RIWAYA: Black star

*************************
Victor Smith akiwa ofisini kwake, uliingia ujume katika simu yake. Alipoufunguwa, ulikuwa ni ujumbe ulioambatana sanduku la posta pamoja na sehemu na nyumba unayokwenda. Damu itamwagika, wakati mwingine havitakuwa viungo vya mtu mwengine bali ni vya kwenu ulisomeka hivyo.

Victor akachukuwa karatasi na kuuandika ujumbe huwo kisha akachukuwa kile kifuko kilichokuwa na vidole pamoja na meno. Akaambatanisha na ujumbe huwo kisha akatia kwenye bahasha. Akanyanyua simu nyingine na kubonyeza tarakimu moja, akaongea na kuirudisha mezani. Baada ya dakika moja akafika mtu, akamkamkabidhi ujumbe na kumwambia pale unapotakiwa kupelekwa.

Mtu huyo baada ya kupokea maelezo hayo akaaga na kuondoka, safari ya kuelekea kule
unapotakiwa kufika ujumbe huwo ikaanza. Kutokana na foleni za jiji la Dar-es-salaam, akachukuwa muda mrefu kuliko ule alokusudia.

Baada ya saa nusu akawasili nje ya mlango wa nyumba alioelekezwa. Akagonga mlango, baada ya sekunde kama ishirinin mlango ukafunguliwa. Alikuwa ni Bahati, nimeambiwa niletee hii bahasha hapa aliongea na kumkabidhi. Hakumpa nafasi ya kuuliza chochote akaaga na kuondoka.

Bahati alipoinuwa kichwa mtu huyo akawa kashapotea tayari katika upeo wake wa macho yake. Akapotezea na kufunga mlango, moja kwa moja mpaka chumbani kwake. Akaifunguwa bahasha hiyo, akajikuta jasho likimtoka bila kutarajia japo feni ilikuwa ianzunguka.

Kwa pupa akatoa simu yake na kutafuta jina kisha akapiga. Ommy, msala ndugu. Misheni imefeli aliongea punde tu baada ya simu hiyo kupokea. Tulia kwanza, nakuja hapo tuongee vizuri Ommy akaongea na kukata simu.

Jasho liliendelea kumtoka bahati, hakutegema hata mara moja kama ndugu yao huyo angeweza kufanya hivyo. Akiwa katika hali hiyo akakumbuka ugomvi mkubwa kati ya Abedi na baba yao.

Abedi ukiendelea kufanya hivyo, mimi nitakukana kama mwanangu. Mimi siwezi kuishi na mtu katili kama wewe.

Lakini kazi yangu ndio inayoleta chakula mezani, kama si mimi tungekuwa tumeshanyauka hapa ndani.

Unathubutu kunijibu mimi baba yako, umekosa nidhamu kiasi hicho. Nasema hivi humu kwangu ondoka

Maneno hayo yalijirudia sana kichwani mwa Bahati maana hakuwa akifahamu kazi aliokuwa akiifanya ndugu yao huyo mpaka kukwazana na baba yao kiasi kile. Akiwa katika dimbwi la mawazo,

Simu yake ikaita. Loh! Akaruka na kujificha nyuma ya kochi, ah kumbe simu akajisemea na
kuipokea. Akatoka chumbani na kwenda kufunguwa malngo, afadhali umekuja Ommy alijisemea
akiongoza njia kuelekea chumbani kwake. Hivi ni vidole na mezo ya yule jamaa tulomtupa
awafuatilie watoto wa Abedi aliongea akimkabidhi kile kijifuko chenye vile viungo.

Ommy akaviangalia kisha akashusha pumzi, hii ni kazi yake bila shaka aliongea akikaa kwenye
kochi. Una maanisha nini, hilo tutaongea siku nyingine ila kwa sasa tunahitaji kukaa kimya. Mara ya pili atakuja kwa ajili ya maisha yetu.

Yule ni mbweha katika ngozi ya kondoo, ni mtu mwema usoni tu, ana roho ya alama ya kuuliza aliongea Ommy. Sasa tunafanya nini, mimi hata hapa sitaki kukaa tena pamoja na kujifanya mbabe ila Bahati alikuwa muoga sana. Alikiogopa sana kifo, ama mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.
Kwa kipindi hiki, tusifanye kitu.

Hatofanya kitu chochote mpaka tumchokonie tena. Inabidi tujipange upya, mali yake lazima iwe yetu kwa njia yeyote ile aliongea Ommy na kukunja ngumi. Wakaendelea kuongea na baada kama saa mbili hivi Ommy akaondoka. Alipotoka tu, Bahati akafunga akafunga mlango kwa funguo, kisha akatia komeo na kukimbilia chumbani na kujifungia.


Akafunguwa kabati na kutoapakiti ndogo yenye unga mweupe, akatoa kichupa kidogo chenye maji ndani. Akachanganya na ule unga kisha akachukuwa bomba dogo la sindano, akavuta ule ule
mchanganyiko kisha akajichomea. Akashusha pumzi na kuegemea kitanda, taratibu mkojo ukaanza
kumtoka. Hapo akajisikia vizuri na kuanza kutabasamu, ute mwembamba ukamchuruzika teja.
 
Kama kuna swali kuhusu kazi hii na nyinginezo ambazo nimewahi kuweka hapa karibuni kwa maswali na maoni.
 
TO THE END (MPAKA MWISHO) Ndiyo nitafuata hivi karibuni na hivyo endelea kutembelea kurasa zangu.. Ni follow Hapa ili iwe rahisi kuona riwaya zangu zote.
 
Black Star 22

Tariq Haji

06240659

Wiki moja baadae.

“Habari mabibi na mabwana na karibuni katika Golden Arena aliongea MC, shwangwe likazuka. Siku ya leo tutakuwa mzunguko wa mtoano, hii ni safari ya awali kwa wale wanaohitaji kushiriki katika mchezo wa kale. Si mwingine bali ni shindano la INDRA na ASURA, hapa leo kutakuwa na washiriki mia moja.

Hichi kiwanja kimoja tu, vipo kama hivi vingine vingi tu. Na kila kiwanja wanatakiwa watu kumi tu ile waendelea na mzunguko wa pili aliendelea kutangaza. Kuna aina mbili tu za kuendelea na mzunguko wa pili wa shindano hili, moja ni kuweza miongonie mwa watu kumi wa mwisho watakaobakia au pili ni kuwashinda wa washiriki wengine zaidi.

Hii ya pili itafanya kazi endapo tu watabakia watu zaidi ya kumi baada ya mchezo kuisha. Na mwisho, wanaotakiwa kubaki wasizidi kumi ila hata kama atabakia mmoja tu, huyo huyo ndie atakaekuwa mshindi alifafanuwa.

Mi nikutakie kazi njema aliongea Don Pizallo akiagana na Fahad, Usiwe na shaka, hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kunitoa katika mzunguko huu alijibu na kutabasamu. Wakaachana na Fahad akaelekea katika koridoo ambayo ilimpeleka mpaka katika ulingo. Yeye alikuwa ni miongoni mwa watu wa mwisho kuingia ulingoni. Sijui niwatoe wote akajisemea huku akizidi kutembea,

Mabibi na mabwana, mzunguko utaanza ndani ya sekunde tatu, mbili na moja ikalia honi ndogo. Hakuna hata mshiriki mmoja aliethubutu kuinuwa mguu, kila mmoja alikuwa akitegea mwenzake afanye hivyo. Na muda waliopewa ni dakika ishirini tu mpaka mzunguko huwo kufikia tamati,

Usifanye hilo kosa, kama unataka kumfata yule jamaa aliekuwa amesimama kama yupo kwenye maonesho, atakuuwa. Kwanini unasema hivyo, yaani nikimwagalia tu nahisi kubanwa na pumzi watu wawili walikuwa wakimuongelea Fahad aliekuwa amesimama huku amakunja mikono.

Mtu mmoja aliekaribu zaidi na Fahad uvumilivu ukamshinda na kumvamia, akajikuta akifyetuka na kubamizwa ukutani. Bahati haikuwa kwake, kichwa ndiyo kilitangulia kufika ukutani kikatawanyika kama tikiti maji. Ch! Inaonekana nimeshinda kudhibiti nguvu alijisemea akirudisha mguu chini, pigo hilo lilikuwa kama kengele.

Vurungumati likaanza, kila mtu akatafuta mtu kumuonea. Kila aliejipeleka kwa Fahadi alikutana na maafa tu. Ndani ya dakika kimu nusu na robo ya watu tayari walishatolewa huku Fahad akiongoza kwa kutoa wengi zaidi, zaidi ya arobaini.

Alipoona hakuna tena anaemfuata akaamuwa kukaa kitako na kuwaacha wengie wakiendelea kusulibiana. Mpaka dakika ishirini zinaisha walikuwa wamebakia watu tisa tu, honi ikalia tena kuashiria kuwa mzunguko huwo umefikia tamati. mabibi na mabwana na sasa tumefikia mwisho mzunguko wa kwanza wa shindano hili aliongea MC.

Washiriki wote watakwenda mapumziko, mzunguko wa pili utaanza baada ya saa na nusu aliongea na washiriki wote wakatoka. Fahad alitembea taratibu kuelekea chumba cha mapumziko, ndio wanajiita wanaMartial Art, wanajitania alijisemea.
 
Black Star 23
Tariq Haji
06240659

Katika chumba viongozi, huyu mshiriki hahitaji kushiriki mzunguko wa pilialiongea mmoja kati ya viongozi wasimamizi wa mzunguko huwo. Artif, mimi naungana nawewe hapo. Black Star naamini
ndio jina lake.

Kwa alichoonesha mzunguko kwa kwanza, naamini kabisa hakuna hata mmoja kati ya waliobaki mwenye uwezo wa kusimama nae ulingo aliongea msimamizi mwingine. Umenena vyema Franklin, mwiteni mmiliki wake tumlipe na kumpa kadi ya kuendelea mzunguko wa tatu mwezi ujao aliongea Montana Kris.

Don Pizallo akapewa taarifa za kuitwa katika chumba cha wasimamizi, akalipwa dola milioni moja na pamoja na kadi ya kuendelea na mzunguko wa tatu ambao utafanyika mwezi unaofata.

Akapokea mzigo huwo na kuondoka, tumepokea ujumbe kutoka kamati kuu, mpambanaji anaemilikiwa na Don Pizallo, Black Star amepita bila kushiriki mzunguko wa pili. Hivyo hata shiriki mzunguko huu badala yake atashiriki moja kwa katika mzunguko wa tatu ambao utafanyika mwezi ujao aliongea
MC.

Fahad akatoka chumba cha kusubiri na kuelekea nje kabisa ya uwanja, akamkuta Don Pizallo akimsubiri. Umefanya vyema kijana wangu, japo sura yako inaonesha kutoridhika kabisa. Ni kweli kabisa, pambano lilikuwa rahisi sana. Hakuna hata mmoja alienichemsha damu yangu leo.

Natumai kuwa mzunguko wa tatu nitakutana na upinzani mkali sana aliongea Fahad akiingia ndani ya gari. Don Pizallo akaingia upande wa pili na safari ya kurudi hotelini ikaanza. Ukiwa unasubiri mzunguko wa tatu, unakusudia kufanya nini.

Nataka niende nyumbani kuwasalimu wazazi, nitarudi ikiwa imebakia wiki moja kuelekea mzunguko wa tatu.

Sawa, hakuna shida. Achana vijana wangu wakuandalie mpango mzima wa safari, utaondoka kesho kutwa ila uwe makini sana. Nina uhakika kuwa kuna watu wameanza kukufutilia maisha yako mpaka sasa aliongea Don Pizallo.

Wafanye tu hivyo lakini wakijichanganya na familia yangu watakumbana na kiama alijibu na kukunja sura. Don Pizallo alihisi kubanwa na pumzi, AURA alijisemea kichwani.

Siku tatu baadae.

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia inakanyaga ardhi Tanzani katika uwanja wa taifa wa Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere. Katika mlango VIP Fahad akatoka akiwa na begi lake la mgongoni.

Alitoka mpaka sehemu ya kusubiri Mizigo, akatoa maelekezo ipelekwe nje ambako alitafuta dereva wa taxi na kuipakia. Akamueleza sehemu ya kwenda, dereva huyo akaweka gia na kuondoa gari.

Siku nyingi, mnaendeleaje nyumbani alijisemea na kushusha pumzi. Baada ya safari ndefu, hatimae akawasili nyumbani kwake.

Mlinzi aliekuwepo akamsaidia mizigo na kuipeleka ndani, za siku nyingi Msola aliongea Fahad.

Nzuri tu bosi, pole kwa safari alijibu.

Ahsante, kwa wiki tatu utapumzika nyumbani na familia yako aliongea Fahad na kumkabidhi bahasha. Si pesa nyingi lakini nina imani zitakusukuma kwa siku hizi chache aliongea. Msola akipokea bahasha hiyo, wala hakuifunguwa.

Akaaga na kuondoka, Fahad akaelekea chumbani kwake na kupanga vitu vyake. Na kwa sababu tayari kiza kilishaanza kuingia, akafunga funga milango na kuingia chumbani kwa ajili ya kuupitisha usiku huwo.Ila kabla hajalala akafungua dirisha na kuliacha wazi kisha akazima taa nda kukaa kwenye kiti. Huna haja ya kujificha akaongea bila kuwasha taa.

Kimya! narudia tena, huna haja ya kujificha. Sitaki nikuone sura ila kama una jambo unataka kusema ni vyema ukafanya hivyo. Nimechoka nataka nipumzike. Bosi wangu anahitaji ujiunge na kampuni yake, atakulipa mara tano kuliko anavyokulipa Don Pizallo aliongea mtu aliekuwa gizani upande wa pili.

Nashukuru kwa ofa yako lakini bahati mbaya sina muda wa kubadilisha bosi. Nenda kamwambie, ikitokea akapambana na bosi wangu basi alete mpiganaji wake mkali na hodari kuliko yeyote. Akinipiga ndio nitajiunga ne. Nimemaliza na unaweza kuenda, ukiongea neno moja tu roho yako.

Siku ya pili mapema asubuhi, Fahad alitoka na kupelekea madukani kwa ajili ya kutafuta simu na laini kwa ajili ya mawasiliano. Alipomaliza harakati zake akatafuta mgahawa na kupata kifungua kinywa kisha akarudi nyumbani.

Baada ya kupumzika kidogo, akawasha ile simu na kuweka laini. Akaingiza tarakimu kadhaa na kupiga. Iliita lakini haikupokewa. Alipoona hivyo akafahamu kuwa mtu anayetafuta huenda akawa kwenye kikao. Baada ya dakika kama kumi hivi, akaingia bafuni na kujimwagia maji kisha akavaa suti na kutoka.

Alipohakikisha maandalizi yamekamilika akatoka na kuelekea ofisini kwa mzee Abedi. Hakutoa taarifa, alitaka kumfanyia Surprise. Baada ya mwendo wa nusu saa akawasili nje ya jengo kubwa. Akaingia sehemu ya maegesho na kuegesha gari. Akashuka na kuelekea ndani ya jengo hilo.

Habari ya saa hizi dada alimsalimu mwanamke alimkuta mapokezi. Nzuri nikusaidie nini alijibu na kumuangalia. Naweza kumuona mzee Abedi aliongea kwa sauti ya chini.

Una miadi nae

Hapana, ila we mwambie tu mtu wa miezi sita amekuja

Samahani kaka, kama huna miadi nae, ni vyema ukaondoka au ukaweka miadi. Lakini kwa leo nafasi haitakuwepo labda kesho aliongea mwanamke huyo na kubenuwa midomo.

Asante kwa maelezo yako, kama hutojali naweza kulifahamu jina lako aliongea tena kwa sauti ya chini. Yule bidada akamuangalia Fahad kwa macho yaliojaa kiburi, akasonya. Jina langu la kazi gani aliongea kwa sauti kubwa kiasi cha watu waliokuwa karibu na mapokezi kusikia. Mlinzi aliyekuwa karibu na hapo akafika, kuna nini akauliza. Mtoe huyu kaka nje, ananipotezea muda wangu tu alifoka.

Yule mlinzi akageukia Fahad na kutaka kuongea lakini midomo ikashindwa kutamka maneno aliyokusudia. Akataka kuongea jambo jingine, Fahad akaweka kidole mdomoni kisha akaongea, fanya kazi yako. Akameza funda kubwa la mate, kijasho chemba kikaanza kumchuruzika. Wewe si nimekwambia mtoe akafoka na kusimama. Akatoka sehemu ya ndani na kwenda kumshika mkono Fahad kwa ajili ya kumtoa.

Huna haja ya kunivuta, mimi ni mtu mzima, nitaondoka mwenyewe aliongea na akmshika mkono na kuutoa. Kisha akageuka na kuanza kuondoka. Tajiri akasikia sauti nzito ikitokea nyuma yake, mbona unaondoka ile sauti ikaendelea.

Nimeambiwa niondoke, na ndio maana naondoka alijibu akigeuka. Nani alokwambia uondoke aliuliza mzee huyo kwa hasira. Mzee Mussa punguza jazba, nina uhakika aliesema hivyo alikuwa anatimiza majukumu yake tu aliongea na kutabasamu kisha akaendelea isitoshe sikuwa na miadi ya kumuona bosi.

Bosi gani huyo, nani aliesema mwenye kampuni anahitaji kuweka miadi ya kuonana na bosi alifoka kisha akaelekea mapokezi. Naomba kitabu cha wageni muhimu akaongea. Yule bidada akakiweka mezani kitabu alichoambiwa.

Mzee Mussa akakifunguwa, ukurasa wa kwanza tu wa kitabu hicho kulikuwa na picha kubwa ya Fahad. Wewe, umeiona hii picha aliongea akmgeuzia kitabu. Yule mwanamke macho yakamtoka, na wakati huwo ndipo alipotambuwa kama kibarua kimeota nyasi. Mzee Mussa, usifanye kitu chochote aliongea Fahad, akamuangalia yule mwanamke na kutabasamu kisha akaondoka na mzee Mussa.

Moja kwa moja alipelekwa mpaka katika ofisi yake, katika kampuni hiyo Fahad alikuwa ndio mtu wa juu kabisa. Akiwepo yeye hata baba ake hushuka cheo na kuwa cheo cha chini. Subiri katika ofisi yako, mzee yupo kwenye kikao.

Atatoka muda si mrefu aliongea mzee Mussa. Ahsante sana, ni matumaini yangu uko salama lakini. Maana wala hatujapata muda wa kuulizana hali aliongea Fahad na kutabsamu. Mi nashukuru Mungu, naendelea vizuri sema tu, kipidni cha nyuma nilipata ugonjwa kidogo ila sasaniko vizuri aliongea mzee huyo.

Nafurahi kusikia hivyo aliongea Fahad na kuinuka, akaelekea dirishani na kufunguwa mapazia kwa ajili ya kuruhusu mwanga wa jua. Unahitaji kinywaji chochote, nipatie chai tu ya tangawizi aliongea na kurudi kwenye kiti chake. Mzee Mussa akatoka na kumuacha Fahad peke yake, pasi na kuwa nyumbani. Bado alihisi kuna kitu anakikosa moyoni mwake. Alitoa simu yake na kutaka kupiga lakini alifahamu kabisa isingewezekana.

Baada ya dakika kama kumi hivi mzee Mussa akarudi akiwa na kikombe vikombe pamoja na chupa ndogo ya chai. Akaweka mezani na kumimina chai, akamsogezea kikombe kimoja. Wakati wanapata chai wakawa wanaongea mambo mbali mbali kuhusu kampuni. Nusu saa baadae mlamgo ukafunguliwa, mzee Abedi akaingia akiwa anahema. Alikuwa haamini macho yake, miezi sita kwakem ilikuwa kama miaka.

Fahad ni wewe baba au macho yang yananidanganya aliongea mzee huyo huku machozi yakijenga michirizi mashavuni mwake. Ni baba, awe Fahad yupi kama sio jembe lako alionge akitabasamu. Hivi ni miezi sita au miaka, katika kipindi hiki mwanangu umekuwa sana aliongea na maneni hayo yalimshtuwa sana Fahad. Kwa duniani kweli ana miaka ishirini kama awali lakini katika ulimwengu wa Dao tayari alishfika miaka ishirini na sita.

Hapana baba ni miezi sita tu alijbu na kwenda kumkumbatia mzee huyo. Nashukuru mungu umerudi salama japo nafahamu kama hutokaa sana aliongea Mzee Abedi. Wakakaa katika ofisi hiyo na na kuongea, bila kushughulika na saa.

Walishtushwa na alarm ya saa sita, vipi utakwenda nyumbani leo, au bado kidogo aliuliza mzee Abedi. Kama ulivyosema baba, mimi sina muda mrefu. Nitakuwepo kwa wiki mbili tu kisha nitaondoka tena aliongea Fahad.

Mi naelewa na sitaki kuingia wala kuuliza majukumu yako, kwasababu ya wewe leo ndio familia yetu ina uwezo angalau wa kusimama. Hivyo mi nakuombea kwa mungu chochote kile unachofanya kifanikiwe aliongea mzee Abedi. Leo tutaenda wote nyumbani aliongea Fahad wakitoka katika ofisi hiyo, walipofika tu mapokezi. Nataka kuongea na yule binti pale, naomba mnipe kama dakika tano aliongea na kuondoka.

Yule binti alivyoona Fahad anakwenda upande wake akaanza kutetemeka. Alikuwa ameshika kopo la sharubati akajikuta likimponyoka, pasi na watu walivyotegemea Fahad akaliwahi na kulidaka. kuwa makini aliongea na kutabasamu. Naomba unisamehe kwa tabia yangu ya awali aliongea akikwepesha macho. Usijali, ila siku nyingine jaribu kuwa mpole zaidi.

Jaribu kumuhudumia kila mtu kwa usawa aliongea na kumkabizi kopo lake la sharubati. Akarudi alipokuwa mzee Mussa na baba ake. Wakatoka katika jengo hilo, nje wakaachana na mzee Mussa. Wao wakatumia gari ya mzee Abedi na kuondoka.

Kilele cha Mlima Sumeru

Kikao cha miungu kumi na mbili kilikuwa kinaendelea, mjadala mkubwa ilikuwa jinsi ya kuiangamiza moja kwa mbili ngome ya Asura. Mimi nasema hivi, huyo mtoto niachieni mimi lazima nikumute aliongea Masya. Kwanini tukuachie wewe wakati ulitulia kipindi anaiangsha moja ya vitongoji vyao.

Kama mungu umeshindwa kutekeleza majukumu yako ipasavyo. Wewe unasema hivyo kama nani, huna hata nchi moja ambayo ipo vizuri katika nchi zako. Kazi yako nikujificha mapango na kujilimbikizia mali tu. Mabishano makali yalizuka kati ya Anubis na Masya.

Nyamazeni Indra alinguruma mpaka kusababisha tetemeko, samahani mfalme tumepitiwa tu aliongea Anubis na kuinamisha kichwa. Tulizeni jazba, kumbukeni tumekubaliana tumuache kwa miaka ishirini kabla ya kumshambulia aliongea. Ndio wengine wakajibu kwa pamoja, na hivyo ndivyo tutakavyofanya aliendelea kuongea.

Manchotakiwa kufanya ni kuwanoa vijana wenu wote, nakusudia wa pande zote mbili. Nimeshaikisha habari kwa mlinzi wa bahari saba, nina uhakika Mfalme Zeusi kashazipata habari pia aliongea Indra na kuachia tabasamu. Kama hatuwezi kumshambulia huku, basi tutamuua akiwa katika ulimwengu wake huko huko.

Hahaha! Kweli mnamuogopa kijana mdogo tu, pamoja kuwa na akili za kujiita miungu. Sikuwa nimekosea kusema kuwa nyinyi ni binaadamu ambao muko na uwezi kidogo zaidi ya binadamu wengine sauti ilisikika chumba kizima.

Asura Indra aliongea kwa hasira, punguza jazba Indra, nimekuja kuwasalimu tu. Hicho ni kivuli changu tu aliongea Asura akiwa anatembea taratibu kuelekea alipo Indra. Ukipiga hatuwa moja tu nakuuwa aliongea Sun Wu Kong. Umesikia wapi kivuli kikafa, acha upuuzu wewe ngedere kauli hiyo ikamkera sana Sun Wu Kong.

Unakasirika nini sasa, kwani wewe sio ngedere. Kajiangalie kwenye kioo halafu ndio uje hapa kutema cheche. Kwasasa nipo hapa hapa kuwapa taarifa tu, Black Star ni silaha ya mwisho nitakayoitengeza. Hiyo ni nyota inayokula mwangaza ili kuishi, kama jina lake linavyojisema.

Huyu ndio mwisho wa uwepo wenu, nawaonya tu hakuna binadamu wa kawaida atakaemuweza hata wale ambawo mnasema mumewabariki kwa kuwawezesha kutumia nguvu zenu katika mapambano. Ishini vizuri maana siku zenu za mwisho zinakaribia alimaliza kuongea na kutoweka.

Ndoto za mwenda wazimu hizo aliongea Kaminotore, Indra alikuwa kimya akimumunya maneno ya Asura. Mpaka kuwapa ujumbe huwo ni wazi kuna mambo bado hawayajui, Black Star ni nani ndio swali lililokuwa linazunguka kichwani mwake. Na kwanini katokea upande wa pili, inafahamika kama Dunia ina kiwango kidogo sana cha Qi ambacho hakiwezi hata kumfikisha mtu DAN ya tatu katika Martial Art.

Anubis, si una ndugu zako ambao wanaishi Egypt aliongea Indra na kumuangalia, ndio wapo. Waambie wamfatilia Black Star, wasiache jiwe bila kufukuliwa. Watafute asili yake, nina wasiwasi kuna kitendawili kikubwa hapa. Na tusipokuwa makini, nina hofu tutakuwa hatarini alisisitiza. Sawa mkuu nitawafikishia ujumbe alijibu Anubis. Kikao kiliendelea huku kila mtu akipewa jukumu lake. Kikao kikaisha na wote wakatawanyika isipokuwa mmoja tu.

Mtukufu mfalme nikusaidie kazi gani aliongea akiinamisha kichwa, nguo yake ikaachanikika sehemu ya kiuno na mikia tisa ikajitokeza. Kuna kazi yangu nataka unifanyie, Kitsubi aliongea Indra na kusimama, maneno yako ni amri kwangu mtukufu mfalme aliongea Kitsubi kwa unyenyekevu wa hali ya juu.

Nahitaji usafiri mpaka upande wa pili na ufanye kila liwezekanalo upate taarifa kuhusu Black Star. Nimesikia, nitaondoka punde tu nitakapomaliza akageuka na kugeukia kiumbe kinachofanana na bweha ila chenye mikia tisa na kupotea.
**********
 
Black Star 24&25
Tariq Haji
06240659

Waliwasili nyumbani na kukaribishwa ndani, mamaake alipiga vigelegele alipomuona tu. Mwanangu kwa muda mchache tu ulioondika nyumbani umekuwa kiasi hicho aliongea na kumkumbatia. Hapana mama, mbona mi niko vile vile tu alijibu, nyamaza huko, we unajuaje kama umekuwa au laa.

Mimi ndio nimekuzaa, ukiongezeka hata sentimita moja nitajuwa tu alijibu na kumfinya. Ama mtoto kwa mama hakui. Wakati wakiwa katika furaha hiyo ya muunganiko kwa mara nyingine ghafla sauti ya kichanga ikasikika.

Mama Fahad akamuachia Fahad na kuelekea chumbani, aliporudi mkononi alikuwa kitototo kichanga cha kiume. Fahad kutana na Mukrim aliongea mama ake na kutabasamu. Nimefurahi kukuona Mukrim aliongea na kumbeba. Mukrim akayulia kabisa jambo lililowafanya mpaka wazazi wao washangae kabisa, walifahamu kabisa Mukrim hakuwa na desturi ua kuwakubali wageni moja kwa moja.

Ila akiwa mikononi mwa Fahad alitulia kabisa utasema sio yeye. Mamake kuona hivyo akawaacha yeye akaelekea jikoni kwa ajili ya kumalizia maandalizi ya chakula. Fahad na babaake wakakaa sebleni wakijadili mawili matatu kuhusiana ma maisha kwa ujumla. "Mwanangu unaonekana kama umekuwa sana, vipi nimeshapata mkwe nini" aliongea babaake kwa utani.

"Hapana, ila nikipata tu utajuwa. Lazima aje hapa afundishwe mambo ya kwetu" alijibu na wote wakacheka. Fahad aliumia kudanganya lakini hakuwa tayari kwa wakati huwo kuwapasulia ukweli. Alifahamu kuganya hivyo kungehatarisha maisha yao. Na yeye hakutaka jambo hilo litokee.

"Mzee inaonekana kuna mambo hayako vuzuri" aliongea.

"Ndio lakini hayo yasikuumize kichwa nitayamaliza mwenyewe. Na mara hii itakuwa pata shila nguo kuchanika" alijibu na sura yake ikabadilika, makunyanzi machache yakajitokeza usoni pake. "Ninaamini katika maneno yako ila ikiwa watafanya lolote litakaloleta shida kwako au mama au wadogo zangu, naapa kwa mungu nitawakausha" aliongea

Tofauti kati ya Fahad na babaake ni kwamba, mzee Abedi alikuwa na uvumilivu ila Fahad alikuwa na tabia ya kutolaza damu. Ukimfanyia jambo atakulipa papo hapo. Hilo lilimfanya awe hatari kuliko babaake.

Fahad alifahamu kwa juu tu kazi aliokuwa amafanya babake enzi za ujana wake na hilo lilimpekea kumuelewa kidogo. Ila sababu ya babaake kuwa kati hali duni kiasi kile ilikuwa ni baba zake wadogo. Hilo likapelekea chuki kaki sana dhidi ya watu hao. Kama si babaake basi angekuwa tayari kashawauwa kitambo tu.

Baada ya nusu saa mama ake akarudi na kuandaa meza. Wakapata chakula cha mchana. Baada ya mlo wakakaa sebleni na kuongea mambo ya kimaisha. Ilipotimu saa tisa mchana, wadogo zake wale mapacha wakarudi shule. Siku hiyo ikajaa futaha katika familia hiyo.

Ulingo mkubwa ulikuwa ukimeremeta kwa kupambwa na mataa mwngi mno. "Karibuni mabibi ma mabwa katika mzunguko wa tatu hatuwa ya mwisho ya mtoano. Baada ya hapa washiriki wote watakaofanikiwa kuendelea watafanikiwa kushiriki katika ligi ya daraja la kwanza bayo itafanyika baada ya mwaka mmoja"aliongea MC. Uwanja mzima ukalipuka kwa shangwe.

"Mzunguko huu utakuwa ni wa ana kwa ana, washiriki wote wanaruhusiwa kutumia silaha isipokuwa bastola tu. Katika mzunguko huu wanatakiwa watu kumi tu ili waendelee na ligi ya daraja la kwanza. Hivyo mzunguko utaisha pale tu watakapobaki washiriki kumi. Niwakumbushe ti washiriki kuwa, wanaweza kuingia ulingoni zaidi ya mara moja" aliendelea kufafanua.

"Black Star, niweke kiasi gani" aliongea Don Pizallo. "Weka kiwango unachotaka, leo tutaondoka na pesa nyingi mno. Kadri unavyozidi kuweka dau kubwa, utahitaji pia kupunguza muda. Kiwango cha chini weka dola milioni mia moja, ukijisikia kuweka zaidi ya milioni mia tano.

Weka dakika moja tu, inatosha" alijibu Fahad na kutoka chumbani. Alikuwa amevaa suruali pana na flana kubwa. Chini hakuwa amevaa viatu, alikuwa peku.

"Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Katazumi Hirogawa kutoka kampuni ya Don Michael Yang na Black Star kutoka kampuni ya Don Pizallo" aliongea na washiriki wote wawili wakapanda ulingoni.

"Nimesikia hukushiriki mzunguko wa pili" aliongea Hirogawa. "Nimepita kwasababu hakuwa na mwenye uwezo wa kunifurahisha. Ni matumaini yangu utanifurahisha" aliongea na kudatisha vidole kisha akatabasamu.

"Unaonaje tukabeti kidogo, milioni mia tano ukiwa utaweza kunishinda ndani ya dakika tatu" aliongea Hirogawa.

"Nitakushinda ndani ya dakika moja, na katika dakika hiyo nitakuwa sekunde arobaini na tano ufanye mashambulizi yako. Sekunde kumi na tano za mwisho ndio nitakuadhibu. Na pia ukiweza kunifanya nisogee hapa niliposimama utashinda" alijibu Fahad na kuinuwa mkono juu.

Akaonesha vidole vitano, "mshiriki wangu atashinda ndani ya dakika moja, nawema milioni mia tano" aliongea Don Pizallo kupitia maiki iliokuwa mbele yake.

"Nakubali" aliongea Michael Yang, "kama tulivyosikia mabibi na mabwana, dirisha la kubeti limefunguliwa" aliongea MC na kuruhusu watu wamwage pesa.

"Bila kuchelewa, mpambano kati ya Black Star na Hirogawa umeanza rasmi" aliongea na kengele ikalia.

Fahad akasimama pale pale alipo, Hirogawa akamsogelea kwa kasi. Akavurumisha teke kali sana. Fahad akalipanguwa bila shida yeyote ile, "huwo ndio uwezo wako wote, kumbuka sekunde zinaisha" aliongea Fahad. "Nahofia nikitumia uwezo wangu wote nitakuuwa, na mimi nataka nikutese kwanza" alijibu Hirogawa. "Umebakiwa na sekunde thalathini tu" aliongea Fahad.

Hirogawa akaanza kufanya mashambulizi ya kasi na kila Muda ulivyokwenda ndivyo nguvu na kasi ya mashambulizi hayo ilivyoongezeka. Fahad alikuwa akiyapanguwa huku akiangalia saa.

Zilipotimia tu sekunde kumi na tano, ni kama vile alijuwa. Aligeuka kidogo kisha akaudaka mguu wa mpinzani wake. Akamvurumisha kama rungu na kumbamiza chini. Hakuuachia, akazunguka kasi na kumrusha ukutanini. Kabla hajavuta pumzi tayari Fahad alikuwa usoni kuzamisha kifuti katika kifua cha Hirogawa. Mtu huyo akaanguka chini na kupiteza Fahamu.

"Sijamuua ila akiendelea kukaa hapa atakufa" aliongea akigeuka na kuondoka. Dakika moja ikatimia, hakuna alietaka kuamini kilichotokea. Wote wakaomba mkanda ulorikodiwa urudiwe kipind Black Star ameanza kufanya mashambulizi. Hata ji wachache sana walioelewa kilichotokea.

Pambano likaisha kwa mfano huwo, Fahad wala hakusubiri kutangawazwa. Sura yake ilikuwa imekunjana, "mara nyingine mnipangie mtu anaeweza kuongea kwa vitendo na si mpiga umbeya" alijisemea akitoka kabisa katika eneo la uwanja.

Mapambano mingine yaliendelea mpaka wakabaki watu ishirini na moja. "Na sasa ndugu watazamji ni ule muda wa nani ni nani. Washiriki ishirini na wanaotakiwa ni kumi tu. Je ni kina nani watazichukuwa kumi hizo. Tusiongee kwa maneno wakati mikono ipo, niwakaribiahe washiriki wote ulingoni.

Kila mshiriki atapewa namba, ikiwa washiriki wawili watapokea namba moja basi hao watabadilishana ujuzi ulingoni. Na bahati ikiwa nzuri basi washiriki watatu watapokea namba zenye kufanana. Hao watapanda ulingoni pamoja. Pambano litakuwaje, wao ndio watakaoamuwa" alitoa maelezo.

Kila mshiriki akapokea kikaratasi chenye namba. "Namba tano" alijisemea Fahad na kurudi nyuma. Washiriki waliopata nambari moja, wasogee ulingoni. Mpambano ukaanza na baada ya dakika tano ukaisha.

Washiriki walopata namba nne wakapanda ulingoni. Mmoja kati ya washiriki hao alikuwa mwanamke. Na alipopita pembeni ya Fahad, Fahad akajikuta akitabasamu.

"Nasema hivi, kubali tu kuwa umeshindwa. Angalau nitakufanya mwanamke wangu nikutumie. Utapata ufahari wa kutumika na mtu kama mimi" aliongea mpinzani wa mwanamke huyo. "Nilikuwa napanga nikuvunje tu lakini unaonekana na kiburi sana. Nitakudanya ushindwe hata kuinuwa kijiko katika maisha yako.

Kengele ikalia na mpambano ukaanza, yule jamaa akamva yule mwanamke kwa kasi. Akajikuta akipiga hewa baada ya kukwepwa. "Ana kasi sana" alijisemea na kutabasamu. "Kitoweo kizuri ni kile kinachohangaisha, hata ukikila unakula huku umetabasamu.

Akaingiza mikono mfukoni, alipoitowa alikuwa tayari amevaa nako. Vyuma fulani hivi vinavaliwa katika vidole. "Umemaliza kuijiandaa" aliongea yule mwanamke na kutoa kitu kinachotaka kufafana na kisu lakini kilikuwa butu. "Unategemea kufanya nini na kisu kisicho na makali".

"Usiwe na haraka, utaijuwa kazi yake muda si mrefu" alijibu. Mpambano ukaendelea, yule alionesha ufundi wa hali ya juu katika kutumia silaha yake. Yule jamaa akarusha ngumi kali sana, bidada akakwepa na kufanya kama anamkatq mkononi. "Nilikuuliza awali unakusudia kufanya nini na kisu butu".

"Inuwa mkono wako", japo alipojaribu kuinuwa akashindwa. Mkono ulikuwa unaning'inia kama kamba tu. Haukuwa na kazi yeyote ile, "umenifanya n.." kabla hajamaliza kuongea, yule mwanamke kwa kasi akamvaa na kuanza kufanya kama anamkata kata. Alipoacha tu, yule jamaa akaanguka chini huku miguu na mikono ikikosa ushirikiano.

"Hichi kisu kimzungukwa Qi yangu, Qi ina sifa ya kupenya mwilini. Nilichokifanya ni kukata mishipa yako yote ya fahamu inayosafiri katika mikono na miguu yako. Nilikuahidi kuwa hutaweza kuinuwa hata kijiko. Nimetimiza ahadi yangu, uwe na maisha mema" alimaliza kuongea na kutoka uwanjani.
 
KWA LEO FARASI KASIMAMA HAPA. TUONANE KWENYE CHAPISHO LIFUATALO MKIMALIZA KUSOMA HAYA.
MKIMALIZA KUSOMA NIJULISHENI.
 

Attachments

  • _cbea0a0f-39f8-4d58-bb62-0bfb9f9573eb.jpeg
    266 KB · Views: 28
Black Star 26
Tariq Haji
0624065911

"Wale washiriki wenye namba tano, naomba wapande uwanjani kwa ajili ya mzunguko wao" aliongea MC. Fahad akatabasamu na kwa mwendo wa taratibu akaelekea uwanjani. Hakuwa na wasiwasi wowote ule. Alipanda mpaka juu na kusimama katika upande mmoja wa uwanja huwo.

Washiriki wengine wawili wakapanda, "ohoo namba tano ina watu watatu, kama tulivyokubaliana washiriki ndio watakaoamuwa wacheze pambano hili katika mfumo gani" aliongea MC.

"Sina muda wa kujadili kitu, kama mtaka nitawachukuwa wote wawili kwa wakati mmoja" aliongea Fahad.

"Aamitbha!" aliongea mmoja kati ya wale wawili. Shingoni alikuwa amevaa kitu kama cheni yenye mipira mikubwa ya mbao. Nguo aliyovaa ilikuwa kama rubegs. Alikuwa ni Monk wa kichina, alikuwa mkubwa kiasi.

"Kwanini tusifanye pambano hili kuwa tamu zaidi" aliongea mwingine. "Nakusikiliza, aamitbha" aliongea yule Monk. "Tushirikiane ili tuondoe huyu mdudu haraka kisha tupambane mimi na wewe".

"Aamitbha, wazo lako ni zuri sana. Vitoto kama hivi ambavyo vina meno ya maziwa, havitakiwi kuwa katika mjadala wa watu wazima" alijibu Monk.

"Kwanini tusiufanye ukawa mtamu zaidi, sheria za mchezo huu, ili kushindwa inabidi mshiriki akubali au awe hawezi tena kupambana au akitolewa nje ya ulingo, si ndio" aliongea Fahad akiwasogelea. "Huu mchezo uwe ni wa kufa na kupona, hakuna kushindwa kwa kukubali au kusalimu amri. Na hakutakuwa na mwisho wa uwanja".

"Kijana kujiamini kwako kutakuponza" aliongea yule mwengine. "Kunishinda hamtanishinda nataka nione watu wenye uwezo kama wenu mukoje" aliongea na kutabasamu. "Aamitabha, usitulaumu ikitokea tukakuumiza kupitiliza" aliongea Monk.

"Nawapa dakika mbili, pangeni mikakati yenu" aliongea na kurudi mpaka kwenye kingo za uwanja na kukaa kitako. Wawili hao walibaki katikati ya uwanja huwo wakijadili jinsi ya kumtwanga Fahad.

"Black Star tupo tayari" aliongea yule mwengine. Fahad akavuta pumzi ndefu na kusimama. Ila kabla hajajiweka sawa akahtukia akijibamiza ukutani, akadondoka chini na kukohoa kidogo. Akiwa katika hali hiyo, teke kali sana likaingia mbavuni na kumfanya aburuzuke.

"Aamitbha" alisikia neno hilo na kabla hajainuwa macho, akatahamaki mkono wa shingo na kuinuliwa. Akatupwa kama jiwe na kudondokea katikati ya uwanja.

"Ile jeuri yote iko wapi sasa" aliongea yule mwengine. Fahad akasimama na kukaa sawa, ila alipoinuwa tu mguu akajikuta yuko hewani kwa kasi kubwa sana. Akajibetuwa na kutuwa kwa miguu katika ukuta wa uwanja huwo.

"Garururu, huu ndio uwezo wenu wa mwisho" alicheka kidogo na kuongea akiwa aeganda ukutani hapo. Miguu yake ilichimba kabisa ukuta, alikuwa amechuchumaa. Ute laini ukimtoka mdomoni, ulikuwa umechanganyika na michirizi membamba ya damu.

"Sasa ni zamu yangu, jiandaeni vizuri" aliongea na kubonyea zaidi ukutani hapo. Mapaja yake yakaanza kutetemeka, mwili ukaanza kutoka jasho.

********
 
Black Star 27
Tariq Haji
0624065911


"Nini kinaendelea" alifika mtu mmoja ndani ya chumba cha wasimamizi na kuongea. "Kiongozi, karibu. Mbona hukusema mapema kama utakuja" aliongea Franklin akiinuka kutoka kwenye kiti. "Nani amewaruhusu Monk na Gram kushiriki katika mechi za chini" aliongea mtu huyo aliefika akionekana kukereka.

"Sisi tumepokea maagizo tu, kwamba wawili hao ndio watakaopambana na Black Star. Na hiyo ni kwasababu kati ya washiriki wote waliokuwepo, imeonekana kuwa hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kupambana nae" alijibu Artif na kuweka miwani yake vizuri.

"Mbona inaonekana kama kazidiwa, si watamuuwa"

"Hapana, ameweka masharti ya kufa na kupona, mechi mpaka mwisho. Hakuna mwisho wa uwanja wala kusalimu amri" alijibi Franklin.

"Oh! Amekamata jicho langu" aliongea mtu huyo na kuvuta kiti, akakaa na kuangalia kwa ukaribu.

Uwanja mzima ulikuwa umelipuka kwa shangwe. Don Pizallo alijikuta katika wakati mgumu sana. Kutokana na pambano lilivyokuwa linakwenda, ni wazi aliona Fahad amezidiwa. Alitamani kughairisha pambano lakini masharti yaliyokuwepo hayakumuwezesha kufanya hivyo. Alibaji jukwaani akiwa na wasiwasi tu.

Fahad akachomoka kutoka kwenye ukuta kwa kasi na kutuwa katikati ya uwanja. "Mkono wa Budha uwe nawe" aliongea yule Monk kurusha konde kali sana. Fahad wala hakulikwepa, lilituwa kifuani lakini hakusogea hata senti mita moja.

Yule Monk kuona hivyo akataka kurudi nyuma, "unaenda wapi, Aamitabha" Fahad aliongea akiwa tayari kashamsogelea. Akamtandika teke kali sana la kifua, Monk akarudi nyumaa mita kadhaa na kukohoa damu.

Gram aliekuwa mbali kidogo na Fahad akasogea kwa kasi na kurusha teke. Fahad akalidaka na kumbamiza chini. Gram akapapatuwa na kufanikiwa kujitoa mikononi mwa mtu huyo ambae wakati huwo alionekana kama mtu mwengine kabisa.

"Monk nahisi huyu jamaa mwanzo alikuwa akitupima tu. Ni muda wa kuweka uwezo wetu wote" alimng'oneza.

"Mnaongea nini, nishirikisheni na mimi" walisikia sauti ikitokea nyuma. "We! Umefi.." Gram hakumaliza kuongea akajikuta akielea hewani na kuanguka mita kadhaa. Monk nae akajikuta yupo ukutani.

"Kama hatuwezi kushinda, inabidi tuanguke kishuja" aliongea Gram na kusimama. "Monk, japo tumeambiwa tusitumie baraka zetu ila ni wazi kabisa hakuna kushinda bila kuzitumia" aliendelea kuongea.

"Ohoo! Kumbe bado kuna jambo hamjanionesha. Nahisi mumenichukulia laini sana, ngoja niwaoneshe kuwa nyingi si kitu mbele ya Mfalme" aliongea Fahad na kujibonyeza sehemu kwenye shingo upande wa kulia. Kiu yake ya damu ikaongezeka, mpaka waliokuwa wanatazama pambano hilo wakaanza kupoteza Fahamu.

"Haiwezekani binadamu kuwa na kiu kiasi hichi. Wewe na nani?" aliuliza Mono huku akijitahidi kuudhibiti moyo wake usije ukatetereka na nguvu ya mtu huyo.

"Gahahaha, tumieni baraka zenu. Nataka nione kati yangu na hao wanakuazimeni uwezo nani bora" aliongea Fahad na kuanza kutembea. Kila alipokanyaga sakafu ilipasuka na kuacha shimo.

"Nakutazamie ee Mungu nikuaminie, nipe baraka zako niweze kumshinda adui alie mbele yangu" alinuia Gram kupaka damu sehemu ya juu ya kiganja chake. Mistari kadhaa ikajichora mwili mwake. Akafyetuka kama risasi na kuruka kisha akavurumisha teke. Fahad akasogea pembeni kidogo na kumuacha apire kisha akamdaka uso na kumbamiza chini.

Haikuishia hapo, akamnyanyua na kumrusha kama jiwe. "Boom" ukuta ulisikika ukilia baada ya kumpokea Gram. Mwili wake ulitulia tuli na wala hakukuwa na dalili ya uhai tena. "Gram" Monk aliita huku machozi yakimtoka. "Naapa sitakusamehe. Nitakuuwa.

"Uwe unaweza kutikiza ahadi zako tu" Fahad alimjibu na kumgeukia, macho yalikuwa yanang'aa. Kiini chake kizungukwa maduara mawili.

Kabla Monk hajafanya kitu, "unaangalia wapi" alisikia sauti ikitokea nyuma. Ila kabla Fahad hajafanya shambulizi lake. Ngumi kali sana ilituwa usoni kwake, ilikuwa ni kama risasi ya shotgun. Ilimrusha na kumbamiza ukutani. "Inatosha, huu ji ushindi wako" aliongea mti aliefika. "Grrrr! Nzi mwengine amefika" aliongea Fahad akisimama.

Alitembea kidogo kisha akasimama na kutema damu iliyokuwa mdomoni. "Kijana inatosha" alipngea mtu huyo alokuwa kwenye suti. "Wewe ni nani kuamua kama hili pambano limeisha" alijibu Fahad akijinyoosha. "Kama hujaridhika, andika ombi kwa viongozi wa juu uombe tena pambano lakini kwa leo siwezi kukuruhusu".

"Nani anahitaji ruhusa" aliisikia sauti ikitokea chini ya sikio lake la kushoto. Ilifuatiwa na ngumi kali iliyotuwa kifuani na kumrusha mita kama tano kutoka alipo. "Nimeongea kwa upole umeshindwa kunielewa, ngoja nikufundhishe adabu" aliongea mtu huyo na kuvua koti lake.

"Francois Chaka nani alokuruhusu uingilie pambano. Hata kama Monk ni mdogo wako, hukuwa na haki ya kuingilia makubaliano yao" aliongea Franklin. "Franklin kama yeyote kati yenu anataka kufa, basi aingie uwanjani kunizuia. Namuua huyu mpumbavu hawezi kuniumizia mdogo wangu kiasi hichi" aliongea Chaka kukaza misuli yake ya juu.

Hilo likasababisha nguo alokuwa nayo juu kuchanika. Mwili wake mkubwa uliotengenezwa na misuli iliyoshiba. Ulijaa na kuwa mkubwa kama mlima. "Kabla hatujaanza tujitambulishe kwanza, mimi naitwa Francois Chaka ni mshiriki wa daraja la kwanza katika shindano hili, na leo nitakuuwa".

"Kwa hiyo nikikuashibu wewe nutakwenda moja kwa moja kwa moja mpaka daraja la kwanza, vizuri sana. Mimi naitwa Black Star, kwasababu umesema leo utaniuwa na mimi huwa sikopeshi. Jitahidi sana uniuwe kwa sababu ukishindwa kufanya huvyo wewe ndio utakaekwenda kuzimu. Na nikutahadharishe, mpaka sasa nimekuwa nikipasha tu ila kwasababu ni wewe ndio umevamia. Nitapambana sirias" aliongea Fahad.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…