RIWAYA: Black star

Black star 2: Astra 24





Vita ilikuwa imepamba moto, Fang Shi alionesha itofauti wake kutoka kwa wengine. Uwezo wake wa kutumia panga iliozungukwa na Qi ulikuwa mkubwa sana. Kuna wakati alirusha na kulifanya likate bila kulishika.



Ghafla akatahamaki akirushwa mita kadhaa kutoka aliposimama, kama sio kuwa na panga lake mkononi basi shambulio hilo lingechukuwa roho yake. Akapiga goti na kuchomeka panga kisha akacheuka damu.



"Mlindeni kamanda" mmoja wa wanajeshi, sita wenye uwezo uwezo mkubwa wakamzunguka. "Kamanda, ni bora urudi nyuma" aliongea mmoja wao.



"Mnafanya nini, mukirudi katika ulinzi ndio mnawapa nafasi ya kushambulia" alifoka Fang Shi. Lakini walikuwa washachelewa, kitendo cha kurudi nyuma na kusita kikawapa maadui zao kufanya mashambulizi ya kasi na kuwakata nguvu.



Fang Shi alijitahidi kupambana na majenerali hao wanne kadri uwezo wake ulivyomruhusu lakini mwisho akazidiwa na kuanza kusukumwa nyuma. "Hali ikiendelea hivi watanimaliza" alijisemea na kupapatua kisha akarudi nyuma na kuwachomoka ili avute pumzi.



"Unadhani unafanya nini" aliongea mmoja kati ya wale majenerali wanne na kuvurumisha mkuki kwa nguvu. Fang Shi akaupangua lakini kwasababu alikuwa amechoka sana akajikuta akitupwa mbali na upanga wake ukamponyoka.



"Nahisi huu ndio mwisho wangu" akainuka na kukunja ngumi "kama kwenda nitakwenda nikiwa ninesimama". Akakunja ngumi na kuzikaza kamq vile mtu aliekuwa akiwaambia maadui zake "bado nipo".



Wale majenerali wanne wakanyanyua silaha zao juu kwa lengo la kummaliza. "Hivyo ndivyo shujaa anavyotakiwa kuwa, kama unakwenda chini, unakwenda huku ukimuangalia adui yako usoni" sekunde chache kabla ya shambulizi kutua, akasikia sauti.



Sauti hiyo ilifuatiwa na mlio mkali mbabatizo na kuwarusha huko wale majenerali wanne. Watatu kati yao walipoteza maisha hapo hapo.



"Umefanya vyema Kamanda" aliongea Fahas akiwa kasimama mbele ya Fang Shi, akajizoa zoa na kuuangalia mgongo wa Fahad uliokuwa na picha kubwa ya ndege mweusi.



"Nilijua tu utatimiza ahadi yako, nilikuwa nakusubiri" aliongea maneno hayo kabla ya kuanguka. Fahad akamuwahi na kumdaka, akamuweka beganni na kuondoka kwa kasi eneo hilo. Safari yake ilikomea nje ya matenti ya matabibu.



"Amechoka tu, mpe kidonge cha kuzalisha Qi kisha mwacheni apumzike" aliongea akimkabidhi kwa wahusika. Hakusubiri jibu akaondoka na kuelekea katika tentu la kamanda msaidizi Lati.



"Kamanda Shi yupo katika kitengo cha huduma ya kwanza" alipofika tu akatoa taarifa. "Samahani wewe ni nani?" Aliuliza kamanda msaidizi Lati.



"Kwasasa jina langu au mimi ni nani havitakuwa na faida kwako, akiamka kamanda atakwambia kila. Mimi nahitaji watu kumi, kama ni wawindaji basi ni kuanzia nyota tano na kama wengine basi angalau wawe daraja la sutra. Na miongoni mwao awepo tabibu mmoja" aliongea Fahad.



"Unawahitaji hao wa kazi gani" aliuliza kamanda msaidizi Lati.



"Tunakwenda mbele, sisi tutatengeza njia wengine watafuata. Lengo ni kwenda kukiwinda kichwa kinachotoa amri" aliongea Fahad kwa mkazo.



Pale wakajitolea sita kuungana na Fahad, "utaondoka baada ya masaa mawili, ndani ya muda huwo watakuwa washapatikana wanne wengine" aliongea kamanda msaidizi Lati.



Saa mbili baadae.



"Nisikilizeni kwa makini, sisi tutakuwa ni kichwa cha mkuki. Tutaengeza njia kwa ajili ya wengine. Tutafanya vurugu mpaka tutakapogakikisha mstari wa mbele wa adui zetu umetawanyika, sijui itachukuwa muda gani lakini nataka niwaahidi kitu kimoja. Ikiwa mtanisikiliza basi hakuna atakaepoteza maisha. Ila kuhusu kuumia, hilo liko nje ya uwezo wangu" aliongea Fahad akiwaangalia watu kumi walosimama mbele yake.



"Kila mtu akusanye kile ambacho tu kitakuwa na msaada kwake, hakuna haja ya mizigo mingi. Tutaondoka baada ya dakika kumi, na ni vyema mkaacha vipando vyenu. Tutakwenda miguu kwa wale wenye kukimbua na anga kwa wale wenye uwezo wa kupaa".



Baada dakika kumi wakaondoka, Fahad alikuwa peke yake ardhini. Walobaki wote walikuwa wakitumia anga, walikwenda kasi sana na baada ya muda mfupi wakawasili mstari wa mbele.



"Mimi nitakuwa mbele, nitashambulia wengine watamalizia. Matabibu wote wawili mtakuwa katikati ya kundi. Uzima wenu ndio ukamilifu wa kazi yetu" aliongea na kuchomoa rungu lake lililokuwa mgongoni, lilipogusa ardhu likapasua.



Akaanza kufanya mashambulizi makali sana na kama walivyokubaliana, wengine walikuwa wakimalizia tu. Zoezi hilo liliendelea kwa siku ishirini na tatu. Ilikuwa ni purukushani mchana na usiku. Hatiamae wakamalizia kikosi cha mbele cha viumbe hao. Kazi iliwapa urahisi wengine kumalizana na wale waliobaki.



Jumla zimekatika siku thalathini tokea kuanza kwa vita hiyo, katika sehemu fulani ndani ya pori kubwa sana.



"Wanaendeleaje hao wawili" aliuliza Fahad akiingia kwenye pango.



"Wamechoka sana, wametumia karibu Qi yao yote" aliongea mmoja kati ya wale matabibu.



"Sawa, hao watapumzika kwa siku mbili. Sisi tulobaki tutaendelea na mawindo" aliongea Fahad na kutoka. Alipofika nje akawakuta wengine wakiwa wanamsubiri.



"Kamanda, tunakusikiliza" aliongea mmoja na kutema kijiti alichokuwa nacho mdomoni.



"Wanajeshi tunaendelea na kazi wakati hao wakipumzika sisi tutaendelea kuwapunguza hawa wanaharamu, tunaondoka baada ya nusu saa" aliongea Fahad na kutabasamu. Aliona kabisa moto ukiwa unawaka katika macho ya sita hao waliobaki.



Muda ulipowadia waliondoka na kuanza kufanya mashambulizi. Wale sita walijitahidi sana kuwa na kasi moja na Fahad lakini kadri muda ulivyokwenda walionesha dalili za kuchoka.



Baada ya siku mbili wakarudi katika lile pango, wote walikuwa hoi. Walikua wamechoka kupita maelezo, kila mmoja alitafuta kipembe na kujiegemeza.



"Nyie endeleeni kupumzika, mimi naendelea na kazi. Ukihsi umepumzika vya kutosha unaeeza kuja kuniunga lakini msijalazimishe" aliongea Fahad na kuondoka kwa kasi.



"Hivi huyu ni binadamu au ni kiumbe tu katika umbile la binadamu".



"Nawaza hapa amepitia mangapi mpaka kufika hapa alipofika leo"



"Hata lile rungu lake si la kawaida, kila lilipotuwa liliondoka na roho za viumbe".



"Natamani nijue hasa uwezo wake halisi".



"Usijisumbue mpaka hivi sasa anatumia theluthi tu ya uwezo wake wote, na anafanya hivyo ili iwe nafuu kwenu. Nimejaribu sana kuchungulia uwezo wake lakini ni kama kitu kisichokuwa na mwisho, kinakwenda milele na milele" alitoka tabibu mmoja ndani ya pango na kuongea.



Ndani ya eneo kubwa.



"Bwana wangu kuna kiumbe kinafanya maajabu huko, yeye peke yake akiongoza kikosi cha watu kumi amefanikiwa kupenya katika mstari wa mbele wa vikosi vyetu" alifika kiumbe mmoja na kutoa taarifa.



"Anha, huyo ndie aliyekuwa ananitatiza moyoni mwangu. Niandalie magwiji hamsini kuanzia daraja la Sutra kwenda juu, nitakwenda nao kulinda namuua huyo binadamu anaeleta shida" aliongea kiongozi.



"Nimesikia bwana wangu, baada ya wiki moja watakuwa tayari. Maana itabidi nizunguke katika uwanja mzima wa vita ili kuchagua kiwango kizuri zaidi" aliitika yule kiumbe mwengine.



"Lima, nataka na wewe uwepo katika hamsini hao" aliongea yule kiongozi.



"Sawa mtukufu Starodastu" aliitika Lima na kuinamisha kichwa, kisha akaaga na kuondoka.
 
Black star 2: Astra 25







Mwezi na nusu sasa ulikuwa umekata huku Fahad na kikosi chake wakiendelea kufungua njia. Hilo likawapa wepesi waliobakia na kufanya mashambulizi ya kasi.



"Wimbi limegeuka sasa" aliongea Fang Shi akiwa anaratibu mpango kazi mwengine.



"Ila hujanambia mtu aliekuwa mstari wa mbele zaidi ni nani" aliongea kamanda msaidizi Lati.



"Yule ni mwanachama mpya aliekuja kutoka Astra, ni mtu mwenye uwezo sana. Mpaka sasa hilo ndio ninalojua, nasubiri maelezo kutoka Astra. Yakifika ndio tutamfahamu vizuri. Ila ninachotaka kukuhusia ni kwamba, usije ukakaa upande mbaya nae maana sidhani kama katika ulimwengu kuna anaeweza kumzuia" aliongea Fang Shi akimuangalia msichana huyo.



"Sawa nimelisikia hilo, pia tumepokea taarifa kuwa kuna kikosi chenye viumbe wachache ambao inaaminika mmoja kati yao ndio kiongozi kipo njiani. Kinaelekea upande ambao Fahad yupo na kikosi chake" aliongea kamanda msaidizi Lati.



"Tuachane nao, hao watakutana na Fahad. Na mini nahisi huu wote ni mpango wa Fahad mwenyewe. Yeye kwa kutokuja mapema, alikuwa anapima uwezo halisi wa adui yetu. Pia, kwa kuenda mbele na kufanya vurugu amejifanya chambo kumtoa samaki mkubwa katika pango lake. Mi nasema hivi, huko tumuachie yeye sisi tuendelee kusafisha hawa samaki wadogo" alifafanua Fang Shi.



********



"Lina tunategemea kufika lini?" Aliuliza Starodastu, "kwasababu inabidi tutembee kwa siri ili kutomshtua adui yetu, itatuchukuwa wiki moja zaidi mpaka kufika alipo" alijibu Lima.



Akaendelea "na taarifa nilizopokea hivi punde ni kwamba, hivi tunavyoongea mimi na wewe huyo bwana anapambana peke yake. Hivyo uhakika wa kushinda upo kwetu kwasababu mpaka tukifika atakuwa kashatumia karibu Qi yake yote".



"Hilo lawezekana lakini itakuwaje ikiwa anatumia DoQi, si unajua ulimwenguni hakuna watu wagumu hao. Kwasababu wengi wana uwezo wa kunyonya Qi kutoka kwenye mazingira. Mtu kama huyo anaweza kupambana bila kupumzika wala kula kwa muda mrefu sana" alionesga wasiwasi wake Starodastu.



"Bwana wangu hilo nalo pia nimelitilia maanani lakini unadhani ni binadamu gani ana uwezo wa kunyonya Qi iliyochanganyika na majini. Mwanzo hatohisi tabu yeyote lakini baadae meridian zake zitachafuka na kuanza kupata tabu hata kuzungusha Qi mwilini mwake" aliongea Lima.



Baada ya mazungumzo hayo wakaendelea na safari kimya kimya na kwa umakini wa hali ya juu sana. Hawakutaka kuwashtua maadui zao kama walikuwa njiani, kidogo wasichojuwa ni kwamba walikuwa wakicheza ngoma aliokuwa akiipiga Fahad mwenyewe.



Wiki moja baadae, upande wa Fahad.



"Nimewaita hapa kuwashukuru kwa kujitolea kwenu, najua kama hatujapoteza mtu lakini wengi mumepata majeraha ambayo yatawachukuwa muda mrefu kabla ya kupona. Mpaka kufikia hapa mumetenda vyema lakini kundi linalokuja hamuwezi kupambana nalo katika hali yenu hiyo" alinyamaza kidogo na kuwaangalia.



Kweli walionesha kuchoka sana, kuna baadhi ili wasimame walitumia miti kwa msaada. "Nataka murudi katika lile pango ili mpumzike, kuanzia hapa nitakuwa mwenyewe na kuwaonya tu naomba hata mkihisi nakufa msitoke. Kwasababu kama hamtakufa kwa mikono ya hawa viumbe basi lipo litakalowauwa. Nakwenda kutumia uwezo wangu wote kupambana, na si kitu ambayo roho zenu zinaweza kuhimili" aliongea Fahad kupepesa macho yake.



Yalibadilika na kuwa kiini kilichozungukwa na pete nne kila upande. "Sawa tumekuelewa, sisi tunakutakia ushindi" aliongea mmoja wao na kuwaangalia wenzake. Akawapa ishara ya kuondoka.



Fahad akaweka rungu lake chini na kukaa kwenye jiwe, umbali wa kilometa kama hamsini hivi kikosi cha Starodastu kilikuwa kinakaribia.



"Kwanini umekubali tuondoke" aliuliza mmoja wao wakati wako njia kuelekea katika pango. Yule tabibu aliekubali kuondoka aliwaangalia kisha akashusha pumzi.



"Nilichokiona baada ya kumaliza ilw kauli yake ni kifo, hivi tunavyoongea najitahidi tu kusimama lakini mwili wangu mzima bado una kumbukumbu ya kile kiumbe. Kamanda Fahad si kiumbe wa kawaida, naweza sema ni mjumbe wa kifo. Njia aliyochaguwa ni kinyume na miungu tunayoamini, kwa maneno mengine Fahad ni kiumbe ambae maisha yake yameandikwa kwenda kinyume na wale tunaowaamini" alifafanua japo alielewa hakuna kati yao ambae angeelewa alichomaanisha nyuma ya maneno yake.



************



"Mumechukuwa muda sana kufika hapa" aliongea Fahad akiinua kichwa, mashavuni alikuwa na michirizi ya machozi ya damu.



"Mumenisubisha sana, koh...koh!" Akakohoa na kutema damu, mwili wake ulikuwa umeumuka kama andazi lililojazwa hamira.



"Bwana wangu nasikitika kusema kuwa kati yetu hapa, ni wewe pekee mwenye uwezo wa kwenda nae ana kwa ana. Sisi wengine tutakuwa mzigo" aliongea Lima. Ila akasikia sauti ikitokea pembeni yake, "nani aliekuruhusu uongee" kabla hajajibu kichwa chake kikapasuka na kusambaratika.



"Shenzi weee, umemuua mshauri wangu" alifoka Starodastu.



"Hahaha! Mi nilijuwa umeniletea hawa kama sehemu ya zawadi kumbe ni wanajeshi. Mi nilijua ni kafara tu" aliongea Fahad na kunyoosha mkono mbele kisha akakunja ngumi, wote waliobaki kasoro Starodastu wakaanguka chini wakitokwa damu mdomoni.



Starodastu kwa hasira akamvaa Fahad na kuanza mashambulizi, ila akajikuta akibamizwa katika miti kadhaa. "Kama huwo ndio uwezo wako basi nimekupa sifa usostahili" aliongea Fahad akizungusha rungu lake na kulikita chini.



"Hahaha! Samahani nimekuonesha upande wangu dhaifu, niruhusu nikuoneshe uwezo wangu halisi" aliongea Starodastu na mwili wake ukaanza kubadilika. Mapembe makubwa yakachomoza kichwani mwake. Mgongo wake ukachanika na kutoka mbawa mbili kubwa zilizokuwa zinawaka moto. Alitoa moshi puani pale alipopumuwa.



Bila taarifa Fahad akatahamaki akibamiza chini kama mpira wa kitenesi. Akabiridhika mita kadhaa kabla ya kugonga kichwa kwenye jiwe kubwa na kulivunja. Wakati anataka kuinuka, Starodastu akatua kifuani kwake kwa teke kali sana.



Macho yakamtoka Fahad na kucheuka damu, mifupa ya kifua ilikua imenjuka. Akapapatuwa na kuchomoka mikononi mwa kiumbe huyo mwenye hasira, "hii ni raha, vingine vyovyote isingekuwa raha" alijisemea na kung'ata mdomo wake chini ili kutuma maumivu akilini asipoteze Fahad.



Mapigo hayo mawili ingekuwa ni mtu wa kawaida basi angekuwa kashakata roho lakini sio kwa kisiki kilichoshidna gurudoza.



Starodastu akazunguka kwa kasi na kufunguwa mbawa zake kubwa, madonge ya moto yakaruka kuelekea upande aliokuwa Fahad. Fahad akarudi nyuma kwa kasi na kuyakwepa, akakaza misuli ya miguu na kufyetuka kama risasi.



Starodastu akakwepa shambulizi hilo, likatua ardhini. Eneo lilipotuwa lisambaratika na kuwa vipande vipande. "Una macho makali sana" aliongea Fahad na kugeuka kwa kasi na kutoweka. Wawili hao waliondelea kushushiana kipondo usiku na mchana bila uhuru.



Walipokuwa wakipambania paliharibika, ardhi ilipoteza sura yake ya asili. Vita yao iliendelea kwa zaidi ya siku hamsini bila mapumziko.



"Nimepoteza hesabu za siku kabisa" aliongea Starodastu akijitahidi kusimama. Alikuwa akitokwa na damu mwili mzima. Upandr Fahad alikuwa amesimama kwa kutumia msaada wa rungu lake.



"Kwanini tusimalize vita hii, unajua kabisa huwezi nishinda na wala mimi siwezi kukushinda. Tutaendelea hivi mpaka mmoja wetu atakapokufa kwa kuchoka" aliongea Fahad akikaza misuli yake tayari kwa kushambulia.



"Hata mimi nahisi tuishie hapa" aliongea Starodastu akifunguwa mbawa zake na yeye tayari kwa kushambulia. Kila mmoja aliweka kila kitu kwenye shambulio hilo akiwa na lengo la kummaliza mwenzake. Wakavaana na mtikisiko mkubwa sana, ardhi ilichimbika na shimo kubwa sana.



"Kama unataka tupambane tena, nipe miaka mitatu" aliongea Fahad akikaa kwenye jiwe.



"Sina huwo mpango, ndani ya miaka mitatu kwako nitakuwa kama funza tu. Ikiwa maisha yatatukutanisha tena, basi naomba yatukutanishe kama marafiki" alijibu Starodastu na kufunguwa mbawa zake, akaruka na kupotelea angani.



"Ikiwa yatatukutanisha hivyo basi itakuwa vizuri zaidi" aliongea Fahad na kulalia rungu lake, macho yake yakaingia kiza na kupoteza nuru.

 
Black Star 2: Astra 26







Peke yake alikuwa amekaa kwenye jabali, mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia rungu kubwa. Rungu hilo lilikuwa na wa karibu mita moja na nusu na lilikuwa na uzito mara mbili ya uzito wake.



Alikuwa amechoka sana, macho yalionesha ulegevu. Mita kadhaa kutoka alipokuwa amekaa walikuwa watu wengine wakimshangaa lakini hakuna aliethubutu kusogea, aliogopeka. Mwili wake mkubwa na mpana uliwatisha wengi. Harufu kali ya kiu ya damu iliwachafua wengi na kujitenga nae.



Alikuwa peke yake katika dimbwi zito la usingizi lililotokana na uchovu uliosababishwa na vita ya siku mia moja, mchana na usiku.



"Nahisi huu ndio mwisho wangu" alijisemea akijaribu kuinuwa mkono ajikune lakini mkono haukutii amri hiyo.



"Hahaha" alicheka ndani ya akili yake tu, hata mdomo ulikataa amri za ubongo wake.



Pasi na matarajio ya wengi katika kundi la waliokuwa mbali akatoka binti mmoja alikuwa na nywele za kijani kibichi. Mkononi alikuwa na gongo kubwa lililobeba gololi yenye rangi kama ya nywele zake.



Taratibu akaanza kumfata alipokuwa amekaa, alipomkaribia akahisi kama anaekabwa. "Tulia, niko hapa kukusaidia" aliongea kwa sauti laini yenye joto la kutoka moyoni. Akajaribu kunuwa kichwa na kumuangalia alieongea.



Macho yake yakakutana na sura nzuri, bila matarajio akatabasamu. "Mungu hamtupi mja wake, mpaka malaika aliekuja kuchukuwa roho yangu amekuja katika sura nzuri. Hata nikifa sasa sina majuto" alijisemea na kushusha pumzi.



Ile harufu ya kiu ya damu, ikakata. Hatimae akalegeza ngao yake. Kama si kuegemea rungu lake basi angeanguka. Yule binti akamfikia na kunena maneno kadha katika ulimi wa kigeni. Mwangaza wa kijani ukamzunguka na taratibu vidonda vyake vikaanza kupona.



"Mi nilijuwa nikifa naenda katika mashimo ya adhabu, ila kwa hali ya joto hili nahisi kama nipo katika bustani ya eden" alijisemea akiwa katika hali ya ndoto. Kwa mbali akahisi kama miale ya jua ikimpiga machoni. Kwa kivivu akafumbuwa macho na kukaribishwa na sura ya jangwa.



Katika mapaja akahisi umoto kwa mbali, akainamisha kichwa na kuangalia. Macho yakamtoka alipomuona msichana akiwa kalala. Kutokana na mshangao huwo ni kama vile mtu alietaka kuruka. Kitendo hicho kikamfanya yule mschana amke, "oh ushaamka" aliongea akifikicha macho.



Hakumjibu, alibaki akimuangalia tu. Akili yake ilikuwa ikifunguwa makabati ya kumbukumbu kujaribu kumkumbuka. "Unaonekana umepona kabisa" aliendelea kuongea.



"Eh n...ndio" alijibu akikwepesha macho, "afadhali maana nilikuwa sujui kama tiba imesaidia ama laa. Ila kwa nikuonavyo sasa, hakuna shaka umepona kabisa" aliongea.



Wakiwa katika mazungumzo hayo, wakasikia kelele zikitoka upande wao wa mashariki. Kelele hizo ziliambatana na watu wakitumuwa mbio. Ghafla akapita mmoja kwa kasi akiwa angani na kujabamiza kwenye jiwe.



"Habankuli" aliongea yule mschana "tukimbie hilo dudu linalokuja lina nguvu na hatari sana". Akainuka na kumshika mkono ili amuinue. "Sijakushukuru sawasawa bado, hebu kaa hapo kwenye jiwe. Nitarudi baada ta kumfundisha huyu chawa heshima".



Kwa kujiamini akainuka na kunyanyua rungu lake, "sijarudi katika ubora wangu lakini hapa nilipo panatosha kwa kumkalishi huyu mpuuzi" alijisemea na kuanza kutembea taratibu.



Ghafla mbele yake akasimama kiumbe mkubwa, alikuwa na mapembe yaliotaka kufanana na ng'ombe. Alikuwa na mikono minne, mikono mitatu ikiwa na silaha na mmoja ukiwa ngao kubwa ya chuma.



"Binadamu unadiriki kusimama katika njia yangu" akafoka kiumbe huyo.



"Inaonekana bwana wako kasahau kukufunga kamba" alijibu na kumzidisha hasira kiumbe yule.



"Nitakutwanga, nitakufinyanga finyanga mpaka ushindwe kutambulika" kiliongea kiumbe hicho.



Yule bwana aliesimama mbele akatabasamu na kuikaza mkono kisha akainuwa rungu lake kubwa. Mbele lilikuwa pana na lilipungua upana kadri lilivyorudi nyuma kama rungu la baseball.



"Acha kubweka, fanya" aliongea na kuvurumisha rubgu hilo kwa kasi. Habankuli akakita ngao yake chini, rungu hilo likakutana na ngao hiyo na kutoa mlio mkali sana. Pia mgongano huwo ukasababisha upepo wa ajabu.



"Haiwezekani binadamu hawezi kuwa na nguvu ya kunisukuma hivi" alijisemea na akiangalia alama zilizoachwa na miguu yake.



"Wewe nani?" Aliuliza.



"Huna heshima wewe, waulizaje jina la mtu baada ya kutangaza vita nae" alijibiwa.



Habankuli akanguruma kwa nguvu, kwa kishindo akamfuata huku mikono yenye silaha ilikuwa juu. Akavurumisha kwa kasi sana lakini akaambulia pakavu.



"Hujaambiwa kama ukishambulia uangalie wapi unashambulia" alisikia sauti ikitokea nyuma yake. Sauti hiyo ikafuatiwa na rungu lililotuwa nyuma ya goti la mguu wa kulia. Habankuli akakosa mihimili na na kupiga goti. "Leo sipo katika hali ya kutamani damu laa si hivyo ungekuwa ushakufa" aliongea akiwa kamshika pembe moja.



Akaweka rungu lake chini, "ngoja nikuadhibu kwa makofi leo. Hujawahi kuchwapwa vibao na binadamu, hifadhi siku ya leo katika kumbukumbu zako. Itakuwa ni siku uliodhalilika katika mkono kiumbe uliedhani ni dhaifu".



Akaanza kumchapa vibao, vilipotuwa katika uso wa habankuli vililia kama fataki. Kila kibao kilitoa mawimbi kadhaa, "nisamehe" alilia habankuli lakini wapi. Kipigo kiliendelea kumshukia kama mtu aliefumaniwa.



"Utanibughudhi tena"



"Hapana mkuu"



"Peleka taarifa kwa wenzako waambie mkinisogelea mimi ama mtu wangu yeyote wa karibu. Ukoo wenu mzima utaangamia katika mikono yangu".



Akamuachia, habankuli akainuka haraka na kutaka kuondoka. "Acha ngao yako" alisikia sauti, hakutaka kubisha, akaishusha ngao yake na kukimbia kama mbwa koko aliepigwa jiwe.



Akainyanyuwa ile ngao na kurudi alipo yule mschana, "samahani nimekuweka sana" aliongea na kutabasamu. Yule mschana alikuwa ametoa macho tu, bado akili yake ilikuwa ikichambuwa kile alichokishuhudia.



"Samahani sijakusudia kukaa kimya lakini akili yangu inakataa kuamini kama umemfanya habankuli aombe msamaha, hivi wewe ni kiumbe wa aina gani".



"Mimi ni binadamu tu" alijibu na kutabasamu.



"Mmmh! Mimi jina langu ni Nephira kutoka msitu wa wachawi" alijitambulisha mschana huyo.



"Jina langu ni Fahad kutoka Dao" alijibu na kumuangalia usoni.



"Fahad, jina laki ni la ajabu" aliongea Nephira na kutabasamu, tabasamu ambalo liliuzidisha urembo wake mara kadhaa. Fahad ikabidi ageuze sura upande wa pili.



Wakati wakiwa hapo wakafika watu kadhaa wakiwa katika vipando vyao.



"Fahad" alisikia sauti alioifahamua, akageuka na kumuangalia aliyemuita. Alikuwa ni Fang Shi akiwa na kikosi cha watu kadhaa.



Bila kuongea jambo Fang Shi akadondokea magoti na "tafadhali kama itakuwa katika kupenda kuwa, kuwa meya wa ngome yetu" Aliongea na kuinamisha kichwa.



"Simama Fang Shi, mambo hayo tutaongea baadae. Vipi wangapi tumewapoteza" aliinuka Fahad na kumshika bega Fang Shi.



"Hatuna idadi kamili lakini tumepoteza karibu waru mia tatu katika vita hii" alijibu na kuonesha sonono katika maneno yake.



"Turudi nyumbani na kuwaaga vizuri waliotutoka" aliongea Fahad na kutaka kutembea lakini mwili wake ukashindwa kutoa ushirikiano. Akayumba kidogo na kuzuia na Nephira.



"Japo nimekuponya lakini unahitaji muda ili kukusanya tena nguvu" aliongea mschana huyo na kumsaidia kukaa.



"Samahani kwa kuwa mzigo" aliongea Fahad kwa tabu huku nguvu zikiusaliti mwili wake. Akajiegemeza kifuani kwa Nephira na kupoteza fahamu.
 
Black Star 2: Astra 27



Hali ya joto lilichanganyika na ubaridi kwa mbali ukamfanya Fahad asisimke japo alikuwa usingizini. Miale ya jua iliyopenya dirishani ikampiga machoni na kumafanya aweweseke kabla ya kufunguwa macho. Mkononi kwake alihisi ameshika kiti laini chenye kubonyea bonyea.



Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, kichwani akajaribu kujiambia kuwa kitu hicho kilaini sicho anachofikiria. Lakini hata kabla hajamaliza shuka yake ikacheza.



"Sijagusa kitu" Akajisemea huku akijaribu kuutoa mkono wake sehemu uliokuwa umegusa. "Anh!" Sauti laini ya kike ikasikika kutoka ndani ya shuka.



Shuka hilo likasukumwa nyuma, kichwa kilichojaa nywele za kijani zenye kutoa aroma nzuri na kusuuza nafsi ndicho kilichomkaribisha. Mschana huyo akainuwa kichwa na kumuangalia Fahad machoni.



"Umeamka bwana wangu" Akaongea. Fahad hakujibu kitu badala yake akameza funda kubwa la mate.



Akainuwa shuka ili kuthibitisha alichokuwa anahisi, hakuwa na nguo hata moja!.



"Umelalaje bwana wangu" alirudia mschana huyo na kujikandamiza zaidi mkononi mwa Fahad.



"Unafanya nini, Nephira" aliongea akijaribu kumtoa mikononi mwake.



"Ah bwana wee, mi bado nina usingizi" alijibu na kujigeuza upande jambo ambalo lilisababisha shuka lote kutoka mwilini mwake. Fahad akashuhudia umbile maridadi la kike, kwa sekunde chache mwili wake uligoma kabisa kutii akili yake. Umbile la mschana lilithibitisha uwanawake wa Nephira. Pasi na matarajio yake, akajisogeza karibu na kukagua kiuno cha binti huyo kwa mkono wake wa kushoto.



"Bwana, niache nipumzike. Siku tatu zotw hukunipa hata nafasi ya kupumuwa" aliongea Nephira kwa sauti ya nataka sitaki. Kama ilivyo kwa rijali yeyote kuushinda mtihani wa matanio na kwa Fahad haikuwa vinginevyo. Hakuna kiungo hata kimoja kilichotii akili yake, vilifuata hisia za asili za kiume na kumfakamia bibie huyo.



Fahad anakuja kuzinduka baada ya kuguswa kifuani na mkono wenye joto. "Umepumzika vizuri bwana wangu" aliuliza Nephira akiwa anajilaza kifuani kwa Fahad.



"Nini kimetokea" akauliza.



"Umenichukuwa na kunifanya wako" aliongea Nephira na kukaa kitako, kisha akatoa shuka mwilini mwake. Chini ya kitovu alikuwa na mchoro wa ajabu ambao Fajad hakuwahii kuuona katika maisha yake.



"Jifunike na uwe na heshima" alitaka kuongea kwa kufoka lakini akili ikamsaliti.



"Hii unayoiyona chini ya kitovu changu inaitwa Sigil" aliongea Nephira.



"Sigil ndio nini?".



" Sigil ni alama ya muuganiko wa mwanaume na mwanamke, muunganiko wa akili, mwili na kiwiliwili".



"Mbona mi sijawahi kuona kitu kama hicho"



"Ni kwasababu hukuwa na muda kuukagua mwili wako, mi najua kama una mke na unampenda sana. Hiyo inathibitishwa na sigil kubwa kifuani kwako" aliongea Nephira na Fahad akajiangalia kifuani. Akakutana mchoro mkubwa ambao hakuuelewa kabisa.



"Hiyo ni sigil ya malikia wa kwanza wa moyo wako, na ni ushahidi kiasi gani unampenda. Unaweza ukahisi kama umemsaliti lakini nina uhakika hata yeye alifahamu kuwa itafika siku ambayo hutakuwa wake peke yake. Katika mkono wako wa kulia kuna alama ya jani lenye kung'ara, hiyo ni sigili yangu. Kwa maneno mengine mwili wako umenichagua mimi kuwa malkia wa pili wa moyo wako" alifafanua Nephira.



Akaendelea, "Fahad wewe huna haki ya kuchagua nani umpende na nani usimpende. Na najua unalijua hilo vyema kwasababu kuna dalili za sigili nyingine ambayo haikufanikiwa kujichora. Mwili na akili yako vinachagua ni mwanamke gani awe mwandani wako, na vinafanya hivyo kuchagua warithi wenye uwezo wa kupokea uwezo wako".



Kwa Fahad maelezo yote yalikuwa yakimchanganya akili tu, alihisi kama hadithi ya abunuasi tu.



"Huko mbeleni unaweza kuwa na wake wengi zaidi, una maisha marefu sana mbele" alimalizia Nephira kusimama, akamuinamia Fahad na kumzawadia busu jepesi la mdomoni.



********



"Fahad tulikuwa tunakusubiri" aliongea Fang Shi punde tu baada Fahad ndani. Hakuwa peke yake, walikuwepo wengine wengi ambao hata Fahad mwenyewe hakuwa akiwafahamu.



"Kuna nini, mbona mumekusanyika hivi" ilibidi aulize maana kwa yeye hakuona haja ya wote kuwa hapo.



"Ulikuwa umelala kwa siku tatu mfululizo, watu wengi walikuwa na wasiwasi sana" alijibu Fang Shi.



"Vipi? mumeshafanya harakati za msiba"



"Ndio tumemaliza jana ila tulikuwa tunakusubiri wewe ukaage kabla ya kutangaza rasmi".



"Sawa, nipelekeni" aliongea.



Fang Shu akaongoza njia mpaka lilipo jiwe kubwa, lilikuwa na majina ya watu wengi sana ambao walipoteza maisha katika vita iliyoisha. Kwa tamaduni za kule, heshima ni kuwasha kijiti maalum chenye kutoa moshi kisha unakichomeka chini. Unakiacha kinawaka mpaka kinaisha.



Fang Shi akamkabidhi kijiti na kukiwasha, Fahad akakipokea na kukichomeka chini kisha akapiga magoti.



"Mumefanya vyema, haikuwa kazi rahisi sana kuacha familia zenu na kwenda katika uwanja ambao mulijuwa wazi kuna uwezakano wa kutorudi nyumbani. Lakini mlikaza meno na kupiga moyo konde, kwa hilo mna heshimza yangu".



"Nina uhakika katika dakika zenu za mwisho, mulikiangulio kifo usoni maana hivyo ndivyo shujaa wa kweli anavyotakiwa kuondoka. Pumzikeni kwa amani, sisi tuliobaki tutailinda amani mlioipigania" alimaliza kuongea na kusimama kisha akainamisha kichwa kama ishara ya heshima.



Hali ya hewa ikabadilika ghafla na mawingu yakajikusanya, mvua nyepesi ikaanza kunyesha. Hakuna alieondoka, mvua hiyo iliwapa nafasi wale walozuia machozi wayaachie. "Pumzikeni, sitamwaga chozi" aliongea Fahad na kugeuka akaanza kuondoka.



Pasi na matarajio yao yake, ilishuka radi kali sana na kumtandika. Radi hiyo haikuwa ya kawaida, kwasababu ilipiga bila kuacha kwa karibu dakika nzima.



Ilipokata, Fahad alibakia amesimama huku mwili wake ukifoka moshi. Nywele zake ziliongezeka urefu na mwili wake ulizidi kutanuka na kuwa mkubwa.



"Hongera Fahad, umevuka daraja" aliongea Fang Shi na kutoa heshima. Akaendelea "umeingia daraja gani".



"Nimeingia daraja la Qin" alijibu Fahad, mwili wake ulikuwa ukizungukwa na Qi ya ajabu. Fang Shi alibaki akimuangalia tu. Alijaribu kutafsiri hali hiyo lakini ubongo wake ukakataa kutoa ushirikiano kabisa.



"Fang Shi unaweza kunikusanyia mtu mmoja mmoja kutoka katika kila familia kwa wale ambao wameshoriki" aliongea na sauti haikumaanisha kama ni ombi. Fang Shi akajikuta akiitika na kukubali hilo bila akili yake kutoa ushirikiano.



"Nitafanya hivyo, nipe muda mchache tu" aliongea na kuondoka, Fahad akabakia eneo hilo na kutafakari sana wakati wengine wakiondoka. Pasi na umakini wake, saa mbili zilikatika kama mchezo.



"Fahad wamefika tayari" alifika Famg Shi na kuongea, Fahad akampa ishara aongoze njia. Wakaelekea katika uwanja mkubwa, walikuwepo watu wengi sana. Vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume.



"Ahsanteni kwa kuja japo nimewaita kwa kuwashtukiza" alianza kuongea, kisha akaendelea. "Kilichotokea wakati huu kiwe fundisho kwenu kwamba katika ulimwengu wetu kila mtu anajali kilicho chake. Hata wakati huku wapendwa wetu wanapambana, walioahidi kutoa msaada hawakuja. Sina cha kuwapa ili kupoza majonzi yenu lakini nina njia ya kuwafanya muwe ngome itakayoogopeka sana" alinyamaza na kuwaangalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…