Black star 2: Astra 13
"Shameless bastard, unadiriki kuuza maisha ili uthibitishe kwamba sikuwezi" aliongea Fahad. Alionekana kutotikiswa kabisa na mabadiliko ya Gahena. Kama mwenda wazimu Gahena akamvamia Fahad na kuanza kufanya mashambulizi ya kasi.
"Ngoja nikusaidie" alionge Fahad, akakwepa shambulizi moja kisha akazunguka kwa kasi na kumchapa ile fimbo ya mgongo. Hakuishia hapo, akamzunguka na kumchapa tena na tena. Na kadri alivyozunguka ndivyo kasi na ukali wa mashambulizi yake ulivyoongezeka.
Shambulizi lake la mwisho aliinuwa fimbo yake juu kwa kuilaza kidogo na kuishusha kwa kasi. Ila kabla haijafika, Rahee akatua mbele ya Gahena.
"Imetosha usiendelee kumuadhibu kakaangu" akaongea machozi yakimtoka. Fahad akamwangalia kwa macho makali sana lakini akaamua kumsiliza.
Wakati wakiwa katika hali hiyo Gahena akaona hiyo ndio nafasi ya kummaliza adui. Kwa kutumia uwezo wake wote akamchoma Rahee panga la mgongoni na kulizamisha kwa nguvu. Likatokea upande wa pili, hakuishia hapo akazidi kulisukuma mpaka likamfikia Fahad.
"Gahena kwanini lakini" aliongea Rahee kwa tabu kidogo.
"Hahaha, katika familia yetu hatuhitaji kuwa na warithi wawili. Na nikwambie kitu, mimi sikuwahi kukuona kama mdogo wangu. Wewe utabakia kuwa mwanaharamu tu" aliongea na kutaka kulichomoa panga.
Fahad akalishika kwenye makali, akazunguka kwa kasi na kufyatua teke kali sana lilitua kifuani mwa Gahena na kumrush mpaka ukutani. "Samahni Fahad lakini (kof kof)" alitaka kuongea lakini akashindwa na kukohoa damu. Akambeba na kumepeleka walipo Yuna na wengine.
"Master Jerome, nataka uwe unamsaidia huyu kijana kwa kuingiza Qi katika mwili wake. Ukichoka utapishana na mtu mwengine lakini zoezi hilo liendelee mpaka nitakapomaliza kazi hapa" aliongea mishipa ya kichwa ikiwa imevimba. Ilikuwa ikitweta kama mapigo ya moyo.
Akarudi ulingoni na kuinuwa mikono juu, "Yuna" akaita kwa nguvu. Yuna akarusha visu viwili vilivyokwenda kugonga katika zile bangili alizokuwa nazo mikononi. Bangili hizo zikaanguka na kusababisha nyufa katika baraza hiyo.
"Baba na wengine kaeni nyuma yangu, kitakachokwenda kutokea sasa si pambano tena bali ni mauaji ya halaiki. Kama mkubwa amevurugwa" aliongea na ile silaha iliyokuwa mgongoni ikahamia mbele na kuanza kuzunguka kwa kasi mpaka ikatengeza ngao ya Qi.
Wakati huwo Gahena alikuwa akijizoa zoa, "nilikwambia kuwa ni takataka zilizooza, sasa ngoja nikuoneshe sehemu yako ni wapi" alisikia sauti hiyo ikitokea pembeni. Ikafuatiwa na kofi kali kali sana lilituwa shavu la kulia. Akarushwa juu huku akizunguka mara kadhaa, kabla hajatua akatahamaki kofi jingine.
Makofi yaliendelea, mwisho yalikuwa yakisikika kama mabomu. Kila lilipotua ulitoka moshi, kofi moja likatua kifuani na kumpaisha Gahena juu. Fahad akavuta pumzi nyingi, wakati anatua akafyatua mkono wake na kiganja kikatua kwenye kitovu. Gahena alifyetuka kwenye mkono huwo kama jiwe kwenye manati yenye mipira mahiri kabisa. Akabamiza ukutani na kucheua damu, alikuwa hatambuliki. Kila mfupa kwenye mwili wake ulikuwa umevunjika.
"Umemtia ulemavu mwanafunzi wangu" aliongea Master Dan akitua na kumuangalia Gahena ambae alikuwa hajitambui.
"Sio ulemavu tu, nimevunja dantian zake zote tatu. Kuanzia leo mpaka mwisho wa maisha yake hataweza kucheza martial art tena. Si hilo tu, atakuwa kichaa maisha yale yote. Tena hapo nimemuonea huruma" alijibu Fahad.
"Wanafunzi wote pamoja shule zote zilizokubaliana kutusaidia hakikisheni huyu mshenzi anakufa" aliongea kwa nguvu. Watu wengi wakaruka na kuingia ulingoni.
"Na mimi nasema hivi, kama hutaki shule yako itoweke ondoka uwanjani. Vinginevyo siku ya kesho haitakuwepo, nitaua walimu wote walioruhusu vijana wadogo kuja kaburini kwao" aliongea kwa nguvu.
Wakajifanya kama hawajasikia na kuanza mashambulizi, Fahad hakutaka kucheza nao. Kila shambulio alilofanya liliwaondoa kadhaa na kuwafanya washindwe kuendelea. Vilikuwa ni vilio tu uwanjani hapo na baada ya nusu saa wote walikuwa chini. Fahad ndie aliekuwa amesimama, mwili wake ulikuwa ukitoka kitu kama mvuke.
"Haiwezekani, hakuna binadamu anaeweza kupambana na watu wote wale. Hasa wakiwa daraja la jin dan na kutoka pasi na kuwa na hata mkwaruzo" alijisemea Master Dan.
"Walimu wote naomba muingie ulingoni" aliongea kwa nguvu na walimu hao wakafanya hivyo lakini hakukuwa na tofauti. Haukuwa mpambano tena bali ni kipigo kwa upande mmoja. Fahad hakuonesha huruma hata kidogo, aliwasulubu kama watoto wadogo ambao wamejuwa kutembea karibuni.
"Huu ndio uwezo wenu wote" aliuliza akimuangalia Master Dan ambae tayari kijasho kilishaacha kumtoka.
"Master Dan, huna haja ya kuingia ulingoni. Niachie mimi huyo mpuuzi" hatimae mfalme aliongea na kutuwa ulingoni kwa kishindo na kusababisha tetemeko dogo la ardhi.
"Nafasi ya yule kijana kushinda haipo tena, mfalme wa ngome hii ndie anajulikana mtu mwenye nguvu kuliko yeyote".
"Masikini kijana wa watu, laiti kama asingechokoza angeishi miaka mia kadhaa lakini ni bahati mbaya sana kwake"
Watu walikuwa wakinong'ona pembeni, Fahad alisikia minong'ono hiyo lakini wala haikumshutuwa sana.
"Unaonaje kijana ukasalimu amri, mimi kama mfalme nitakupa adhabu ndogo sana. Nitaivunja dantian yako ya tumboni pamoja na kukukata miguu na mikono yote kisha nitakuacha uishi. Hakika ya mimi ni mfalme mwenye busara sana" alijigamba mfalme huyo.
"Acha upumbavu, unaonaje ukawaambia watu ukweli pamoja na kuwatajia daraja lako halisi. Tong san ni daraja la maonesho tu kwako, eti mfalme wa majini" aliongea Fahad.
"Mfalme wa majini?"
"Ndio nani huyo?"
"Huyu kijana kweli anataka kufa, mpaka kumsingizia mfalme jambo baya kama hilo" watu waliongea.
"Mumeona nimewaambia kuwa huyu ni mwana martial art anaejufunza aina za kijini lakini mkaona si kweli. Sasa anamsingizia mfalme kuwa ni mfalme wa majini" Master Dan alitumia nafasi hiyo kuwasha moto wa chuki katika mioyo ya watu.
"We mfalme juha, ukiwa hutapambana na mimi kwa uwezo wako wote nasi jihesabu kama umekufa. Huwezi ujasiri na mimi ukiwa unatumia mbinu za daraja la tong san, kama unadhani kuficha uwezo wako na kudanganya watu ni vyema basi nasikitika sana" aliongea Fahad.
"Hahaha, kijana inabidi uchague kati ya maisha yako ama ya mzee huyu" aliongea mfalme na kuinuwa mkono juu. Wakafika walinzi wawili wakiwa na mzee Mash, alionekana kupigwa kiasi.
"Fahad usimisikilize, anajua kabisa kutoka katika kina cha wake kuwa hawezi kukupiga. Anapanga mbinu chafu ili usalimu amri" aliongea mzee Mash. "Nyamaza maluuni mmoja wee" alichezea kibao kutoka kwa mmoja kati ya walinzi.
Moyo wa Fahad ukauma sana, akahisi kama anachanwa kwa kitu kikali sana.
"Nini maamuzi yako Fahad, tunafahamu kuwa huyu mzee nae anajifunza martial art za majini ndio maana nikamkamata. Nina imani una huruma sana na wazee, kubali na usalimu amri" aliongea mfalme bila hata chembe ya aibu.
"Fahad kumbuka kilichokuleta huku, na pia kumbuka sio kila kinachoonekana kwa macho basi ndivyo kilivyo kiuhalisia" aliongea mzee Mash. Mlinzi mmoja kwa hasira akamkita kisu cha shingo, mzee Mash akaanguka chini taratibu damu zikimtoka. anamuangalia Fahad kwa macho nakavu na tabasamu kisha akanena maneno kadhaa kabla pumzi haijaacha mwili wake.
Bila mategemeo machozi yakaanza kumtoka, akadondokea magoti na kujiinamia. "Laiti ungekubali mapema tusingefika huku" aliongea mfalme akijifanya kusikitishwa na jambo lililotokea.
"Si mulikuwa mnataka vita, sasa nimeipata" aliongea na kuonua uso wake. Macho yake yalikuwa yamebadilika kiabisa. Viini vyake vilikuwa na alama.ya yin na yang, akazigonga zile bangili zilizokuwepo miguu na kuzivunja.
"Master Jerome, baba na wengine hakikisheni mnapeleka Qi nyingi kichwani. Kaka mkubwa amekasirika kweli kweli, aliwahi kunambia ikiwa atatuyumia theluthi moja ya uwezo wake basi hakuna anaeweza kusimama nae sawa katika ulimwengu wa Astra. Na kwasasa amefunguwa meridian moja, mnachokwenda kukiona sasa Fahad mwengine. kabisa" aliongea Yuna kukaa kitako.