Black star 2: Astra 25
Mwezi na nusu sasa ulikuwa umekata huku Fahad na kikosi chake wakiendelea kufungua njia. Hilo likawapa wepesi waliobakia na kufanya mashambulizi ya kasi.
"Wimbi limegeuka sasa" aliongea Fang Shi akiwa anaratibu mpango kazi mwengine.
"Ila hujanambia mtu aliekuwa mstari wa mbele zaidi ni nani" aliongea kamanda msaidizi Lati.
"Yule ni mwanachama mpya aliekuja kutoka Astra, ni mtu mwenye uwezo sana. Mpaka sasa hilo ndio ninalojua, nasubiri maelezo kutoka Astra. Yakifika ndio tutamfahamu vizuri. Ila ninachotaka kukuhusia ni kwamba, usije ukakaa upande mbaya nae maana sidhani kama katika ulimwengu kuna anaeweza kumzuia" aliongea Fang Shi akimuangalia msichana huyo.
"Sawa nimelisikia hilo, pia tumepokea taarifa kuwa kuna kikosi chenye viumbe wachache ambao inaaminika mmoja kati yao ndio kiongozi kipo njiani. Kinaelekea upande ambao Fahad yupo na kikosi chake" aliongea kamanda msaidizi Lati.
"Tuachane nao, hao watakutana na Fahad. Na mini nahisi huu wote ni mpango wa Fahad mwenyewe. Yeye kwa kutokuja mapema, alikuwa anapima uwezo halisi wa adui yetu. Pia, kwa kuenda mbele na kufanya vurugu amejifanya chambo kumtoa samaki mkubwa katika pango lake. Mi nasema hivi, huko tumuachie yeye sisi tuendelee kusafisha hawa samaki wadogo" alifafanua Fang Shi.
********
"Lina tunategemea kufika lini?" Aliuliza Starodastu, "kwasababu inabidi tutembee kwa siri ili kutomshtua adui yetu, itatuchukuwa wiki moja zaidi mpaka kufika alipo" alijibu Lima.
Akaendelea "na taarifa nilizopokea hivi punde ni kwamba, hivi tunavyoongea mimi na wewe huyo bwana anapambana peke yake. Hivyo uhakika wa kushinda upo kwetu kwasababu mpaka tukifika atakuwa kashatumia karibu Qi yake yote".
"Hilo lawezekana lakini itakuwaje ikiwa anatumia DoQi, si unajua ulimwenguni hakuna watu wagumu hao. Kwasababu wengi wana uwezo wa kunyonya Qi kutoka kwenye mazingira. Mtu kama huyo anaweza kupambana bila kupumzika wala kula kwa muda mrefu sana" alionesga wasiwasi wake Starodastu.
"Bwana wangu hilo nalo pia nimelitilia maanani lakini unadhani ni binadamu gani ana uwezo wa kunyonya Qi iliyochanganyika na majini. Mwanzo hatohisi tabu yeyote lakini baadae meridian zake zitachafuka na kuanza kupata tabu hata kuzungusha Qi mwilini mwake" aliongea Lima.
Baada ya mazungumzo hayo wakaendelea na safari kimya kimya na kwa umakini wa hali ya juu sana. Hawakutaka kuwashtua maadui zao kama walikuwa njiani, kidogo wasichojuwa ni kwamba walikuwa wakicheza ngoma aliokuwa akiipiga Fahad mwenyewe.
Wiki moja baadae, upande wa Fahad.
"Nimewaita hapa kuwashukuru kwa kujitolea kwenu, najua kama hatujapoteza mtu lakini wengi mumepata majeraha ambayo yatawachukuwa muda mrefu kabla ya kupona. Mpaka kufikia hapa mumetenda vyema lakini kundi linalokuja hamuwezi kupambana nalo katika hali yenu hiyo" alinyamaza kidogo na kuwaangalia.
Kweli walionesha kuchoka sana, kuna baadhi ili wasimame walitumia miti kwa msaada. "Nataka murudi katika lile pango ili mpumzike, kuanzia hapa nitakuwa mwenyewe na kuwaonya tu naomba hata mkihisi nakufa msitoke. Kwasababu kama hamtakufa kwa mikono ya hawa viumbe basi lipo litakalowauwa. Nakwenda kutumia uwezo wangu wote kupambana, na si kitu ambayo roho zenu zinaweza kuhimili" aliongea Fahad kupepesa macho yake.
Yalibadilika na kuwa kiini kilichozungukwa na pete nne kila upande. "Sawa tumekuelewa, sisi tunakutakia ushindi" aliongea mmoja wao na kuwaangalia wenzake. Akawapa ishara ya kuondoka.
Fahad akaweka rungu lake chini na kukaa kwenye jiwe, umbali wa kilometa kama hamsini hivi kikosi cha Starodastu kilikuwa kinakaribia.
"Kwanini umekubali tuondoke" aliuliza mmoja wao wakati wako njia kuelekea katika pango. Yule tabibu aliekubali kuondoka aliwaangalia kisha akashusha pumzi.
"Nilichokiona baada ya kumaliza ilw kauli yake ni kifo, hivi tunavyoongea najitahidi tu kusimama lakini mwili wangu mzima bado una kumbukumbu ya kile kiumbe. Kamanda Fahad si kiumbe wa kawaida, naweza sema ni mjumbe wa kifo. Njia aliyochaguwa ni kinyume na miungu tunayoamini, kwa maneno mengine Fahad ni kiumbe ambae maisha yake yameandikwa kwenda kinyume na wale tunaowaamini" alifafanua japo alielewa hakuna kati yao ambae angeelewa alichomaanisha nyuma ya maneno yake.
************
"Mumechukuwa muda sana kufika hapa" aliongea Fahad akiinua kichwa, mashavuni alikuwa na michirizi ya machozi ya damu.
"Mumenisubisha sana, koh...koh!" Akakohoa na kutema damu, mwili wake ulikuwa umeumuka kama andazi lililojazwa hamira.
"Bwana wangu nasikitika kusema kuwa kati yetu hapa, ni wewe pekee mwenye uwezo wa kwenda nae ana kwa ana. Sisi wengine tutakuwa mzigo" aliongea Lima. Ila akasikia sauti ikitokea pembeni yake, "nani aliekuruhusu uongee" kabla hajajibu kichwa chake kikapasuka na kusambaratika.
"Shenzi weee, umemuua mshauri wangu" alifoka Starodastu.
"Hahaha! Mi nilijuwa umeniletea hawa kama sehemu ya zawadi kumbe ni wanajeshi. Mi nilijua ni kafara tu" aliongea Fahad na kunyoosha mkono mbele kisha akakunja ngumi, wote waliobaki kasoro Starodastu wakaanguka chini wakitokwa damu mdomoni.
Starodastu kwa hasira akamvaa Fahad na kuanza mashambulizi, ila akajikuta akibamizwa katika miti kadhaa. "Kama huwo ndio uwezo wako basi nimekupa sifa usostahili" aliongea Fahad akizungusha rungu lake na kulikita chini.
"Hahaha! Samahani nimekuonesha upande wangu dhaifu, niruhusu nikuoneshe uwezo wangu halisi" aliongea Starodastu na mwili wake ukaanza kubadilika. Mapembe makubwa yakachomoza kichwani mwake. Mgongo wake ukachanika na kutoka mbawa mbili kubwa zilizokuwa zinawaka moto. Alitoa moshi puani pale alipopumuwa.
Bila taarifa Fahad akatahamaki akibamiza chini kama mpira wa kitenesi. Akabiridhika mita kadhaa kabla ya kugonga kichwa kwenye jiwe kubwa na kulivunja. Wakati anataka kuinuka, Starodastu akatua kifuani kwake kwa teke kali sana.
Macho yakamtoka Fahad na kucheuka damu, mifupa ya kifua ilikua imenjuka. Akapapatuwa na kuchomoka mikononi mwa kiumbe huyo mwenye hasira, "hii ni raha, vingine vyovyote isingekuwa raha" alijisemea na kung'ata mdomo wake chini ili kutuma maumivu akilini asipoteze Fahad.
Mapigo hayo mawili ingekuwa ni mtu wa kawaida basi angekuwa kashakata roho lakini sio kwa kisiki kilichoshidna gurudoza.
Starodastu akazunguka kwa kasi na kufunguwa mbawa zake kubwa, madonge ya moto yakaruka kuelekea upande aliokuwa Fahad. Fahad akarudi nyuma kwa kasi na kuyakwepa, akakaza misuli ya miguu na kufyetuka kama risasi.
Starodastu akakwepa shambulizi hilo, likatua ardhini. Eneo lilipotuwa lisambaratika na kuwa vipande vipande. "Una macho makali sana" aliongea Fahad na kugeuka kwa kasi na kutoweka. Wawili hao waliondelea kushushiana kipondo usiku na mchana bila uhuru.
Walipokuwa wakipambania paliharibika, ardhi ilipoteza sura yake ya asili. Vita yao iliendelea kwa zaidi ya siku hamsini bila mapumziko.
"Nimepoteza hesabu za siku kabisa" aliongea Starodastu akijitahidi kusimama. Alikuwa akitokwa na damu mwili mzima. Upandr Fahad alikuwa amesimama kwa kutumia msaada wa rungu lake.
"Kwanini tusimalize vita hii, unajua kabisa huwezi nishinda na wala mimi siwezi kukushinda. Tutaendelea hivi mpaka mmoja wetu atakapokufa kwa kuchoka" aliongea Fahad akikaza misuli yake tayari kwa kushambulia.
"Hata mimi nahisi tuishie hapa" aliongea Starodastu akifunguwa mbawa zake na yeye tayari kwa kushambulia. Kila mmoja aliweka kila kitu kwenye shambulio hilo akiwa na lengo la kummaliza mwenzake. Wakavaana na mtikisiko mkubwa sana, ardhi ilichimbika na shimo kubwa sana.
"Kama unataka tupambane tena, nipe miaka mitatu" aliongea Fahad akikaa kwenye jiwe.
"Sina huwo mpango, ndani ya miaka mitatu kwako nitakuwa kama funza tu. Ikiwa maisha yatatukutanisha tena, basi naomba yatukutanishe kama marafiki" alijibu Starodastu na kufunguwa mbawa zake, akaruka na kupotelea angani.
"Ikiwa yatatukutanisha hivyo basi itakuwa vizuri zaidi" aliongea Fahad na kulalia rungu lake, macho yake yakaingia kiza na kupoteza nuru.