Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nouma hadi rahaBlack star 2: Nemesis 50
Tariq Haji
0624065911
Siku ya pili mapema sana, Fahad na kikosi chake wakatoka sehemu waliokuwa wampumzika. Nje Fahad akaangaza kulia na kuhsoto na kugundua kwamba bado watu walikuwa hajachangamka.
"Mzee Maa unafahamu sehemu naweza mpata mkufunzi wa vyuma" aliuliza Fahad akimgeukia mzee huyo.
"Ndio namjua lakini watu wengi wanasema siku hizi amechanganyikiwa" alijibu.
"Kwanini"
"Kwasababu amesema hawezi kutengeza bidhaa yeyote ambayo haiifanyi damu yuake ichemke".
"Nipeleke" alitoa amri.
Mzee Maa akatangulia mbele, walitembea mpaka walipokaribia sehemu ilipo nyumba ambayo ilionekana kuchakaa sana.
"Mzee Yang ni mimi rafiki yako" aliongea mzee Maa kwa nguvu, baada ya sekunde chache mlango ukafunguliwa. Akatoka mtu mmoja alieonekana kama ametoka kulala. Kutokana na kukaa ndani kwa muda mrefu, macho yake yalijifinya na kiganja chake katika paji la uso akijikinga na mwanga wa jua.
"Mzee Maa asubuhinyote hii kuna nini tena" aliongea mzee huyo kivivu.
"Nimekuletea mteja" aliongea na kusogea pembeni, nyuma yake alikuwa Fahad.
"Mwambie aende zake kama kaja kunidhihaki kama wengine na naendelea kushikilia msimamo wangu. Sitatengeza bidhaa yeyote ile kama haitaifanya damu yangu ichemke" aliongea na kugeuka akiwa na lengo la kuingia ndani.
Wakati huwo huwo Fahad akatikisa mkono na jiwe kubwa jeusi likatokea mbele yake na kusababisha tetemeko dogo. Mzee Yang akageuka na kuliangalia jiwe hilo, akaona kama vile halioni vizuri akasogea karibu.
"Umelipata wapi hili" aliongea akionesha wazi furaha yake.
"Nimepewa zawadi" aliongea na kujifanya kama hajui thamani ya jiwe hilo. Mzee Yang akamungalia kwa macho ya mshangao.
"Kijana unataka kutengeza bidhaa gani" aliongea akisugua mikono yake kama vile nzi.
"Nyundo mbili kubwa" aliongea Fahad na kuwafanya wote waachie midomo idondoke. Walitegeme angetaka kitu kama mkuki au panga. Silaha ambazo zimezoeleka na zinatumiwa na wengi.
"Nyu... Nyu.. Nyundo, mbona unataka kupoteza chuma kizuri kwa silaha ambayo ni ya ujenzi" aliongea mzee Yang na kumuangalia Fahad.
"Utatengeza au hutengezi" aliongea Faha akikunja sura, ilitosha kusema kwamba hakuwa akitania. Mzee Yang akahisi kitu kutoka kwa mteja wake huyo lakini hahkutaka kukifatilia sana.
"Una kitu kingine unachotaka kichangnywe na chuma hichi" aliongea.
Fahad akatikisa mkono, vikatoka vito viwli vikubwa, vilikuwa ni ile mioyo ya Myor. "Unaweza kuyayusha hivi" aliongea. Mzee Yang akainama ili aviokote, kwa mshangao akastaajabu kuona kuwa vilikuwa vizito kupita maelezo.
"Hapana siwezi kuviyayusha" aliongea akionekana kuwa na huzuni usoni kwake.
"Wewe yayusha hicho chuma, hivi niachie mimi" aliongea Fahad na kuviokota kama vile havikuwa na uzito wowote ule.
Mzee Yang akalibeba lile jiwe kubwa na kuelekea katika jengp jingine lililokuwa pembeni ya nyumba yake. Fahad akawageukia wengine na kuwapa ishara wasubiri. Yeye akamfuata mzee Yang katika jengo hilo.
Ndani.
"Unataka nyundo ya aina gani" aliuliza mzes Yang.
"Yenye mikono mirefu kama mkono wangu, vingine nakuachia wewe" aliongea Fahad. Mzee Yang akaiangalia mikono ya Fahad kisha akatabasamu. Tayari kichwa alishapata wazo ambalo lingempa kitu anachokitaka.
Mbele yake kulikuwa na kitu kama chungu kikubwa, mzee Yang akalishusha liwe jiwe na kuliweka pembeni kisha akakaa kitako mbele ya chungu hicho. Akasafirisha Qi yake ndani ya chungu hicho na baada ya muda mfuniko mkubqa ukafunguka. Akampa ishara Fahad alibebe jiwe hilo na kulitumbukiza ndani ya chungu.
Ule mfuniko ukajifunga na mzee Yang akaacha kusafirisha Qi kwa muda. Akainuka na kuvua nguo yake ya juu. Fahad akastaajabu kuona mwili wa mzee huyo ulivyojijenga. Hata yeye mwenyewe akakiri kuwa misuli yake japo kuwa ilikuwa imejikata na kujiweka sehemu zake husika lakini haikujitafsiri kama ilivyojitafsiri ya mzee huyo.
Akakaa tena kisha akainua mikono yake juu, Qi iliyotoka sasa ilibadilika na kuwa moto mkali sana. Akaanza kukichoma chungu hicho. Mzee huyi alifahamj kabisa kuwa jambo kwanza ambalo halikuwa gumu sana ni kuhakikisha chuma kinayeyuka katika joto husika. Kwasababu kila chuma kila kina nyuzi joto yake ya kuyayuka.
Katika ulimwengu wa martial dao, chuma kikigawanywa katika madaraja nane. Yaani daraja la kwanA mpaka la nane, huku daraja nane kikiwa ni chuma cha kawaida ambacho nyuzi joyo za kuyayuka ilikuwa mia nane na daraja la kwanza kilikuwa ndio chuma kigumu zaidi kuyayuka.
Lakini huwo haukuwa ukweli, juu ya daraja la kwanza kulikuwa na daraja jingine lililopewa sifuri. Vyuma vinavyopatikana katika daraja hilo vilihitaji lisilo la kawaida kuyayuka. Na hicho alichokuwa anakifuabmzee Yang wakati huwo ni miongoni mwa vyuma hivyo.
Baada ya muda kidogo, moto uliozaliwa kutokana na Qi ya mzee Yang ukabadilika na kuwa buluu. Ukali wa moto huwo ukaongezeka, baada ya muda tena ukabadilika na kiwa mweusi. Ukali ukaongezeka tena, mpaka hapo mikono ya mzee Yang mpaka kwenye kiwiko ilikuwa mekundu.
Haa!
Akapiga kelele na kujaza mapafu yake hewa, ghafla moto ule mweusi ukapotea lakini sio kama ulizima. Ulipoteza rangi na kuwa kama mvuke, jashi likaanza kumtoka Fahad. "Moto wa asili" alijisemea.
Taratibu kilw chuma ndani ya chungu kikaanza kuyayuka, mpaka kikabadilika kabisa na kuwa uji. Kaa kawaida imezoeleka kuwa ili kutoa uchafu katika uji wa chuma basi, ilihitajika uji huwo ukingwe. Lakini mzee Yang hakuwa mfua vyuma wa kawaida. Akatafutisha chuma safi kutoka katika takataka ndani ya xhungu hicho hicho, "zamu yako" akaongea.
"Tayari" alijibu Fahad, katika mikono yakw uji mweupe ulikuwa unaelea, mfuniko wa kile chungu ukafunguka tena na Fahad akaumwaga uji huwo ndani ya chungu.
"Nenda nje" aliongea mzee Yang, Fahad hakutaka kuuliza kwanini. Kila mfua vyuma alikuwa na siri yake na hakuitaka ijulikane na mtu mwengine.
Kwa tambwe za haraka akatoka na kufunga mlango. Akawakuta wengine wakimsubiri kwa hamu, walipotaka kuuliza akaweka kidole mdomoni. Alijua kabisa hatua aliyofikia mzee Yang wakati huwo ilikuwa ndio muhimu zaidi. Hakutakiwa kupoteza umakini hata kidogo, akawapa ishara wasoge mbali.
Baada karibu saa mbiili, wakaanza kusikia chuma kikigongwa. Kadiri muda ulivyokwenda ndivyo nguvu ya kugonga ilivyoongezeka mpaka ikafika wakati tetemeko dogo likawa linatokea.
Saa tatu baadae mlango ukafunguliwa, mzee Yang akatoka lakini mkononi hakuwa na kitu kitu. Usoni alikuwa na tabasamu kubwa sana "kijana ingia ukachukue silaha yako" aliongea na kwenda kukaa na wengine. Mikononi alikuwa kajifunga vitambaa, Fahad akaelekea ndani.
Macho yake yakatuwa kwenyw nyundo mbili kubwa, akatoa kisu kitu na kukata katika viganja vyake vyote viwili kisha akazishika nyundo hizo na kuita. "Myor, itika".
Nyundo hizo mbili zikaanza kutikisikika, " Master" sauti nzito ikagonga katika ngome za masikio. Fahad akazinyanyua na kutoka nazo nje. Alipokanyaga tu ardhi, wingu likabadilika rangi na kuwa jeusi ti. "Master hii hatua ya mwisho, niinue juu nipigwe na radi ili kusafisha punje punje zanuchafu zilizobaki". Fahad akatabasamu na kuziinua nyundo hizo juu, ghafla radi kali sana ikashuka.
Binge la story alosto sasaBlack star 2: Nemesis 50

Nyundo hizo mbili zikaanza kutikisikika, " Master" sauti nzito ikagonga katika ngome za masikio. Fahad akazinyanyua na kutoka nazo nje. Alipokanyaga tu ardhi, wingu likabadilika rangi na kuwa jeusi ti. "Master hii hatua ya mwisho, niinue juu nipigwe na radi ili kusafisha punje punje zanuchafu zilizobaki". Fahad akatabasamu na kuziinua nyundo hizo juu, ghafla radi kali sana ikashuk
Hujawahi feli mkuu 🙏🏾🙏🏾🙏🏾Black star 2: Nemesis 51
Radi zilipoacha kupiga, Fahad alikuwa katika mavazi yake ya kifalme na kichwani alikuwa na taji kubwa la dhahabu. Ila vazi hilo lilikuwa tofauti kidogo na lile walilotengeza Nephira na wengine. Katika kila bega kulikuwa na kichwa cha kiumbe ambae hawakuwahi kumuona.
"Vazi la kifalme la Myor" sauti ilisikikaka katika ngome za masikio. Fahad akazishusha nyundo zake chini kisha akaachia pumzi ilioambatana na moshi.
Rahee na Nephira wakashindwa kujizuia na kupiga goti moja kisha wakainamisha vichwa, "umetukuka mfalme Asura, uishi maisha marefu" kwa pamoja na kwa utii wa hali ya juu sana. Mzee Yang na mzee Maa walikuwa mdomo wazi, walikuwa katika mshangao mkubwa.
"Nimepokea" aliongea na sekunde hiyo hiyo kama upepo bila hatua zake kusikika kama vile anaelea. Akafika mbelenya Nephira na kumshika kidevu, "malkia hatakiwi kupiga goti" aliongea akimuinua.
Rahee hakuthubutu hata kuinua kichwa, mbele yake kulikuwa na uwepo wa mtu aliemtukuza sana katika moyo wake. Sekunde hiyo hiyo, sauti kali sana ikasikika kutoka angani.
Krrrrrr!
Akatokea ndege mkubwa mweusi na kushuka kwa kasi mpaka alipokaribia katika mgongo wa Fahad akafungua mbawa zake na kubetua kifua. "Umetukuka mfalme Asura" sauti ikasikika.
********
Sayari ya Dai, matika kilele cha mlima Sumeru.
Indra alikuwa amekaa kwenye kiti chake, hata hivyo hakuonekana mwenye furaha. Kichwani kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa likimtatiza. Akiwa katika hali hiyo mtu mmoja akafika, sura yake haikuonesha kama taarifa aliokuwa nayo ni nzuri.
"Mtukufu mfalme" alianza kuongea ila akasita kuendelea.
"Ongea"
"Asura Karakantha amekata kamba" aliongea kwa sauti ndogo. Ghalfa viini vya Indra vikajiminya kabla mwili wake kuachia harufu kali sana ya damu.
Ah!
Alimaka na kuinuka kisha akaelekea katika mlango uliokuwa nyuma yake. Akaingia na kushuka chini kabisa mpaka katika shina la mlima huwo. Mbele yake kulikuwa na mlango mkubwa wa mbao. Akausukuma na kuingia, macho yake yakadondokea katika mwili wa mtu uliokuwa umelala chini bila uhai.
"Hahahaha! Indra mwishowe kabisa hujapata ulichokuwa unakitaka" mwangwo wa sauti ulisikika katika kila kona ya chumba hicho.
"Kama sijakipata kutoka kwako basi nitakichukuwa kutoka kwa mwamafunzi wako" alifoka.
"Hutafanikiwa" alijibiwa.
Pamoja na Indra kuwa na uwezo mkubwa kuliko wengine wote katika ulimwengu wa Astra ambao ulikusanya jumla ya sayari kumi na moja lakini hakuwahi kuridhika na uwezo huwo. Aliamini kabisa ili aendelee kuongoza ni lazima waliobaki wote wawe chini yake.
Hilo likamfanya atengeze sheria maalum ambayo ingemfanya aweze kudhibiti wenye alama za kuwa na uwezo kuliko wake.
Akasambaza maneno kuwa yeyote atakaefika daraja la Mythril basi ingebidi achague njia moja kati ya mbili. Njia ya wema au ubaya. Wote waliochagua njia ya wema walipokea insignia yake na kuwa chini yake. Na waliokataa aliwauwa. Na kutokana na hilo ndio akazaliwa Asura, ambae Karakantha ndio pekee alieamua kuenda kinyuma na matakwa yake na kuapa kuwa adui yake wa milele.
Hivyo akamtangaza kama adui wa watu wote japo kuwa imezoeleka kuwa katika ulimwengu wa martial dao mwenye nguvu ndie yuko sahihi. Ila asilimia kuwa wakaamua kuamini maneno hayo na kumfanya Karakantha kuwa adui wa watu.
Baada ya Karakantha kufa ndio wakati mchachr mbele Fahad akavuka na kuingia katika daraja la Mythril. Kwa kutumia nafasi hiyo Indra akamvuta Fahad katika ukimwengu wa mawazo na kumpa yale masharti mawili. Achague kati ya zile njia mbili, lakini akakutana na kisiki kilichoshindikana. Fahad angechagua njia ya wema basi angepata insignia ya Indra na kuwa chini yake. Na angechagua njia ya ubaya, basi angefuata nyayo za mzee Karakantha.
Yeye gakuchagua hata moja kati ya hizo na kuamua kutoka kwenye ulimwengu huwo kwa nguvu. Mpaka wakati huo Indra akawa tayari ameshindwa kupata alichokitaka.
"Kuanzia muda huu, namtangaza Fahad kuwa adui wa watu. Hivyo natoa ruhusa kwa yeyote kati yenu kupambana nae popote pale atakapomuona" aliongea kwa hasira akiwa na hasira kupita maelezo. Kauli hiyo ikawafurahisha karibu wote waliokuwa hapo. Kila mmoja kwa namna moja au jingine alitaka kumpima mrithi wa Karakantha.
Vagra.
"Natumai mlichokiona leo kitakabakia katika mioyo yenu tu" aliongea Fahad akairudisha kikombe cha chai mezani. Mzee Maa na Yang walikaa kimya, "unadhani nani anataka kufa" maneno hayo yalizunguka ndani ya vichwa vyao.
"Oh! Mzee Yang kama unataka unaweza kuungana na kikosi changu, najua umechoka kutengeza na kurekebisha silaha za kawaida. Ukijiunga na mimi utakuwa na uwezo wa kucheza na silaha ambazo umewahi tu kuzisikia katika vitabu vya kale" aliongea Fahad na kumuangalia.
Hata mzee Yang alitambua kama huwo ni mtego, lakinj hata hivyo alitamani sana kucheza na silaha zilizo nje ya fikira za watu wa kawaida.
Nephira kuona hivyo akatabasamu na kuita, "nyoika". Ile fimbo ya chuma ikatokea mkononi mwake. Akaiangalia kwa makini kisha akashusha pumzi ndefu. "Nahisi kama inahitaji kupigwa msasa hivi" aliongea akiikagua.
Mzee Yang akameza funda kubwa la mate, jambo moja alifahamu ni kwamba maamuzi yake ndio yangemponza au kumfaidisha. Macho yake hayakutoka katika fimbo aliyokuwa ameishika Nephira. Mzee huyo ni kama alikuwa na kipele kilichomuasha kila alipoona silaha ambayo hajawa kuiyona katika maisha yake.
Hatimae uvumilivu ukamshinda, akameza funda kubwa la mate kabla ya kuongea "mama naweza kuiona kama inahitaji msasa nitajua". Aliongea kwa upole huku akisugua viganja vyake, Nephira akafanya kama anasita huku akimuangalia Fahad.
Fahad akatikisa kichwa na kumruhusu amkabidhi fimbo hiyo. Mzee Yang akaipokea, macho yakamtoka. " Nikiunganae nae nitakuwa macheza na silaha za namna hii kadri ninavyotaka. Aaah! Hata nikifa, nitakufa hali ya kuwa nimetabasamu".
Akatikisa mkono, mbele yake kikatokea chungu kikubwa. Akakifungua na kuitumbukiza fimbo hiyo kisha akaanza kufanya kazi yake. Baada ya saa mbili akafumbua macho, ile fimbo ikatoka na kutua mikononi mwake.
Akairudisha kwa Nephira na kumuangalia usoni, baada ya kuipokea mwanamke huyo akajaribu kusafirisha Qi yake ndani ya fimbo hiyo.
Macho yakamtoka Nephira, tabasamu jembamba likajichora usoni kwake. "Kweli unaishi kwa jina lako" aliongea kama sehemu ya kumpongeza. Taratibu machozi yakatengeza njia yake katika mashavu ya mzee Yang kabla ya kuangukia magoti.
"Mi niko tayari kukufuata" aliongea, kwake yeye si tu kwamba angepata muda wa kukaa silaha adimu. La! Hatiamae alipata watu ambao walimuona tofauti na watu wengine, na hilo likamfurahisha sana.
"Simama" aliongea Fahad na kutikisa mkono wake, kutoka kwenye pete aliyovaa ukatoka mkataba na kutua mbele ya mtu huyo. "Weka sahihi yako kwa damu" aliongea. Mzee Yang wala hakuwaza mara mbili, akang'ata kidole gumba na kuweka alama ya damu kisha akausogeza mkataba huwo kwa Fahad. Na akatoa kisu na kukata kidogo kidoleni kisha ajaweka alama ya dile gumba. Baada ya hapo mkataba huwo ukawaka moto na kusambaratika majivu yake.
NoumaBlack star 2: Nemesis 51

🤣🤣🤣🙌Umepanga hii isomwe kwa miaka mingapi
Mkuu mwendelezo lini😭😭Black star 2: Nemesis 52
Mbali sana na mji wa Kunlun, katika kabila la uwaridi jekundu. Watu wengu walikuwa wamejaa kushuhudia majibizano yaliokuwa yakiendelea kati ya binti mwenye umri kati ya miaka kumi na tano na kumi na nane. Alikuwa akilumbana na mwanamke mkubwa sana kuliko yeye.
"Mama nimeshakwambia, mwanamke mwenye nguvu ni kwa ajili ya mwanaume mwenye nguvu. Hao wanaumw wote unaoniletea kwa ajili ya ndoa hawana tofauti na dada zangu. Watoto wa kiume warembo na walaini kama watoto wa kike. Sitaki mwanaume wa hivyo mimi" alifoka binti huyo.
"We mtoto kuwa na adabu, huwezi kuwakosea heshima wanaume" mama ake alijibu kwa hasira.
"Adabu itakuwepo ikiwa kutakuwa na heshima, mpaka atakapokuja mwanaume mwenye haiba kama ya marehemu baba yangu. Nasema hivi sitaolewa na mwanaume legevu mimi" aliongea, alionekana kuwa na hasira sana.
"Sijui kwanini nilikubali kuolewa na baba ako, mwanaume ambae hakuwa na uzuri hata kidogo. Alichokuwa anawaza yeye ni vita tu, alikuwa ni misuli bila akili" aliongea mama ake akisikitika.
"Unasemaje wewe?" aliuliza swali yule binti.
"Hujanisikia vizuri ama, nimekwambia babaako alikuwa misuli bila akili" akirudia kauli yake.
Ghafla upepo mkali sana ukavuma, viini vya macho vya yule binti vikabadilika na kuwa rangi ya damu. Kivuli cha sokwe mkubwa kikatokea nyuma yake, akanguruma. Wakati huwo huwo akahisi kama kudungwa na kitu shingoni kabla ya kile kivuli kupotea.
Akahisi uwezo wake unapotea, "hahaha! Kweli kabisa, hapa nimevuna" sauti nzito ilisikika ikitokea miongoni mwa watu. Mtu mmoja mzee kiasi akaibuka kutoka kwenye kundi hilo kubwa, mkononi akiwa na kola fulani hivi. Akafika mpaka alipo binti huyo na kumvika kola ile shingoni.
"Nimefurahi kufanya kazi na wewe" akaongea na kumrushia mama ake binti huyo kifurushi. "Tael za dhahabu milioni tatu zimo humo" Akamalizia na kuinua mkono juu.
"Yaani umeniuza kwa wafanga biashara za watumwa" aliongea binti huyo kabla ya macho yake kupoteza nuru na kupoteza fahamu.
Wakafika watu kadhaa na kumbeba kisha wakamtupa ndani ya banda kubwa la chuma. Ndani ya banda hilo kulikuwa na wanawake wengine. Yule mzee akapanda farasi wake na kuondoka, kundi la watu likafuata nyuma.
Siku chache baadae, Kunlun.
Wakati Fahas na kikosi chake wakirudi kutoka kwa mzee Yang, njiani wakapishana na msafara wa muuza watumwa. Macho ya Rahee Yakatua kwenye banda kubwa. Ndani ya banda hilo kulikuwa na mabinti wengi. Ila macho yake yakatua kwa binti mmoja aliekuwa ameshika vyuma vya banda hilo.
Fahad akamuangalia Rahee na kushusha pumzi, "kama kuna kitu kimekuvutia, nenda sisi tutakuunga baada ya kununua gari jipya la farasi" aliongea Fahad.
"Ahsante kaka mkubwa" aliongea Rahee na kuufuata msafari huwo.
"Si vizuri kumuacha akajihusisha na biashara za kununua watumwa" aliongea Nephira akionesha kukereka kidogo.
"Umewahi kumuona Rahee akitamani kitu?" aliuliza Fahad.
"Hapana lakini si kumruhusu ajihusishe na watu wale"
"Utajua kwanini nimefanya hivyo baadae" hakutaka kuendelea na mabishano na mwanamke huyi. Alifahamu fika kuwa wasingeelewana kwasababu tayari alishaakasirika.
Katika uwanja mkubwa juu ya jukwaa pana.
"Habari zenu mabibi na mabwana, siku ya leo nimewaletea bidhaa nzuri na lukuki" aliongea yule mzee kwa nguvu na watu wakaanza kukusanyika. Rahee alikuwa mbele kabisa, macho yake hayakutoka kwa binti aliekuwa ameshika vyuma hata mara moja.
Watumwa wote wakatolewa kwenye mabanda na kuoandisha katika jukwaa hilo. Wanaume walikuwa mbele na wanawake wakafuata nyuma.
"Bila kuchelewa mabibi na mabwana, zoezi la mnada wa watumwa limeanza" aliongea kwa nguvu. Mtumwa mmoja baada yaa mwengine akaletwa mbele na kupigwa mnada. Watu wala hawakujali kama walio mbele yao walikuwa binadamu kama wao. Waliendelea kupandishiana bei wakigombaniana kuwanunua wanadamu wenzao, waliwaona kama bidhaa tu.
Baada ya karibia nusu saa, wanaume wote wakawa tayari wameshauzwa. Bwana yule akawaagiza vijana wake wakawabhi kwa wahusika wao na kukusanya pesa.
"Wanaume ule muda mliokuwa mnausubiria kwa hamu umefika, wale ambao vigori watakuwa mwisho" aliongea na shangwe kubwa zikazuka. Wanawake wakaanza kuuzwa, wale wa mwanzo walikuwa bei za kawaida. Na wengi walinunuliwa na watu wenye kipato cha chini ambao hawakutaka kushindana na watu wenye madaraka na pesa.
"Sasa zinazofuata ni bidhaa adimu" aliongea yule mzee na kuinua mkono. Mmoja kati ya wanawake watano waliokuwa wamebaki akaletwa mbele. Baada ya mashindao ya muda hatimae akauzwa, hali iliendelea hivyo alipobakia mmoja.
"Huyu ndie atakaefunga biashara kwa leo" aliongea, yule binti akaletwa mbele.
"Kutokana na bidhaa hii kuwa ya hali ya juu sana, bei ya kuanzia itakuwa tael za dhahabu milioni nne" akainua mkono juu akiashiria mashindano yamefunguliwa.
"Jamani, mimi ni mtoto meya wa mji huu, natumai mtanipa sura na kuniachia huyu mtumwa" sauti ya kukwangua ilisikika. Ilitoka kwa kijana mtanashati mwenye mavazi ya kupendeza.
Watu wote wakaogopa hata kujibu kutokana na kujua desturi ya mtu huyo. Wakati huwo kila mtu alikuwa ameshakata tamaa, "milioni tano" sauti ikasikika.
Awwwe!
Kundi zima likamaka na kuangalia ni nani aliechoka kuishi. "Milioni sita" alioandisha dau yule kijana wa meya.
"Milioni tisa" Rahee akakomaa.
Yule kijana wa meya akataka kupandisha dau, akazuia na mlinzi wake. "Master, huna haja ya kuendelea kupambana nae. Muache amnunue kisha tutamuua na kumchukuwa, huoni kama utakuwa umeokoa hela yako nyingi" aliongea mlinzi huyo. Tabasamu jembamba likajichora usoni mwa kijana huyo na kuamua kukaa kimya.
"Tisa mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu, ameuzwa" akaongea mzee yule. Rahee hakutaka kusubiri, kwa hatua kubwa akatembea mpaka juu ya jukwaa hilo. Akatoa noti tisa za dhahabu na kumkabidhi yule mzee, yule binti akamuangalia Rahee kwa machi makali.
Hakujali, akainama na kwa mkono mmoja akamuinua na kumuweka begani kabla ya kuondoka. Alioofika chini tu akazungukwa na watu wengi waliokuwa na silaha mikononi.
Wakati huwo huwo, Fahad na kikundi chake nao wakawasili. Nephira akataka kuingilia lakini Fahad akamuwekea mkono na kumzuia.
"Kijana master wangu ametokea kumpenda huyo mwanamke, anakushukuru kwa kumnunulia na sasa anataka aondoke nae" aliongea mzee mmoja alievaa kofia ya ukili.
"Hahahaa!" Rahee akacheka kwa nguvu, na kuongea "mtoto mrembo unatakiwa ujue mwanamke unaemuweza".
Kauli hiyo ikamshtu mpaka yule binti, Rahee akamshusha na kupita mbele yake. Akavua nguo yake ya juu na kubaki kifua wazi, akaitumia nguo hiyo kumfunika binti huyo kifuani.
"Katafute mrembo mwenzio, mwanamke ngangari ni kwa ajili yetu sisi wanaume ngangari" alijibu, kwa mara ya kwanza hata Fahad anaushuhudia mwili wa Rahee. Mgongo wake mkubwa ulitoa kivuli cha mlima nyuma yake.
"Subiri kidogo nimtengeneze huyu mtoto mzuri na warembo wenzie" aliongea na kutabasamu, yule binti akabaki ametoa macho tu.
Black star 2: Nemesis 53
Yule mfanya biashara ya kuuza watu akavutiwa sana na mwili wa Rahee. Kichwani mwake akaanza kuwaza faida tu, akatoa kipini kidogo mfukoni na kutaka kumrushia rahee. Wakati huwo akahisi mkono begani, "ukipata mawazo yeyote utakufa" sauti ya Fahad ikanguruma. Alipogeuka hakukuta mtu nyuma, hakuna hata mmoja alieona hilo, si Nephira sio wengine.
Yule muuza watumwa akajikuta akitokwa na jingi, akairudisha sindano yake mfukono na kutulia. Alihisi kama jinamizi limemuinamia alipoguswa na Fahad.
"Umesema nini wewe?" aliuliza yule mzee mwenye kofia ya ukili.
"Hujasikia au vipi, huyu mwanamke anastahili mbavu ya maana sio hicho kimburu hapo. Unataka kuuharibu mwili wake mzuri kwasababu ya hamu zako za kimwili" aliongea na kutunisha misuli yake. Mgongo wake uliokuwa mkubwa toka awali ukazidi kutanuka na kuchora alama ya kipepeo kwenye kivuli.
Yule mzee mwenye kofia ya ukili akawaoa ishara watu wake, kwa kasi wakamvamia Rahee. Ila kabla hawajafika, Rahee akapiga hatua moja mbele na kubonyea kidogo kama vile wanamichezo ya masumbwi. Alipoinuka akavurumisha konde la mkono wa kulia kabla ya kugeuka na kuvurumisha jingine la mkono wa kushoto.
Hakuwapa hata nafasi ya kufikiria, akanesa kulia na kuchapa ngumi ya chembe. Wakati huwo huwo kuna wengine walikuwa wakimfata yule binti. Macho ya Rahee yakazunguka na kufika kwenye vipembe. Kwa kasi ya ajabu akazunguka na sekunde hiyo hiyo akafika pembeni ya binti huyo na kuachia teke kali sana lililotua shavuni mwa adui yake na kufanya kichwa kizungunguke mara mbili na kutupwa huko.
Akaachia pumzi iliyotoka na moshi mweupe, "ukimgusa unakufa" akanguruma. Kati ya kumi waliokuwa wamzunguka, wawili walikuwa wamekufa na wawili wengine walikuwa wamepoteza fahamu.
Walibakia nane pamoja na yule mzee mwenye kofia ya ukili pamoja na mtoto wa meya. "Rudini nyuma, hamumuwezi huyo" aliongea yule mzee mwenye kofia ya ukili na kupita mbele. Akachomoa upanga wake na kuushika kwa mikono miwili. Akavuta pumzi nyingi, Qi ikaanza kutiririka na kuelekea kwenye upanga huwo.
Rahee akaachia tabasamu na kukutanisha viganja vyake, mwili wake ukazidi kutanuka. Viini vyake vikabadilika rangi na kuwa vya dhahabu. Nyuma yake kivuli kikubwa kikajichora, king kong. Sokwe kubwa jeusi likaonekana, likafungua mdomo wake na kunguruma.
"Njoo" aliongea Rahee na kukaza miguu yake, misuli yake ikatutumka na weigong ikaanza kunyonywa na kuingia katika mwili wake. Yule akafyetuka kama risasi, ncha ya upanga wake ikiwa imetangulia na kulenga shingo ya Rahee.
Clang!
Upanga huwo ni kama ulikutana na chuma cha pua na kukatika vipande kadhaa. Kabla mshangao wake haujaisha ngumi yenye kasi kama ya risasi ikatua tumboni. Kwa sekunde chache ni kama kila kilikuwa katika mnato. Mzee huyo akavurumishwa kama jiwe lililotoka kwenye manati yenye mipira madhubuti na kubamiza katika ukuta mkubwa.
Mtoto wa meya akabaki ametoa macho kama mjusi alobanwa na mlango. Fahamu zake zilirudi baada ya kuhisi kitu chenye kasi kubwa kikitua katikati ya miguu.
Plop!
Vilitumbuka vitu flani hivi na kusababisha shoti kali sana kwenye ubongo wa mtu huyo. Rahee akashusha mguu, ulipokanyaga tu chini akazunguka kwa kutaka kuachia fataki nyingine.
"Inatosha" aliongea Fahad kwa sauti kubwa, sentimita chache kabla ya teke hilo kutua shingoni mwa mtoto wa meya likasimama na kusababisha upepo mkali sana. Fahad akafika pembeni ya Rahee na kumgonga maeneo kadhaa hivyo kuzifunga baadhi ya meridian.
"Kaka mkubwa" aliita huku viini vyake vikirudi katika ya kawaida. Wakati huwo huwo Nephira akafika kwa yule binti na kumpa mkono. Akasita kidogo na kumuangalia Rahee, Rahee akajibu wasiwasi huwo kwa tabasamu ndipo yule binti akaupokea mkono wa Nephira.
Fahad akamuangalia Nephira na papo hapo wote wawili wakatoeka kama vile hawakuwepo tokea mwanzo.
Katika uwa wa nyumba fulani.
"Rahee tulia basi, akitoka si utamuona" aliongea Fahad akipata chai ya majani ya dawa. Rahee alikuwa akihangaika huku na kule kama vile baba aliekuwa na mke alietaka kujifungua.
Mlango ukafunguliwa, Nephira akatangulia nyuma yake akafuata msichana aliependeza sana. Rahee akajikuta akitokwa na damu za pua. Fahad akamuangalia kijana wake kisha akatabasamu. Akasimama na kumfanyia ishara Nephira ishara ya kumfuata. Wakawaacha yule binti na Rahee wakiangaliana.
Rahee akabaki ametoa macho asijue wapi pa kuanzia, "jina langu ni Rahee" aliongea akichezea kichogo chake kwa mkono.
"Anusha" aliongea yule binti akiinamisha macho yake chini, japo alikiwa akipiga kelele kuwa ataolewa na mtu mwenye nguvu kama baba ake. Lakini mbele yake alikuwa mwanaume aliemzidi babako katika kila kitu.
Rahee akatoa kitana alichoachia na mamaake na kumpatia. Anusha hakukipokea badala yake akageuka na kungua nywele zake. "Nichanw nywele" akaongea na kukaa katika kiti.
"Waangalie makinda wanavyoota mbawa" aliongea Fahad aliekuwa anaelea juu akiwa amemshika Nephira kiuno. "Ile ndio sababu kwanini niliamuachia Rahew ashiriki katika lile tukio. Katika ulimwengu huu ni vigumu sana kupata mtu ambae ana kila kitu unachokitaka. Lakini jicho moja tu Rahee amefanikiwa kuona asili hasa ya Anusha" aliongea.
Baada ya muda Fahad na Nephira wakaelekea chumbani kwao kupumzika wakimuacha Rahew na Anusha wakiendelea kuongea huku Rahee akiwa anamchana nywele.
Asubuhi siku ya pili.
Rahee anafungua macho kivivu, akamfunika Anush vizuri kabla ya kuvaa nguo zake na kutoka nje. Macho yake yanatua kwa Fahad ambae alikuwa mgongo wazi akifanya mazoezi.
"Karibu" aliongea Fahad na kumuangalia Rahew ambae sura yake ya kitoto haikuwepo tena. Sasa alionekana kupevuka zaidi, hata hewa iliyomzunguka ilitoa viashirio vya ukubwa.
"Ahsante" alijibu na kuvua nguo yake ya juu na kusimama pembeni ya Fahad.
"Niangalie kwa makini, kuanzia leo nitakuwa nakufundisha martial art ya Asura" aliongea Fahad.
"Lakini hiyo si ndio martial art yako" akauliza.
"Awali ilikuwa hivyo lakini saa hivi haina faida tena kwangu. Kuanzia sasa nitakuwa najifunza martial art niliyoitengeza mwenyewe, Black Star Art. Hivyo wewe utakuwa mrithi wangu kwa martial art ya Asura" aliongea Fahad.
"Nipatie muongozo kaka mkubwa" aliongea Rahee.
"Unajua kwanini nimesubiri mpaka sasa hivi kabla ya kukufundisha".
"Ulitaka uonje ladha halisi ya maisha kabla ya kujifunza. Mwana martial art yeyote anakuwa uwezo mkubwa pale anapojua kuwa kuna maisha anatakiwa kuyalinda kwa hali na mali. Kwangu mimi nyinyi wote ni muhimu sana ila kwako wewe kuanzia sasa kila maamuzi utakayotaka kufanya mfikirie Anusha kwanza ndio uamue".
Rahee alikuwa akimsikiliza Fahad kwa makini bila kutambuwa kuwa tayari alisharithi martial art ya Asura.
Anusha anatoka ndani, mbele yake watu wawili walikuwa wamesimama miili yao ya juu ikiwa wazi huku ikitikisika kushoto na kulia. Aliutambua mgongo wa Rahee lakin pembeni yake hakukuwa na binadamu wa kawaida.
"Mtu na mdogo wake, wanyama wawili wasio wa kawaida" sauti ya Nephira ikasikika akiwasiki pembeni ya Anusha.