwa lakoni wakati huwo huwo nahisi kuna jambo linapungua. Tatizo ni kwamba hilo jambo lenyewe silijui" aliongea Fahad kwa sauti ya kukereka.



"Unajua kipindi hiki umekuwa ukiwasaidia wanafunzi wako waliochelewa kuvuka madaraja, nahisi una upungufu Qi mwilini mwako. Wewe mwenyewe unafahamu kabisa kutoka daraja ulilokuwa sasa kuingia katika daraja la milele unahitajika uwe na Qi isiopungua ujazo wa miaka karibi elfu moja. Kwa kukuangalia tu sasa hivi, Qi yako haifiki hata nusu ya namba hiyo niliyoitaja" aliongea Nephira.



"Najua hilo lakini sidhani kama hilo, nahisi kuna kitu nahitaji ili kukamilisha lakini hakipo katika mawazo yangu. Ah! Achana na mambo ya kusononesha, ukifika muda nitajua" aliongea na kumbusu mkewe shavuni na kuingia ndani.



Baadae, katika kiwanja cha mafunzo.



"Bado wangapi kufika daraja la tong san" alifika Fahad na kuuliza.



"Hamsini na moja tu" alijibu Fang Shi akitoa ishara ya heshima,.



"Kati ya hao wangapai wanaonekana kuwa angalau afadhali"



"Kumi tu, wengine hawana hata dalili"



"Hao kumi endelea nao, waliobaki nikusanyie nataka nionane nao tena, inawezekana aina ya martial arts walizochagua baada ya kufika Jin dan hazioani vizuri na matakwa yao". Fang Shi akaikpokea amri hiyo na kuondoka, baada ya dakika kama saba hivi watu arobaini na moja wakakusanyika mbele ya Fahad. Wote walionekana kukaribia kukata tamaa.



"Musiwe na sura hizo, ugumu kama huu hutokea sana katika mafunzo. Inawezekana tatizo si wewe bali ni aina ya martial uliochagua haiendani na mwili wako. Nitafanya ukaguzi wahara, kila mtu atoe Qi yake kwa wingi" aliongea Fahad.



Wote wakafanya hivyo akawaangalia kwa makini, akahisi kama kitu katika moyo wake. Alihisi kuna aina ya nguvu katika mwili wake ikioana vizuri zaidi na Qi za watu hao.



"Inatosha" akatoa amri na kila mmoja akaacha kufanya hivyo. Walionesha kuwa na wasiwasi sana kwasababu walilifahami jicho la busara la Fahad liliweza kuona yale wao walioyaficha.



"Nasikitika kuwa hamtaweza kuendelea kujifunza" aliongea Fahad na kuwaangalia, kila mmoja akainamisha kichwa. "Mbona sura zimekuwa hivyo, sijamaliza nilichokusudia kuwaambia" aliongea na matumaini yakaonekana katika nyuso zao.



"Nyinyi mna uwezo wa kujifunza Dark Martial art, martial arts ambazo zimebebea zaidi katika uchunguza na ukusanyaji taarifa. Kawaida hizi huwa hazifundishwi kabisa kutokana na kumfanya mtu kuwa muuaji wa baridi. Katika kuchunguza unaweza ukakutana na watu ambao itakubidi uchukue uhai wao ili kulinda kazi yako. Kwa maneno mingine, nyinyi mnaweza kuwa mfumo wangu wa taarifa katika ulimwengu huu. Kila taarifa ni muhimu na wala haijalishi kuwa ni ndogo kiasi gani" alifafanua.



Mpaka wakati huwo karibia wote walikuwa katika bumbuwazi, vinywa vikiwa chini. "Nitawafundisha aina ambayo itawawezesha kukusanya taarifa kwa wepesi zaidi. Aina ambayo itawafanya muweze kuficha Qi zenu na kuweza kujichanganya na watu wengine kama watu wa kawaida. Pia itawawezesha kufanya mavamizi ya siri hata katika ngome zenye ulinzi mkali sana" aliendelea.



"Mimi ni miongoni mwa ambao sijaelewa, lakini katika mikono yako naamini hakuna la kunipa wasiwasi. Naomba muongozo wako" alipita mmoja mbele na kuongea.



"Safi sana, jina lako ni nani"



"Zola ndio jina langu" alijibu.



"Zola unaonekana una kipaji sana na hiyo ni sifa moja ya mtu anaetakiwa kuvamiwa na kuiba siri 'maamuzi'. Maamuzi ni kitu cha muhimu sana kwa mpelelezi. Maamuzi yako ndio yatakayokufanya utoke na uhai wako au mauti yakuchukue. Wepesi wa kufanya maamuzi mapema katika kila aina ya hali ni karata ya ushindi kwa wale wote wanaoganya kazi gizani au mbele ya macho ya watu pasi na kuonekana" aliongea Fahad.



Akaendelea "Zola wewe utakuwa kiongozi wa kikosi cha kwanza, wakati tukiendelea na mafunzo nitakuwa machagua viongozi wengine. Vikosi vitakuwa saba tu na kila kikosi kitakuwa na watu wasiozidi saba akiwepo na kiongozi wao isipokuwa kikosi kimoja tu, hicho kitakuwa na watu sita.".



Baada ya maelezo hayo akawaamuru wote wajipange, akapita kwa mmoja mmoja na kumugusa katika paji la uso mpaka wote wakaisha. "Kila mmoja amepokea zawadi niliyompa, na hazifanani. Kila mtu hapa atajifunza martial art aina yake. Haitachukuwa muda mrefu kwa nyinyi kufika daraja la tong san. Endeleeni kujifunza kwa mazingatio. Nitarudi baada ya wiki mbili kuwaona" alimaliza kuongea na kuondoka.



Kila mmoja akatafuta kipembe chake na kuanza kujifunza kile alichokipokea kutoka kwa Fahad.



********



Msitu wa wachawi.



Watu wengi walikuwa wamjipanga pembeni ya njia ambayo ilikuwa inaelekea kwenye mti mnene na mkubwa. Mwanga mkali ukatokea na ulipotoweka, mbele yao alikuwa amesimama Fahad, Nephira na mtoto wao mdogo wa kike Sena.



"Karibu nyumbani mlezi" watu wote waliokuwa hapo wakisubiri wakaongea kwa pamoja. Fahad akatabasamu na kuonamisha kichwa kama sehemu ya kuipokea salamu hiyo ya heshima. Kwa mwendo wakatembea kuelekea ulipo mti huwo ambapo Magdalena alikiwa amesimama akiwasubiri. "Karibu" aliongea.



"Nimekaribia" alojibu Fahad na kuinamisha kichwa,



"Bibiiii! Sene akajitoa mikononi mwa mamake na kumkimbialia Magdalena."Umekuwa mkubwa mjukuu wangu" aliongea na kumbeba na kumkumbatia.



"Natumai maandalizi yote yako tayari" aliongea Nephira.



"Ndio, sherehe kukabidhi utawala imeandaliwa. Na muda si mrefu watafika wazee kwa ajili ya kubariki na sala ya kuomba mti mtukufu itapita. Kwanza atakabidhiwa jani ambalo ndio litakuwa kitabu chake cha manuizi. Baada ya hapo ndio itafuata makabidhiano" aliongea Magdalena akimshusha Sena chini.



Wakati Sena anageuka kuelekea kwa wazazi wake, Fahad akachomoka kwa kasi kubwa sana na kumzunguka mwanae. Ndani ya sekunde chache hakuna aliejua nini lakini mkononi mwa Fahad matokeo na mshale alioudaka huku ncha ya mshale ikiwa imegusa kidogo ngozi ya koo ya Sena. Tone la damu lilionekana kwa mbali.



Ikasikika sauti ya kicheko "hahaha! Wajinga sana nyinyi, nilijua tu kama mama hukuwa tayari kunipa umalikia". Ilikuwa na ya mwanamke akiwa anaelea angani.



"Janima, nani aliekuruhusu kuingia ndani ya msitu huu" aliongea Magdalena.



"Kuna mtu anahitaji ruhusa ya kuingia nyumbani kwake" alijibu kwa kejeli. Mwili wake ulikuwa umezungukwa na guo zote lenye kutoa moshi mweusi. "Na sikutegemea kama huyo mpuuzi unaemuita mume kuwa na kipaji kiasi hicho" akaendelea akimuangalia Fahad.



"Katika maisha yako yote umefanya kosa moja kubwa sana, nalo ni kugusa kilicho changu" aliongea Fahad akipumua kwa nguvu kabla ya hali ya hewa kuwa tulivu. Kwa sekunde chache kila kitu kiliacha kutikisika, mpaka upepo uliacha kuvuma. Alipoinua uso wake, viini vya macho yake vilikuwa na umbile la nyota.

 
Black Star 2: Nemesis 37







Viini hivyo havikuwa na umbile la nyota ya kawaida, ilikuwa ni nyota ya pembe sita. Fahad akakutanusha viganya vyake na kwa kasi vidole vya kiganja cha mkono wa kulia vikaangalia chini na kufanya viganja hivyo vigusane katika matumbo yake.



Akakunja kidole cha kidogo cha mwisho na cha pete na kubakisha vitatu vikiwa vimenyooka. Kila msuli katika mwili wake ulitutumka na kupumua. Sena alikuwa nyuma akiushangaa mgongo wa babaake ulianza kujichochora katika mavazi yake takatifu.



Wakati hayo yakiendelea, Nephira alikuwa ametoa macho tu. "Usimuache akapotea" alizinduliwa na sauti lakini sauti hiyo aliisikia kutokea ndani ya kichwa chake. "Ulichelewa zaidi atamaliza kufungua meridian zake zote, kifo cha dadaako ndio kitakachofuata" sauti hiyo iliendelea kuongea.



"Wewe ni nani" aliuliza Nephira ila ghafla akajikuta akiwa sehemu nyingine kabisa. Alikuwa juu ya kilele cha mlima, na kulikuwa na baridi sana. Baridi ambayo haikuwa ya asili kabisa hasa ukizingatia kilele hicho kilikuwa kikavu kama jangwa.



Mbele ya macho yake alikuwa amesimama mwanamke mwengine, na hapo ndio akagundua kuwa baridi hiyo ilikuwa ikitoka katika mwili wa mwanamke huyo.



"Nephira, kama unampenda bwana wetu. Mpoze kwa kumgusa begani tu, Fahad ana udhaifu mkubwa sana linapokuja suala la kuumiziwa familia yake. Muda huu anachowaza kuuwa tu" aliongea mwanamke huyo.



Nephira akazinduka na kujikuta akiwa alipokuwa mwanzo, akatembea kwa kasi na kumgusa Fahad begani. "Punguza jazba" akamnong'oneza sikioni. Fahad akazinduka na kutabasamu, "ahsante, niko sawa" alijibu.



Wuush! Akachomoka kwa kasi na kutokea nyuma ya Janima, akampiga kwa kutumia kiganja chake karibu na kiungo. Bang! Janima alitupwa na kujigonga katika jiwe, akacheuka damu na kupoteza fahamu.



Fahad akatuwa alipoa Sena na kumuangalia shingoni sehemu ambayo mshale ulikuwa umegusa. Alishangaa kutoona hata kidonda eneo hilo, muda wote Sena alikuwa ametoa macho huku akiwa ametabasamu. Mchoro wenye alama ya mtu wenye matawi matatu ukatokea katika paji lake la uso.



"Stigma" aliongea Magdalena kwa nguvu na kupiga magoti huku machozi yakimtoka. "Wote pigenu magoti, malkia mpya amechaguliwa na mti wa enzi" aliongea kwa nguvu na wote waliokuwa hapo wakatii na kufanya hivyo kasoro Fahad na Nephira tu.



"Stigma ndio nini?" Aliuliza Fahad.



"Stigma ni alama aliyokuwa nayo malkia wa kwanza kabisa na muanzilishi wa msitu huu" alianza kuelezea Nephira.



******



Miaka mingi sana hapa kulikuwa jangwa tu, hakukuwa na dalili yeyote ya maisha. Ilikuwa ni sehemu iliyojaa mifupa ya watu, wengi walifika hapa na kusubiri safari yao ya mwisho. Mara moja akafika mtoto mdogo wa kike, alikuwa dhoofu sana. Na yeye kama wengine alifika hapa kwa ajili ya kusubiri safari yake ya mwisho. "Ardhi ya wafu" ndio jina la asili la eneo hili.



Akiwa katika kusubiri alikuwa ni maji kidogo ambayo ndio yalikuwa chakula chake. Kiu kali ilikuwa imemshika na alipotaka kunywa, mbele yake akamuona mtu mzima akiwa anahaha na kiu. Japo yeye alikuwa na kiu lakini allijikongoja mpaka alipo bibi huyo na kumywesha maji hayo kidogo yaliobaki.



"Mjukuu wangu kwanini unanipa maji mimi wakati wewe midomo imekupasuka" aliuliza yule bibi akimuangalia yule biniti.



"Najua kama una muda mrefu hujatia kitu mdomoni mwako na safari yako imefika. Nikaona ukipata haya maji utaenda hali ya kuwa unakumbuka ladha ya kitu cha mwisho ulichokipata" aliongea na kutabasamu.



Sekunde chache tu yule bibi akatangulia, yule binti akamfunga macho. "Ukifika huko waambie kwamba wametusaliti sisi tuwaombao na ni matumaini yangu utaishi katika bustani ya kijani yenye uhai wa kutosha" aliongea huku machozi yakimtoka.



Inasemekana muda mchache tu baada ya maneno yake hayo ikaanguka mbegu kutoka angani. Ilipotoka wala asili yake haijulikani. Katika vitabu wameandika kuwa mbegu hiyo ilikuwa ni chozi la mungu wa uponyaji. Ilipogusa tu ardhi ikazama na baada ya sekunde chache mche ukachomoza.



Akasikia sauti ikitokea katika mche huwo, "nioshe kqa chozi lako na mimi nitakupa kile moyo wako unataka". Akauinamia na chozi likadondoka katika mti huwo. Ghafla mti huwo ukaanza kukuwa na ulipofika ukubwa wa mita moja, majani yakaanza kuota kuuzunguka.



"Binti sogea karibu" alisikia tena sauti kutoka katika huwo, nae akafanya hivyo. Alama ya mti wenye matawi matatu ukatokea katika paji lake la uso.



"Nitakupa msitu wenye matunda, hutakaa uijue njaa tena. Malipo yako yatakuwa ni kazi ya uponyazi, utakuwa tabibu wa miujiza. Mkono wako utamponya kila utakae mgusa. Kuwa malkia wa msitu huu na unilinde, ugonjwa hautaingia niwapo mimi".



Historia imeandika kuwa walioshuhudia hilo wote walipona na miili yao ikajaa afya. Walieleza kuwa mungu alikuwa ameshuka na kuwabariki uhai.



Malkia wa kwanza, japo hakuna aliejua jina lake ila wengi walimtambua kama tabibu mtakatifu. Ndani ya siku moja tu, msitu mkubwa ukaota na miti yake ikazaa matunda mengi na ya aina mbali mbali.



Taarifa za maajavu hayo zikasambaa maeneo mbali mbali, vibaka, majambazi na wenye uwezo na majina makubwa akajaribu kuuvamia lakini hakuna aliepona na hatimae ukapata jina la "MSITU WA WACHAWI" na baada ya miezi kadhaa malkia akatangaza msitu huu kuwa ni taifa huru lisilo naafungamano na mtu yeyote yule.



Historia ilimuandika malkia huyu kama mwenye huruma na utu wa hali ya juu. Kwasababu baada ya muda alianza kufundisha wengine jinsi ya kutoa tiba kwa kutumia njua zisizo za kawaida.



Aliishi kwa miaka mingi kifo kwake kilikuwa ni ndoto isiyotimia. Kwasababu alikuwa huru kutokana na kila aina ya ugonjwa. Mwili wake mtakatifu haukuweza kuathirika hata na sumu yeyote ile. Hakuna aliejua kuwa ameishi miaka mingapi ila siku moja watu waliamka na kujikuta na simaniza.



Chini ya mtitukufu na jani kubwa lililoandikwa, "muda wangu umefika, malkia wa pili atachaguliwa na mti wetu mtukufu. Ila nawaahidi nitazaliwa tena, nikifika miaka jani lenye nyekundu litaanguka kutoka mti huu. Jani hilo litakuwa na jina na jina hilo ndio jina langu la sasa na ndio litakuwa jina langu nitalopewa baada ya kuzaliwa. Ni matumaini yangu mutaulinda mti huu badala yangu, Malkia".



Tokea hapo kila malkia alikuwa na kazi moja tu nayo ni kuulinda mti huu kwa maisha yake akisubiria ujio wa malkia wa kwanza.



**********



Nephira alimaliza kumsimulia Fahad na pumzi. Na wakati huo huo jani lenye rangi nyekundu likadondika kutoka katika kilele cha mti huo. Lilianguka mbele Magdalena. Kwa hofu kubwa akaliokota na kuligeuza ili asome kilichoandikwa.



Mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda mbio, walio karibu yake walimuangalia wakitegemea awaambie alichokiona.



"Ahadi imetimia, niliahidi nitarudi kwa kuzaliwa tena" alisoma kwa nguvu.



"Tutajiw jina la malkia wetu wa kwanza" wengi wakaongea.



Akarudisha macho katika jani hilo "Jina langu ni Sena" alisoma kwa nguvu.

 
Black Star 2: Nemesis 38





*******



"Ondokeni, mimi nitawazuia hapa" aliongea mtu mmoja aliokuwa na upinde mkubwa wa chuma mgongoni. Na mkononi alikuwa na upinde mwengine mdogo wa mbao ngumu. Katika paja la mguu wa kulia alikuwa alikuwa amefunga podo ndogo yenye mishare mingi.



"Mkuu lakini mwili wako unakaribia kufika uwezo wa mwisho kuvumilia" aliongea mmoja kati ya watu wake. "Usalama wa huyo mtoto ni muhimu sana kuliko kitu chochote kwa wakati huu. Ni lazima afike msitu wa wachawi" aliongea akitoa mishale mitatu, akaiweka kwenye upinde na kuivuta kabla ya kuiachia.



"Tutafanya kama unavyotaka, na tutakusubiri msitu wa wachawi" aliongea mwanamke na kushika mkono mtoto mdogo wa kiume. Wakageuka na kuanza kukimbia, "afadhali, sasa hata nikifa nitakufa hali ya kuwa nikifahamu kazi niliyopewa imekamilika" aliongea na kutoa mishale, akaendelea kufanya mashambulizi.



Nusu siku imekatika, nje ya lango kuu la kuingia msitu wa wachawi. "Tafadhali tunaomba kuonana na malikia, ni muhimu sana" aliongea mwanamke aliekuwa na mtoto mdogo. Alikuwa na majeraha kadhaa mwili mwake.



"Samahani hatuwezi kufanya hivyo, sherehe ya kumuapisha malkia inaendelea. Na tumepewa amri ya kutoruhusu mtu kuingia ndani" aliongea mlinzi aliekuwa langoni hapo.



"Kama hamuwezi kuniruhusu mimi, mpelekeni huyu mtoto tu mbele ya malkia. Ataelewa nini maana ya huyu kuwa mbele yake" aliongea akimsukua mtoto mbele.



Wakati wakiendelea kuzozana, akafika mlinzi mwengine ambar alionekana kuwa kiongozi wa watu hao. "Kuna nini?" Aliuliza.



"Huyu mwanamke amesema anahitaji kuonana na malkia" alijibu mlinzi mmoja kati ya waliokuwa zamu.



"Sawa mimi nitampeleka, hakuna haja ya kuendelea kuzozana" akaongea na kumpa ishara ya kufata. Yule mwanamke akambeba yule mtoto na kumfata yule mlinzi.



Alitembea kwa mwendo wa wastani na kuomba niia mpaka mbele ambako ndiko malkia mpya alikuwa akikabidhiwa taji.



"Malkia, huyu mwanamke amesema anahitaji kukuona" aliongea yule mlinzi na kusogea pembeni. Magdalena akageuka kumuangalia huyo alieletwa lakini hakumtambua. Alipotaka kuongea akashikwa mkono na Sena, "muache aje mbele yangu, namjua".



Kila mtu akapigwa na butwaa, inakuaje mtoto wa miaka mitatu anamjua mtu ambae ni mgeni mbele ya macho ya watu wote.



"Yuko wapi mrithi wa upinde wa Asura" aliongea Sena, Fahad akamuangalia mwanae kwa macho ya mshangao.



"Hivi sasa yuko peke yake anawazuia waliokuwa wanatufukuza" alijibu yule mwanamke aliekuja na mtoto.



Sena akamuangalia baba ake usoni, "huhitaji kusema zaidi" aliongea Fahad na kutabasamu.



"Sikujui... koh koh... wewe ni nani lakini naomba umsaidie Oberoi" aliongea yule wa kiume akijitoa mikononi mwa yule mwanamke na kupiga magoti. Aliongea kwa tabu, alionekana kuwa na maumivu sana.



"Natumai nitapata majibu nitakapo rudi" aliongea Fahad na kuanza kuondoka.



"Gorigo, wewe utabaki hapa kuhakikisha usalama"



Ndege mkubwa akatokea ghafla na kupaaa angani kwa kasi ya ajabu sana kiasi cha kutoonekana na jicho la kawaida.



Wakati wote wakishangaa kiumbe kilichopaa, waliporudisha macho yao chini Fahad hakuwepo tena.



**********



Oberoi anajiegemeza kwenye jiwe kubwa pembeni yake, alikuwa akihema sana. Damu zilikuwa zikimtoka maeneo kadhaa ya mwili wake, alijitahidi sana asifumbe macho maana aliamini kufanya hivyo ndio ingekuwa usingizi wa moja kwa moja usio na mwisho.



Akatupa upinde wake mdogo na kutoa upinde mkubwa wa chuma alouvaa mgongoni. Akapapasa katika paja lake la kushoto na kuchomoa mshale mkubwa wa chuma na kuukita chini.



"Ikiwa nitautumia huu, leo ndio itakuwa siku yangu ya mwisho kuutumia. Bahati mbaya iliyoje hii" alijisemea na kutokwa na machozi. Akakusanya nguvu zake zote na kusimama kabla ya kuuchomoa ule mshale na kuuweka katika upinde.



"Kuna mtu ameyapa thamani kubwa sana maisha yako na anakutaka uendelee kuwa hai" mkono wenye joto ukamshika begani. Kwa sekunde kadhaa alihisi kama kainamiwa na jinamizii. Akameza funda kubwa la mate kabla ya kugeuka kumuangalia aliegusa.



Macho yakatua usoni mwa kipande cha mtu kilichokuwa kinatabasamu. Alihisi mapigo yake ya moyo yakisimama, miguu yake ikamsaliti na kuanza kuttetemeka.



"Tulia na upunguze hofu, niko hapa kukupa msaada" aliongea Fahad na kumfanya Oberoi atulie kwanza maana alikuwa anaelekea kupoteza fahamu.



"Naona misuli yako ya mikono yote imechanika, ukipiga huwo mshale wa mwisho mifupa yote katika mikono yako miwili itavunjika kufikia kiwango cha kutorekebishika tena".



Akashusha pumzi na kuendelea "nipe huwo upinde" kwa sauti ya kuamrisha. Oberoi mpaka wakati alifahamu kabisa kupambana na mtu huyo aliefika isingekuwa jambo la busara kwake. Hata angekuwa katika hali ya unondo kabisa basi uwezekano wa kushinda ulikuwa ni asilimia sifuri.



Akameza funda jingine kubwa la mate kabla ya kumkabidhi Fahad upinde. Akaupokea na kuutikisa tikisa kidogo, akatabasamu na kuutoa mshale. Akamrudishia Oberoi kisha akaongea "sina haja na huwo mshale".



"Lakini bila mshale utapiga nini?" Alama ya mshangao na kuuliza zilijichora machoni mwa Oberoi.



"Hahaha, inaonekana kuna mpuuzi mmoja amebadilisha maelekezo ya kutumia hii silaha" aliongea Fahad kana kwamba alikuwa akiijua silaha hiyo. Wakati huwo kichwani mwa Fahad taaluma na makala jinsi ya kuitumia silaha hiyo zilikuwa zikimiminika.



"Kitu kimoja naweza sema, wewe jamaa una akili sana. Kuja kwako hapa ulikuwa unatega wanaokufukuza wapite kwenye lile korongo pale uwamalize wote kwa shambulizi moja tu" alionhea Fahad akitazama eneo ambalo kulikuwa na milima miwili mikubwa iliotengeza njia nyembamba katikati.



Tayari vivuli vya watu wakiwa juu ya farasi vilianza kuonekana, walikuwa wengi na kwa makadirio hawakuwa chini ya mia.



Fahad akaunyanyua ule upinde na kuuzungusha kwa nguvu. Akaushika utari uliokuwa umefungwa kati ya sehemu mbili za mwisho za upinde huo.



"Ni muda mrefu sana ulikuwa umelala" alisema akiuangalia upinde huo.



"Ni kwa mamlaka niliyonayo, na kwa jina lako ninalolifahamu nakuamuru wewe ulielala kwa muda mrefu uamke na utekeleze kazi yangu. Amka Kaldiriyus" alinena maneno hayo na kuuvuta utari.



Mbele ya upinde vikafunguka vitundu viwili na kuwa kama macho. Fahad kuuvuta utari huku misuki yake mikubwa ikimuka na imani ya damu kuonekana ikitweta na kupelekea mwili huo kung'ara.



Mgongo wake utanuka na kuwa kama mbawa za kipepeo mkubwa. Mkono wake wa kushoto uliokuwa umeshika sehemu ya kati ya upinde ukakaza, akafungua kidole cha shahada. Upepo mkali sana ukaanza kuvuma na kujikusanya kwenye kidole hicho. Baada ya sekunde kadhaa, kichwa cha mshale kikaichora.



"Oberoi, huu upinde haukutengezwa kutumia mshale unaonekana au kutengezwa kutoka katika vitu vya asili. Bali ulitengezwa kwaajili ya kutumia Qi na upepo kutengeza mshale ambao mtumiajia anaona unamfaa zaidi" aliongea Fahad na kuzidisha ufundishaji. Taratibu akaanza kutiririsha Qi yake kuelekea katika upinde huo.



Ghafla ukatokea mshale uliotengezwa kwa upepo na kuzungukwa na Qi. Upepo ndani ya mshale huwo ulikuwa ukizunguka kwa kasi kiasi kwamba jicho la kawaida lingeona ni kama mshale wa chuma. Fahad akakaza meno na pumzi nyingi sana kisha akaachia utari.

 
Black Star 2: Nemesis 39

"Kaldiriyus, nguruma" aliongea baada ya kuuachia, kwa nusu sekunde ni kama kila kitu kilikuwa kimesimama. Oberoi hakuamini kabisa macho yake, kasi ya mshale uliotoka kwenye upinde huwo haikuwa ya kawaida.



"Usipepese macho angalia kinachokwenda kutokea" aliongea Fahad. Oberoi akageuka na kuangalia kilichoachiwa kutoka kwenye upinde wake. Macho ya yakakutana na ndege mkubwa aliekuwa anasafiri kwa kasi.



"Kaldiryus, ni ndege wa enzi na enzi. Alikuwa miongoni mwa wanyama waliofika daraja la juu zaidi. Lakini alisalitiwa na wale aliowaamini na kuwapa msaada kila walipohitaji. Nao ni binadamu, waliamua kumuwinda baada ya kupata taarifa kuwa yeyote atakaekula moyo wake ataweza kupasua anga na kuwa na nguvu zaidi. Wana martial art wengi walikusanyika kuhakikisha wanatekeleza hilo".



"Mwanzo Kaldiriyus alipambana sana lakini kadiri muda ulivyokwenda ndivyo watu walivyoongezeka na baada ya vita ya zaidi ya miaka kumi hatimae akachoka. Hata hivyo hakutaka kufia mikononi mwa watu aliyokuwa anawasaidia".



"Hivyo akapaa juu kuliko siku yeyote ile na baadae akaanza kushuka kwa kasi mbawa zake akiwa kazifunga. Walioshuhudia walisema kwamba alikuwa akisafiri na upepo na baada dakika chache akatoweka ndani ya upepo. Baada ya kuweka nyuma yake likafuata jiwe kubwa na lilipotuwa ardhi lilichimba na kupotelea katika kina kikubwa cha ardhi. Ambacho hawakukijua ni kwamba, jiwe lile ndio lilikuwa makazi yake ya mwisho".



Aliongea Fahad akimrudishia Oberoi Oberoi upinde wake kisha akageuka "tuondoke kazi imekwisha". Baada ya kali hiyo ile milima miwili ikasambaratika na kuwa tambarare kabisa. Hakukuwa hata na alama kama eneo hilo kulisimama miwili mikubwa sana.



"Umewezaje kuutumia bila kuumia" aliuoiza Oberoi.



"Nitakueleza tukifika kwa sasa tumia damu yako kuupaka sehemu ya kushikia. Kwa kufanya hivyo utaweza kuhisi roho ya Kaldiriyus katika huwo upinde"



Oberoi alikuwa akisikiliza kwa makini, akagusa sehemu aliokuwa anatoka damu na kufanya kama alivyoelekezwa. Hakuhisi kitu, akajaribu tena 'kimya'. Hakukuwa na jibu lolote.



"Chana kiganja chako sio kupaka" aliongea Fahad, bila kugeuka. Oberoi akatoa kisu kidogo na kukata kiganja sehemu katika kiganja chake kisha akaushuka upinde.



"Binadamu unataka kuingia mkataba na mimi" alisikia saiti kichwani mwake na ghafla akajikuta amesimama mbele ya ndege mkubwa mwenye rangi ya kijivu.



"Leo siko hapa kuingua mkataba, nilitaka nikuone tu. Nimekuwa na wewe tokea nilivyokuwa mtoto. Ila mara zote nilizotumia upinde nilihisi majonzi" alijibu Oberoi. Akasogea mpaka pembeni kabisa ya ndege huyo na kugusa bawa likilokuwa limelala chini.



"Sitakulazimisha kuingia mkataba na mimi" aliongea, mara akazinduka baada ya kuguswa.



"Tumefika" aliongea Fahad na kumuangalia Oberoi, bila kutegemea akajikuta akitabasamu. Oberoi hakujuwa kwanini Fahad anatabasamu ila hakutaka kuuliza. Wakaingia ndani, "Oberoi" yule mtoto mdogo akafika na kumkumbatia.



"Nisamehe kwa kuwa katika isiyokupendeza machoni mwako" aliongea Oberoi. Mwili wake ulionekana kuwa na maumivu makali sana yaliyotokana na vidonda vingi.



Sena akatembea mpaka alipokuwa Oberoi na kumgusa, ghafla maumivu yakapotea na vidonda vyote vikapona na misuli ya mikono yote iliyokuwa imechanika nayo ikapona pia.



"Ahsante kwa kuhakikisha usalama wake, umetimiza jukumu lako na kwa kusema hivyo namaanisha kuanzia sasa huna ulazima wa kukaa nae tena. Unaweza kuchagua kufanya chochote" aliongea Sena.



"Kwa mamlaka nilionayo, naondoa vikwazo na kufuli zote zilizo katika mwili na kutamka jina lako, amka Rolia" aliongea Sena huku macho yake yote mawili yakiwa yanang'aa rangi ya kijani.



Papo hapo yule mtoto wa kiume akazungukwa na mwanga mwekundu, mwanga huwo ulipopotea likabakia tunda kubwa. Wakati wakishangaa, mwili wa sena nao ukazungukwa na mwanga wa kijani na ulipopotea kukabakia tunda kubwa la kijani.



Matunda hayo mawili yakaanza kuelea na kuelekea katika kilelel cha mti huwo na kujibadika katika tawi kubwa.



"Wataamka muda ukifika, kwasasa nawaacha chini ya uangalizi wako" aliongea Fahad na kumuangalia Magdalena. Mwanamke huyo akatikisa kichwa kama ishara ya kuelewa.



"Nephira, tuondoke" aliongea Fahad na kugeuka, "mwalimu naomba kuungana na wewe" sauti ya Oberoi ilisikika. Fahad akageuka na kumkuta akiwa kapiga magoti.



"Oberoi njia yangu mimi ni njia ya vita na damu, ukiamua kunifuata lazima ujiandae katuja mambo hayo mawili" aliongea Fahad.



"Katika huu ulimwengu ni wewe pekee mwenye uwezo wa kunifundisha na nina amini kabisa nikiwa upande wako nitafika katika kilele ambacho sijawahi na wala sitawahi kufika katika maisha yangu" aliongea Oberoi.



"Oberoi, hutaki kumtumika mtukufu Rolia tena" yule mwanamke ambae alikuja na Rolia aliongea.



"Nina imani baada ya leo huduma yangu haitahitajika tena" aliongea Oberoi bila kusita. "Oh! Sawa, mi nikutakiw maisha mema na ahsante kwa msaada wako katika kipindi chote hiki" aliongea yule mwanameke kuinamisha kichwa.



"Oberoi karibu katika familia yangu" aliongea Fahad na kugeuka mbele, taratibu akaanza kuondoka. Nyuma yake akafuata Nephira na Oberoi aliekuwa amevaa upinde mkubwa wa chuma.



Zinga.



Katika uwanja mkubwa, mwanga mkali sana ukawaka na baada ya mwanga huwo kupotea wakaonekana watu watatu. Watu hawakuwa wengine isipokuwa Fahad, Nephira na Oberoi.



"Karibu nyumbani Meya" mtu wa kwanza kufika na kutoa salamu akawa Garaaji. Sekunde chache akafika na Fang Shi pamoja Rahee



"Ahsanteni, naona Fang Shi na Rahee mumefika daraja la KyoDan" aliongea na kutabasamu.



"Ni kwa maelekezo tu, leo tumefika hapa" wote wawili wakajibu na kuinamisha vichwa.



"Mukijitahidi sana ndani ya miaka miwili mtafika daraja la uzima na kifo" aliongea Fahad na kuachia tabasamu kubwa sana.



"Tupe muongozo" wote watatu wakajibu kwa pamoja hayo yote yalitokea wakati Oberoi akishuhudia. Alijua kabisa kuwa Fahad hakuwa mtu wa kawaida lakini hakutegemea kama chini kungekuwa na wana martial art ambo walikuwa na uwezo mkubwa. Katika akili yake maneno mawili tu ndio yalitoa tafsiri ya kikundi hicho "viumbe wa ajabu".



"Oh! Kabla sijasikiliza chochote naomba niwatambue kwenu komredi mwengine, Oberoi mtaalamu wa upinde" aliongea Fahad akionesha kiganja chake upande ambao Oberoi alikuwa amesimama.



"Nitawasumbua kwa kuhitaji maelezo kutoka kwenu" aliongea Oberoi na kukutanisha ngumi na kiganja kisha akainamisha kichwa.



"Karibu katika familia" wote wakaongea kwa pamoja na kufanya kama alivyofanya Oberoi.



"Rahee, mpeleke Oberoi akaugane na wengine" alitoa amri Fahad na kumgeukia Oberoi. "Kuanzia leo mpaka utakapofikisha daraja la KyoDan, mafunzoni".



"Nashukuru mwalimu" aliongea na kutoa ishara ya heshima.



"Na baada ya muda nitaazima silaha yako" alimalizia na kurudisha mikono yake nyuma kabla ya kugeuka na kuondoka.



Nyuma yake akafuata Nephira, Garaaji na Fang Shi, wakaelekea katika jengo la meya kwa ajili ya kutoa taarifa.



"Siku moja atakuwa mfalme wa wafalme, mtu mwenye nguvu zaidi katika limwengu zote" aliongea Rahee wakati wakielekea katika eneo la mazoezi. "Mpaka sasa sijaona mtu au kiumbe mwente nguvu zaidi yake".



"Bado hujaona kitu, yeye ni kama mlima usioonekana kilele au kitu kisichoonekana na mwisho" aliongea Rahee na kutabasamu.

 
Black Star 2: Nemesis 40





Ndani ya ofisi ya meya.



Baada ya kuingia ndani ya ofisi hiyo, Fahad akasimama mbele ya dirisha. Kivuli chake hakikufanana kabisa na umbile lake.



"Rondelif" aliita na kuwashangaza wote waliokuwa ndani humo. Maana kati yao hakukuwa na mtu mwenye jina hilo.



"Master" sauti ilisikika kisha kutoka kwenye kivuli chake akaanza kuonekana mtu mtu akiinuka. Nephira, Fang Shi na Garaaji wakarudi nyuma huku kila mtu akijiweka tayari kwa ajili ya kupambana.



"Tulieni" ilitoka amri kwa Fahad, baada ya muda yule mtu akaonekana kabisa. Alisimama pembeni ya Fahad. Alikuwa ndani ya mavazi meusi kuanzia kichwani mpaka miguuni. Hakuna hata sehemu moja ilioonekana zaidi ya macho.



"Huyu ni Rondelif na ni jenerali wa saba" aliongea Fahad.



"Wengine ni kina nani?" Aliuliza Nephira kwa mshangao.



"Jenerali wa kwanza hamumjui, anaitwa Fu Shu mtaalamu wa kutumia mkuki. Pia anajulikana kama mkuki wa radi wa Behemoth. Jenerali wa pili ni Rahee, mtaalamu wa mkono wa karibu. Pia anajulikana ngumi ya chuma ya Asura. Jenerali wa tatu ni Nephira, mtaalamu wa tiba pia anajulikana mikono ya uponyaji" akanyamaza kidogo na kuwaangalia kabla ya kuendelea.



"Jenerali wa nne ni Fang Shi, mtaalamu wa upanga mmoja pia anajulikana kama upanga wa moto wa phonix. Jenerali wa tano ni Garaaji, mtaalamu na kudhibiti wanyama wa kiroho pia anajulikana kama mfalme wa kuzimu Veremin na wa sita ni Oberoi mtaalamu wa kutumia upinde pia anajulikana kama upinde wa ghadhabu wa Kaldiriyus".



Aliponyamaza tu wote wanne wakapiga magoti na kutoa heshima, "tutakuwa ngao yako mpaka mwisho" kwa pamoja wakaongea. "Nyinyi mtasikiza amri kutoka kwangu tu" aliongea Fahad na kuwapa ishara wasimame.



"Rondelif nipe taarifa" alitoa amri na kukaa.



"Inaonekana ndani ya miezi sita vikosi vya mfalme Lorei vitaanza safari ya kuja huku. Vikosi hivyo vina jumla ya wanajeshi zaidi ya elfu kumi, na miongoni mwao kuna mia mbili ambao wako daraja la QinDan, na sita wapo daraja la KyoDan. Walobakia wote ni kuanzia daraja la TongSan na kushuka chini, nawasilisha" aliongea Rondelif.



"Ikiwa wanasubiri bado maana yake kuna ambao hawajafika" aliongea Fang Shi.



"Ndio, kutokana na taarifa zisizo na uhakika ni kwamba kuna watu watatu bado hawajafika na inasemekena wote hao ni daraja uzima na kifo" aliongezea Rondelif.



"Ahsante kwa taarifa Rondelif" aliongea Fahad na kusimama kisha akaangalia nje kupitia dirishani huku mimono yake ikiwa imekutana nyuma.



"Tunasubiri amri yako" aliongea Garaaji.



"Nyinyi endeleeni na majukumu yenu kama kawaida, mimi nitaondoka kuelekea milima ya Zinga kwa ajili mafunzo. Wakianza kuja, Rondelif urakuja kunambia" aliongea na kupotea.



"Mpaka siku nyingine tena" aliongea Rondelif na taratibu akaanza kusambaratika na kuwa moshi mweusi na sekunde chache ukapotea.



"Sisi humu ndani tu ndio tunatakiwa kujua kama meya ametoka. Yeyote akitaka kujua habaei zake, tutamwambia yupo ndani ya nyumba yake na amesema asisumbuliwe kama hakuna kitu cha maana" aliongea Nephira na kugeuka kisha akaondoka.



Milima ya Zinga.



Fahad anatua kutoka katika mgongo wa Gorigo, "Gorigo unaweza kwenda kucheza" aliongea na kuingia ndani ya pango kubwa. Gorigo akapiga ukwenzi mkali na kupotelea angani kwa kasi. Ni kama vile aliekuwa akiisubiria nafasi hiyo kwa muda mrefu.



Ndani ya pango hilo Fahad akatafuta jiwe na kukaa, akakunja miguu na kufumba macho.



"Ohohoho, kijana umeweza kuja bila kutumia nguvu sana ahahaha" sauti ya kizee ilisikika. Fahad akafumbua macho na kujikuta kasima nyuma ya mzee Karakantha.



"Samahani mwalimu kwa kukuweka sana" aliongea na kuinamisha kichwa.



"Ahahaha usijali najua una mambo mengi ya kushughulikia" aliongea mzee Karakantha na kusafisha koo kabla ya kuendelea "mpaka ulipofika sasa, mimi sina tena cha kukufunza na bahati mbaya sana muda wangu una karibia. Nimekidanganya na kukitoroka kifo kwa muda mrefu sana" aliongea na kumgeukia Fahad.



"Usiwe na huzuni sana, kifo kama ilivyo kuzaliwa ni wajibu kwa kila mtu. Ila kabla sijakupa mafunzo ya mwisho, nataka nikuusie. Fahad, usije ukafanya kosa kama nililofanya mimi" alionekana kuwa mwenye na huzuni.



"Nihusie mwalimu" aliongea Fahad kwa heshima.



"Katika kukimbiza na kutafuta uwezo mkubwa niliamua kukata hisia zote. Niliacha kila kitu mpaka wale nilowapenda, moyo wangu ulikufa ganzi ukawa wa baridi. Niliua bila sababu katika njia yangu ya kuelekea utukufu. Mwisho kabisa kutokana na moyo wangu kuwa mweusi, nilipofika daraja la Mythril ikabidi nichague njia moja kati ya mbili, njia ya wema au ubaya. Kwasababu nilishakuwa na kutu sikufikiria hata mara mbili kabla ya kuchagua njia ya ubaya. Japo katika martial art hakuna ubaya wala uzuri mwenye nguvu ndie anaeheshimiwa lakini usije ukapotea kama nilivyopotea mimi".



Fahad alitulia kwa makini akisikiliza maneneo hayo, alihakikisha hapitwi na kitu. Kimoja alichofahamu ni kwamba angefika pahali na kutakuwa achague maisha yake ambayo ndio yangemuongoza katika njia yake ya martial art.



"Tembea na mimi uone vita yangu ya mwisho" aliongea Karakantha na kuanza kuondoka. Fahad akafuata nyuma, ghafla chini kukawa kama kioo, ukaonekana uwanja mkubwa. Magharibi mwa uwanja huwo alikuwa mtu mmoja na upande mwengine walikuwa watu kumi nambili.



*******



"Asura, ukisalimi amri nitakufa kifo laini sana" aliongea Indra ndie alikuwa kiongozi wa kikundi hicho cha watu kumi na mbili.



"Hahahah! Indra leo ndio siku ambayo utakufa. Kosa kubwa ulofanya katika maisha yako ni kukatiza katika maishanyangu. Siku ya leo nitachukuwa kila kitu unachokithamini katika maisha yako" aliongea Asura kwa hasira.



"Unasema vitu ambavyo mimi sivielewi, mimi na wewe hatujawahi kukatiza njia moja hata siku moja" aliongea Indra.



"Tafsiri ya mungu ni uwepo ambao unajua jana, leo na kesho. Kama unashindwa kunitambua leo, basi umenithibitishia kuwa wewe si mungu bali ni muongo tu" aliongea Asura na kuachia tabasamu.



"Hahaha, mungu ni yule ambae ana uwezo wa kuamua kitu na kikatokea. Mimi huwo uwezo ninao na sababu leo nimeamua leo utakufa basi niamini mimi kama nitakufa" alijitamba Indra.



"Mpumbavu sana wewe, leo ni siku ambayo mimi Asura nitakunywa damu ya mungu muongo. Leo ni siku ambayo Indra utakwenda kuzimu kwa njia yeyote ile hahahaha!" Kicheko kikali na kilichojaa hasira kikatoka kinywa cha Asura.



"Sun Wu Kong" Indra akaita kwa nguvu, kwa kasi ya kali sana ikatua fimbo ya chuma na kuchoma ardhini. Juu ya fimbo akatua kiumbe aliefanana na ngedere lakini alikuwa katika umbili la binadamu.



"Amri yako mtuku mfalme" aliongea Sun Wu Kong, na kujikuna kichwani. Tabia zake hazikupishana na za ngedere.



"Niletee kichwa cha yule mjinga" alitoa amri Indra, Sun Wu Kong bila kuuliza mara ya pili akachomoka kwa kasi kuelekea alipo Asura.



"Alambara, lia" Asura akapiga kelele na nyuma yako ikatau ngoma kubwa na kuanza kulia. "Ngoma ya vita alambara" aliendelea kuongea na kuinua mikono. Vikatoka vigongo viwili katika ngoma hiyo na kutua katika mikono yake.



Kama radi akachomoka, kasi yake ilisababisha mpaka ardhi kupasuka. Kwa kasi hiyo hiyo akakutana na Sun Wu Kong, kitendo cha kugusana tu mpaka radi zilipasuka na maana ngurumo zilzosikika mpaka kuzimu. Sun Wu Kong akatupwa nyuma, bila matarajio yake akacheuka damu.





 
Black Star 2: Nemesis 41





Asura hakutaka kutoa nafasi ya adui yake kujikusanya, kama radi akachomoka. Indra akatambua kabisa kuwa kama shambulio hilo lingeunga basi angempoteza Sun Wu Kong. Akainua mkono juu, "Anubis, Mesya mzuieni". Wawili hao waliotajwa wakatowekea na kutokea mbele ya Sun Wu Kong, na wakati huwo Asura alikuwa kashafika tayari.



Wote wawili wakaanchia Qi yao iliojaa harufu ya kifo, Asura akatupwa nyuma kwa kasi. Alipotuwa akakita vigongo vyake chini na kuburuzika mita kadhaa.



"Unataka kunichosha kisha ndio uwatume hao vibwengo wako unaowaamini sana" aliongea na kutema mate pembeni yalikuwa yamwchanganyuka na damu.



Akavirusha vigongo vyake juu, vigongo hivyo vikarudi ndani ya alambara. "Mkuki wa radi Behemoth" akaita na kuinua mkono juu. Mkuki mkubwa wenye kitambaa cheusi ukatoka katika alambara na kwa kasi ukatua mkonono. Akauzungusha mara kadhaa kabla kuukita chini.



"Hawa watatu hawana uwezo wa kupambana na mimi, kama kuna ambao unaweza kuwaongeza waongeze tu" aliongea na kuaanza kuuzungusha. Aliuzungusha kwa kasi kiasi cha kuonekana kama duara. Radi ndogo zilizochanganyika na moto na zikaanza kuonekana.



Indra akakunja ndita, ni kweli kabisa alichokisema. Ageukwa nyuma na kuwapa amri wengine sita, nao wakaondoka kwa kasi kwenda kuungana na wenzao. Asura hakutaka kupoteza muda, akanesa kulia na aliporudi tu kukaa sawa akatoweka na kuacha michirizi ya radi ikifuata nyuma.



Sun Wu Kong na wengine wakaziweka silaha zao vizuri kwa ajili ya kumkabili Asura alieonekana kushambulia kama mbogo aliejeruhiwa. Kitu ambacho hawakukitegemea na mtu huyo kuwa na nguvu za kuwafanya wote watoke jasho.



"Tumia silaha za divai" alitoa amri Indra, wote wakatupa silaha zao chini na kuinuwa mikono juu. Wakanena maneno kadhaa kwa sauti ndogo, kutokea angani kukaonekana kama vitu viking'ara. Vikashuka kwa kasi na kutua katika mikono ya watu hao.



"Hehehe! Vizuri sana, acheni na mini nikuonesheni makusanyo yangu ya silaha" aliongea Asura na kuucheka kwa nguvu.



"Peke yako huna uwezo wa kutumia silaha zaidi ya moja" aliongea Mesya na kuachia tabasamu.



"Kuna mengi sana ambayo hujayaona kijana, wakati wewe unarama nyayo za Indra mimi nimekuwa nikizunguka kusina na kaskazini na magharibi na mashariki. Unadhani nilikuwa nacheza makida makida" alijibu Asura kwa dharau.



"Enyi mlokosewa na kupewa majina na sifa mbaya kutokana na maumbile yenu. Mukawauwa ili wachache wafiche makucha yao na kuongoza kwa uongo kwa kujiita miungu. Sikieni maneno yangu na muamke kutoka ndoto zenu, muda wenu wa kulipiza kisasi umefika" Asura alinena maneno hayo kwa nguvu.



Silaha kadhaa zikatoka kwenye Alambara na kuelekea alipo. Zilopofika wala hakuzishika bali zilikuwa zikielea pembeni yake.



Akauachia mkuki aliokuwa nao mkononi nao ukaungana na silaha nyingine. Sekunde chache baadae ukatoka upinde na kutuwa mikono mwake.



"Acheni niwatambulishe kutokea kulia kwangu, mkuki wa radi wa Behemoth, upanga wa moto wa Phonix, ngao isiyovunjika ya kobe mwenye kichwa cha nyoka, panga mbili fupi za chui mwekundu wa kuzimu, firimbi ya wafu ya kuzimu, mkononi kwangu ni upinde ndege mpole Kaldiriyus, kuelekea kushoto kwangu ni mkuki wa ncha mbili wa simba mwenye mbawa za dhahabu, kisu cha sumu cha Gideol, panga kubwa na zito la Terantos, mkia wa taa wa tai anaeishi katika volkano, fimbo ya mti wa eden na nyuma yangu ni ngoma ya vita Alambara iliotokana na mungu asili wa bahari Kraken".



"Baada ya kutueleza hivyo, ukitegemea tuogooe au" aliuliza Sun Wu Kong.



"Hahaha! Hapana sio kuwaogopesha, lakini muangalieni mnaemuita mfalme. Sura yake imekunjana kwasababu anaujua ukweli" aliongea Asura na wote wakageuka. Na kweli japo Indra alijikaza asioneshe kukereka kwake lakini kero ilikuwa imejichora katika uso wake wote.



"Muueni" Indra akatoa amri, wote tisa wakaruia mbele na kuchomoka kwa kasi kuelekea alipo Asura. "Sherehekeni" aliongea Asura kwa sauti ndogo. Silaha zote hizo zikachomoka kuelekea walipokuwa wanatokea watu wa Indra.



Asura akavuta utari wa upinde aliokuwa nao mkononi na kuuachia. Si Indra wala wale watatu walobaki waliokuwa wanajua nini kinakuja. Lakini walishangaa ardhi ikichimbika na kupasuka.



"Upinde bila mshale" aliongea mmoja kati ya wale watatu, "inaonekana na sisi muda si mrefu tutaingua ulingoni" mwengine akajibu. Hawa watatu walikuwa hawana hata majina lakini baada ya Indra, hawa ndio waliokuwa na uwezo mkubwa kuliko wengine wote wote.



Wakati zile silaha zikiendelea na mashambulizi, Asura alikuwa akiachia mishale ya Qi iliyosafiri kwa kasi na kuasababisha madhara makubwa kwa maadui zake.



"Mfalme, turuhusu tuingie uwanjani" aliongea mmoja kati ya wale watatu.



"Hapana, hamumuwezi. Nikitoa alama, ingieni na kuhakikisha mnaziharibu zile silaha kisha ondokeni na hao wajinga. Hii vita ni kati yangu na adui yangu mkubwa. Nisubirini Nirvana japo sijui vita hii itaisha lini. Ikifika miaka mia sijarudi. Nendeni Dao, isambaratisheni ngome yake kisha kaeni katika mlima Sumeru, nitawakuta hapo" alitoa maelekezo.



Akavuta pumzi nyingi kali kabla ya kuachia Qi yake, hiyo ndio ilikuwa alama. Wale watatu kama umeme wakafyetuka, ila kabla hawajafika Asura akashtukia na kuamuru silaha zake zote zirudi.



Walipofika na kukuta wamechelewa, wakawakusanya wengine na mmoja kati yako akafanya kama anakata hewa kwa mkono, ukatokea mpasuko na bila kuchelewa wakapita na mpasuko ule ukajifunga.



"Asura muda wa kucheza umeisha unaonaje tukaweka upuuzi pembeni na kufanya kilichotuleta hapa" aliomgea Indra.



"Kabisa hata mimi nakuunga mkono ila kabla sijafanya hivyo ngoja nirudishe silaha zangu" aliongea. Indra hakuwa na haraka, akakaa kitako kabisa akimsubiri afanye alivyosema.



"Tawanyikeni katika ulimwengu, ipo siku mtapata bwana wa kufuata atakaejua thamani yenu. Pia upo uwezekano wa mimi nyinyi kuonana tena, nawaahidi tukionana tena basi nitawashughulikia vizuri" aliongea na baada ya maneno hayo kila silaha ikatawawinyika upande wake isipokuwa alambara tu.



"Bwana wangu mimi nitakusubiri katika ngome yako, sitalia mpaka siku tutakayoonana tena" aliisikia sauti ya alambara ndani ya kichwa chake kabla ya ngoma hiyo kupotea.



"Asura nakushauri upambane na kila kitu chako, mimi si wale" aliongea na kuanza kuchezehsa vidole vyake katika alama maalum. Taratibu Qi ikaanza kuvuja mwilini mwake, ikazunguka mwili mzima na ghafla ikapaa angani kama mnara. Nywele za Indra zikabadilika rangi na kuwa nyeupe na macho yake yakawa yanameremeta yakionesha vitu kama radi zikicheza katika viini vyake vya manjano.



"Hahahaha nashukuru kwa ukumbusho wako lakini tokea mwanzo sikuwa na mpango kucheza na wewe nusu nusu" alijibu Asura na kukutanisha viganja vyake. Qi nyekundu ikapaa angani na kutengeneza mnara mwengine.



Macho yake yakabadilika rangi huku jicho la kulia likiwa na kijani na ndani lilikuwa na mchoro wa alama ya V, crest ya wachawi. Kiini cha jicho lake la kulia kikabadilika na kuwa rangi ya buluu. Katikati baisna ya nyusi zake juu kidogo kukapasuka na kutokea jicho la tatu ambalo kiini chake kilikuwa na rangi mbili, nyeusi na nyupe, jicho la yin na yang.

 
Black Star 2: Nemesis 42







Wote wawili wakapotea ghafla na kukutana kati, Qi zao zilipogusana tu kila kitu ndani ya maili miatano kilisambaratika. Hakukuwa na milima wala miti iliyopona, ndani ya maili mia tano lilibaki jangwa la tambarare.



Tap tap tap.



Kila mmoja akarudi nyuma kwa hatua zaidi ya kumi, kama mishale miwili iliyoachiwa kutoka kwenye upinde. Wakafuetuka na kuvaani tena, kila walipokutana ardhi ilibadilika. Makorongo na milima ilijichonga, wawili hao waliendelea kupambana mpaka kiza kikaingia. Hawakuacha, vita iliendelea.



Kila mmoja katika akili yake alijiapiza kutokumuacha mwenzie salama. Asubuhi kukakucha bado wawili hao walikuwa vitani.



Bam!



Ngumi zao zilipokutana zikasababisha moto mkali sana na kila mmoja akarudi nyuma. Ila hakuna alietulia, kila mmoja akazunguka huku kochwani akiwa na shambulio linalofuata. Katika shambulio hilo kila mmoja alijaza Qi yake mkono na kuvamiana tena. Walipokutana, kwa sekunde kadhaa hakukusikika kitu.



Ghafla kukasikika kama kitu kikidata na baada ya hapo ufa mkubwa ukajitokeza katika uso wa sayari hiyo. Na baada ya hapo moyo wa sayari hiyo ukachemka na hatimae sayari ikashindwa kuvumilia kishindo cha watu hao wawili na kusambaratika.



Wote wawili wakajikuta wakielea katika anga la stari, anga lilikusanya zaidi ya sayari elfu moja. Asura alipoufungua macho hakumuona Indra mbele yake. Kwa kutumia hisia yake ya kidivai akakagua eneo eneo lote hilo na kufanikiwa kuweza kuhisi alipo adui yake mkubwa.



Walikuwa wametengenishwa zaidi ya maili elfu moja, kwa kasi kubwa sana Asura akaanzaa kusafiri kuelekea alipo Indra. Wakati yeye akifanya hivyo kumbe na indra alikuwa akifanya hivyo. Wawili hawa walikuwa na uadui ulioota mizizi katika mioyo yao.



Walipokutana vita ikaendelea, na kwasababu hawakuwa katika sayari yeyeote ile hata muda hawakufahamu ulivyokuwa unakwenda. Wao waliendelea kupambana, ni kama alpha wawili ambao hawakutakiwa waishi pamoja.



Wakati wakiendelea kupambana, Asura akazubaa kidogo tu. Indra akatumia nafasi kufanya shambulizi takatifu na lenye nguvu. Asura akashuka kama kimondo na kujibamiza katika uso wa sayari iliyokuwa karibu.



Koh koh!



Akatapika damu nyingine, karibu viungo vyake vya ndani vyote vilikuwa vimevurugika. Wakati akiendelea kujikusanya ili ainuke, Indra akatua kwa kasi na nguvu kubwa katika kifua chake na kusababisha mbacu kadhaa zivunjike. Watu hawa wawili hawakuwa binadamu tena, walikuwa miungu wawili wasiopendana.



"Ruhje" alipiga kelele Asura na kuinua mkono juu. Kutokea sayari ya Dao, ndani ya ghala kubwa ilionekana shoka iliokuwa imewekqa ukutani. Kelele ya Asura iliifikia shoka hiyo, ikatoka sehemu iliyokuwa imewekwa na kuitika wito wa bwana wake. Ikapasuwa anga na kusafiri kwa kasi ya radi na baada ya sekunde chache, kitu kama nyota kikaonekana kiking'ara angani.



Kilikuwa kikishuka kuelekea katika sayari waliokuwepo wawili hao. Indra akahisi hatari isiyo ya kawaida, japo alikuwa na mkono wa juu lakini ikabidi arudi nyuma kwa kasi. Shoka kubwa likatuwa mkononi mwa Asura, ilikuwa nyekundu na ikifoka mvuke kuashiria kwamba ilikuwa ni ya moto.



Asura baada ya kuidaka tu akaanza kuinuka na kuelea, macho yake yote matatu yakabaidilika na kuwa mekundu. Michoro kadhaa ikajichora usoni kwakena kushuka kuelekea mwili mzima. Mapembe mawili makubwa yakajitokeza katika paa la uso wake.



"Hahahaha! Sasa najua kwanini nilikuwa nahisi kuna kitu hakipo sawa" aliongea Indra na kulamba midomo yake huku tabasamu lenye kuashiria uwana haramu uliopitiliza.



"Asura umebarikiwa meridian nane za dragon, nazitaka hizo meridian zako" aliongea kwa nguvu na kukutanisha viganja vyake. "Ukilinganisha meridian zangu za yang tu na za kwako za dragon, nikizipata nitakuwa na meridian kumi na mbili za ziada. Za yang nne na dragon nane, haya ni mavuno yenye faida kubwa" aliendelea kuongea huku mwili wake ukibadilika.



Juu ya kichwa chake ikatokea pete kubwa nyeupe iliokuwa ikielea, mgongo wake ukachanika na kutokea mbawa nyeupe mbili kubwa. Akainua mkono wake juu na radi zikaanza kupiga, na zote zililenga katika kiganja chake na baada ya muda mfupi tu mkuki mkubwa uliokuwa unameremeta ukatokea mkononi mwake. Mkuki huwo ulitengezwa kwa radi na ulikuwa ukiwaka waka huku radi zikipiga pembeni.



"Kendo arak deiti Indra" akanena maneno hayo na suti ya radi ikajitokeza katika mwili wake. Asura akafahamu kabisa kuwa alikuwa akicheza na nguvu isiyo na mipaka na wakati huwo ilikuwa ndio wakati kuamua mwisho wa vita yao iliyodumu kwa muda mrefu.



"Hahahaha! Halafu watu wajinga wanaamini wewe ni mungu. Mimi na wewe hatuna tofauti sema mimi nimekubali tu" aliongea Asura na kujikonga kwa vidole viwili baadhi ya maeneo ya mwili wake. Alikuwa akiondoa vipingamizi vyote.



Ghafla mgongo ukachanika na mbawa kubwa nyeusi zikaonekana. Zilikuwa ni mbawa za dragon, jicho lake la tatu lilikuwepo juu kidogo kati ya nyusi zake likawaka moto mweusi. Suti iliyotengezwa kwa magamba ya dragon ikajitokeza katika mwili wake. Akabadilika kabisa.



Alipoteza kabisa sura ya kibinadamu, "grrrrr" akanguruma kwa nguvu. "Ittou-ache mage Asura" akanena maneno hayo, akazungkwa na moto mkali sana mweusi. Ulipotoweka, mkia mkubwa ukagonga ardhi.



"Huyu lazima nimuue leo" alijisemea Indra, wote wawili wakati huwo walikuwa katika uwezo wao wa juu zaidi. Katika hali hiyo wote wawili walikuwa wakichoma maisha yao. Walikuwa wakitumia nguvu ya asili ya maisha yao kusukuma na kuminya kila aina ya tone la nguvu ndani ya miili ya miili.



Waliamua kuwa katika sayari hiyo ndipo vita yao ya muda mrefu ingeishia japo hawakuwa wakijuwa ni muda gani wamekuwa wakipigana.



Wakasogeleana kwa kasi na kuanza kufikia matokeo, kila shambulizi lililotoka lililotoka na kusudio la kuuwa. Walibamizana, wakapasuana na mwisho ikawa ni vitu vya muda tu. Nani angdwahi kuyamaliza maisha yake mwenyewe, atakebaki ndie atakuwa mshindi.



Bam!



Kila mmoja akarudi nyuma kama mita mia mbili, Asura akakita shoka yake chini akihema kwa nguvu. Ule moto mweusi katika jicho lake la tatu upoteza nguvu na hatimae ukazima.



"Hahaha! Pamoja na maandalizi yote bado nimeshindwa kulipa kisasi" aliongea huku ile suti ya magamba ya dragon ikianza kukatika.



"Tumepigana kwa muda mrefu sana, kabla sijakumaliza. Hebu niambie ni wapi mimi na wewe tulipokatizana" aliongea Indra wakati akimfuata. Wakati huwo Asura alishapoteza uwezo wote wa kupigana.



"Dao, wakati wa mashindano ya miungu. Mlisambaratisha kijiji kilichokuwepo mlimani. Na mimi ukanipiga radi kwa sababu niliamua kupingana na nyinyi" alijibu Asura na kutafuta sehemu ilioinuka kidogo aegemee.



Macho yakamtoka Indra, hakuamini kama mtu wa kawaida angefika uwezo huo alokuwa nao Asura. Kama si mapema basi pale chini angekuwa yeye.



"Umewezaje" ilibidi auulize.



"Najua kama kuna mguvu mwingine, nguvu ambayo ndio imekubariki uwezo wako ila ya uroho ukaamua kuutenda ulimwegu wa Astra kutoka mfumo mzima wa Stari na kujitangaza kuwa wewe ni mungu. Nguvu hiyo ndio itanibariki na mimi na kinifanya kuwa adui yako mkubwa" alijibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…