Riwaya; CONNECTION

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
RIWAYA YA CONNECTION


Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Riwaya; CONNECTION
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300
Maandishi ya Robert Heriel Kwa Lugha ya Kiswahili. Hairuhusiwi kunakili na kusambaza kazi hii bila ruhusa ya Mwandishi.
TAIKON PUBLISHERS.

CONNECTION Ep 01
WAHUSIKA

1. Peter Mirambo
2. Kalage Nyundo
3. Lucy Njama
4. Koloa Katani
5. Julieta RangiMoto
6. Beatrice Saimon
7. Amanda Ka
8. Amini Boko
9. ( Na wengineo)

DAR ES SALAAM
Ni nje ya jengo refu la Ghorofa, Asubuhi majira ya saa moja kasoro, watu kadhaa pamoja na polisi walikuwa wamezunguka Maiti ya mwanamke iliyopasuka vibaya matumbo yakiwa yamemwagika nje na damu zikiwa zimetapakaa pale chini. Polisi waliendelea kufanya kazi yao kwa kuzungushia eneo lile utepe maalumu kwaajili ya uchunguzi wa tukio lile ambalo lilikuwa la kutisha na lililoacha hofu, huzuni na taharuki kwa kila aliyekuwa shuhuda. Alikufa kifo kibaya sana.. Kadiri muda ulivyosonga ndivyo watu walivyokuwa wanazidi kuongezeka eneo lile.
Nini kimetokea, ilikuwaje, nini kimempata mwanamke mrembo kama huyu ambaye licha ya kuharibika vibaya lakini bado uzuri wake haukuweza kupotezwa. Maswali mengi kwa kila aliyekuwa eneo lile yalikuwa yakizichaji akili za mashuhuda. Huku baadhi ya mashuhuda wakianza kugeuka watunzi wa kusimulia tukio lile.
“ Mrembo kama huyu hawezi kujirusha kwenye jengo hili. Nini kimfanye ajiue, kwanza anaonekana maisha safi. Lazima kuna mkono wa mtu. Huyu kasukumwa ghorofani” Kijana mmoja ambaye angetambulika kama dereva bodaboda alikuwa akiongea ongea huku akiwatazama Polisi waliokuwa wakihangaika kila mmoja na kazi yake. Polisi wengine walikuwa wakipiga picha kila jambo waliloona linafaa kwa kuweka kumbukumbu. Mwanaume mmoja aliyevalia kiraia alikuwa akiandika jambo Fulani kwenye kidaftari chake. Polisi Mwingine alikuwa akiukagua mwili wa Yule mwanamke aliyekufa akiwa amevalia gloves mikononi. Polisi mwingine alikuwa ameshaita Gari ya kubebea wagonjwa.
“ Acha ujinga! Unaakili sawasawa? Angekuwa Dadaako au mkeo ungempiga picha? Kuwa muungwana” Polisi mmoja alifoka huku akimnyang’anya simu kijana mmoja aliyekuwa akirekodi lile tukio. Kisha akaipiga chini kwa hasira, ile simu ikapasuka, na isingefaa kwa matumizi. Jambo hilo likafanya wengine waliokuwa wakirekodi tukio lile kuficha simu zao.
“ Nisamehe Afande. Nisamehe sana nakuomba” Yule kijana alikuwa akimsihi Polisi ambaye alikuwa amemkwida. Yule Polisi akamtazama Yule kijana kwa macho makali kisha akamsukuma huko. Yule kijana akaanguka chini.

“ Afande, hamkufanikiwa kupata simu yake?” Mwanaume mmoja aliyevalia kiraia aliuliza, ndiye Yule aliyekuwa anaandika kwenye kidaftari. Tofauti na Askari wengine waliokuwa wamevalia sare. Askari huyu hakuwa amevaa sare, alikuwa amevaa Suruali ya kadeti ya rangi ya ugoro, Tisheti nyeusi yenye kola, kapero ambayo ilificha Draid zake ndogo zilizoko kichwani. Jina lake ni Peter Mirambo, Jasusi na Komando ambaye taifa lilikuwa linajivunia kuwa na mtu wa aina yake.
“ Inashangaza Mkuu. Hatujaona simu yake” Afande mmoja akasema.
“ Sawa. Nafikiri alianguka pengine kuangushwa kutokea pale” Peter Mirambo akasema huku akatazama juu, watu wote eneo lile pamoja na askari nao wakanyanyua nyuso zao kutazama kule alikokuwa anaonyesha. Muda huo Gari ya kubebea wagonjwa iliyokuwa inapiga ving’ora ilikuwa ikiingia watu wakiwa wanaipisha. Baada ya gari ya wagonjwa kusimama, mlango wake wa nyuma ukafunguka kisha kitanda chenye matairi kikateleza mpaka chini. Alafu wanaume watatu waliovalia makoti ya kidaktari waliokuja na gari ya wagonjwa wakashuka, wakiwa wamevaa Gloves mikononi mwao wakaubeba ule mwili na kuupakiza kwenye kile kitanda chenye matairi, kisha wakauingiza ule mwili ndani ya gari kwa usaidizi wa polisi.

Vyombo vya habari vikubwa na vile vidogo vilikuwa vimeshapata habari hiyo. Vilikuwa vikikimbizana kufika eneo lile. Huku waliokwisha kutangulia wakijaribu kupata fununua na habari za kile kilichotokea.
“ Bado ni mapema mno. Hatuwezi kusema amejiua au kauawa. Jeshi la Polisi litatoa taarifa rasmi baada ya uchunguzi. Ila kwa sasa tunaweza kusema aliyekufa katika tukio hili ni mwanamke ambaye jina lake halijajulikana bado, umri wake upo kati ya miaka ishirini na nne mpaka ishirini na saba. Mweupe. Tunaomba wananchi muwe na utulivu katika wakati huu huku taratibu zingine za kipolisi zikiendelea. Nitoe rai kwa yeyote ambaye anaishi na mwanamke mwenye sifa nilizozieleza anaweza kuja kituoni kisha tutaenda kwaajili ya utambuzi” Kamanda Mkuu wa Dar akamaliza.

Picha na video za kutisha na kuhuzunisha za maiti ya Yule mwanamke aliyekutwa chini ya ghorofa zilikuwa zikivuma na kusambaa kwa kasi mitandaoni. Huku wengine wakilaani kwa kitendo cha watu kurusha picha na video hizo mtandaoni ambapo ilionekana kama ukosefu wa maadili. Kwa upande mwingine waandishi na waandaji wa maudhui mtandaoni waliiona kama fursa ya kujipatia fedha. Yalizuka makundi mawili ya wachangiaji wa maoni huko mtandaoni juu ya tukio la kifo cha Yule mwanamke. Kundi la kwanza lilikubali kuwa mwanamke Yule alijirusha ghorofani. Huku kundi jingine likikataa hoja hiyo kwa kusema kuwa mwanamke Yule aliuawa. Basi ilimradi kila mtu na uhuru wa kutoa maoni na vile akili yake ionavyo.
************

“ Siwezi kukusaidia katika hilo. Wewe mwenyewe unafahamu unachoniomba ni kosa kisheria. Unataka nivunje sheria?” Akasema,
“ Nafahamu profesa, lakini nitafanya nini? Wewe pekee ndiye wakunisaidia?”
“ Huna chakufanya zaidi ya kukubali kuwa umefeli kozi hii na itakupasa urudie mwakani. Wakati huo wenzako watakuwa wapo mitaani wakitafuta kazi, huku wengine wakiwa tayari wamepata kazi. Wewe utarudi hapa kukimbizana na coursework na vimbweta” Profesa alikuwa akisema hayo huku akimtazama Lucy Njama, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika kitivo cha sheria.
“ Hakuna njia yoyote ya kunisaidia Profesa?” lucy akauliza kwa masikitiko huku akimtazama Profesa kwa macho ya kutaka huruma.
“ Unamaana gani Lucy?”
“Nipo tayari kufanya chochote utakachoniambia, hata kutoa pesa nitatoa Profesa” Lucy akasema huku akimtazama Profesa, kisha akaendelea,
“ Prof nipo tayari, namaanisha nipo tayari hata unambie nikupe hii..” Hapo akawa amesimama, akawa anajidengulisha na kuuonyesha urembo wake.
“ Uko serious Lucy?” Profesa akasema huku akiutazama mwili wa Lucy ulivyokuwa unavutia. Lucy alikuwa mwanamke mrembo sana. Alikuwa mzuri mwenye umbo namba nane, mwenye macho mazuri ya kisu, mwenye rangi nyeupe. Usingekataa kama ungemwona Lucy yakuwa ni moja ya wanawake wa kiwango cha juu cha uzuri ambaye uzuri wake haukuwa mbali kufanana na malaika.
“ Nipo Serious Prof, wewe niambie unahitaji pesa au penzi. Nitakuwa mwaminifu katika kuhakikisha unafurahia ilimradi unisaidie” Lucy akasema, wakati huu aliamini kuwa Prof ameshaingia kwenye mtego wake. Lakini haikuwa hivyo.
“ Mimi sipo kama unavyodhani binti. Ni kweli wewe ni mwanamke mzuri. Lakini uzuri wako hauwezi kushinda heshima niliyonayo. Ninajiheshimu, ziada ni kuwa mimi ni mwanaume bora ninayeweza kushindana na tamaa ya mwili. Mbali na hayo, wewe ni kama binti yangu”
“ Profesa sijasema wewe sio mwanaume bora, wala sijasema wewe hujiheshimu. Nakuona kama mwanaume bora ambaye unaweza kunipa msaada. Hilo tuu ndio naomba. Sahau kuhusa nilichokisema, tena uniwie radhi” Lucy aliongea kwa unyonge baada ya kugundua kuwa Profesa hakushawishika na ofa aliyoitoa.
“ Njia pekee ilikuwa kusoma, mimi nilishamaliza kazi ya kukufundisha. Kozi yenyewe inaitwa Criminology. Unataka nifanye uhalifu? Nimekuwa Profesa wa sheria kwa sababu kuu tatu. Mosi, nilikuwa napenda haki na kuchukia uhalifu na dhulma. Hii ikanifanya sio tuu nisome sheria bali kuwa mwalimu wa sheria ambaye nitawafundisha vijana na mabinti kama wewe waweze kusimamia na kulinda haki katika jamii. Pili, Kwa sababu ninaakili na ninaimudu taaluma hii. Mwisho, napenda kuona haki inatendeka hasa ikiwa katika njia yangu. Binti, ninasikitika kusema kuwa sina lolote la kukusaidia. Zaidi ninahasira kwa kuwa sijivunii wewe kuitwa mwanafunzi wangu. Ni haki yako kurudia mwaka, huna ziada..” Lucy akagonga meza kwa hasira kisha akakaa na akasimama akiwa anamtazama Profesa kwa hasira, akasema “wewe ni panya mdogo mbele ya Paka. Tutaona kama mimi na wewe nani atashinda katika hili” alafu akatoka na kubamiza mlango.
************

Ilikuwa imebaki juma moja ili wanachuo waingie katika mitihani ya mwisho ya kufunga mwaka. Lucy bado hakuwa anajua hatma yake. Ingawaje Profesa alikataa katakata kumsaidia lakini haikumfanya kukata tamaa. Lucy alikuwa akijiamini sana. Uzuri wake wa ajabu, rangi yake nyeupe ambayo ilikuwa rangi inayopendwa na wanaume wengi wa kitanzania ilichochea jeuri yake. Umbo lake lenye mfanano na namba nane liliimarisha kiburi katika nafsi yake. Asingejiamini bure, lilikuwepo jiwe kuu la msingi ambalo alilitegemea katika kuhakikisha mambo yake yanaenda. Jiwe hilo ndilo lililomsaidia kwa miaka yote tangu akiwa mwaka wa kwanza mpaka hivi leo yupo mwaka wa mwisho. “ Profesa Saimon hawezi kunishinda. Atajua mimi ni nani. Kama alizoea kuwakazia wengine kwangu amekikwaa kisiki. Kwanza nimemfanyia upendeleo tuu. Nitamwonesha” Lucy alikuwa akiwaza akiwa mwenyewe ameketi katika Moja ya Fukwe nzuri za kulipia majira ya saa moja jioni, mbele yake ikiwepo meza yenye vinywaji. Akiwa anachati na Dora ambaye ni rafiki yake anayesoma naye chuoni kozi moja. “Shoga huyo profesa ndivyo alivyo. Mwaka jana wali carryover watu arobaini. Sidhani kama kama utafanikiwa” Ujumbe kutoka kwa Dora alikuwa akiusoma Lucy. Naye akamwandikia; “Subiri utaona. Mimi ndiye Lucy. Hapa amekikwaa kisiki. Utaniambia” Akaituma, kisha akaiweka simu yake mezani alafu akatoa kioo kwenye mkoba akaanza kujiangalia kwenye kioo na kujiremba mahali alipoona hakuko sawa. Lucy alijipenda sana.

Baada ya kujiridhisha kuwa amekaa sawa Akairejea simu yake kisha akabonyeza bonyeza kwenye kioo likatokea jina la Mhe. Casto Baruani ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, wakati akibonyeza bonyeza mbele yake akasimama kijana mmoja mwenye urefu wa kati, mweusi ambaye upaa umemuanza kwa mbali. “Naweza kuketi?’ Yule kijana akasema huku akimtazama Lucy aliyekuwa kaboreka, Lucy akamtazama kwa macho ya koboreka kisha akaendelea kubonyeza simu na kuiweka sikioni. Yule kijana akawa amesimama tuu asijue chakufanya, “ Sorry Cute May i sit here..” kabla hajamaliza kuongea Lucy akaanza kuongea kwenye simu.
“ Hello Honey! Nimefika… uko wapi, annhaa! Nimekuona! Angalia mkono wa kushoto, nimevaa kigauni cha maruni kile ulichoninunulia, sio huko angalia upande wenye hizi boat zenye parachute nimenyosha mkono… muonee” Lucy akaachia tabasamu baada ya Mhe. Casto kumwona.
“ What is wrong with you? My Big Dady already here, Please naomba upotee uniondolee kiwingu” Lucy akasema, kisha akazipindua nywele zake zilizoko mgongoni akazileta mbele zikafunika uso wake kisha akazirudisha kwa mapozi na kuziweka sawa na mkono wake laini wenye kucha zilizopakwa rangi zenye kuvutia, na bangili tatu za rangi ya silver zilizokuwa zikiushikilia mkono wake na kuufanya uwe mkono wenye thamani. Yule kijana hakushangazwa na mashauzi ya mrembo aliyembele yake asiyemfahamu japokuwa alimwona kama moja ya malaika walowezi waliopo duniani. Yule kijana pasipo kusema neno lolote akaingiza mkono mfukoni akatoa businesicard na kuiweka meza. “ Sorry if i mistaken. It was not my intention. Hii ni contact. Please naomba tuwasiliane” Lucy akamkatisha “ Ngoja ukutwe hapa, shauri yako”
Yule kijana akaondoka baada ya kushtushwa kumwona Mhe. Casto akiwa anakuja, moja kwa moja akajua huyo ndiye Big Dady wa mrembo Yule.
Lucya kwa upesi akaichukua ile businesicard ili Mhe. Casto asijekuikuta pale. Akaiweka kwenye Mkoba wake. Tayari Mhe. Casto alikuwa amefika, Lucy akasimama na kumkumbatia kimadeko kisha akaanza kulia. Mhe. Casto akawa anambembeleza kwa kumpapasa na kumgongagonga mgongoni kimahaba. Wakaketi wakiwa wamekaribiana sana.
“ Unajua nimetoka kwenye kikao muhimu kwaajili yako Mpenzi?” Mhe. Casto.
“ Kwa sababu mimi ni muhimu kuliko hicho kikao. Mimi ni Malkia wako. Kwani nasema uongo?”
“ Hahaha! Sure! Kwangu wewe ni malaika wa furaha, unanipa raha wewe mtoto. Kila siku nakuambia naomba nikuoe….”
“Hilo tulishamaliza Mpenzi. Wewe ndiye huna maamuzi. Unampenda mkeo kuliko mimi…. Mbona najua mimi kwako ni kama mdangaji..”
“Usiseme hivyo..”
“Unataka nisemeje? Huo ndio ukweli. Nilikuambia siwezi kuwa mke mwenza on my deadbody. Sina nilichokosa. Mimi ni mwanamke mzuri kuliko, alafu nijidhalilishe kuolewa kwa mafungu.”
“Tuachane na hayo. Vipi lakini mambo mengine vipi. Maana simu hizi za ghafla lazima kutakuwa na jambo”
“ mmmh!” Lucy akashusha pumzi kama mtu aliyechoka, kisha akaendelea, “ Kuna kijibwa kinanitafuta ubaya. Nataka nikionyeshe kuwa mimi ni zaidi ya anijuavyo” Akachukua glass ya wine kisha akameza fumba kadhaa alafu akairudisha kwenye meza. Mhe. Casto alikuwa akimtazama pasipokusema chochote, akimsubiri aendelee kuzungumza.
“Nimekuwa muungwana sana kwake. Nikuulize swali?”
“ Uliza tuu Mpenzi”
“ Ukiniangalia mimi ni mtu wa kurudia mwaka chuo?”
“ Kwani vipi umefeli?” Mhe Casto akauliza swali ambalo likamchefua sana Lucy.
“ Mimi ni mjinga? Unaniona sina akili kumbe. Kumbe na wewe ni walewale. Kama huwezi kunisaidia I can handle this issue myself”
“ No Lucy! You got me wrong. Sikumaanisha hivyo. Nimekuuliza tuu. Mimi najua wewe unaakili. Sasa kama huna akili ungefikaje mpaka chuo tena ukachukua kozi ngumu ya Sheria. Hakuna asiyejua kuwa kozi ya sheria inahitaji mtu mwenye akili za juu ili aweze kuimudu” Mhe. Casto alijitetea, alivyokuwa akijitetea mbele ya Lucy ambaye ni binti mdogo aliyemzidi miaka ya kutosha ambayo ingetosha kumuita binti yake. Mbali na hivyo yeye ni Waziri cheo ambacho ni kikubwa katika taifa letu.

Lakini ndio hivyo mapenzi hayana mbabe. Hayaangalii umri wako, cheo chako, taaluma yako au vyovyote uwavyo. Mapenzi yanaweza kukufanya ufanye vitu ambavyo kikawaida ni ngumu kuvifanya.
“Nilikuambia nipo kwaajili yako Lucy. Nambie unahitaji nikusaidie nini?” Hapo Lucy akatabasamu alivyosikia maneno hayo.
“ Nataka umpigie simu sasa hivi pofesa Saimon, umwambie…..”
“ Profesa Saimon ndio nani?” Mhe, Casto akamkatisha.
“ Sikujua kuwa unaweza ukawa mjinga na ukawa Profesa. Hivi hilo kwenu wanasiasa inawezekana?” lucy akasema mara hii akiwa ameimarika.
“ Kisiasa inawezekana kabisa mjinga kumfundisha mwerevu. Mpumbavu kumwongoza mwenye hekima. Kipofu kuona zaidi ya wenye macho..”
“ Basi ndivyo ilivyo kwa Yule Profesa wa ujinga ambaye anafundisha sheria pale chuo cha taifa. Yeye anataka nirudie mwaka lakini yeye ndiye atarudia kusoma huo uprofesa wake sio mimi”
“ Sasa unataka nifanyaje?”
“ Nataka umfundishe adabu profesa Saimon?”
“ Nikadhani unataka umalize chuo,,,”
“ Nataka vyote. Kumaliza chuo na kumfundisha adabu huyo profesa wa ujinga. Atajuta. Nimejikomba kwake kumstahi yeye analeta ujuaji”
“ Sikiliza Lucy. Yote hayo yanawezekana lakini mimi nafikiri cha muhimu sasa wewe umalize chuo. Hizo zingine ni hasira tuu. Msamehe” Mhe. Casto akasema,
“ Unamtetea? Hujui alivyonifanyia nilipomfuata. Mimi sio wa kudharauliwa na mjinga kama Yule. Kwanza mimi sio level zake”
“ Najua! Embu tulia mpenzi. Kunywa hii hasira zipungue. Alafu hili tutalimaliza kirahisi sana” akammnywesha Lucy Wine akiwa kamshika kwenye bega. Lucy alipomaliza kunywa akasema,
“ Naomba simu yako?”
“ Simu yangu!” “Ndio”
“Mmmh!” Mhe. Casto akaguna hapohapo Lucy akamnyang’anya simu, “ toa lock” lucy akasema huku akimrudishia Mhe. Casto simu.. “ Mbona nimekamatika, yaani naendeshwa na haka kabinti kama mtoto” Mhe. Akawaza huku akitoa Lock ya simu yake kisha akampa.

Lucy akachukua simu na kuanza kunakili namba Fulani kutoka kwenye simu yake kwenda kwenye simu ya Mhe. Casto. Baada ya kunakili akaipigia ikawa inaita. Muda wote Mhe. Casto alikuwa akitazama alichokuwa anakifanya Lucy kwenye simu yake.
“ Shika! Ongea naye” Lucy akasema,
“ Nani?” “ Profesa mjinga”
“ Subiri kwanza, unataka nimwambie nini mpenzi?” “
“ Hujui cha kumwambia….” “ Shiiii” mara simu ikapokelewa. Mhe. Casto akamnyamazisha Lucy.
“ Hello! Habari yako Profesa Saimon” Mhe. Casto akasema, Lucy akasogea karibu zaidi na kubonyeza simu sehemu ya sauti kubwa, kisha sauti ya Profesa ikawa inasikika.
“ Salama kabisa, samahani nazungumza na nani?”
“ Huyu ni Waziri wa Nishati na Madini”
“ Waziri wa Nishati na Madini? Unamaanisha Mhe. Casto Baruani?”
“ Naam! Ni mimi Profesa”
“ Habari yako Mhe. Waziri” Sauti ya profesa ilikuwa ikizungumza kwa mashaka na kutokuamini.
“ Huku tuko salama. Kuna ishu nahitaji unisaidie kama mkubwa mwenzangu”
“ Mimi nikusaidie wewe au wewe unisaidie mimi? Hahaha! Wewe ni mkubwa kwangu kicheo, sidhani kama kuna jambo naweza kukusaidia, wewe ndiye unaweza kunisaidia” Profesa akasema,
“ hahahah! Hamna Profesa, Ukubwa haimaanishi huwezi pata msaada kutoka kwa waliochini yako. Nisaidie”
Hapo kukawa kimya kwa kitambo, bila shaka Profesa alikuwa anawaza ni jambo gani ambalo Waziri wa Nishati na madini anahitaji msaada. Yeye hakuwa na mazoea na wanasiasa. Pengine aliwaza litakuwa jambo la kisheria hasa sheria za Mambo ya madini.
“ Profesa! Profes..” Mhe. Casto akaita “ Nipo hewani Mheshimiwa”
“ Embu msaidie Lucy amalize shule salama, Lucy ni binti yetu. Mchukulie kama mtoto wako. Hutokosa chochote kitu. Nitaandaa donge nono kwaajili yako”
“ Mhe. Casto nakuheshimu sana. Ten asana. Lakini kwa hili utanisamehe. Nilishamalizana na Lucy mwenyewe. Nilimuelewesha akaelewa. Anahitajika kurudia hiyo kozi ili awe bora zaidi. Hiyo ndio nzuri niliyoamua kumsaidia. Na sheria za chuo ziko wazi” Profesa akasema kwa utulivu mkubwa na kila neno akiwa ameliwekea msisitizo.
“Nafahamu maadili yako ya kazi hayakutaki uvunje kanuni na sheria. Lakini hii kwako ni kama amri. Hizo sheria zinatungwa na serikali. Wewe sio serikali. Mimi kama moja ya viongozi wa serikali ambaye pia ni kiongozi wako ninayomamlaka ya kupita juu, juu kabisa ya hizo sheria. Hiyo sheria kwangu ipo chini kabisa, wala sio kitu. Ni sheria ndogo ambayo inasimamia watumishi na wanafunzi. Sio mimi” Mhe. Casto alikuwa akiongea hasira zikianza kumchochea, hakutegemea kuwa angepata upinzani kutoka kwa Profesa kutokana na cheo chake cha uwaziri.
“ Mhe. Casto, unakosea sana. Lakini sihitaji kukufundisha kuhusu hizo sheria unazoziita ndogo na kubwa. Ninachoweza kukuambiwa siwezi kukusaida chochote. Kama kuna jambo jingine unaweza kunambia lakini katika hilo jalada lake nilishalifunga hata angekuja nani..” Profesa akasema lakini Lucy akaingilia.
“ Wewe ndiye utarudia huo uprofesa wako ambao sijui hata umeupataje. Lakini sio Mimi Lucy. Umeingia sehemu mbaya sana Mzee..” Mhe. Casto akamziba Mdomo Lucy asiendelee kuongea. Kisha akasema.
“ Profesa, nashukuru sana kwa kuniabisha. Nimekubali.”
“ Sijakuabisha Mhe.. Wewe ndiye umejiingiza kwenye aibu isiyo na ulazima. Mimi nafanya kazi kwa kanuni na maadili. Hayo ndio yanayoniongoza” Profesa akasema lakini kabla hajamaliza Mhe. Casto akakata simu.

“ Bastard!” Mhe. Casto akasema akiwa amefura kwa hasira.
“ Nilikuambia huyu Profesa anadharau sana. Unaona ambavyo amekujibu na wewe” Lucy akasema huku akimchochea Mhe. Casto azidi kuchukia. Mhe. Casto alikuwa kimya akitafakari jambo kwa kitambo.
“ Kwa hiyo tunafanyaje my Bigdad? Maana sasa sio jambo langu tena, limegeuka letu. Sikutegemea akudharau mbele yangu. Bora angenidharau mimi binti mdogo nisiye na cheo, lakini vipi wewe?” Lucy akasema akiwa kamsogelea zaidi Mhe. Casto huku akishika ndevu zake. Mhe. Casto hakuongea kitu akaangalia saa yake ya mkononi, ilikuwa saa mbili na nusu za usiku.
“ Muda umekimbia, nitalishughulikia jambo hili. Ni ishu ndogo mno. Wala usiwe na hofu” Akasema,
“ Lakini siku zilizobakia ni chache, hili lifanyike kwa upesi. Mimi sitaki kurudia mwaka”
“Usijali. Lipo ndani ya uwezo wetu” “ Unauhakika Mpenzi? Maana huyu profesa kama ulivyomsikia inaonekana yupo tayari kwa lolote hata kupoteza kazi”
“ Mimi ni mwanasiasa, nadili na taifa mtu mmoja hawezi kunishinda. Nishakuambia hii ni ishu ndogo. Zimebaki siku ngapi?”
“ Siku nne Mpenzi. Nimeanza kuingiwa na hofu” Usihofu, siku nne ni nyingi. Mpaka kesho kutwa hili litakuwa limeisha”
“Utafanyaje?” “ Ninajua nini nitafanya, subiri simu kutoka kwa huyohuyo Profesa yeye mwenyewe ndiye atakupigia akikuambia hautarudia mwaka na utaingia kwenye mitihani yako ya mwisho, utamaliza malkia wangu” Mhe. Casto akasema, macho yake muda mwingi yalikuwa yakiangalia saa yake ya mkononi.
“ Nimefurahi mpenzi. Nakupenda Bigdad wangu. Kwako najihisi salama. Kwa kweli nitakupa zawadi kubwa kama utanisaidia nimalize chuo. Sitaki kurudia. Kwanza nimechoka kusoma”
“ Nafikiri nikuache, ninakikao kingine na Rais majira ya saa tatu. Muda umekimbia, nina kama dakika ishirini tuu.”
“ Sawa mpenzi. Kama ukiona inakusumbua mwambie hata shemu Darlin Rais, huyu Profesa ajue kuheshimu wakubwa zake”
“ Hahahah! I will handle it myself. Shika hii ya pizza leo usiku” Mhe. Casto akasema akimkabidhi Lucy kiasi cha shilingi laki moja. Kisha wakaagana


ITAENDELEA

Pia itakuwa inaendelea kwenye Channel ya WhatsApp. Bonyeza Link hii 👉🏼Tibeli Star | WhatsApp-Kanal
0693 322 300
 
RIWAYA YA CONNECTION EP 02
Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300

ILIPOISHIA
“ Sawa mpenzi. Kama ukiona inakusumbua mwambie hata shemu Darlin Rais, huyu Profesa ajue kuheshimu wakubwa zake”
“ Hahahah! I will handle it myself. Shika hii ya pizza leo usiku” Mhe. Casto akasema akimkabidhi Lucy kiasi cha shilingi laki moja. Kisha wakaagana.

*************
ENDELEA

Siku mbili zilipita lakini Lucy hakupokea simu yoyote kutoka kwa Profesa kama alivyoahidiwa na Mhe. Casto, na kila alipojaribu kumtafuta Mhe. Casto kwenye simu hakuwa anapatikana kwenye simu. Hofu na mashaka vikaukonga moyo wake. Kule kujiamini kote kukayeyuka. Sasa alihisi huenda kweli atarudia mwaka jambo ambalo aliapa kuwa isingewezekana. Kwake ilikuwa bora aache chuo kuliko kurudia mwaka.

Unajua Lucy tangu alipopevuka na kugundua yeye ni mzuri aliwachukulia wanaume kama watumwa wake. Aliamini kuwa hakuna mwanaume ambaye asingeitii amri yake. Miaka yote tangu akiwa sekondari mpaka hivi leo amekuwa kama Jinni Mahaba la kike lenye mamlaka ya kuendesha wanaume vile atavyo. Chochote alichokitaka kwa wanaume aliowahi kukutana nao alikipata. Chochote alichoamrisha wanaume walikifanya pasipo kusita wala maswali. Hii ndio imemfanya aishi maisha ya kifahari na anasa tangu awe huru alipofika chuoni. Alishawahi kuamrisha vigogo wakubwa serikalini na wamiliki wakubwa wa makampuni na wakatii amri zake sembuse Profesa wa chuo ambaye kwake alimuona sio lolote sio chochote.

Alijua kuwa Ukufunzi wa chuo kikuu haukuwa na pesa nyingi ukilinganisha na watu aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano ambao wengi wao ni matajiri. Akakumbuka maneno ya Profesa Saimon ““ Mimi sipo kama unavyodhani binti. Ni kweli wewe ni mwanamke mzuri. Lakini uzuri wako hauwezi kushinda heshima niliyonayo. Ninajiheshimu, ziada ni kuwa mimi ni mwanaume bora ninayeweza kushindana na tamaa ya mwili. Mbali na hayo, wewe ni kama binti yangu”

“mfyuuuuu” akaachia sonyo baada ya kukumbuka maneno ya Profesa. Muda wote alikuwa kitandani katika nyumba aliyopangiwa na Mhe. Casto.

“ What I will do now! I can not allow that little rat to defeat me. I swear he will regrets” “But nitafanye nini? Casto naye hapatikani, jumbe zangu za Whatsapp hazijapokelewa. Hayupo mtandaoni tangu juzi. Aarrrgrrii! This is Stupid! Ngoja nimpigie dereva wake” Alikuwa akiwaza, na jambo hilo akaliafiki, “ Nilimhifadhi kwa jina gani.. nananan…nana.. yes huyu hapa” simu ikawa inaita kisha ikapokelewa.

“ Hello, Mambo. Sorry! Ninayeongea ni Lucy. Hhahaha! Kumbe ulikuwa na namba zangu, nikajua siku zile tulivyoongea hukuzihifadhi. Anyway! Mhe. Yupo wapi maana simpati. Whaaat! Nimekwisha. Anarudi lini? No! Hapana jamani! Sawa. Ahsante” Lucy alichoka mwili na akili alipopewa taarifa kuwa Mhe. Casto alisafiri nje ya nchi yeye pamoja na Rais. Tena walisafiri ule usiku walipoachana kule ufukweni.

“Sasa naye kwa nini hakuniambia, alishindwa hata kunijulisha ili nijue cha kufanya. Huu upuuzi wakumtegemea mwanaume mmoja hii ndio shida sasa. Hii ngoma ishakuwa nzito. Sasa nitafanyaje. Huyu Panya huyu! Sitaki kuamini kama nimeshindwa na kizee kama kile. Ati Profesa! Profesa my foot” akachukua simu akampigia Profesa lakini simu haikupokelewa. Akajilaza kitandani na kuachia pumzi kama mtu aliyemaliza mbio ndefu. Punde simu yake ikaingia ujumbe. Kuangalia ilikuwa ni ujumbe kutoka kwa Profesa, akaamka na kukaa kitandani kwa upesi. “ Tayari suala lako nimeshaliwasilisha kwenye idara kuu ya kitivo cha sheria na limeshafikishwa kwa mkuu wa chuo. Unahitajika kesho mchana ufike kwenye ofisi ya Mkuu wa chuo kutakuwa na kikao maalumu. Ukiweza uje na huyo Mtu aliyejitambulisha kama Waziri wa Nishati na Madini”

Lucy alihisi moyo wake ukichanganyikiwa, mambo yalizidi kumwia magumu. Hii ilimaanisha taarifa yake ipo kwenye idara yote ya sheria pale chuoni, zaidi kwa jinsi ujumbe ule uliotumwa ulivyo aliamini kuwa Wakufunzi na wakuu wa idara wote wamekubaliana kuwa kitu kimoja. Kama ni hivyo hii ilimaanisha kuwa Lucy angerudia mwaka ikiwezekana kusimamishwa chuo kwa kosa la kinidhamu kwa Profesa Saimon. Lucy kama mwanafunzi wa sheria alijua kabisa kuwa pengine angeweza kushtakiwa kwa makosa ya kumshawishi Profesa Saimon kupokea rushwa yake ya Ngono au pesa.

Akiwa amechanganyikiwa akawa anaishika simu mara aiweke kitandani, alitaka kuijivu ule ujumbe aliotumiwa na Profesa lakini akasita, akawa anazunguka zunguka mule chumbani kama mtu aliyechanganyikiwa. Akaenda kwenye Jokofu dogo lililokuwa mule chumbani, akatoa Wine yenye kilevi, kisha akamimina kwenye glass na kuanza kunywa. Wakati akinywa akakumbuka kitu kwenye mkoba wake. Akachukua mkoba, akatoa simu ndogo lakini wakati anaitoa kuna kitu kikaanguka chini kutoka kwenye mkoba wake. Ilikuwa ni ile businesicard ya Yule kijana. Akaiokota na kuanza kuisoma huku akiwa anakunywa wine yake. “ Kalage Nyundo” lilikuwa jina la Yule kijana, chini yake kulikuwa na mawasiliano ya simu, emaili yake na anuani ya kampuni yake iliyopo mjini ambapo ilikuwa ikiitwa. “Mask Ltd” Hakujua nini kilichomshawishi azipigie namba zile. Akajikuta amezipigia kwa kupitia simu ndogo.

Haikuita sana, ikapokelewa.

“Habari! Samahani kwa usumbufu. Sijui unanikumbuka.. ni Yule mwanamke uliyeniachia businesicard yako kule fukweni. Muone! Nipo poa tuu. Hamna bhana. Mbona hata sio mkali. Ile siku nilikuwa na majanga yangu. Ulijuaje. Aaha wapi! Kwamba? Hahahahah! Unavituko. Mwenzangu bado hayajaisha. Acha utani bhana sidhani kama unaweza kunisaidia. Wapi? Usiku umekuwa mkubwa na nimechoka labda wewe uje. Sawa ngoja nakutumia location” Simu ikakatika. Lucy akamtumia Kalage anuani ya makazi yake. “ But why! Mbona najishusha kirahisi hivi” Aliwaza baada ya kuituma location kupitia whatsapp. Akabwia fumba kadhaa za Wine kisha akaenda kuwasha Muziki ambao ulikuwa mule ndani. Kisha akaanza kunengua polepole huku akiwa amesimama mbele ya kioo cha kikabati cha kujirembea. Muziki laini uliendelea kupiga huku akishushia na Wine. “ Nahitaji Akili yangu unambie nini chakufanya” akasema akiwa bado anacheza muziki. “ uzuri wako wa mwili leo umeshindwa cha kufanya?” mawazo yake yakamwambia. “ kila siku nimetumia uzuri wangu kukufikisha hapo ulipo. Bila mimi kutumia uzuri wangu leo ungekuwa kwenye kasri hili? Ungekuwa hapa?” Lucy akasema huku akicheza na kunywa wine aliyoishika mkononi huku akijiangalia kwenye kioo akijibizana na mawazo yake. “ Upo kimya eeh! Ukweli umekugusa. Wangapi unaowajua wanatumia akili na hawatowahi kuishi maisha ninayoishi mimi? Uzuri kwangu ni silaha kubwa ambayo imenipa maisha bora ambayo ni wateule wachache wanayoyaishi chini ya jua” “ usinichekeshe! Mteule hujui chakufanya sasa unaniuliza mimi. Mimi sina msaada..” Nooo! Don’t talk to me like that. You know how crazy am I” Lucy akafoka akikemea mawazo yake. Kisha akaanza kunengua kwa kukata mauno kadiri muziki ulivyokuwa ukipiga. Kuna wakati uso wake aliulegeza na kung’ata midomo yake, kisha akaachama na kutoa ulimi nje na kuanza kulamba midomo yake. Alafu akawa anainama huku akikisogelea kioo karibu kabisa. Akawa anatazamana na taswira yake ambayo iliakisi sura na umbo lake kwa asilimia mia moja. Kisha akaachana na kusemeshana na mawazo yake akaitazama taswira yake kwenye kioo ambayo nayo ilikuwa ikimtazama. Akaiambia; Wewe! Nini unakosa? Kitu gani unakosa nakuuliza? Usinitazame! Kila kitu unacho sio?” Wakati anaiambia taswira yake kwenye kioo mawazo yake yakaingilia mazungumzo yakamwambia “ Kuna kitu kimoja unakosa?” Ghafla akaacha kucheza kisha akakunja uso wake kwa hasira. “ Nini nakosa wewe mjinga” “Mimi ni akili. Mjinga ni wewe. Unakosa hekima, maarifa ya busara na hujui uzuri wa kweli ni upi. Hivyo vyote ungekuwa navyo usingekuwa unataabika hapa, sasa unakoelekea kuchanyikiwa. Mtu aliyechanganyikiwa ni mtu aliyegombana na akili yake. Uzuri bila mimi Akili unafaida gani?” “Kitu pekee ambacho uzuri amekushinda wewe akili na ndicho ninachompendea ni kimoja” Lucy akasema akiiambia akili yake.

“ mjinga hana macho” Akili akasema, “ acha kujitetea. Uzuri unaonekana lakini vipi wewe akili, nani anakuona?” “Nijitetee! Nimekuambia mjinga hana macho. Wenye akili huona akili. Wewe hunioni lakini kama ungekuwa na hekima ungejua akili inaonekana” nakuhakikishia utayaharibu maisha yako kama hutaamua kushikamana na mimi” akili akaongeza.

“Shut…! Shut fucker up! Tulia. Tena usiwe kiherehere, unasikia kuna mgeni wangu ameshafika. Ukae kwa adabu” Lucy akasema akiwa ameona simu yake ikiita na namba za Kalage. “Nimekuelewa” mawazo yake yakamjibu, kisha Lucy akapunguza sauti ya muziki na kupokea simu. “ Umefika, okay nakuja”

Akashuka ghorofani moja kwa moja akaenda getini kumfungulia Kalage aliyekuja na gari lake la kifahari. Lucy hakutegemea Kalage kuja na gari zaidi kilichomshangaza ni aina ya gari aliyokuja nayo. Alijikuta akiropoka “ Vijana wa mjini kwa kuazima magari hamjambo. Kwa hiyo umeona ukija na huu mtambo ndio utaukonga moyo wangu. Hhahahah!” “Unakosea Mrembo! Kuna msemo unasema, usimdharau usiyemjua” Kalage akasema huku akimthaminisha Lucy aliyekuwa amevalia nguo nyepesi ya kulalia ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imeuacha mwili wake wa kuvutia uchi. “ Mimi sio muumini wa misemo hasa hiyo ya wahenga kwa jadi” Lucy akasema huku akiwa amefungua geti na kumruhusu Kalage aingie.

Baada ya Kalage kukaribishwa ndani akiwa ameridhishwa na mandhari ya jumba lile la kifahari ambalo moyoni alikiri kuwa Lucy alistahili kumringia siku ile. Kwa mwanamke mwenye kuishi maisha ya aina ile sio rahisi kuwa mnyenyekevu. Wanawake wengi wakiwa na maisha ya juu huishi kwa kiburi na jeuri. Ni nadra sana kukuta mwanamke msomi, mzuri na mwenye maisha ya kifahari kuwa mnyenyekevu. Hii hupekelea vijana wengi na wanaume kuogopa kukabiliana nao ili kuepuka dharau za jumla au zile za rejareja.

“Haya niambie nini kinachokusumbua. Wakati wengine wakitegemea Msaada na wokovu kutoka kwa malaika. Mimi ndiye hutoa wokovu kwa malaika wazuri kama wewe. Unajua hata malaika kuna wakati hunaswa kwenye mitego ambayo huwashinda kujinasua. Imekuwa bahati kwako kukutana na mimi..” Kalage akasema. Ufunguzi wake huo ulimtambulisha kwa Lucy kuwa ni mwanaume anayejiamini asimamapo mbele ya wanawake wazuri. Lucy hakuzoea kukutana na wanaume wa aina ya Kalage. Lucy alizoea kukutana na wanaume waliomtetemekea kutoka na uzuri wake licha ya kuwa wanaume hao walikuwa na pesa au cheo au umaarufu lakini hiyo haikuwafanya wajiamini pale waliposimama mbele yake. Leo kwa mara ya pili alikutana na mwanaume ambaye anamchukulia yeye kama mwanamke. Mwanaume wa kwanza akiwa Profesa Saimon. “ Kwa nini anajiamini sana huyu kijana “ Lucy akawaza akiwa anamtazama Kalage. Mazungumzo hayo yalifanyika ukumbi wa sebuleni ambao ulijaa samani za kifahari. Walikaa masofa yaliyokuwa yanatazama. Hivyo kila mmoja alikuwa na nafasi ya kumtazama mwenzake kwa uzuri kabisa.

“ Usifikiri juu ya kumkomboa malaika kwanza. Nahitaji kujua wewe ni nani kabla sijahitaji msaada wako” Lucy akasema,

“ Nimekueleza mimi ni Mkombozi, na ndio maana niko hapa” Kalage akasema, jambo ambalo lilimfanya Lucy atabasamu huku moyoni akifikiri kuwa huenda kijana Yule amejua matatizo yake. Wote wakanyanyua glass ya wine kisha wakabwia fumba kadhaa alafu wakashusha kwa pamoja kwenye meza ndogo ambazo kila mmoja aliyokuwa nayo mbele yake. Juu ya meza hizo kila mmoja ilikuwepo chupa kubwa ya wine na Glass iliyokuwa na kinywaji.

Lucy akawa anamtazama Kalage kwa namna ya kumpima kama ni mtu kweli mwenye uwezo wa kumpa msaada. Lakini kila alivyokuwa akijitahidi kujishawishi ili amuamini hakuweza. Mwonekano wa Kalage haukulingana na mtu mwenye kutoa ukombozi. Kijana mweusi, mwenye urefu wa kati, upaa ukiwa umemuanza, hakuwa na rutuba yenye kumshawishi yeyote. Hata matapeli wa mjini wangetumainiwa kutoa msaada lakini sio Kalage.

“siku ile pale ufukweni ulienda kufanya nini?” Lucy akaibua mjadala mwingine baada ya ukimya kidogo. Alihitaji muda zaidi ili kumwamini na kumweleza shida zake.

“ Nilienda kupunga upepo kidogo”

“ Mwenyewe?”

“ Yeah! Nahitaji kuwa mwenyewe pale ninapohitaji utulivu?”

“Unamaanisha kuna mambo ambayo nawe yanakunyima utulivu?”

“ Haina maana hiyo?”

“Sasa utulivu upi unauhitaji kama haukupotezwa”

“Unajua kusimamia na kuendesha kampuni inahitaji muda wa kupumzika?”

“ Ni kweli. So hata hiyo gari hapo nje uliyokuja nayo niya hiyo kampuni unayofanyia kazi?”

“Hahaha! Unafurahisha sana. Hivi unaitwa nani?” Kalage akasema akichukua glass na kunywa fumba kadhaa. Kisha akapeleka mkono wake kwenye mfuko wa shati alilokuwa amelivaa. Akatoa pakti ya sigara, akachomoa sigara moja. Huku akimtazama Lucy kama mtu anayehitaji kuruhusiwa kuvuta sigara.

“ Ni sawa usijali. Ngoja nikakuletee kibiriti”

“ Haina haja. Ninacho. Labda unisaidie chombo cha kutupia haya majivu”

“ Kumbe uko full! Ngoja nikakuletee” Lucy akasema huku akinyanyuka kwenda kumchukulia chombo cha kutupia majivu. Muda huo Kalage alikuwa ameshaiwasha sigara na ameanza kuivuta, akawa anamtazama Lucy aliyekuwa akiondoka kwenda kuchukua chombo. “Huyu mwanamke ni mzuri sana. Huu mzigo wote ni wake au ndio waturuki washafanya yao?” Kalage akawaza akiwa anatazama mswambanda wa Lucy ulivyokuwa unatikisika ndani ya nguo ya kulalia aliyokuwa ameivaa. Mbaya zaidi Lucy hakuwa amevaa nguo ya ndani kuyawekea rufaa makalio yake yasiendelee kutingishika.

“Ahsante! Hukuniambia jina lako”

“ Niite Lucy. Alafu unaongea kama mtu unayeniamrisha. Unamamlaka yoyote juu yangu”

“ Hahaha! Lucy bhana” Kalage akacheka huku akiikung’uta sigara kuondoa majivu. Kisha akamtazama kwa macho ya kumtathimini. Akasema,

“Mkombozi yeyote lazima awe na mamlaka. Unanihofia?”

“ Mimi ni kuhofie wewe?”

“ Najua! I know hilo kwako ni ngumu. Lakini kwangu ni mahiri na bingwa wa kushughulikia mambo magumu. Tabia hiyo hunifanya wengi wanione kama najiamini au ninamamlaka dhidi yao”

“ Mambo magumu?”

“ Ndio!” Kalega akajibu, kisha akaweka sigara mdomoni akaivuta pafu ndefu, kisha akaachia moshi puani na mdomoni kwa pamoja uliozagaa kwenye sebule ile. Kisha akaangalia saa yake ya mkononi iliyoonyesha ni saa tano na robo alafu akasema,

“Muda unakimbia sana. Kesho nitakuwa na ratiba ngumu, usiku huu kuna sehemu natakiwa niende”

“Una appointment na mtu?” “Wala! Mambo ya kazi”

“Kazi gani? Au umeoa unamuwahi mkeo?”

“ Kuoa bado. Ila kuhusu kazi mbona kwenye businesscad niliyokupa inaonyesha ninajishughulisha na nini?’

“ Sikuangalia!”

“Haidhuru! Sikia Lucy utaniambia unasumbuliwa na nini au niondoke maana nimekuja tuu kighafla”

“ kwamba unataka kuondoka?” “ Muda umekimbia sana”

“ Bora usingekuja kama ulikuwa na mambo yako. Sipendi mtu akutane na mimi akiwa na harakaharaka. Kwangu ni dharau na kuniona kama mtu wa ziada nisiye na umuhimu. Kama kuna mambo muhimu kuliko mimi ni afadhali usingekuja” Lucy akaongea kwa mashauzi akiwa amekasirika.

“ Sikia Lucy. Mimi sio aina ya wanaume unaowajua. Unapoongea na mimi lazima utumie akili kuliko mihemko yako. Kama unahitaji twende sawa mimi na wewe zingatia hilo” Kalage akasema sauti ikiwa imekaza kidogo akimaanisha amekasirika, kisha akakitupa kishungi cha ile sigara kwenye kisosi cha kuwekea majivu ya sigara.

“ Umekuja kunikoromea nyumbani kwangu. Wewe ni kichaa nini?”

“ Anyway! Ngoia niondoke, sihitajai kugombana na mtoto mzuri kama wewe lakini sipo tayari pia kuendeshwa na kuvunjiwa heshima yangu” Kalage akasema akiwa amesimama tayari kwa kuondoka, “ Nifanye nini?” Lucy akawaza, “ Uliniambia nitulie nisilete kiherehere mbele ya mgeni wako” Akili yake ikamjibu.

Lucy akajishika kichwa huku akifumba macho kama mtu anayeumwa na kichwa, alikuwa hataki akili yake imueleze kitu. Muda huo Kalage alikuwa yupo mlango wa sebuleni akitoka.

“ Hivi kweli unaondoka?”

“ Unadhani natania. Tutaonana siku nyingine ukiwa tayari.”

“ Subiri. Nitakuambia kila kitu. Njoo!” Lucy akasema macho yake yakimsihi Kalage arudi. Kalage akaitazama saa yake ya mkononi akiwa ameushika mlango uliokuwa tayari upo wazi. Akamtazama Lucy kisha akaufunga mlango na kurudi mahali alipokuwa ameketi.

“Sorry bhana! Mbona unahasira za haraka.” Lucy akasema huku akiyalegeza macho yake. Kalage hakumjibu kitu alikuwa akimtazama tuu.

Lucy akamueleza kila kitu Kalage.

“ Kwa hiyo kama nitakusaidia utanipa nini?”

“ Chochote nitakupa Kalage”

“ Chochote?” “ Ndio chochote”

“ Kama kitu gani?” “ Nimekuambia chochote kilichondani ya uwezo wangu. Iwe pesa au hata mwili wangu”

“Mbona kirahisi hivyo” “ Ninashida Kalage. Mimi sio wa kulala na mtu kama wewe lakini nitafanayaje?”

“ Hahahah! Au sio. Hata mimi sio mtu wa kulala na binti kama wewe. Na wala sitahitaji pesa wala mwili wako”

“ EEH! Sasa utahitaji kitu gani?”

“Muda ukifika nitakuambia. Kwa sasa tubaki kwenye makubaliano”

“Usije ukanitoa kafara maana ninyi vijana ambao pesa zenu hazieleweki mnahusishwaga na mambo ya nguvu za giza”

“Usinichekeshe Lucy. Ondoa shaka katika jambo hilo”

“ Mmmh! Haya!”

“ Kwa hiyo dili lipo?” “Yes we have deal”

Mimi ngoja niondoke. Lucy hakuamini kabisa Kalage angeondoka pasipo kumwomba penzi. Hii kwake ilikuwa zaidi ya maajabu saba ya dunia. Kwa jinsi kile kinguo alichokuwa amekivaa kilivyomkaa hovyo hakudhani kuwa kuna mwanaume yeyote ambaye angemuacha vivihivi.

Kalage alimpa ahadi Lucy kuwa ampe masaa saba mpaka asubuhi huyo profesa atakuwa amemruhusu aingie kwenye mitihani. Lucy alipouliza kwa namna ipi atamfanya Profesa alegeze msimamo wake. Kalage akamwambia subiri ajionee mwenyewe. Licha ya Lucy kumwambia kuwa Profesa kamkatalia mpaka Waziri sembuse yeye asiyejulikana na asiye na cheo chochote. Kalage alimhakikishia kuwa atajua kuwa wapo watu wenye nguvu wasiojulikana.

“Lucy nimekuwa mtu wa kuamini vijana wa namna ya Kalage kirahisi hivi” Lucy alijisemesha akiwa ameshafika kitandani baada ya kumsindikiza Kalage. Usingizi ukamchukua.

************

Profesa Saimon akiwa katika viunga vya chuo kikuu cha taifa akiwa anaelekea ofisini kwa mkuu wa chuo kwaajili ya kumshirikisha suala la Lucy na kutishiwa na Waziri wa Nishati, akiwa ameukaribia mlango wa mkuu wa chuo ghafla simu yake inaita. Akaitoa mfukoni, alipoitazama ilikuwa namba ngeni. Akili yake ilimwambia asiipokee simu hiyo akidhani kuwa huenda ni simu ya Lucy au ya Waziri wa Nishati na Madini. Lakini akili nyingine ikamshawishi apokee, akaamua kupokea.

“ Hello!” Sauti ya kisomi ya Profesa Saimon ikajivinjari katika eneo lile ambapo Profesa Alikuwa ameshika kitasa cha mlango wa Mkuu wa chuo tayari kwa kukifungua kwani tayari alikuwa amekaribishwa.

“ Nina zawadi yako Profesa:”

“ Wewe nani? Zawadi ya nini”

“ Usiwe na haraka Profesa. Utanijua tuu”

“ Niambie wewe nani?”

“ Tayari umeshinda jackpot, upo kwenye anga la waliofanikiwa, Hongera sana Profesa”

“ Naomba ujitambulishe, naingia kwenye kazi. Tusipotezeane muda, ninakata kisha naomba usinipigie tena. Sio mchezaji wa kamari za mitandaoni. Ukinisumbua tena nitakuchukulia hatua na kisheria” Profesa akasema akiwa amekasirika huku aking’ata midomo yake;

“Hahah! Wewe ndio utanisumbua muda mfupi ujao. Kama ni kukata wewe kata tuu lakini nakuhakikishia zawadi yako nimeshakutumia kwenye simu. Kama umeipenda utanipigia tujue unaipataje, kama hujaipenda achana nayo. Kazi njema Profesa” Simu ikakatika. Punde ujumbe ufupi wa Whatsapp uliingia katika simu yake. Moja kwa moja akajua aliyemtumia ujumbe ule alikuwa ni aliyetoka kuongea naye muda mfupi uliopita. Hata hivyo akili yake ilitambua Yule atakuwa mtu wa Waziri, Mhe. Casto. Akaufungua ule ujumbe. Alishtuka sana, mapigo ya moyo yakaanza kupiga kwa nguvu huku shinikizo la damu likimpanda, akaufuta ujumbe ule kisha akaanguka chini na kupoteza fahamu.

************

Lucy alimaliza mitihani yake akiwa haamini kama kweli Kalage ndiye amemsaidia. Siku hiyo alikuwa ndio amemaliza mtihani wake wa mwisho ambapo alipanga ataenda kukutana na Kalage kwaajili ya kumshukuru. Lakini alipoipigia simu ya Kalage ikawa haipatikani. Alipiga na kupiga lakini ujumbe ulikuwa ni uleule kuwa anayempigia hapatikani. Siku zikapita lakini namba ya Kalage ikawa haipatikani. Jambo hili lilimshangaza mno. Inawezekana vipi namba ya Kalage isipatikane kwa zaidi ya wiki nzima. Kama Kalage ni mmiliki wa kampuni inawezekana vipi namba yake haipatikani. Hilo kikawaida lisingewezekana. Lucy ingawaje hakuwahi kufanya biashara hata ya kuuza maandazi lakini alijua fika kuwa mawasiliano kwa mfanyabiashara yeyote ni muhimu na lazima yapatikane muda wote.

Hii ilimfanya afikiri kuwa huenda Kalage ni Usalama wa taifa. Kutokana na uzoefu wake alipoingia katika mahusiano ya kimapenzi na baadhi ya wanausalama. Alikuwa akiwapigia hawapatikani isipokuwa wakipiga wao. Pia walikuwa wakipiga na kubadili namba tofautitofauti na nyingi kati ya hizo ni namba maalumu zisizo na kawaida.

“Ndio maana kalikuwa kanajiamini sana” Lucy akasema akiwa anarudi na gari yake nyumbani alipopangiwa na Mhe. Casto. Alipofika nyumbani alikuta simu ndogo ikiwa na jumbe kutoka kwa Mhe. Casto ikimtaarifu kuwa amerudi kutoka nje ya nchi, pia ilikuwa na ujumbe wa kumtaka amsamehe kwani ilikuwa safari ya ghafla na kama vipi leo wakutane katika hoteli waliyozoea kukutana. Lucy akasonya na kuachia tusi la nguoni alafu akaitupa ile simu kwenye sofa lililokuwa mule chumbani. Kisha akaenda kuoga. Aliporudi akajaribu kuipigia ile namba lakini bado ikawa haipatikani. Akaingia mtandaoni kuperuzi peruzi, hakukuwa na jipya. Hakuwa na sababu ya kuendelea kuwa macho ukizingatia wiki nzima alikuwa akikimbizana na mitihani. Akalala.

**********

Alfajiri na mapema simu ya Lucy ilikuwa ikiita. Iliita ikakata. Ikaita na kuita lakini Lucy alikuwa fofofo akiwa amelala. Mpigaji wa simu hakukata tama kirahisi aliendelea kupiga bila kuchoka. Mpaka Lucy aliposhtuka kutoka usingizini. Aliisikia akawa anaitazama kwa mbali bila kuichukua. Lucy alitaka ikate na kweli ikakata lakini ikapiga tena. Akasonya, alipoamka na kuikairibia akaona kumbe aliyekuwa akimpigia alikuwa Dora. “Kuna nini! Mbona Dora anapiga hivi” Akawaza huku akiipokea.

“Hello Dora, sio kwa kupiga huku”

“ Lucy unahusika na kilichotokea?”

“ Nini kimetokea? Sikuelewi!”

“ Lucy usinifanye mimi mtoto mdogo. Unajua kila kitu”

“ Unazungumzia nini Dora. Embu ongea kitu ueleweke”

“ Lucy wewe mbaya sana. Sikudhani mngefikia huku. Kumbe wewe ni mbaya sana hivi”

“ Dora.. Dora usinichanganye. Yaani unanipigia asubuhi asubuhi ili unambie vitu visivyoeleweka”

“ Kwa hiyo mkaamua mumuuwe?”

“ Nani? Profesa ameuawa?”

“ Lucy nimeamini wewe ni nyoka. Alafu unavyojifanya hujui”

“ Profesa ameuawa? Wewe umepata wapi hiyo habari?”

“Lucy usiniambie hujui. Embu ingia mtandaoni ujionee mwenyewe” Dora akasema, hapohapo Lucy akakata simu akiwa ameamka na ameshikwa na wendawazimu.

“ Profesa kauawa! Nani kamuua sasa!” akawa anajiongelesha mwenyewe huku akiingia kwenye mitandao ya kijamii. Kuingia tuu habari ya kwanza aliyokutana nayo ilikuwa ni kifo cha Profesa Saimon ambaye amejirusha kwenye jengo refu la ghorofa.

“Ooh My God! Uuuwii! Ni kweli! Nini kinaendelea. No! Haiwezikuwa” Lucy alikuwa anaongea mwenyewe mara hii alikuwa amesimama akizunguka zunguka kwenye kile chumba huku akipangusa simu yake. Kila alikopita habari aliyotana nayo ilikuwa ni hiyo ambayo haikuwa na masaa mawili tangu iwekwe mtandaoni. Hii ilimaanisha kuwa Profesa Saimon alijirusha usiku.

“Hapana! Mimi sio mbaya kiasi hiki. Nisingeruhusu mtu auawe kwaajili yangu”

“ Mhe. Casto anamkono wake hapa?” “au Kalage?” Maswali yalikuwa mengi ambayo yalizidi kumfanya Lucy achanganyikiwe. Akiwa anafikiria ampigie Mhe. Casto ghafla alishtuka simu ikiita, ilibaki kidogo aidondoshe. Aliyekuwa akipiga ni nani mwingine kama sio Mhe. Casto. Akapokea na hapohapo akaanza kuropoka;Top

“ Hayakuwa makubaliano yetu! Sikukuagiza umuue. Ulichokifanya ni nje ya makubaliano yetu. Mimi sihuhiki na damu ya huyo mtu. Oooh! Mikono yangu itafanya kila kitu lakini sio kumwaga damu. Kwa nini umemfanyia hivi Profesa wa watu?”

“ Lucy! Lucy!”

“ Usiniite jina langu. Muuaji mkubwa wewe. Sitaki unitafute na namba yako naifuta. Kama utataka na nyumba yako nitatoka. Salala! Salale! Uuuuh!” Lucy akakata simu. Ilikuwa taarifa kubwa ambayo ilimshtua sana Lucy. Aliamini kuwa kama isingekuwa yeye basi Profesa angekuwa hai.

“Nifanye nini mimi! Huu mkosi huu! Maskini Profesa Saimon. Alikuwa anaipenda sana kazi yake. Hii imeenda mbali jamani!” Lucy alijiongelesha mwenyewe. Akaamua aende kuoga ili mwili na akili vitulie.

ITAENDELEA
+255693322300
 
RIWAYA YA CONNECTION EP 03
Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300

ILIPOISHIA
“Nifanye nini mimi! Huu mkosi huu! Maskini Profesa Saimon. Alikuwa anaipenda sana kazi yake. Hii imeenda mbali jamani!” Lucy alijiongelesha mwenyewe. Akaamua aende kuoga ili mwili na akili vitulie.

*************
ENDELEA

Hili ni tukio la pili ndani ya mwezi la mtu kujirusha kwenye jengo refu la ghorofa. Huku chanzo cha wahusika kufanya tukio hilo kikiwa hakijulikani. Marehemu hakuacha ujumbe wowote ulioonyesha sababu ya yeye kuchukua uamuzi huo. Hata hivyo hakukuwa na uhakika wa moja kwa moja kuwa wahusika walijirusha wenyewe au walirushwa. Jeshi la Polisi liliahidi kufanya uchunguzi.

“Hii sio hali ya kawaida. Akili yangu inaniambia kuna jambo halipo sawa. Kuna kitu kinaendelea katika Mji huu. Mwezi haujaisha anajirusha mtu mwingine. Wakwanza ni Yule mwanamke ambaye tulikuja kujua jina lake ni Yasinta ambaye mpaka sasa uchunguzi wake bado haujakamilika ingawaje uchunguzi wa awali unaonyesha alikuwa ni mfanyakazi wa bank moja hapa jijini. Tukio la pili sasa ni huyu Profesa Saimon wa chuo kikuu cha taifa akiwa kama mhadhiri. Kuna ulazima wa kufanya shughuli zetu kwa upesi kuzuia tukio jingine la namna hii. Sisi kama Polisi tunachokiapo cha kulinda wananchi na mali zao. Nitaonekana siwajibiki ikiwa mambo haya yataendelea tena kwa mfuatano mfupi nama hii. Sitakuwa tayari kuonekana mzembe.” Mkuu wa polisi wa Mkoa alisema akiongea na polisi wenzake katika kikao ambacho kilifanyika ofisini kwake.

“ Ukitaka kujua tukio hili sio la kawaida ambalo lazima liwe na uhalifu mbaya, angalia mfanano wa matukio. Wahusika wote ushahidi unaonyesha kuwa walijirusha ghorofa ya kumi na sita. Wahusika wote wamejirusha majira ya usiku mwendo wa saa saba hivi mpaka saa tisa. Wahusika wote simu zao hazijulikani zilipo. Hata tulipojaribu kuzifuatilia hatukuona dalili ya uwepo wake. Mfanano huu unatoa picha kuwa kuna jamabo linaendelea na kama hatutakuwa makini yatatokea makubwa zaidi” akameza mate.

“ Afande Peter Mirambo!”

“ Ndio Mkuu”

“ Hii kesi unaionaje?’

“ Kama ulivyoeleza Mkuu. Kesi hii ni ngumu na ni ngeni katika nchi yetu. Tunahitajika kuchukua hatua mapema kuzuia tukio jingine”

“ Nafikiri wewe ungeendelea na kesi hii pia kwa sababu zinakaribiana kwa namna kubwa. Kuwaweka wapelelezi wawili kila mmoja achunguze inaweza ikaathiri uchunguzi. Lakini kama utahitaji usaidizi tupo kwaajili ya kukusaidia. Hakikisha wahalifu wote wa tukio hili wanapatikana mapema iwezekanavyo. Naamini katika uwezo wako. Naamini kabla hawajapanga kufanya tukio jingine tutakuwa mlangoni mwao” RPC akamaliza. Kisha kikao kikao kikavunjwa na kila mmoja akaenda kwenye majukumu yake.

**************

Peter Mirambo akatoka, hapa alikuwa yupo njia panda, kuna tukio la Yasinta na Tukio la Profesa. Kwa upande wa Yasinta alikuwa ameshapiga hatua ya kiuchunguzi ingawaje haikuwa kubwa kivile. Kutokana na tukio la mwanzo ambalo hakupata ushahidi wowote wa CCTV Camera kutoka katika jengo lilipotokea tukio la Yasinta, sababu kubwa ikiwa kufutwa kwa video hizo. Jambo ambalo lilimfanya asione ni wakati gani Yasinta aliingia katika Hotel ile. Ushahidi pekee walioupata na kujua kuwa Yasinta alijirusha ghorofa ya kumi na sita ni baada ya kukuta kitambaa cha kujifutia ambacho walikichukua na katika kupeleleza wakagundua kilikuwa kitambaa chake.

Uzoefu wa Peter akajua kuwa kama atafuata kanuni za eneo kufuata protokali za kiuchunguzi kama kuanzia tukio lilipotokea basi hii inaweza kumchelewesha katika kazi yake. Aliamua kuelekea chuo kikuu cha taifa mahali ambapo profesa alikuwa akifanyia kazi, alipofika akaonyeshwa ilipokuwa ofisi ya Profesa Saimon.

Akawa anakipiga picha na kuchukua pembe mbalimbali. Alipomaliza, akaenda kukaa katika kiti alichokuwa anakaa profesa Saimon, hapo akawa anaangaza macho yake huku na huku kwenye kabati, mara kwenye shelfu zilizopo pale ofisini. Macho yake yakagota kwenye Dairy iliyokuwa juu kabisa ya kabati. Akaenda kuichukua, kisha akaanza kuifungua na kusoma kama atapata lolote la maana. Hakuona chochote, akaifunga kisha akawa anairudisha lakini akaghairi baada ya kuona maandishi nyuma ya jalada la ile Dairy. Lilisomeka jina moja Casto ambapo liliandikwa kama mtu ambaye alikuwa anaandika huku akifanya jambo jingine kama vile anaongea na simu huku akiandika. Hivyo ndivyo alivyokuwa akiwaza Peter. Hakuona jambo linguine la maana. Akaamua kuondoka pale ofisini akilenga kwenda kwa msaidizi wa Profesa ambaye walikuwa wanakaa ofisi moja, alipotoka akamkuta msaidizi wa Profesa akiwa amesimama na baadhi ya wanafunzi.

“ Samahani kwa kuwaingilia. Ninahitaji mnipe dakika tano tuu nizungumze na mwalimu wenu” Peter akasema akiwa ameachia tabasamu lake la uongo kuonyesha uungwana. Wale wanafunzi walimruhusu huku wakishangaa Draid za Peter mirambo. Msaidizi wa Profesa na Peter wakaingia ofisini.

“ Kuna mwanafunzi anaitwa Casto au mfanyakazi?”

“ Casto! Mmmh! Kwa kweli sijui kama kuna mwanafunzi au mfanyakazi mwenye kuitwa Casto”

“ Jana ulikuwa na Profesa?”

“ Ndio tulikuwa wote”

“ Alikuwa katika hali gani?”

“ Alikuwa kawaida sana. Tupo katika wiki za mitihani na usahihishaji. Alikuwepo hapa akisahihisha mitihani ya wanafunzi. Sikuona kama alikuwa anatatizo katika wiki hii”

“ Wiki ipi uliona anatatizo?” Peter alikuwa akimhoji huku akiwa anamtazama kwa umakini mkubwa.

“ Kuna wiki nyuma kidogo alikuwa anachangamoto na wanafunzi walio-carry kozi ambao walitakiwa kurudia mwaka. Hawa ndio walikuwa wakija mara kwa mara kumwomba awasaidie” Hapo Peter akachukua kidaftari chake na kuanza kuandika mambo aliyoyajua mwenyewe huku akimtazama Msaidizi wa Profesa.

“Waliokuwa wanatakiwa kurudia mwaka walikuwa wangapi?”

“ Ni wengi sana Afande”

“ Kama wangapi?”

“ Hamsini hivi”

“ Wote walikuwa wakija au walikuwa wanakuja mmojammoja?”

“ Hapana! Walikuwa wakija kila mmoja kwa muda wake”

“Uliwahi kushuhudia ugomvi wowote kati ya Profesa na moja ya hao wanafunzi waliokuwa wanatakiwa kurudia mwaka?”

“ Kwa kweli hapana! Wengi huja kwa kulia na kupiga magoti ingekuwa ngumu kwa wao kugombana na mtu wanayehitaji msaada kutoka kwake”

“ Sasa unafikiri ni jambo gani limepelekea Profesa kujiua kwa kujirusha ghorofani ukiwa kama mtu wake wa karibu, namaanisha msaidizi wake?”

“ Sidhani kama wanafunzi wanaweza kuwa sehemu ya yeye kujirusha, labda mambo mengine”

“ Mambo mengine kama yapi? “

“Mimi sijui Afande”

“ Jana uliachana na profesa wapi na saa ngapi?”

“ Jana tuliachana hapahapa ofisini majira ya mchana tofauti na siku zote ambazo huondoka jioni au usiku”

“ Hakukwambia alipoelekea..”

“ Alinambia kuna mtu anaenda kuonana naye, lakini hakuniambia mtu huyo na wapi wanapoenda kuonana”

“ Kisha?” “ akaondoka na ndio ilikuwa mara yangu ya mwisho”

“ Nani aliyekupa taarifa ya Kifo chake?

“ Mkuu wa chuo. Nafika hapa ofisini asubuhi ninashangaa watu wamekaa kimafungu mafungu. Sikuwa na shida na hilo, naingia hapa ofisini nashtuka kukutana na Mkuu wa chuo”

“ Kwa nini ushtuke?”

“ Unajua afande tangu nianze kazi sijawahi kumwona Mkuu wa chuo akija kwenye ofisi hii. Hivyo kitendo cha kumwona ofisi hii kilinipa mashaka”

“ Ratiba ya profesa kwa leo ilikuwa ni ipi?”

“ Nilimsikia jana akisema kuwa kuna jambo anataka kuonana na Mkuu wa chuo ili amshirikishe?”

“Hakukudokeza!”

“ Alinigusia kuwa ni kuhusu hawa wanarudia mwaka katika kozi yake”

“ Bado unasema kujirusha kwake hakuhusiani na hao wanafunzi?”

“ Sidhani kama inahusiana”

“ Kwa nini?”

“ Kwa sababu kozi zipo nyingi ambazo zimerudisha wanafunzi mwaka tena wengi kuliko kozi yake”

“Vizuri. Nashukuru sana kwa ushirikiano wako”

“ Nashukuru pia Afande”

Peter Mirambo akatoka na moja kwa moja akaelekea kwa Mkuu wa chuo, akafika na akakaribishwa.

“ Profesa Saimon kuna jambo lililokuwa linamsumbua tangu wiki mbili na nusu zilizopita kabla ya kuanza hii mitihani. Kuna siku asubuhi siku tatu kabla mitihani haijaanza alifika katika ofisi yangu akabisha kabisa hodi. Nikamkaribisha lakini hakuingia, nilimsikia akipokea simu, kisha akawa anafokeana na mtu aliyekuwa anaongea naye kwenye simu. Ni kama kulikuwa na mgogoro Fulani hivi. Sina uhakika. Lakini mazungumzo yake yalionyesha hakuwa anajua anazungumza na nani. Kwani kila muda alikuwa akimshinikiza aliyekuwa akiongea naye kwenye simu ajitambulishe. Kwa siku ya jana usiku alinipigia simu akaniambia kuwa leo asubuhi angekuja kuniambia jambo Fulani tata ambalo anahitaji msaada. Nilijaribu kumwambia jambo hilo haliwezi kuzungumzwa kwa simu akasisitiza kesho ambayo ndio leo kwamba angekuja ofisini tuzungumze. Maskini! Sijui nini kilitokea asubuhi Napata habari amejirusha ghorofani” Mkuu wa Chuo akasema akiwa mwenye huzuni.

“ Casto ni nani?”

“ Casto..!”

“ Ndio. Hujawahi kusikia jina hilo hapa chuoni?”

“ Mmmh! Casto hapa chuoni. Embu! Yupo lakini yeye ni Mkutubi wetu katika maktaba ya vitabu vya sayansi kule chini”

“ Ni Mkutubi umesema?”

“Ndio, katika maktaba ya vitabu vya kisayansi”

“Unahisi ni jambo gani ambalo Profesa alitaka kukuambia ambalo alishindwa kukuambia kwa njia ya simu” “Mmmmh! Nashindwa kukadiria Afande”

Peter Mirambo akamuaga Mkuu wa chuo moja kwa moja akaelekea kwa Mkutubi wa makataba ya kisayansi. Huko alikofika hakupata jambo lolote la maana. Hakukuwa na uhusiano wowote baina ya Casto Mkutubi na Profesa Saimon. Alibakiza sehemu moja pekee. Huko kama asingepata chochote kitu basi angehitimisha kuwa kesi ile ni ngumu na itahitaji muda zaidi. Huyo akaongoza njia akiwa ndani ya gari yake akiwa anaelekea mahali alikokuwa anaishi Profesa ambaye alikuwa akiishi Bunju. Ilimchukua nusu saa kufika nyumbani kwa Profesa. Alipofika alikuta tayari taratibu za msiba zikiwa zinaendelea ingawaje bado maiti ilikuwa hospitalini chini ya uangalizi wa polisi.

Baada ya kusalimiana na watu aliowakuta pale waliokuja kwaajili ya kumpa pole Mke na watoto wa Profesa. Peter alimtambua mke wa Profesa ambaye alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa anahuzuni nyingi. Uso wake ulikuwa umevimba na macho yakiwa mekundu kwa majonzi. Pembeni yake walikuwepo wanawake wawili waliokuwa wakimsaidia kumpa faraja. Alikuwa mama wa makamo ambaye kwa muonekano alionekana ni mtumishi wa serikalini. Peter baada ya kusalimia na kutoa pole, alijitambulisha kisha akaeleza sababu ya uwepo wake pale. Mke wa Profesa naye hakuwa na majibu ya moja kwa moja. Mazungumzo ya Peter na Mke wa Profesa waliyafanya wakiwa wametoka pale sebuleni na kwenda chumba cha kingine ambacho kulikuwa na faragha.

“ Mwanzo wa mwezi huu nilikuwa katika mgogoro na Profesa. Ni migogoro ya kifamilia kama zilivyofamilia nyingi. Lakini sidhani kama mgogoro ule ndio uwe chanzo cha Mume wangu kujiua”

“ Mgogoro wenu ulikuwa unahusu nini?”

“ Ni mambo ya siri ndugu afande”

“Enhee! Endelea”

“ Mgogoro huu ulisababisha mwezi huu mzima tusiwe na mawasiliano mazuri baina yetu. Hatukuongea tangu mwanzo wa mwezi huu. Ilikuwa tunaishi kama mabubu humu. Mpaka leo asubuhi nilipopata taarifa amejiua. Jamani mume wangu..” Anaanza kulia tena kisha Peter anajaribu kumbembeleza.

“ Nisamehe Mume wangu, huenda mimi ndiye chanzo cha yeye kujiua”

“Kwa nini unasema hivyo Mama?”

“ Kama tungezungumza na kuwekana sawa yasingefikia huku. Sasa nini kimetokea, ipi faida ya vile tulivyokuwa tumenuniana jamani! Aaah! Umelala Saimon”

“Kwa hiyo unahisi amejiua kwa sababu ya mambo ya kifamilia?”

“ Bila shaka:”

“ Inamaana mlikuwa na ugomvi mkubwa kiasi hicho?”

“Sasa ndio natambua kuwa kumbe mwenzangu kwake ilikuwa serious” Mke wa Profesa anazungumza kwa Kwikwi,

“ Kuna jambo unanificha Mama, tafadhali eleza kila kitu kuisaidia polisi ili tujue namna ya kutoa msaada. Siku ya jana ilikuwaje kwa Profesa”

“ Afande hakuna nilichoficha hapo labda kama unataka nieleze siri za nyumba yetu. Kuhusu jana, kama nilivyokuambia humu ndani tangu mwezi uanze tulikuwa tunaishi bila kuwasiliana. Hujui mwenzako akitoka anaelekea wapi na wala naye hajui unaelekea wapi. Zaidi utajua anaelekea kazini” anameza mate.

“ Wewe bado ni kijana, mambo ya ndoa ni very complicated hasa migogoro ya usaliti ikiingia kwenye familia. Sijui hata nieleze kwa namna ipi?” akawa anafwinafina makamasi mepesi yaliyokuwa yameanza kumtoka puani.

“ Ndio nataka unieleze kwa namna hiyo Mama, sipo hapa kama mwandishi ambaye nitatoa habari zenu. Nipo hapa kama Afisa wa upelelezi. Mambo mengi utakayoniambia ambayo niya kifamilia yatabaki kuwa siri. Kanuni za kazi yangu hainitaki kutoa taarifa kama hizi kwa mtu yeyote. Muhimu ni kujua nini kimetokea kwa sababu mtu kujiua kama ujuavyo ni jinai. Kujiua ni uhalifu mkubwa kama kuua mtu mwingine. Kikawaida mpaka mtu anafikia kujiua mara nyingi hutokana na kufanyiwa mambo mabaya ambayo kwetu sisi polisi tunayaita uhalifu. Ndio maana niko hapa.” Peter akameza mate. Kisha akaendelea,

“ Unakumbuka wiki mbili zilizopita tukio la binti kujirusha ghorofani kam mumeo?”

“ Ndio nakumbuka”

“ Matukio haya sisi kama polisi tunayaona kama yanahusiana. Tunaomba uisaidie polisi, kueleza kila kitu”

“ Kama nilivyojieleza, nothing else zaidi ya migogoro ya kifamilia. Kama unataka nimuabishe mume wangu mbele yako hilo sipo tayari kulifanya”

“Basi wewe polisi itakuchukulia wewe kama mhusika wa tukio hili. Utakuwa sehemu ya chanzo cha uhalifu uliotokea ambao mumeo kaufanya. Kama ujuavyo mfanyaji wa uhalifu na msababishi wote wanakuwa wahalifu”

“ Sikuelewi Afande”

“ Huwezi nielewa kwa sasa. Tutaondoka wote kwenda kituo cha polisi utatoa maelezo huko alafu tutakushikilia kwa muda. Kwa sababu ushaeleza kuwa mlikuwa na mgogoro basi hii inaonyesha chanzo cha moja kwa moja ni wewe”

“ Afande nafikiri utakuwa hujui unachokisema. Mimi Yule ni mume wangu. Nawezaje kumuua?”

“ Umeshindwa kujieleza ipasavyo, mimi nimekuuliza kwa uzuri, tulianza vizuri kabisa, lakini naona unazuia jeshi la polisi kupata taarifa muhimu juu ya tukio hili. Nani alikuambia siri zenu za familia jeshi la polisi litazitoa. Ulisikia wapi na lini jeshi letu likitoa siri za familia za watu?”

“ Naona yanataka kuwa makubwa..”

‘Mtu akishajiua au kuuawa tayari ni makubwa. Uhalifu wowote hupelekea mambo kuwa makubwa. Ukileta mzaha yanaweza kuwa zaidi yakakugeukia wewe. Sidhani kama upo tayari”

“Nimekuelewa” Mke wa Profesa akajibu, hofu ya kuwekwa korokoroni ilimuingia. Akashusha pumzi kisha akainama chini. Alafu akainua uso wake na kumtazama Peter.

‘Niligundua mume wangu anamahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine ambaye nilifumania jumbe zake kupitia simu ya mume wangu. Inaonekana kabisa tayari mahusiano yao yalikuwa ya muda mrefu. Kama ujuavyo usaliti unaumiza mno. Nikagombana sana na mume wangu”

‘ Subiri! Samahani kwa kukukatisha. Huyo mwanamke aliyekuwa anatoka na mumeo unamfahamu?”

“ Simfahamu! Ila nilizichukua namba zake na kuzihifadhi ili nimfuatilie”

“Hizo namba uko nazo”

“ Yaani! hapana!”

“ Kivipi?’

“ Tukagombana sana siku ile, nakumbuka hatukulala tukiwa tunapigishana makelele. zile namba nilikuwa nimezificha kwenye pochi yangu, nikilenga kuwa kesho yake ningezifuatilia. Kesho yake asubuhi nikatoka nikiwa nimemkasirikia sana Profesa. Nikiwa ndani ya gari yangu nikiwa naelekea kazini ile natoka kwenye hicho kibarabara ulichokuja nacho, nikakuta vijana wawili, mmoja akiwa kalala chini kama anashida, alafu wa pili akiwa anaomba msaada. Mimi nikiwa ndani ya gari sina hili wala lile. Nilipoona tukio lile kama mwanadamu nikajua wale vijana wanahitaji msaada. Nikasimamisha gari langu, nikashuka. Nilipofika pale, Yule kijana aliyekuwa mzima anamsaidia akaniambia kuwa walikuwa wakifanya mazoezi ya kukimbia, ghafla mwenzake akaanguka. Ndio hali ile. Nikamwambia tusaidiane tumpakize kwenye gari. Lakini Yule kijana..” Mke wa Profesa akameza fumba la mate, kisha akaendelea,

”Yule kijana akaniomba kama ninamaji kwenye gari tumsadie kummwagia ndipo tumpeleke hospitali. Nikaenda kuchukua maji, Kisha akammwagia Yule kijana aliyezimia pale chini. Ghafla Yule kijana akazinduka. Nikawa nashangaa huku nikimtathimini. Licha ya kuwasisitiza tumpeleke hospitali wakasema anajisikia vizuri. Wakanishukuru. Kisha tukaagana mimi nikarudi kwenye gari nikaondoka zangu kwenda kazini. Nafika kazini natafuta mkoba siuoni. Tafuta wapi. Khee! Nikajua labda nimeuacha nyumbani. Nikapiga simu nyumbani kwa dada wa kazi. Naye akaniambia mkoba haupo na aliniona nikitoka nao. Moja kwa moja nikajua wale vijana ndio waliniibia. Ile ilikuwa mbinu tuu ya kuniibia. Huenda wakati nimesimama na wale vijana wawili kulikuwa na kijana mwingine aliyeenda kuchukua mkoba wangu kwenye gari kwani sikufunga mlango wa gari”

“Mmmh! Hao vijana unawajua?”

“ Siwafahamu. Ila najua walitumwa na mume wangu?”

“ Kivipi?”

“ SI kile kikaratasi cha huyo mchepuko wake. Nahisi hakutaka niwasiliane naye”

“ kwa nini isiwe vibaka tuu?”

“Kwenye gari ilikuwepo simu na pesa kwenye kiti lakini mbona hawakuchukua vitu hivyo”

“Endelea”

“Tangu siku hiyo ambayo ndio mwanzo wa mwezi huu tukaingia katika mgogoro rasmi na mume wangu. Huku yeye akijitahidi kunibembeleza. Nami nikimwambia siwezi msamehe mpaka anipe namba za huo mchepuko wake. Tukaishi kwa kuwekeana vikwazo. Wiki moja baadaye nilimuona akiwa katika sonona na akiwa kila mara anahangaika kuongea na simu za hapa na pale. Nakumbuka kuna binti mmoja alikuwa anaongea naye kwenye simu kuhusu mambo ya kurudia mwaka, ni kama Yule binti alikuwa amemtia katika shinikizo”

“Unamaanisha nini? Wewe ulikuwa karibu ukisikiliza mazungumzo yake?”

“ Mimi nilikuwa nimelala kitanda kingine lakini chumba hichohicho. Sikuwa namsikia huyo binti lakini mazungumzo ya mume wangu yalionyesha kabisa wapo katika mgogoro na huyo binti. Ni kama tayari Mume wangu alikuwa ameshalala na huyo binti lakini profesa akawa anakataa kutimiza ahadi yake ya kumsaidia. Moja kwa moja nikahisi ndio uleule mchepuko wake ”

“ Hukufanikiwa kusikia akitaja hata jina lake?” Peter Mirambo akamkatisha,

“ Sikufanikiwa”

“ Casto anahusiano gani na Mumeo?”

“ Waziri wa Nishati na Madini sio?” Mke wa Profesa akasema, jibu hilo lilivuruga utulivu wa Peter, hakutegemea kusikia kitu kama hicho. Peter akasema akijifanya anajua uhusiano uliopo baina ya Casto na Profesa

“ Yeah!”

“ Mimi sijui. Lakini wiki mbili zilizopita waliwasiiana mara moja hivi. Nikiwa jikoni nilimsikia akimtaja Mhe. Casto kwenye simu kana kwamba alikuwa akizungumza naye”

“ Hapo mwanzo hawakuwahi kuwa na mahusiano na Mhe. Casto?

“ Kwa kweli nipo ndoani mwaka wa thelasini sijawahi kusikia wala kujua kama Profesa na Casto wanazungumza. Hii ilikuwa mara ya kwanza”

“ Hakuna kingine ulichosikia siku hiyo Mumeo akiongea na Casto kwenye simu?”

“ Sikusikia kitu kingine kwa sababu jina lake nililisikia mwishoni mwa mazungumzo yao. Alafu kama nilivyosema nilikuwa jikoni”

“ Pole sana kwa msiba na matatizo” Peter akasema, alikuwa akiandika andika jambo Fulani kwenye kidafari chake kidogo cha kumbukumbu, maelezo ya mke wa profesa yalimpa mchoro na kiramani cha kufuata. Sasa kazi yake ilianza kumpa matumaini. Akaagana na mke wa profesa kisha akaondoka nyumba ile akiwa sasa moyo wake umepata nguvu.

“Kuna Mchepuko, alafu kuna wanafunzi wanaorudia mwaka, alafu kuna Wezi waiba mkoba, alafu kuna Mhe. Casto. Sidhani kama mchepuko wa Profesa atakuwa ni moja ya wanafunzi kama alivyosema mke wa Profesa. Lakini you never know. Wezi wanahusiana na Profesa hili nalo linanipa kigugumizi. Vipi kama Yasinta ndiye aliyekuwa mchepuko wa Profesa? Mmmh! Sidhani! Hakuna uhusiano wowote. Uhusiano upo. Upo? Ndio. Huoni wote wamekufa kifo kinachofanana. Sio kirahisi hivyo Afande” Peter Mirambo alikuwa akichorachora kwenye kikaratasi kingine vile alivyoona uhusiano wa wahusika ambao wamejitokeza katika uchunguzi wake. Alikuwa kwenye gari akiwa ameliegesha kilometa chache kutoka iliponyumba ya Profesa.

Katika mambo ya kipelelezi jambo kubwa zaidi ni uhusiano wa wahusika, matukio, na mandhari. Hicho ndicho anachojaribu kukitafuta Peter katika kazi yake hiyo. Kipi kinatangulia. Iko hivi. Mazingira au mandhari ndio hutangulia, kisha wahusika alafu tukio. Vyote huwa ndani ya Muda.Uhusiano wa mazingira na mazingira, uhusiano wa wahusika ambapo hupelekea na kuchochea utokeaji wa tukio. Uhusiano wa mazingira na mtu, uhusiano wa tukio na mazingira, uhusiano wa tukio na mtu. Uhusiano wa tukio na muda.

Mazingira yanahusiana kama vile watu wanavyohusiana. Mfano Dar es salaam na Pwani kuna uhusiano wa karibu zaidi kuliko Kigoma au Katavi. Tanzania na Uingereza au Ujerumani kuna uhusiana tofauti na Tanzania na Peru. Katika mambo ya kiuchunguzi, matukio huenda kwa mahusiano. Kimazingira, watu wanaoishi maeneo ya karibu mfano Wakwere na wazaramo au wandendereko wanaongea lugha zinazokaribiana na kusikilizana na hata mila hufanana tofauti na jinsi unavyozidi kwenda mbali kama vile uende Dodoma na jamii zake hupishana na jamii za pwani. Ukaribu wa mazingira huathiri uhusiano wa wahusika na matukio.

Vivyo hivyo katika mambo ya kipelelezi na uchunguzi, Tukio linapotokea na haupo basi mambo ya kuzingatia ni pamoja na hayo. Tukio limetokea na mazingira yapo hivyo kinachotafutwa na wahusika. Au mazingara hayafahamiki lakini tukio linafahamika au vivyohivyo.

“Kuna nafasi mbili ambazo zinahitaji kipaombele ili kutoathiri uchunguzi na kuufanya uishe upesi. Kati ya Mhe. Casto na Huyo mchepuko wa Profesa nani nianze naye?” Peter alikuwa anawaza huku kalamu ipo mdomoni. Kichwani alikuwa amevaa kofia iliyoficha Draid zake fupi.

“ Nitaanza na Mhe. Casto kwa sababu ndiye mhusika ambaye yupo dhahiri ninayemjua”

Akawasha gari yake na kuondoka eneo lile.

**************

ITAENDELEA
0693322300
 
Aisee ..kali snaaa 🙌🙌🙌🙌
 
RIWAYA YA CONNECTION EP 04

Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300
ILIPOISHIA
“Kuna nafasi mbili ambazo zinahitaji kipaombele ili kutoathiri uchunguzi na kuufanya uishe upesi. Kati ya Mhe. Casto na Huyo mchepuko wa Profesa nani nianze naye?” Peter alikuwa anawaza huku kalamu ipo mdomoni. Kichwani alikuwa amevaa kofia iliyoficha Draid zake fupi.

“ Nitaanza na Mhe. Casto kwa sababu ndiye mhusika ambaye yupo dhahiri ninayemjua”

Akawasha gari yake na kuondoka eneo lile.

**************
ENDELEA

THE BLACKCROSS CASINO, DSM.

Wanaume wawili wanaolingana umri wameketi kwenye sofa ndogo wakiwa wametenganishwa na meza ndogo yenye vichwaji. Kelele za muziki na watu ndani ya Casino zinaendelea ingawaje hazizuii mazungumzo yao. Vimulimuli vya taa zenye rangi mbalimbali zinafanya eneo lile liwe na mwonekano wa kipekee. Wanawake warembo waliovalia nusu uchi walikuwa wakiendelea kujivinjari na muziki na kuzungukazunguka mule ndani kwa miondoko ya kikahaba na kufanya pawe na hekaheka. Wengine wakiwa wamebeba vinywaji mikononi, wengine wakiwa na wanaume wakiwa wanacheza, wengine wakivuta shisha. Kwa kweli kulikuwa kumechangamka haswa.

Amini Boko muda wote alikuwa mdomo wazi akishangaa vioja na uchafu uliokuwa unaendelea mule ndani. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia Casino. Na kama asingeletwa na Koloa Katani ambaye ni rafiki yake huenda angemaliza maisha yake yote pasipo kufika maeneo ya namna ile. Amini na Koloa urafiki wao ulianza miaka kumi iliyopita walipokuwa wakisoma katika chuo kikuu cha utabibu, wote ni madaktari, Medical Doctor. Miaka mingi ilishapita tangu wamalize shule. Amini akiwa ameenda Morogoro maeneo ya Gairo kwaajili ya Kilimo. Alichukua uamuzi huo baada ya kuona hapati ajira hapa mjini huku muda nao ukisonga kwa upesi. Kukaa miaka mitatu na nusu mjini kwa kuungaunga pasipo kazi rasmi kulibadilisha mtazamo na msimamo wake. Ndipo alipochukua uamuzi mgumu wa kwenda kufanya kilimo maeneo ya Gairo. Kwake ulikuwa uamuzi mgumu kutokana na kuwa hakuwahi kufikiri kuwa maisha yatamfikisha katika hatua ile. Kama walivyo wasomi wengi wenye matarajio na tegemeo katika elimu walizozisotea kwa miaka karibu miongo miwili, alafu mwisho wa siku wanajikuta katika shimo lenye ukingo ambao mbele kuna shimo jingine lenye giza ambalo hawajui mwisho wake. Nidvyo ilivyokuwa kwa Amini Boko.

Ndiye huyu leo yupo katika Casino hii ambapo Mbele yake alikuwa ameketi rafiki yake ambaye kwa muonekano tuu usingeshindwa kujua kuwa ni kijana mdogo mwenye ukwasi usiopimika. Mikono ya Koloa ilikuwa imepangwa na mikufu ya shaba huku vidole vyake vikiwa vimelindwa na pete za dhahabu. Shingoni ukiwepo mkufu wenye vito vya thamani. Mkufu huo ulionekana kutokana na aina ya nguo ya juu aliyokuwa ameivaa. Alikuwa amevaa kaushi katamikono iliyoacha makwapa yake wazi, huku mikono yake ikiwa na michoro mbalimbali ya Tattoo.

Amini hakushangazwa pekee na Casino hilo bali pia tabia na mwonekano mpya wa rafiki yake kipenzi ambaye wakati wanasoma chuo alikuwa muumini mzuri wa dini. Koloa alikuwa akipenda sana kuimba nyimbo za injili. Ratiba yake ilikuwa chuoni, cafteria na kwenye ukumbi wa kufanyia ibada. Hakuna aliyewahi kudhani wala kutabiri kuwa siku moja Koloa angebadilika kwa kiwango cha kutisha namna ile.

Lakini ndivyo ilivyo katika maisha. Mambo huenda nje ya matarajio ya wengi. Maisha hubadilika na yanapobadilika wengi hubadilika nayo huku wachache huthubutu kufurukuta. Mwema huweza kugeuka kuwa mbaya. Na Yule aliyeonekana kuwa mbaya wakati mwingine watu hushangaa anageuka na kuwa mwema. Hiyo wala sio hadithi isipokuwa ni kweli kwa sababu inatokea kila siku na watu ni mashahidi

“ Umechagua uamuzi wa ajabu sana Koloa. So haya ndio maisha yako Mapya?”

“ Huu ni uamuzi niliochelewa kuufanya. Kuna wakati najuta kwa nini sikufanya maamuzi haya mapema. Nilijitesa bure. Nililaumu wengi bure. Sasa kwa maamuzi haya nimegundua kuwa sipaswi kufikiri kwa namna ya zamani. Siku zote nitabaki kutazama mbele” Koloa alisema huku akionyesha meno yake ambayo baadhi yalikuwa na rangi ya dhahabu na mengine ya silver. Huku mara kwa mara akivuta sigara.

“ Mimi naona hii njia uliyochukua sio sahihi. Unakosea My friend” Amini akamwambia,

“ Hahaha! Kijana.. Sikiza Amini. wakati nimekukuta pale kituo cha daladala nilipokuchukua na gari unakumbua uliniambia nini?” “ Uliniambia kuwa hujui jambo gani umemkosea Mungu. Maisha yako huyaelewi na huoni mbele nini kitatokea. Kurudi nyuma huwezi na mbele huoni. Ukasema kuwa mambo yameenda kwa namna ya kuogopesha. Ukaniambia kwa sasa unaishi kwa hofu. Leo wewe usiyeona mbele utaniambia kweli njia niliyoichukua sio sahihi. Wewe njia uliyopo ni sahihi?” Koloa akasema,

“Lakini sio maisha haya”

“ Kuingia hapa umetumia dola za kimarekani ambazo ninauhakika hukuwahi kuzishika. Kule gairo hizi pesa hazipo. Unajua mimi na wewe imetugharimu dola ngapi humu? Zaidi ya dola elfu moja. Unajua maana yake hiyo. Pesa madafu kama milioni mbili na chenchi. Hivi vinywaji hapa, kisha hao Malaya hapo unajua nitatumia nao ngapi?” Anamtazama amini akiwa anatabasamu kisha anaachia kicheko cha dharau na kuchukua kinywaji chake kilichokuwa mezani na kubwia fumba kadhaa.

“Udaktari haikuwa njia sahihi. Ulikuwa utoto tuu ule. Utoto na kujidanganya. Na make dola za kutosha. Nikikuambia niliyonayo kwa sasa unaweza pandisha Bp hapa. Nitakuua rafiki yangu. Hahahaha!” Anacheka kisha anamvuta kahaba aliyekuwa anapita karibu, Yule kahaba anajizungusha kimadoido kisha akamkalia Koloa kwenye paja lake na kuanza kumpapasa kifua na kushika ndefu zake. Amini mambo hayo alikuwa akiyaona kama anaangalia tamthilia Fulani ya wakamaria wa Newyork. Yule kahaba aliyekuwa amevaa kichupi aina ya bikini huku maziwa yake yakiwa yamechikiliwa na vinyoya vyenye muundo wa kipepeo. Sehemu zingine za mwili zikiwa uchi. Kahaba Yule mwenye macho ya ajabu na makeup ya kishetani akamtazama Amini kwa macho ya kishenzi, alafu kwa upesi akanyosha mkono na kumpokonya Shisha kahaba mwingine aliyekuwa akijivinjari na muziki aliyekuwa akipita pale. Yule kahaba akachukua ule mrija wa shisha na kuvuta vyakutosha kisha akajibetua kwa mshtuko kama anatawanya mkiono yote miwili kwa nyuma, punde kwa sekunde akairudisha mikono kwa mbele ikiwa haina ile shisha. Kwani ilikuwa imechukuliwa na kahaba mwingine aliyekuwa meza ya nyuma.

Amini akiwa anashangaa jambo hivyo, Yule kahaba akapanda juu ya ile meza yao ndogo yenye vinywaji kisha akainama mpaka ulipo uso wa Amini, kisha akampulizia moshi usoni, jambo ambalo likamfanya Amini kufumba macho. Alipofumbua macho yake hakumwona Yule kahaba, isipokuwa cheko la starehe kutoka kwa Koloa.

“Haya ndio maisha ndugu yangu. Furahia dunia. Chukua hii. Hizi ndio za kitasha. Achana na Local beer”

“ Daaah! Sijajua! Hizi pesa umepata wapi Koloa. Kufuru yote hii. Umenichangaza sana”

“ Hujashangaa! Utashangaa…” wakati Koloa akiongea ghafla anakuja mwanamke mmoja anamuinamia kwenye sikio lake na kumnong’oneza jambo Fulani. Koloa anageuka nyuma kabisa jambo ambalo linamfanya Amini naye aangalie anapotazama Koloa. Mbele kabisa kama mita ishirini hivi wanaonekana wacheza kamari wakiendelea kucheza kamari lakini kuna kijana mmoja mweusi mwenye upaa uliomuanza akiangalia upande waliokaa Amini na Koloa. Mwanaume Yule anatabasamu na kumpa ishara Koloa. Kisha anageuka kuendelea kucheza kamari.

“Nani Yule”

“Muite Kalage Nyundo. Huyo ndiye Mastermind na Gamechanger katika maisha yangu. Tangu nilipokutana naye miaka mitatu iliyopita kila kitu changu kilibadilika. Kwangu ni Mkombozi. Walinitesa sana” Anameza fumba la mate kisha anamtazama Amini, alafu anafutua mashavu yake na kubeua.

“Nani walikutesa?”

“ Sio story mpya Ankoli. Sikia twende pale kwenye kamari ukajionee pesa zinavyotafutwa”

Wakanyanyuka. Wakiwa wanapita kwenye njia zenye msongamano wa watu waliokuwa wakijivinjari kwa kucheza. Baadhi ya makahaba walikuwa wakijichetua na kumsonga kama sio kumchombeza Amini kutokana na mwonekano wake ambao uliwafanya wamuone kama sio mwenyeji na mzoefu wa maeneo ya namna ile.

“ Eeeh! Winga! Huyo nani?” Kalage aliongea akiwa amekaa huku nyuma yake wakiwa wamesimama makahaba wawili waliovalia viguo vyeusi vya ajabu vilivyoacha miili yao uchi. Mbele ilikuwepo meza kubwa yenye kete kadhaa na karata za kamari. Meza hiyo ikiwa imezungukwa na wanaume na wanawake walioketi wakicheza kamari. Hao ni Wakamaria.

“ Huyu ni Ankoli wangu. Mshikaji wangu sana” Kolowa akajibu akiwa anamtambulisha Amini. Wakamaria baadhi wakamtazama Amini huku wengine wakionyesha kutokujali uwepo wao. Walichojali ni kujituliza na kujivinjari kwa starehe zilizowafanya wajione hawapo duniani na hakuna kama wao.

“Isijekuwa umetuletea njangu hapa”

“ Hahaha! Hapana Mkuu”

“ leo ni siku tasa, nimeshapoteza milioni kumi hapa” kabla hajamaliza Amini akaguna baada ya kusikia kiasi hiko. Wakati yeye akahangaika kila siku kutafuta pesa kwa udi na uvumba, kwa kusudi na kuomba lakini haambulii chochote. Tangu azaliwe na kumaliza chuo miaka zaidi ya mitano iliyopita hakuwahi kupata hata milioni moja kwa pamoja. Leo kwa macho yake na wala si hadithi anashuhudia watu wakichezea mamilioni ya pesa kwa usiku mmoja. Akajikuta akalengwa lengwa na machozi. Aliwaza kama angezipita basi angeweza kutimiza malengo yake ya kufungua Kliniki kwaajili ya kutoa huduma ya afya, ukizingatia yeye ni Tabibu.

Lakini siku zote mawazo ya mkosaji huwa kama ulimi wa bubu usioweza kuumba maneno. Kushindwa kuyauamba mawazo yatokee ni tatizo linalokabili wengi tangu zamani. Mawazo ni kama maji yanayayohitaji mkondo wa kufuata. Utekelezaji wa mawazo ni jambo kubwa na lamaana ambalo wengi hushindwa kutokana na visingizi mbalimbali, moja ya visingizio maarufu duniani ni pamoja na ukosefu wa mtaji. Vijana wengi huchukulia pesa kama msingi mkuu wa kutimiza mawazo na maono yao. Pesa ni jambo moja lakini kuna ziada ya muhimu na kubwa kuliko ambayo ni; nia na uthubutu. Nia ili itimie inahitaji mipango na utekelezaji unaochochewa na uthubutu.

“Mimi kwa leo acha niwahi kuondoka. Sipo vizuri” Kalage akasema, huku akichukua kofia yake iliyokuwa juu ya meza ya kamari kisha akaivaa kichwani.

“ Sisi tupo! Nipo na rafiki yangu huyu. Acha nimuonyeshe dunia asiyoijua. Ankol nataka ujione haupo serious kwenye haya maisha.. hahahahah” Kolowa akasema kisha wote wakacheka pamoja na wale makahaba isipokuwa Amini. Angewezaje kucheka kwa dhihaka anazofanyiwa.

Kalage akaondoka akiwa ameambatana na wanawake wawili waliovalia nguo za kikahaba mmoja akiwa amemshika upande huu na mwingine upande mwingine, kalage akiwa katikati .

“ Twende huku” Kolowa akamwambia Amini. Wakapanda juu upande wa ghorofani. Huko kulikuwa na tafrani zaidi. Watu walitumia pesa kujivinjari kama wendawazimu. Muziki uliokuwa ukipigwa ulikuwa wa kimataifa kulingana na idadi kubwa ya watu waliokuwa mule ndani walikuwa wageni kutoka mataifa ya nje. Wazungu kwa jamii zao, wachina, waarabu, wahindi na waafrika kutoka bara la afrika. Hata makahaba wa upande huu walikuwa wakimataifa. Lugha kuu ilikuwa kingereza. Kila kitu alichokuwa anakiona Amini kilikuwa kama filamu ya kuharibu maadili yake. Ni zile filamu ambazo hutolewa angalizo na onyo kali kwamba hairuhusiwi chini ya miaka kumi na nane kutazama au kuiangalia na mtu unayeheshimiana naye.

“Unaona chuma hicho” Kolowa akasema huku akimtazama Amini aliyekuwa akimshangaa mlimbwende mwenye uzuri wa ajabu. Amini alimfananisha Yule mrembo na mwanamuziki aitwaye Beyonce.

“Unahitaji kulala naye? Sema nikununulie. Hello cute..” Kolowa akasema huku akimshika Yule kahaba wa kizungu aliyefanana sana na Beyonce, lakini Amini akamzuia.

“ Kwa nini unanizuia? Dola mia tano tuu unalala naye usiku mzima” Kolowa akasema akiwa amekereka kwa kitendo cha Amini kumzuia. Muda wote walikuwa wakiongea kwa sauti kubwa ili wasikilizane kutokana na sauti kubwa ya muziki uliokuwa ukipiga.

“ Kwa leo hapana ndugu” Amini akasema,

“ Noo! Ankol unajua mpaka sasa hivi hujamaliza laki moja. Sasa ndio kujivinjari gani. Nimekuleta hapa usafishe macho, uoshe koo, na utakase rungu lako. Acha ushamba Ankoli”

“ Sio hivyo Bro. kwanza hapa nilipo nimechoka, nilitamani sana kuona mambo haya akili yangu ikiwa imetulia. Unajua ndio nimerudi Dar miezi mitatu iliyopita. Bado mambo yangu hayajakaa vizuri. Pale ninapoishi nimeshakueleza nadaiwa kodi. Hapa penyewe sijui kama Yule Landlord hajatoa vitu vyangu. Maana asubuhi alinambia kuwa nkirudi niwe na kodi yake..”

“ Oyaa! Hayo tushajadili. Nikakuambiaje?” Nakuelewa lakini mpaka usiku huu sina hakika na usalama wa vitu vyangu”

“ Anyway! Usijesema nakuendesha. Shika hii itakusaidia kwa kiasi”

“Nashukuru sana ndugu yangu. Lakini nisamehe sana kama nimekuharibia furaha yako”

“ Sio kitu! Nia yangu ilikuwa nifurahi na my bestfriend, wewe ni kama ndugu yangu. Tumetoka mbali. Tumepitia mengi sana” kolowa alikuwa akiongea huku akinywa, pombe zikiwa zimeanza kumkolea. “Sikia Ankol, wewe ni ndugu yangu. Kuwa na amani. Rudi home kamalizane na huyo mwenye nyumba wako. Tutapanga siku nyingine” Kolowa akaongea akiwa anamgonga gonga Amini kwenye kifua. Wakaagana. Amini akaondoka akiwa amepewa milioni moja.

********************

Peter alikuwa ameliegesha gari lake umbali wa mita hamsini toka ilipo ofisi ya Waziri wa nishati na madini jijini Dar es salaam. Wapi pengine angempata kwa urahisi zaidi ya mahali ofisi yake ilipo. Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili jioni. Upepo wa bahari ukiwa unapuliza vilivyo na kulifanya eneo lote lile liwe limepoa. Baadhi ya ofisi za eneo lile zilikuwa zimeshafungwa. Peter alikuwa macho akimsubiria Mhe. Casto atoke. Haichelewi pa mwenye subiri. Punde Peter akaiona gari ya Mhe. Casto ikitoka. Hiyo! Hiyo! Hiyo! Ikampita mahali alipokuwa amepaka. Akajihakikishia aliyekuwa anaendesha ni Mhe. Casto baada ya kumwona akiwa kavaa suti yake ya kijivu. Jambo moja lililomshangaza Peter ni kumwona Mhe. Casto akiendesha gari mwenyewe badala ya kuendeshwa na dereva. “ Ni leo tuu au ni siku zote anaendesha mwenyewe” Peter akawaza huku akiwa amelifungia mkia gari la Mhe. Casto.

Walienda kwa kitambo huku Peter akiwa makini kuepuka kushstukiwa. Wakafika Makumbusho, akaiona gari ya Mhe. Casto ikiingia sheli. Peter akapita na kwenda kusimama mbele ya mataa ya Makumbusho, kituo cha sayansi. Macho ya Peter yalikuwa kwenye vioo vya pembeni vya kutazamia nyuma akilitazama gari la Mhe. Casto, ambapo aliliona likiwa linatoka kituo cha mafuta kisha likavuka mataa na kumpita. Naye akaingiza gari barabara na kuanza kumfukuzia. Tayari giza lilikuwa limeanza kuingia huku foleni ikiwa kero kwani walikuwa wakisimama mara kwa mara.

Peter akatoa sigara na kuiweka mdomoni kisha akawa anavuta huku akiyapa mawazo yake nafasi katika kichwa chake. “Mke wa Profesa amenifungua macho kwa kiasi kikubwa. Naamini kutakuwa na kitu baina ya Mhe. Casto na kesi inayoendelea. Lakini kwa nini Mhe. Casto awe chanzo cha Profesa kujirusha ghorofani? Wapi wamegongana. Ni maslahi yapi yam he. Yameguswa. Lakini hapana.” Anavuta pafu kadhaa za sigara kisha anaendelea;” nikisema Mhe. Casto anahusika kwa kujirusha na kujiua kwa Profesa saimon, vipi pia anahusikaje katika kifo cha Yasinta? Hii haiingii akilini. Kuna kitu bado sijakijua. Lakini acha kwanza nijue uhusiano uliopo baina ya Mhe. Casto na Profesa Saimon, kisha itajulikana.”

Wakati huo walikuwa wakikatisha eneo moja liitwalo mbuyuni wakakata kulia kuchukua uelekeo wa kunduchi. “ Mhe. Anaenda wapi huku” Peter alikuwa akiwaza kwani alijua kuwa Mhe. Casto anaishi Mbezi Beach. Hii ikazidi kumpa mchecheto na kuamini kuwa yupo sahihi.

Wakapita Kunduchi na sasa walikuwa wakiikabili bahari beach. Saa yake ilionyesha ni saa mbili na nusu za usiku. Kutokana na wingi wa magari yaliyokuwa barabarani ya watu waliokuwa wakirudi majumbani mwao. Mwendo haukuwa wa kasi, walikuwa wakiendesha polepole. Muda wote Mhe. Casto hakujua kama nyuma yake anafuatiliwa. Wakapita kituo cha daladala cha ununio kisha wakasonga kwa dakika wakakata kulia. Kisha wakasonga mpaka walipovuka daraja ambapo mkono wa kulia kulikuwa na bahari. Wakasonga mbele kidogo kisha gari ya Mhe. Casto ikakata kushoto kwenye barabara ndogo yenye moramu. Peter akapunguza mwendo akaiacha gari ya Mhe. Casto iende mbali zaidi kwani aliamini kuwa tayari wapo karibu kufika kutokana na mwendo wa gari ya Mhe. Casto, ilikuwa ikienda polepole sana. Hazikuzidi dakika tatu akaiona gari ya Mhe. Casto ikiwa imesimama mbele ya geti kubwa la kisasa ambalo ndani yake kulikuwa na jumba kubwa la ghorofa ambayo imepakana na bahari kwa upande wa magharibi kaskazini.

Peter naye akasimamisha gari, kisha akaipaki kwa pembeni, akiwa anaitazama gari ya Casto iliyokuwa imesimama nje ya geti. Zikapita dakika kama tano kukiwa kimya. Tayari ilikuwa saa tatu usiku. Ghafla Peter akashangaa kumwona mwanamke mmoja mweupe pee mwenye umbo namba nane aliyevalia kigauni kifupi kilichoacha mapaja nje akitokea ndani ya lile geti. Mkononi akiwa amebeba simu janja. Yule mwanamke akafungua mlango wa mbele wa gari kisha akapanda. Zikapita dakika tatu hivi zilizomuacha Peter akijiuliza mwanamke Yule ni nani lakini bila ya kupata majibu akashtuliwa na taa za lile gari la Mhe. Casto kuwaka. Mawazo yake yakarejea tena.

Ile gari likageuza likawa linarudi kisha likampita Peter. Hii ilimaanisha Mhe. Casto alikuja kumchukua Yule mwanamke mweupe.

Peter naye akaunga tela. Safari ya kurudi njia ileile waliyoitumia kujia ikaanza. Mara hii hakukuwa na foleni sana kutokana na kuwa usiku ulizidi kuimarika lakini pia hii ilitokana na kuwa watu wengi kwa muda ule hawakuwa na safari za kwenda mjini. Wakafika bagamoyo road. Kidogo hapa wingi wa magari ukaongezeka jambo ambalo likawafanya waende mwendo wa nidhamu. Haikuwachukua muda walikuwa wakikatisha maeneo ya Morocco wakitafuta daraja la Salenda. “Casto anampeleka wapi Yule mwanamke. Ni naniake? Au ni hawara wake”” Peter akawaza. Tayari walikuwa wameshaingia mjini, ilikuwa tayari ni saa tano za usiku. Jiji likiwa limepambwa na taa za majumba na maghorofa pamoja na vyombo vya usafiri ambavyo vilikuwa vinazidi kupungua kadiri muda ukisogea.

Ghafla akaiona gari ya Mhe. Casto ikisimama mbele ya geti la kuingilia katika casino iliyoandikwa; THE BLACKCROSS CASINO. Moja ya Casino la watasha na watu wenye vipato vya juu. Baada ya kuruhusiwa na walinzi gari ya mhe. Casto ikaingia ndani ya eneo la maegesho ya ile Casino. Peter naye hakupoteza muda akafika pale getini.

“Habari za kazi wakubwa” Akasalimu kwa lugha ya uungwana na unyenyekevu.

“ Salama kabisa. Karibu”

“ Ahsante”

“ Tunaomba..” Wale walinzi wakasema, Peter kwa harakaharaka akajua wanaomba kadi maalumu ya kuingilia.

“Nipo na mhe” Akawajibu,

“ mmh! Mhe. Gani?”

“ Mhe. Gani? Aliyepita hapa ni nani kama sio Waziri wa Nishati na Madini?”

“ Lakini hapa haturuhusu kuingia kwa kujuana”

“ Ngoja nimpigie nimwambie mmenizuia hapa” Peter akasema, kisha akatoa simu yake.

“ Mwache aingie. Usitake mambo yawe mengi. Unajua hawa wakubwa hawa hawapendi vizingiti hasa kwa watu wachini kama sisi. Mhe hatafurahishwa na hizi taarifa” Mlinzi mwingine akaingilia.

“ Haya pita..”

“ Sawa Mkuu…” Peter akasema kisha geti likafunguliwa akawa anapita lakini akakumbuka jambo.

“ Mnaweza nipatia kadi au kitambulisho isionekane nimeingia kimagendo wakati Mhe. Akiwa busy niwe huru” Peter Mirambo akasema huku akirudisha gari nyuma akisogea kwenye ofisi ya walinzi. Wale walinzi pasipo kufikiri vizuri wakamwona Peter kama anahoja. Wakatoa moja ya kadi wakampa. “ Nashukuruni wakubwa” Peter akasema, kisha akatabasamu akiwaona wale walinzi wazembe wasioweza kufanya kazi yao kwa weledi. Peter alijua kuwa watanzania wengi ni waoga hasa wakiwa mbele ya watu wasiowajua ambao hujinasibisha na vigogo wa nchi. Hilo kwake alilitumia kama faida.

Akasonga akitafuta mahali pakuegesha gari yake huku tayari akiwa ameshaliona gari la Mhe. Casto. Alipojiegesha sehemu nzuri akatulia akiangalia huku na huku. Akaangalia saa yake ya mkononi iliyoonyesha ni saa tano unusu za usiku. Eneo la nje la ile Casino lilikuwa limependezeshwa na miti jamii ya minazi lakini sio minazi, bustani za kuvutia, pamoja na magesho ya kisasa ambayo yalikuwepo magari mengi ya kifahari yaliyosimama hapo.

Akachukua bastola yake na kuiweka mafichoni kwenye kiuno chake lakini akakumbuka kuwa huenda pale mapokezi wanapoingilia akakaguliwa na kuzuiwa kuingia nayo. Wazo hilo likamfanya aitoe ile bastola kutoka mafichoni na kurudisha kwenye gari chini ya kiti ilipokuwepo awali.

Akiwa bado yupo ndani ya gari ghafla anakaona gari la Mhe. Casto liikifunguliwa milango huku na huku. Kisha wakwanza kutoka alikuwa ni Lucy, Mhe. Casto akiwa amechelewa kama nusu dakika. Punde kwa mbele yalipomapokezi ya ile Casino anatokea kijana mmoja mwenye urefu wa wastani, mweusi ambaye kavaa kofia. Kofia ile inamfanya Peter asimuone vizuri usoni. Kitu kilichomfanya Peter amzingatie kijana huyu ni namna ambavyo Yule mwanamke mweupe mrembo aliyekuja na Mhe. Casto alivyoshtuka baada ya kumwona huyu kijana. Mshtuko ule ulimjulisha Peter kuwa wanafahamiana.

Peter kwa haraka akatoa Kamera yake kisha akachukua picha kadhaa akiwachukua Yule kijana, Yule mwanamke mweupe, lakini Mhe. Casto hakuonekana kwani bado alikuwa hajatoka kwenye gari. Yule mwanamke mweupe akawa na kiwewe, akawa anageuka kumtazama Mhe. Casto kisha kumwangalia Yule kijana. Ni kama alikuwa akitaka kumwita lakini angemwitaje ilhali yupo na mheshimiwa. Hilo likashindikana. Yule kijana hakumwona, akawa anatembea kivivu kama mtu ambaye pombe zimeanza kumshinda. Yule kijana akasonga mpaka ilipokuwa gari aina ya Range Rover. Akabonyeza rimoti, kisha mlango ukafunguka akaingia ndani ya gari. Yule mwanamke mweupe alishtuka aliposhikwa kiuno na Mhe. Casto. Akamgeukia, lakini Mhe. Casto akawa anatazama ilipo ile Range Rover. Alikuwa ameona mwanamke aliyekuwa naye jinsi alivyokuwa anamtazama Yule kijana. Ile Range Rover ikaondoka ikiacha sintofahamu katika mapenzi ya wawili hawa ambao hawajui kuna kiumbe cha hatari kinawafuatilia nyendo zao. Peter akawapiga picha. Kisha akawaona wakiondoka kuelekea kwenye mapokezi katika lango la kuingilia kwenye ile Casino. Hawakukaguliwa sana kutokana na cheo alichonacho Mhe. Casto wakaingia ndani.

Peter naye akatoka ndani ya gari lake kisha akasonga mpaka mapokezi, alipofika akawapa ile kadi maalumu, wakampekua kama anasilaha, walipojiridhisha wakamruhusu. Peter akazama ndani naye akiwa na kofia yake iliyoficha draid zake. Mbele yake akakabiliwa na mlango mwingine wa kuteleza, hapo akawa anawaona Mhe. Casto wakiwa wanaenda kupanda lifti lakini kulikuwa na mapokezi tena. Akawa anataka kuwawahi lakini Walinzi wa pale wakamzuia. Akiwa anashangaa sababu ya kuzuia, sauti nyembamba ya kike ikamuita;

“Kaka! Unaanzia hapa” Akasogea mpaka kwa Yule dada wa mapokezi huku mara kwa mara akiangalia jinsi lifti ilivyokuwa ikienda na namba zikihesabika, alitaka kujua wanaenda ghorofa ya ngapi.

“Mambo kaka”

“ Salama!”

“ Bila shaka wewe ni mgeni humu. Utaratibu ni kuwa unatakiwa upitie hapa ujaze taarifa zako kisha ueleze unaenda wapi?” Maelezo hayo ya Yule mdada wa mapokezi yakamfanya Peter kutoa kitambulisho bandia chenye picha yake na kumkabidhi Yule dada. Baada ya Yule dada kujaza taarifa za Peter mirambo akamrudishia kitambulisho.

“ Unaelekea wapi?”

“ Niko na mhe. Alikoelekea”

“oooh! Kumbe ungesema tangu mapema” Yule dada akaongeza uchangamfu baada ya kusikia hivyo.

“VVIP. Unalipa kwa Cash au unaswapu?”

“ Bei gani?’

“ Milioni tatu kuingia tuu. Huduma zingine utapewa kulingana na utakavyozitumia huko.”

“ Naswapu!” Peter akajibu huku akitoa kadi yake ya bank yenye majina bandia yanayofanana na majina ya kile kitambulisho bandia. Baada ya kukamilisha taratibu akaingia kwenye Lifti mpaka ilipo ghorofa ya kumi ambapo ndio kulikuwa na ukumbi wa VVIP. Akakaribishwa na bango kwa juu lenye jina la ile Casino. Kisha milango ya kioo ya ule ukumbi ulikuwa unaonyesha video ya wadada warembo waliovalia uchi wa mnyama. Peter akausogelea mlango ule kisha wenyewe ukatawanyika kumpisha apite katikati. Kitendo cha mlango ule kufunguka sauti kubwa ya mziki kutoka ndani ya ule ukumbi zilimlaki na kumkaribisha Peter kwa shauku ya ngono. Kila alichokuwa akikiona Peter kilikuwa kinahamasiaha ngono. Wanawake wote waliokuwa mule ndani walikuwa wapo uchi.

Macho ya Peter yalikuwa yakiangaza huku na huku kumtafuta Mhe. Casto lakini haikuwa rahisi kumwona. Akasonga akipita katikati ya watu waliokuwa wapo hoi kwa starehe, jasho la raha, harufu ya pombe za gharama ziliweza kujaza eneo lile huku sauti ya mwanamke ikiendelea kuimba kwa madeko ya ngono na beat ya muziki ikizishinda kwa nguvu hisia zao. Ilikuwa furaha katika pepo za mashetani walioamua kujitengenezea mbingu yao. Peter akasonga mbele kuifuata sauti ya mwimbaji wa kike ambaye hakuwa anamwona ila aliamini yupo mbele ya kundi kubwa lilomziba mbele yake. Moshi spray wenye ubaridi na harufu nzuri ilipulizwa mule ndani nakufanya eneo lote liwe na ukungu kisha zile taa za rangirangi zikileta mwonekano wa muujiza. Peter sasa angewezaje kumwona Mhe. Casto. Watu walikuwa hawatulii. Haya hata Yule mwanamke angemwonaje ilhali wanawake wote watakaoingia mule ndani huingia kwa sharti moja la kuvua nguo zao zote. Peter hakufanikiwa kuona mwanamke yeyote aliyekuwa amevaa nguo isipokuwa mwanamke mmoja tuu ambaye watu ndiye waliyekuwa wanamshangaa.

Wakati huku duniani watu wakishtuka kwa kihoro kushangaa mwanamke aliyeuchi hali ni tofauti katika ukumbi wa VVIP katika Casino ya BlackCross. Casino hii ukiingia utastaajabu kwa utakayoyakuta humu. Huku wanaoingia uchi wa mwanamke huuona kama anga hapo juu. Na mwanamke mwenye nguo ndiye watu humshangaa. Unaweza ukadhani basi hata huyo aliyevaa hizo nguo amevaa nguo za namna gani. Lakini utashangaa mwenyewe kwani naye hana tofauti na wanawake waliokuwa uchi.

Peter sasa alikuwa mbele kabisa akiwa anakabiliwa na mwanamke huyo aliyekuwa kasimama juu kidogo ya jukwaa akitumbuiza na kuimba kwa sauti ya aina yake. Alikuwa kavaa bikini nyekundu iliyoziba uchi wake. Lakini maziwa yalikuwa hayana nguo isipokuwa yamepakwa rangi nyekundu inayofanana na bikini. Kama usipoangalia kwa umakini unaweza kudhani maziwa yale yamefunikwa. Kwenye chuchu ilipakwa rangi nyeusi. Mwanamke Yule aliweza kuzikonga nyoyo za wote waliokuwa eneo lile. Haikuwa rahisi kujua sura yake kwani alikuwa kavaa barakoa nyekundu iliyoficha vyema uso wake huku ikimfanya aonekane kama mdoli wenye uswahiba na majini.

“Nani huyo! Nani huyo

Yuko wapi! Yuko wapi!

Aje hapa! Aje hapa!

Namwona! Namwona!

“Nani huyo! Nani huyo” Yule mwanamke kwenye jukwaa akawa anaendelea kuimba kwa sauti tamu ajabu. Ukumbi ukawa unaitikia kila alipokuwa akiimba;

“Nani huyo! Nani huyo!?” akiimba hivi watu wote hung’anganiana kwa ajabu kuitikia na kila mmoja akitaka kuwa wa kwanza au sauti yake isikike zaidi kuliko wenzake.

“Mimi hapa! Mimi hapa!” wanaitikia watu wote.

“ Yuko wapi! Yuko wapi!?” anaimba

“Niko hapa! Niko hapa” Wanaitikia

“ Aje hapa! Aje hapa!” anaimba kwa sauti kali ya kubembeleza huku akishaka makalio yake ambayo hata hivyo sio makubwa sana kutokana na umbo lake la kizungu. Akiimba hivyo basi watu huparamia jukwaa wakitaka kupanda kwenda kumfuata lakini wote wanashindwa kwani uzio wa jukwaa lile kwa pembeni chini kuna waya uliowekwa shot ya umeme.

Mambo hayo Peter yalizidi kumchanganya lakini hakusahau kazi iliyompeleka. Wakati anaangaza macho yake huku burudani ikiendelea punde akamwona Mhe. Casto upande wa pili akijivinjari na Yule mwanamke mweupe ambaye muda huu alikuwa yupo uchi wa mnyama. Walikuwa upande wa pili ambao watu walikuwa wameketi kwenye viti wakishuhudia burudani iliyokuwa ikiendelea pale.

Kabla hajafanya chochote akiwa anashangaa ghafla iliyoudhoofisha moyo wake kishindo cha kipekee akashangaa bega lake limeshikwa upande wa nyuma. Huku ukumbi wote ukiwa kimya kwa ghafla. Peter akageuka nyuma kumtazama aliyekuwa amemshika bega lake. Moyo wake ukapondeka na kusagika alipokutana na uso uliovikwa barakoa. Alikuwa ni Yule mwanamke mwimbaji mwenye umbo la kizungu na sauti ya ajabu. Akiwa na rangi ya kahawia. Peter akawa anatazama na Yule mwanamke. Ukumbi bado ulikuwa kimya ingawaje dakika ilikuwa haijaisha.

“Huyu hapa! Huyu hapa!” Yule mwanamke akaimba, vipaza sauti vikiipa nguvu na kujaza ukumbi mzima kwani Yule mwanamke alikuwa kavaa wireless maiki. Ukumbi mzima ukalipuka shangwe. Peter alikuwa anashangaa huku akivutwa kuelekea jukwaani palipo na ulingo wa burudani. Walipofika jukwaani Yule mwanamke akawa anaimba huku wakicheza na Peter kwa miondoko ya twisti, kisha wakaanza michezo ya hatari ya kubebana kama waitaliano. Hakuna ambaye angeamini kuwa mwanaume aliyechaguliwa na Yule mwanamke mwimbaji ambaye ni Peter Mirambo angeweza kuendana na kasi ya Yule dada. Peter hakuwa nyuma alikuwa mjuzi wa kucheza.

Katika ujasusi pia muziki ni muhimu kwa jasusi kuujua. Kucheza na kuishi maisha ya kisanii. Kwa sababu muziki ni lugha ya dunia. Na jasusi lazima awe mahiri kujua ishara na lugha kuu na kubwa zinazoeleweka na wengi duniani. Ni katika ujasusi ambapo lazima itafikia hatua jasusi atafika maeneo ya starehe kama NightClub, Casino au kwenye matamasha.

Peter akiwa anacheza na Yule mwanamke akawa anacheza huku akiangalia kule alipokuwa amemwona Mhe. Casto lakini alishtuka kutokumwona. Akaangaza macho yake huku na huku akiwa anaendelea kucheza ingawaje sio kwa umakini. Hakumwona.

ITAENDELEA
0693322300
 
RIWAYA YA CONNECTION EP 04
Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300

ILIPOISHIA
Peter akiwa anacheza na Yule mwanamke akawa anacheza huku akiangalia kule alipokuwa amemwona Mhe. Casto lakini alishtuka kutokumwona. Akaangaza macho yake huku na huku akiwa anaendelea kucheza ingawaje sio kwa umakini. Hakumwona.

ENDELEA
Akaondoka pale jukwaani, akawa anashuka akisonga upande alikokuwa amemwona Mhe. Casto. Alipofika akawa anaangaza macho yake huku na huku pasipo tumaini la kumwona. Ulikuwa uzembe wa wazi ambao hakustahili kuufanya mtu kama yeye ambaye ni mzoefu wa kufuatilia nyendo za watu.. Punde akashtuka kuwaona Mhe. Casto na Yule mwanamke mweupe wakitokea upande wa nyuma, Peter akajua walikuwa wanatoka chooni. Tayari walikuwa wameanza kulewa. Hawakurudi eneo lao la mwanzo walilokuwa wamekaa, Peter aliwaona wakitembea kuufuata mlango wa kutokea. Walikuwa wanaondoka. Peter naye hakuwa na sababu ya kubaki eneo lile. Akawaungia laini. Wakashuka mpaka chini yalipo maegesho wa magari. Peter naye akatoka akiwa nyuma yao wala hawakuwa na habari naye, walikuwa katika wingu la mapenzi lililowafanya wasimwone yeyote aliyekuwa maeneo yale. Peter aliweza kumsikia Mhe. Casto akimuita Yule mwanamke, Lucy wakati alipokuwa akiwapita akiwa anaelekea kwenye gari yake. Alipofika ndani ya gari akachukua kidaftari chake kisha akaandika jina Lucy, Mbweni. Kisha akawasha gari yake akaondoka akiwaacha Mhe. Casto na Lucy eneo lile.

***********

MASK INFORMATION TECHNOLOGY LTD.

Ni katika kampuni ya Information Technology iliyopo katika ya jiji la Dar es salaam. Kampuni hii inajihusisha na masuala ya IT, kidijitali, utengenezaji wa Applications mbalimbali za simu, uundaji na mipangilio bunifu ya tovuti, blogu, ukarabati wa mifumo ya kidigitajili ya makampuni binafsi, taasisi na mashirika hata ya serikali. Pia kampuni hii hujihusisha na kuunda mifumo ya ulinzi ya virusi vya kimtandao ambavyo hutumika kushambulia mifumo ya Tehama. Mara nyingi wadukuaji na wahalifu wa kimtandao hutengeneza virusi maalumu kwaajili ya kudukua mifumo ya watu au makampuni kwa malengo yao.

Mmiliki wa Kampuni hii ni kijana mdogo aitwaye Kalage Nyundo mwenye umri wa miaka ishirini na tisa tuu lakini tayari ndani ya muda mfupi amelitawala soko la kidigitali na masuala yote yahusuyo IT. Kalage Nyundo ni bingwa haswa, wengi humuita mchawi wa Tehama. Wengine humwona kama sio mtu wa kawaida kutokana na uwezo wake wa kucheza na mifumo ya Tehama. Serikali na mashirika binafsi na hata nchi jirani zimekuwa zikimtumia kwa shughuli mbalimbali za Tehama.

Wengi waliposikia kazi zake walifikiri huenda Kalage amesomea nje ya nchi kutokana na ile dhana iliyopo kwenye jamii kuwa elimu ya nchi yetu haina viwango wala viungo vya kumpika mwanafunzi awe katika kiwango cha kuishangaza dunia. Lakini ajabu ni kuwa Kalage Nyundo ni msomi ambaye taaluma yake ameipata hapahapa nchini katika chuo kikuu cha taifa ambapo alihitimu akiwa mwanafunzi bora katika kozi yake kwa kupata GPA ya 4.8. akiwa amebakiza point mbili tuu kufikisha GPA ya 5. Pointi hizo mbili hazimfanyi mtu yeyote kutokumwona Kalage kama mwanafunzi mwenye akili za masomo za kiwango cha juu. Ndoto yake kubwa tangu akiwa mdogo huko kwao Kagongwa wilayani Kahama ilikuwa kubwa bingwa wa masuala ya kikompyuta. Zaidi alikuwa na malengo ya kuanzisha kampuni kubwa ya masuala ya Tehama pindi tuu atakapohitimu shahada yake ya kwanza.

Leo hii Amini Boko alikuwa ameketi kwenye ukumbi wa mikutano iliyopo katika kampuni ya Kalage ambayo kwa kifupi huitwa Mask Ltd. Kitu kilichomshangaza Amini ni umri wa Kalage ambaye alikuwa mdogo kwake kwa miaka miwili hivi. Huku Kolowa akiwa mkubwa kwa wote wawili.

“ Hii maana gani hasa. Kwamba mimi sifikiri nje ya boksi. Kipi kinanikwamisha, au mimi ndiye kikwazo cha mafanikio yangu mwenyewe? Kwani maneno ya Kolowa yalikuwa sahihi? Kwamba kuna jambo natakiwa nifanye? Kujifunza! Ndio kujifunza kwa waliofanikiwa. Mtu aliyefanikiwa anapaswa kuwa Mentor wako na sio mshindani wako. Lakini mafanikio ya hawa mbona yanautata mwingi. Haiwezekani kijana mdogo hivi amiliki kampuni na ofisi kubwa kama hii tena iliyo katikati ya jiji. Lazima kuja jambo limejificha hapa sio bure” Amini Boko alikuwa akiwaza mwenyewe. Akachukua juisi iliyokuwa kwenye glass juu ya meza akameza mafumba kadhaa kisha akaendelea kuwaza,

“ Lakini mambo ya Tehama yanapesa mno. Dunia kwa sasa inahamia kiganjani. Unakubaliana na hilo?” Akawa anajiuliza mwenye katika mawazo yake.

“ Hata kama lakini sio kwa muda mchache hivi. Embu subiri. Nani huyu! Huyu mmiliki wa Facebook huyu! Nani huyu..! aaah! Nimemsahau Jina lake. Yupo top ten ya matajiri wa dunia na chanzo cha utajiri wake ni hizi ishu. Haya kuna huyo mwingine huyu Bwana Elon Musk, humjui huyo. Naye ni tajiri mkubwa na sehemu ya utajiri wake upo kwenye mambo hayahaya anayofanya huyu dogo. Mmiliki wa Alibaba je? Vipi huyu wa Tiktok?” Amini alikuwa akishindana na mawazo yake, kuna muda aliyakubalia kuna muda aliyakataa.

Akiwa anawaza mambo hayo punde mlango ukafunguliwa na aliyekuwa amekuja ni Kolowa.

“ Vipi Ankoli! Umekuwa mpweke eeh! ” Kolowa akamsalimia Amini.

“ Hamna mbona kawaida”

“ Usijali nilikuwa namshawishi Boss kama vipi na wewe upige mishe hapa. Usiishi kinyonge.”

“ Nashukuru sana! Ahsante sana rafiki yangu. Sijui niseme nini uelewe vile nilivyokushukuru”

“ Huna haja ya kunishukuru, wewe ni rafiki yangu mkubwa. Nimembembeleza sana mshikaji mwanzoni amenikazia akidai ati hakuamini alafu anasema unaonekana kazi huwezi na ni mwogamwoga”

“ Kazi naweza Rafiki yangu. Mimi sio mwoga”Amini Boko alipokuwa akiongea punde mlango unafunguliwa kisha anatokea Kalage akiwa amevalia suti iliyomkaa vizuri.

“Mimi kwa kweli niseme ukweli. Wewe sio chaguo langu. Nimekupa kazi kwasababu ya Kolowa. Vinginevyo wala nisiwe mnafiki nisingekupa kazi. So hilo nimeamua kulisema mbele yako Kolowa ili huko baadaye akiharibu uamini”

“ Boss nakuahidi nitatimza matarajio ya kampuni yako. Sitakuangusha” Amini akasema huku akipiga magoti. Jambo hilo likawafanya Kalage na Kolowa watazamane kisha waangue kicheko.

“ Kijana! Embu amka! Fanya kazi! Kolowa atakupa maelekezo yote utakayotakiwa kuyazingatia. Sihitaji excuses zozote. Sawa”

“ Ndio Mkuu” Amini akajibu huku akiwa amejikunyata. Hiyo ndio tafsiri ya nguvu ya pesa katika karne hii. Umri wako hauna maana yoyote kama huna pesa. Wahenga wa kizungu walikwisha kusema Umri ni namba tuu. Ukweli wa msemo huu ulikuwa dhahiri leo katika macho ya Amini ambaye licha ya ukubwa wake wa kiumri mbele ya Kalage lakini hiyo haikumaanisha chochote. Alimtetemekea ungedhani ni mfalme. Hata hivyo wanasema mtumikie kafiri upate mkate wako. Ndicho alichokuwa anakifanya Amini. Alihitaji pesa za kujitunza. Alikuwa nyuma kwa kila kitu.

Amini aliondoka akarudi nyumbani akiwa amepangiwa tarehe ya kuanza kazi. Siku mbili zijazo angetakiwa kuwa sehemu ya wafanyakazi wa kampuni kubwa la Mask Ltd. Akiwa nyumbani kwake ndilo Ghetto lake ambalo ni chumba kimoja pekee chenye Makororo. Akakitazama chumba chake huku uso wake ukiwa umezingirwa na udhaifu wa mawazo ya huzuni yaliyokuwa yanakilemea kichwa chake. “ Umri wangu huu miaka thelasini na moja bado naishi kwenye chumba kama hiki. Godoro lililoisha ambalo nililinua miaka mitano iliyopita. Kitanda hiki kisicho na hadhi ati ndio kinanitunzia ndoto zangu. Kweli! Mimi sio wa kulala kwenye chumba kama karakana la kabwela. Nimejificha watu wasijue taaluma yangu hapa mtaani. Watanidharau. Wataidharau elimu yangu. Ile kusema elimu ni ufunguo wa maisha kwangu hawatanielewa.” Alikuwa akiwaza. Amini akainama chini ya uvungu wa kitanda kisha akatoa kibubu ambacho alikuwa ameziweka hela zilizobaki baada ya kulipa kodi. Ni zile milioni moja alizokuwa amepewa na Kolowa kule kwenye Casino.

Akaanza kuzihesabu, zilikuwa zimebaki kama laki tano hivi. “ Nitanunua nguo za kazini. Lazima niwe mtanashati. Ninahitaji kuendana na mwonekano wa ile ofisi. Lakini pale watakuwa wamenipangia kazi gani. Bado sijajua.” Alipofikia hapo akawa anajaribu kujihusisha na kazi zilizokuwa pale alizoona kuwa anaweza kuambiwa afanye. “Ngoja nikanunue nguo kisha nikirudi nipitie saluni niweke nywele na ndevu zangu vizuri. Kwenye ile laki tano akatoa laki mbili kisha akatoka nayo kwenda Kariakoo kwaajili ya kununua nguo.

**************

Jioni ilikuwa imefika. Amini alikuwa amerudi nyumbani huku majirani zake ambao ni wapangaji walikuwa wakimshangaa kwa jinsi alivyobadilika mwonekano wake baada ya kunyoa. Sasa alionekana kijana handsome tofauti na awali kabla hajanyoa ambapo alikuwa anaonekana ni mzee. Ingawaje hakuwa na mazoea na majirani lakini baadhi ya wanawake majirani uvumulivu ukawashinda wakawa wanamsifu na kumpongeza kwa kunyoa. Huku wengine wakitaniana kuwa Amini ni shemeji yao.

Amini akaingia ndani ghettoni mwake akazijaribu nguo alizozinunua. Zote zilikuwa zimemkaa vizuri. Siku ya kesho alitamani ifike ili aende kufanya kazi asiyoijua wala asiyojua mshahara wake.

****************

Video chafu ya ngono ya mwanamitindo maarufu iliyovuja ilikuwa ikivuma mtandaoni. Ilikuwa ikimwonyesha mwanamitindo huyo akiwa anafanya mapenzi huku yeye na mwanaume mmoja asiyejulikana wote wakiwa uchi wakiwa katika mahaba mazito. Ingawaje jambo hilo lilikuwa la fedheha lakini wala usingeamini mapokeo yake huko mtandaoni. Vijana wa kike na wakiume walikuwa wakipigana vikumbo kwa hali na mali kuhakikisha wanaipata video hiyo.

Wachache sana walikuwa wakipinga na kulaani kitendo kile. Kijana mmoja wa mtandaoni alitoa maoni yake akisema” Hii sio sawa kabisa. Jamii tusishiriki kufurahia aibu na fedheha ya mtu mwingine. Huyu kafanyiwa uhalifu. Kadhalilishwa. Kama jamii tulipaswa kulipigia kelele tukilikemea. Na serikali inatakiwa ihakikishe wote wanaofanya mambo haya wanakamatwa na kupewa adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine”

Mtoa maoni mwingine akamjibu “ Wewe kaa kwa kutulia. Usijifanye wewe ni mwema kuliko. Hakuna aliyemtuma ajirekodi hizo video za uchi. Yeye mwenyewe ndio anapaswa kulaumiwa. Kwanza wanafanyaga makusudi ili kukuza na kujipa promo kwenye biashara zao za ukahaba. Nani asiyejua kazi za wadangaji wa mjini na mitikasi zao. Tuache sisi tugawane dhambi. Kama vipi zima data na tupa simu janja usiingie mtandaoni ili usione mambo kama haya. Ebooo!”

Maoni hayo yaliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na watu wengi huku wengine wakionyesha hisia zao za furaha kwa kuweka alama maalumu ziitwazo imoji za kucheka, kutabasamu, dole gumba la kukubali na imoji ya upendo.

Utandawazi huo ulifanikiwa kuacha moyo na ubongo wazi kwa watu. Hakukuwa na kitu kinaitwa akili tena miongoni mwa watu wengi hasa vijana. Ujinga na uchafu vilizidi kupewa utukufu na kupewa thamani kiasi kwamba wenye akili walionekana washamba. Vitu vya kijinga vilizidi kuteka soko ndani ya jamii na kufanya wale wote waliopa kutosaliti maadili na maarifa kutetereka kiasi kwamba wakawa wanakosa mpaka pesa ya kula. Upendo na kuthaminiana baina ya mtu na mtu kulizidi kupungua. Utandawazi huo. Kila kitu kilidhamiriwa kuwekwa wazi kwa watu. Hata yale zamani yaliyotakiwa kuwekwa ndani na kufichwa sasa ulikuwa wakati wa kuyatoa nje na hadharani kila mtu ajionee.

Tukio hilo la kuvuja kwa picha za uchi za mwanamitindo likazua tukio jingine kubwa zaidi kesho yake. Tukio la kujinyonga kwa mwanamitindo ambaye picha zake za uchi jana yake zilivuja. Huku akiwa ameacha ujumbe uliosomeka “ Nimejiua kwa sababu nimeshindwa kuhimili aibu na fedheha niliyoipata. Nitaweka wapi sura yangu. Nitawaambia nini wazazi wangu. Nitasema nini kwa mwanangu. Kwa kweli nimeshindwa! Acha nipumzike” Mbaya zaidi alikuwa mke wa mtu ambaye alikuwa anafanya ngono na mwanaume mwingine aliyeonekana kwenye ile video ya ngono.

Jambo moja la kushangaza ni kuwa, watu wote walikuwa walioitizama ile video ya uchi ya mwanamitindo iliyovuja walikuwa wameweka umakini wao zaidi kwa mwanamitindo, hakuna yeyote aliyemkumbuka Yule mwanaume aliyekuwa akifanya mapenzi na mwanamitindo. Isipokuwa Peter mirambo ndiye aliyekuwa amempa umuhimu mtu Yule.

“ Huyu mwanaume atakuwa ni nani? Watu wanamjadili Mwanamitindo pekeake vipi huyu mwanaume?” Peter alikuwa akiwaza akiwa ameegesha gari lake umbali kidogo tokea ilipo nyumba ya Lucy. Imezoeleka kwenye nchi yetu jambo la ngono na aibu linapotokea kama kuvuja kwa video au picha za utupu basi ni mwanamke pekee ambaye ataonekana kama mhanga na mwenye makosa huku mwanaume akionekana hana hatia. Jambo hili sio halali. Yote haya alikuwa akiyawaza Peter Mirambo aliyekuwa bado yupo ndani ya gari akimuwinda Lucy.

Punde akamuwona Lucy akitoka akiwa amevaa nguo za mazoezi. Lucy akaanza kukimbia mdogomdogo huku akiwa ameweka wireless earphone maskioni. Akaipita gari ya Peter. Wala hakuwa na habari naye. Peter akashuka upesiupesi baada ya Lucy kufika mbali na kukata kona. Akaharakisha kwenda kwenye jumba la Lucy. Akatoa funguo maalumu kisha akafungua lile geti alafu akarudishia.

Moja kwa moja akalakiwa na mandhari nzuri ya kuvutia yenye bustani zenye maua mazuri sana. Hakujishughulisha na mandhari ya pale zaidi alikazana kuufuata mlango wa kuingilia wa lile jumba. Akatoa ileile fungua maalumu kisha akafungua, alipofungua alishtuka kupokelewa na kimbwa kidogo cha kizungu ambacho kilikuwa na manyoya mengi. Kimbwa kile kilikuwa kikimrukia rukia na kumfanya awe katika kero.

Peter akawa anaikagua ile sebule huku akiendelea kupata kero kutoka kwa kale kambwa. Hakuona jambo la maana pale sebuleni akazifuata ngazi zinazopandisha ghorofani kisha akaanza kupanda, alikuwa akipanda kwa tahadhari huku kila mara akisikilizia na kupima utulivu wa eneo lile. Akafika upande wa juu ambapo alipokelewa na sebule nyingine. Huku kidogo kulikuwa pamechangamka tofauti na sebule ya chini. Hii ikampa ujumbe kuwa Lucy alikuwa akipenda kuitumia Sebule ya juu kuliko ile ya chini.

Luninga ilikuwa inaonyesha muziki ingawaje bila sauti. Kwenye sofa moja kulikuwa na mkoba wa Lucy pembeni ya mkoba kilikuwepo kioo na simu ndogo. Peter akavisogelea kisha akaanza kupekua ule mkoba. Akakuta dola miatatu, kisha akakuta pesa za kitanzania elfu themanini. Nje ya hapo palikuwa na vipodozi pamoja na wanja. Hakukuwa na ziada ya muhimu. Peter akachukua ile simu ndogo aliyoikuta pale kwenye meza. Kale kambwa bado kalikuwa kakimsumbua sumbua. Lakini ghafla akasikia kuna mtu anapanda kwenye ngazi akija kule juu. Peter akanyanyuka upesi kisha akaenda kujificha nyuma ya pazi la dirisha. Kale kambwa nako kakamfuata. Peter akakapiga teke kakaangukia upande zilizokuwepo zile ngazi. Hapo hakakurudi. Alikaona kakitingisha mkia huku kakikimbia kushuka kwenye ngazi. Akiwa kajificha punde akamwona Lucy akiwa amekabeba kale kammbwa akiwa anapandisha ngazi. Moyo ukakazana kupiga kwa kuhofia kiherehere na umbeya wa kale kambwa. Hakukaamini hata kidogo.

Lucy bila kujua kuna mtu nyuma ya pazia anayemtazama, akajibwaga kwenye sofa. Kisha kale kambwa kakamrukia kwenye sofa kakawa kanajikombakomba katika mapaja ya Lucy ambaye naye alikuwa akikapetipeti kwa kukapapasa kuanzia kwenye kichwa mpaka mgongoni jambo lililokafanya kasahau uwepo wa Peter aliyekuwa nyuma ya pazia.

Lucy akachukua rimoti ya AC iliyokuwa juu ya meza kisha akaibonyeza. Haikuzidi dakika moja sebule yote ilijawa na ubaridi hali iliyofanya mwili wa lucy kuburudika kiasi cha kuanza kusinzia. Peter alipoona Lucy anasinzia akawa anajipa muda mpaka pale usingizi utakapokuwa umemkolea kusudi atoke pale alipokuwa amejificha. Alihesabu dakika kama tano tangu Lucy afumbe macho yake akajihakikishia kuwa Lucy asingeweza kumsikia pindi atakapotoka kwa kunyata. Akawa anatoka lakini kabla hajapiga hatua ya tatu kale kammbwa kakaanza kumbwekea. Kitendo hicho kilimshtua Lucy na kumfanya aamke. Lakini Peter alikuwa ameshajiviringisha kama jongoo na kujificha upande mwingine wa sofa. Hiyo haikukafanya kale kambwa kasimuandame. Kalimfuata huku kakiendelea kubweka. Lucy alikuwa akikashangaa kammbwa kake. Kale kambwa kakawa kamesimama huku kakibweka huku mkia wake akiutingisha. Anabweka akimuangalia Peter aliyejificha kisha anabweka tena huku akimtazama Lucy ambaye alikuwa amelala sofani akikatazama. Lucy akagundua kuwa kale kambwa kalikuwa kakimpa ujumbe Fulani. Akaamua kuamka kwenda kuona kile kinachomfanya mbwa wake abweke. Akasonga, huku kammbwa akake kakiwa kanamtazama na kutingisha mkia wake kama ishara ya kueleweka, lucy na mbwa wake wote walikuwa wameshikwa na mshangao baada ya kuona jambo la tofauti. Aliuona mdoli wa Tiger mkubwa ukiwa pale chini. Kambwa nako kalibaki kameduwaa kakiwa hakaelewi nini kipo mbele ya macho yake. Kaliacha kutingisha mkia wake huku kakiwa na mshangao wa hofu. Kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua ambacho kisingewezekana kirahisi. Peter alikuwa amehama eneo lile huku akiwa ameuweka ule mdoli wa Tiger Mkubwa ambao ulikuwa kwenye meza ya sofa iliyokuwa upande wa nyuma wa yale maasofa.

Lucy naye alishangaa uwepo wa ule mdoli pale chini. Je ulidondoka au nani kauweka. Kwa ukubwa wa ule mdoli kuangushwa na upepo ni jambo ambali lisingewezekana kwani vioo vyote vya madirisha vilikuwa vimefungwa hivyo hakukuwa na nafasi ya kuruhusu upepo kuingia mule ndani. Hata hivyo alipuuzia.

Peter alikuwa amekimbilia chumbani, akiwa chumbani hakuona jambo lolote la maana. Ghafla akamsikia Lucy akifungua mlango. Kwa upesi akaingia uvunguni mwa kitandani.Lucy akawa ameingia bila kale kambwa. Akabadili nguo zake kisha akaelekea kuoga pasipokujua kuwa kuna mtu yupo chini ya uvungu wa kitanda chake. Peter akiwa chini ya uvungu alikutana na kikaratasi, alipokiangalia vizuri ilikuwa ni ile businescard ya Kalage Nyundo. “Mask Ltd. Mjini kati. Nkuruma Tower Floor 09” yalikuwa maelezo yaliyokuwa kwenye ile kadi. Peter akaiweka mfukoni.

Muda huo Lucy naye alikuwa akitoka bafuni. Akachukua nguo kwenye kabati la nguo kisha akaisogelea kabati lenye kioo maalumu kwa kujirembea. Akawa anajiandaa huku akizungumza mwenyewe mambo ambayo Peter hakuwa anayaelewa. Baada ya kujiremba akawa anatafuta ile businesicard aliyokuwa amepewa na Kalage. Aliitafuta lakini hakuipata.

“Yule alikuwa Kalage. Haiwezikuwa nimemfananisha. Lakini kadi yake niliiweka hapa. Sasa itakuwa wapi?” Alikuwa akiongea mwenyewe. Peter alishtuka kusikia hivyo. Kadi aliyokuwa ameiweka mfukoni ndiyo iliyokuwa inatafutwa. Maelezo ya Lucy yalimjulisha Peter kuwa Yule mwanaume mweusi mwenye upaa unaomuanza aliyemuona jana kule The Blackcross Casino alikuwa ndiye Kalage mwenyewe. Kuhangaika kwa lucy mule ndani katika jitihada za kutafuta ile kadi kulimfanya Peter aone umuhimu mkubwa wa ile kadi kwa Lucy. Peter alikumbuka usiku wa jana jinsi Lucy alivyokuwa anababaika baada ya kumwona Kalage.

Lucy baada ya kuchoka kutafuta akiwa amesahau sehemu moja tuu ambayo ni uvunguni mwa kitanda. Alikata tamaa akaamua kuondoka, lakini akiwa anatoka akasimama akiwa amefika mlangoni. Peter kuona hivyo hisia zake zikamwambia kuwa Lucy atarudi kwa ajili ya kuchungulia chini ya uvungu. Kabla hajamaliza kuwaza Lucy alikuwa akirudi uelekeo wa kitanda . Peter kwa upesi akaingiza mkono mfukoni kisha akaitoka ile kadi na kuiweka karibu na mwanzo wa uvungu. Lucy kabla hajainama akaiona ile kadi ikiwa ipo pale chini. Akainama kuiokota. Kisha akaondoka.

Peter hakuwa na haja ya kumfuatilia tena Lucy kwa sababu alijua wapi anakoelekea. Yeye alichotaka ni kuchunguza nyumba yake. Baada ya kujihakikishia Lucy ameondoka. Akatoka uvunguni na kuanza kuipeleleza nyumba ya mrembo Yule. Aligundua Lucy alikuwa amehitimu chuo wiki tatu zilizopita. Lakini zaidi aligundua kuwa Lucy alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliosoma sheria na waliokuwa wanatakiwa kurudia mwaka. Hilo lilimfanya Peter aone uhusiano uliopo wa Lucy na kifo cha Profesa Saimon ingawaje hakujua ni kwa namna ipi.

Ukaribu wa Mhe. Casto na Lucy uliimarisha kile alichokuwa anakiamini. “Kama Profesa Saimon hakuwa na ukaribu na Mhe. Casto inawezekana mawasiliano yao yaliunganishwa na Lucy. Hii inaingia akilini sasa” Peter alikuwa akiongea mwenyewe akiwa bado yupo katika chumba cha Lucy. Hakuona jambo la maana zaidi akaamua kuondoka.

ITAENDELEA
0693322300
 
RIWAYA YA CONNECTION EP 05
Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300

ILIPOISHIA
Ukaribu wa Mhe. Casto na Lucy uliimarisha kile alichokuwa anakiamini. “Kama Profesa Saimon hakuwa na ukaribu na Mhe. Casto inawezekana mawasiliano yao yaliunganishwa na Lucy. Hii inaingia akilini sasa” Peter alikuwa akiongea mwenyewe akiwa bado yupo katika chumba cha Lucy. Hakuona jambo la maana zaidi akaamua kuondoka.

*********************

ENDELEA
“Ataanza kazi kama Customer Care Excutive, majukumu yake makuu yatakuwa kupokea simu na kuelezea bidhaa zetu, kutatua matatizo ya wateja wetu watakaokuwa wanatupigia simu. Kupanga miadi na wateja kwaajili ya kuja kupata huduma zetu miongoni mwa majukumu mengine. Hivyo siku hizi saba zitakuwa kwaajili ya kumpa semina na kumfanyia majaribio kama anauwezo wa kufanya kazi hii. Kama akiwa vizuri basi tutampngia majukumu mengine” Kalage alikuwa akimwambia Kolowa. Wote walikuwa wamevalia kiofisi wakiwa katika ofisi ya Kalage ambaye ndiye mkurugenzi wa kampuni ya Mask Ltd”

“ Sina pingamizi kabisa” Kolowa akajibu.

“ Wewe ndio utafanya jukumu hilo. Hakuna mtu mwingine kwa sababu hatukuwa na ratiba yoyote ya usahili na kuajiri mtu mwingine. Connection yako kwake ndio imefanya uwepo wa ongezeko lake katika kampuni yetu. Jitahidi uwe macho naye” Kalage akasema huku akifungua laptop yake iliyokuwa pale juu ya meza. Hii ilimaanisha kuwa mazungumzo yalikuwa yamefikia kikomo. Kolowa akatoka moja kwa moja akaenda kwenye ukumbi wa mikutano ambapo alimkuta Amini akiwa anamsubiri. Kolowa akamwambia Amini amfuate. Wakiwa wamefuatana wakafika kwenye Lifti kisha wakaingia ndani yake. Kolowa akabonyeza namba tisa kwenye ile lifti papohapo lifti ikaanza kushuka mpaka ghorofa ya tisa, kwani walikuwa wametoka ghorofa ya kumi. Haikuwachukua dakika moja wakawa wamefika. Mlango wa lifti ukafunguka wakakutana na bango kubwa lenye maandishi yaliyosomeka SS CUSTOMER SERVICES CALL CENTER Kisha kulikuwa na milango mingi na madirisha ya alluminium ambayo ndani yake kulikuwa na wafanyakazi waliokuwa wapo busy wakiongea na wateja huku masikioni mwao wakiwa wamevaa earphone. Ilikuwa ofisi kubwa sana.

“ Huku ndio utakapokuwa unafanyia kazi. Hii yote ni kampuni yetu. Kote huku, mpaka ofisi zile kule kote ni kampuni yetu” Kolowa alikuwa akimwonyesha Amini ofisi zilizokuwa katika ile ghorofa ya tisa. Amini yeye alikuwa akishangaa fahari ya ofisi zile na mara chache akisoma maandishi yaliyokuwa kwenye mabango yaliyobandikwa kwenye kuta za zile ofisi. Kiyoyozi kilikuwa kikimpa nafasi nzuri ya kupumua tangu alipofika kwenye kampuni hiyo. Aliridhishwa na mazingira ya kazi ingawaje hakuwa anajua ni kazi gani anayoenda kupewa.

Wakasimama kwenye mlango mmoja ambao juu yako kuwalikuwa na maandishi yaliyotoa ujumbe wa ofisi ya mkuu wa Customer Care. Kwenye ule mlango kulikuwa na sehemu ya kuwekea dole gumba ili uruhusiwe kuingia. Kolowa akaweka dole gumba kisha mlango ukafunguka, wakaingia huku Kolowa akimwambia Amini kuwa naye itampasa asajiliwe dole gumba lake ili mlango ule umtambue kusudi aweze kuingia na kutoka katika hiyo ofisi.

“ Wewe ni mtu wa tatu kusajiliwa dole gumba lako kwenye ofisi yako. Mimi na Kalage tulitangulia kabla yako. Hii inamaanisha kuwa ofisi hii wenye uwezo wa kuingia humu ni sisi watatu” Kolowa alisema huku akitembea kwa madaha, Amini alikuwa akishangaa ukubwa na uzuri wa ile ofisi. Ilikuwa ofisi yenye hadhi ya juu kabisa. Meza kubwa ya kisasa ambayo ilikuwa na kiti cha kiofisi cha kuzunguka. Juu ya ukuta kulikuwa na picha ya Rais wa sasa, upande wa pili wa ukuta ilikuwepo Luninga kubwa yenye ukubwa wa inchi hamsini ambayo iliangaliana na Kile kiti cha kiofisi ambacho Amini alijua ndipo atakapokuwa anakaa. Juu ya ile meza zilikuwepo Kompyuta kubwa mbili za kisasa kabisa. Upande wa mbele ambao ulikuwa ukiangaliana na mlango wa kuingilia kulikuwa na milango midogo miwili. Amini bila kuambiwa akajua ilikuwa milango ya chooni.

“ Hii ndio ofisi yako Ankol. Utakuwa ukifanyia shughuli zako hapa” Kolowa akasema huku akizunguka upande wa pili kwenye kile kiti cha kiofisi, kisha akaiwasha Kompyuta moja.

“zunguka huku nilipo” Akasem, hapohapo Amini akamfuta na kumkaribia, “ Chukua kiti kile ukae hapa” Akasema. Amini akachukua kiti kingine ambacho kilikuwa upande wanaokaa wageni watakaoingia ofisi ile. Kisha akaketi karibu na Kolowa aliyekuwa amekaa kwenye kile kiti kikubwa cha kiofisi.

“ Hii kompyuta ndio sehemu yako ya kazi. Utaiwasha kama kawaida kwa kubonyeza hapa, kisha itakuja sehemu ya kuingiza jina ulilosajilia hapa na neno la siri. Hapa mimi nitaingiza yangu kwanza ili ifunguke, kisha tutasajili akaunti yako” Kolowa akaingiza jina na neno lake la siri kisha Kompyuta ikafunguka. Kwenye kioo ilitokea picha ya Mwanamke mrembo aliyevaa bikini huku maziwa yake yakiwa uchi. Jambo hili lilimshtua sana Amini. Kolowa akamwangalia alafu akatabasamu, lakini lilikuwa tabasamu lenye kipimo cha udadisi. Kisha akaigeukia Kompyuta. Akabonyeza bonyeza kwenye Keyboard ya ile Kompyuta kisha akasema,

“ Tuandike jina gani?” “ mmh! Andika tuu Amini Boko”

“ aaah! Jina gani hilo. Tuandike B mnasaji. Unalionaje hili” Kolowa akasema huku akiwa ameliandika, kisha akamgeukia Amini akiwa anamtazama na tabasamu la furaha kama mtu anayejivunia utunzi huo.

“Mnasaji wa nini?” Amini akauliza akiwa na mshangao.

“ Unaujua urimbo?” Kolowa naye akamuuliza.

“ Naufahamu”

“ Urimbo unanasa nini?” Kolowa akasema, wote wakacheka.

“ Hii ni username tuu ankol haina uhusiano wowote na kazi yako wala mambo ya kiserikali. Haya weka neno lako la siri mwenyewe” Kolowa akasema akiwa anampa Amini Keyboard ili aandike neno lake la siri. Akaandika. Kisha Kolowa akainama chini ya meza na kuvuta kijidroo kdogo cha ile meza, akatoa kifaa Fulani cha kiteknolojia. Kisha akakiunganisha kwenye ile kompyuta kikawaka. Akakibonyeza bonyeza kama mtu anayeunganisha kile kifaa na kompyuta kwa wireless. Ilipokubali, akamwambia Amini aweke dole gumba lake kwenye kile kidude. Amini akaweka, kioo cha Kompyuta kikawa kinaonyesha asilimia zilizokuwa zikiongezeka kuanzia sifuri mpaka ilipofika mia moja, kisha ikatokea alama ya tiki kuwa dole gumba la Amini limekubaliwa.

“ Haya nafikir hatua ya kwanza imekamilika. Kompyuta hii inakutambua kama B Mnasaji. Mlango ule unakutambua pia kupitia dole gumba lako. Jambo moja ni kuwa unauwezo wa kuingia ofisi yoyote zilizokuwa kwenye ghorofa hii lakini wafanyakazi wengine hawana huo uwezo wa kuingia katika ofisi yako. Ushakuwa Boss Ankol. Hahahah!” Kolowa akacheka sana amini akiwa anamwangalia bila kusema neno lolote.

“ Majukumu yako yatakuwa kuangalia wafanyakazi wengine wanafanyaje kazi, kuwasimamia wafanye kazi kwa bidii. Utakuwa unawaona kupitia Kompyuta hii nyingine” akawa anaiwasha. Ilipowaka akabonyeza bonyeza punde na ile luninga iliyokuwa pale ukutani ikawaka. Hapohapo wakawa wanaona video za matukio yanayoendelea kwenye ofisi zingine.

“ Utakuwa una scroll hapa kuangalia kila ofisi nini kinaendelea. Lakini mtu unaweza kumwona anafanya kazi lakini kumbe akawa hafanyi. Hivyo utaingia hapa, kila ofisi na kila kumpyuta na kila simu itakayopigwa ipo kwenye huu mfumo hapa. Ufanyaji kazi unaonyeshwa hapa. Mfano tuingie kwenye ofisi hii” Luninga hapohapo inamwonyesha dada mmoja ambaye yupo ofisini anafanya kazi. “Umemwona?” “ Ndio” Hapa kwenye Kompyuta unamtambua kwa majina yake halisi anaitwa Maria Hadadi. Lakini WPT Yaani working Perfomance yake kwenye mfumo upo chini, unaona ipo asilimia sitini wakati anatakiwa awe juu ya themanini. Kazi yako ni kumsimamia afanye kazi”

“ Kwa namna ipi?’

“Utamtumia ujumbe kupitia email yake kwa kubonyeza hapa, ukiona hajibu utampigia simu ukiona hajibu unamfuata. Mfanyakazi yoyote ambaye WPT yake ikiwa chini ya themanini zaidi ya mara tatu kwa siku unamtumia barua ya onyo. Ikiwa hataleta mabadiliko akarudia jambo hilo ndani ya wiki hiyohiyo atafukuzwa kazi” Kolowa akasema,

“Nani sasa atakayemfukuza kazi”

“ Hahaha! Nani mwingine kama sio wewe? Floor hii wewe ndio Boss” Kolowa alikuwa akiongea kwa majivuno sana.

“ Utaanza kazi sasa hivi nione’ akasema tena huku akimpisha Amini kiti. “Akainama chini na kutoa kitu mfano wa headphone akaingunisha kwenye ile Kompyuta ya kazi. Kisha akamwambia Amini aivae masikioni. Amini akaivaa “Mpigie huyu Maria maana bado WPT yake ipo chini”

Amini akabonyeza kwenye kompyuter simu ikaanza kuita huku muda huo wakiwa wamenyanyua nyuso zao wakitazama luninga iliyokuwa ikimuonyesha Maria akiiangalia simu iliyokuwa inaita. Maria akapokea simu.

“ Habari Maria. WPS yako iko chini kwa zaidi ya dakika tano sasa. Kama utaendelea hivi hatua za kinidhamu zitafuata Ahsante” Amini aliongea kisha akakata simu. Hapohapo kolowa akanyanyuka kwenye kiti kisha akapiga makofi huku akimpongeza Amini.

“Ankol nilijua kazi hii utaiweza. Yaani sikutegemea kabisa. Umefanya vizuri. Bila shaka hata wewe umeona sio kazi ngumu”

“Huuu! Sio sana ila ninahitaji muda zaidi” Amini akasema.

“Sawa tutatoka twende nikakutambulishe kwa wafanyakazi wengine ili wakujue boss wao mpya” Kolowa akasema akiwa anachukua simu na kupiga,

“Wakusanye watu kwenye ukumbi wa mkutano nina kikao na wafanyakazi wote” Kolowa aliongea akimpa maelekezo mtu aliyekuwa anaongea naye kwenye simu ambaye Amini hakuwa anamjua.

“ Twenzetu!” Kolowa akasema,

“ Ndio tayari kwani?”

“ Hahahah! Tayari Ankol. Ulidhani ni mikazi ya kusumbuana?”

“Mmmh! Kolowa! Inamaana siku nzima kazi yangu itakuwa ni hii tuu”

“ Utajionea mwenyewe. Humu tunawafanyakazi hamsini. Sio wengi sana lakini pia sio wachache. Kusimamia watu hasa katika kazi hii ni kazi ngumu kuliko unavyofikiria. Kuongoza watu ni kazi sana. Utaona mwenyewe”

“ Alafu kitu kingine, unapotoka kwenye ofisi yako usiache Kompyuta yako ikiwa inafanya kazi. Izime au Logout kwenye akaunti yako ndipo utoke kwenye ofisi yako. Usikubali kumwachia tu yeyote Kompyuta hii. Hata kama anafanya kazi kwa dakika moja. Sawa Ankol” Kolowa akasema.

“Sawa”

“Twenzetu nikakutambulishe New Boss mpya kwenye Kampuni kubwa hapa nchini”

“ aanhaa! Lakini Boss hujanambia Mshahara kwa mwezi ni kiasi gani?”

“ https://jamii.app/JFUserGuide! I’m sorry kichwa kina mambo mengi. Mshahara ni milioni moja na laki tano kwa mwezi”

“ Umesema!”

“Umenisikia Amini. Milioni Moja na nusu ni kiasi kidogo sana. Nitamwambia Mkurugenzi akufiirie. Lakini itakupasa hii miezi sita uonyeshe uwezo ili hata Boss nikimwambia aone haja yaw ewe kuongezewa mshahara. Unajua mshahara unatokana na thamani ya mtu vile anavyozalisha kwenye kampuni. So tutaanza na hiyo”

“Ahsante sana Ndugu yangu. Mungu akubariki sana kaka” Amini alikuwa akiongea kama mtu aliyepagawa. Furaha yake ilishindwa kujihifadhi katika moyo wake na ndipo ilipokuwa imetapakaa katika pembe za uso wake.

“ Lakini kila siku utakuwa unaenda kwa mhasibu atakuwa anakupa elfu ishirini kama posho ya kujikimu” Kolowa akasema, maneno yake yalimfanya amini ashindwe kuzuia machozi ya furaha yaliyokuwa yamejikusanya katika macho yake. Akamkumbatia rafiki yake.

Wakatoka wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwaajili ya utambulisho. Walipofika walikuta tayari wafanyakazi wote walikuwa wamekusanyika wakiwasubiri. Kitendo cha wafanyakazi wale kumwona Kolowa akiingia mlangoni kiliwafanya kila mmoja akae sehemu yake kwa utulivu mkubwa. Jambo hili aliliona Amini. Hii ilimfanya aone kuwa Kolowa alikuwa akiogopwa na wafanyakazi wa kampuni ile.

“Naamini kila mmoja yupo salama ndio maana wote tupo hapa. Nimekuja kwa jambo kuu moja. Huyu aliyembele yenu anaitwa Amini Boko, ndiye Mkuu wenu wa kazi kuanzia leo. Yeye ndiye atakuwa anahakikisha kazi zenu zinafanyika kwa namna ya kulinda na kuimarisha heshima ya kampuni yetu. Mumpe ushirikiano. Matatizo yoyote mtawasiliana naye. Uzembe wowote na mapuuza yoyote hayatavumiliwa. Nafikiri sheria na kazi yetu kila mmoja anazijua. Ujio wake hautabadili hata nukta moja ya kile kilichokuwepo. Isipokuwa yeye ndiye atahakikisha malengo ya kampuni yetu yanafikiwa bila kizuizi”Kolowa alikuwa akisema kama mtu mpya ambaye Amini hakuwa akimjua. Sio Yule Kolowa aliyekuwa akisoma naye chuoni wala sio Yule Kolowa ambaye siku chache walikuwa Casino akiwa anajivinjari na makahaba huku mwili wake ukiwa na michoro ya tattoo. Wala wale wafanyakazi wasingeamini kuwa ndani ya ile suti aliyokuwa ameivaa Kolowa kulikuwa na michoro ya tattoo iliyoupamba mwili wake.

Kolowa akamgeukia Amini alafu akamuita;

“Amini!”

“ Yes Boss” Amini aliitikia akiwa ameshtuka. Uhusika wa kolowa wa wakati huu ulitosha kumfanya uogopeke kama wale maboss wakaksi wasiopenda mchezomchezo kwenye kazi. Hofu nyingine ni kuwa hakuwa tayari kupoteza hizo milioni na nusu pamoja na posho. Kwake ilikuwa ni pesa nyingi ambazo hata angeajiriwa akiwa daktari asingekuwa analipwa pesa hizo. Wingi wa pesa hizo ukichanganya na uhitaji wake ndivyo vilivyomfanya amuogope Kolowa kwani ndiye aliyekuwa ameyashikilia maisha yake ya mafanikio kwa muda huo.

“Hawa ndio wafanyakazi wako. Naamini kazi yako itakuwa nyepesi kutokana na vile nikujuavyo. Wewe ni zaidi yangu” Kolowa aliposema hivyo wafanyakazi wote walikuwa wakaiangaliana kisha wakawa wanamuangalia Amini Boss wao mpya wakimpima kama analingana na maneno ya Kolowa au ulikuwa ni mkwala tuu.

Macho ya wafanyakazi wengi yalitoa majibu ya kutoamini maneno ya Kolowa. Amini alionekana kama kijana mwenye uso mzuri wenye haya. Sura yake isingewezekana kufananishwa na aina yoyote ya ubaya. Vyovyote iwavyo angekuwa anasingiziwa kama angekutwa na shutuma za uhalifu. Wanawake ambao ni zaidi ya nusu ya wafanyakazi pale walimwona Amini kama Handsome boy anayefaa kwa matumizi yao ya kikubwa. Wengine waliiona nafasi ya wao kutupa karata zao kwaajili ya kumshawishi Amini awe mume wao. Huku wengine wakipanga mipango kabambe ya kuuteka moyo wake kwaajili ya maslahi yao ya kiuchumi. Hayo yote yalikuwa yakiendelea katika akili za wafanyakazi hao wakike.

“Unaweza kuwasalimu” Kolowa akampa nafasi Amini ya kuzungumza.

“ Habari zenu”

“Salama” wakajibu wote lakini wanawake wakiwa wamejibu kwa sauti zaidi.

“ Nimefurahi kujiunga nanyi hapa. Nahitaji kila mtu afanye kazi yake bila kuleta longolongo. Nitakuwa Boss mzuri kwa mtu atakayetimiza wajibu wake. Lakini sitakuwa na simile kwa mtu mzembe na asiyejua kwa nini yupo hapa. Tupo hapa kwaajili moja tuu. Kufanya kazi na kutimiza malengo ya kampuni. Tunajua kutimiza malengo ya kampuni ni kutimiza malengo yetu binafsi kwa kila mmoja wetu. Kweli au uongo”

“Kweli Boss”

“Vizuri. Kila wiki nitahitaji ripoti ya kazi kwa kila mmoja wenu. Tupo pamoja?”

“ Ndio Boss” Wakajibu lakini mmoja wao akanyosha mkono. Aliporuhusiwa akasema;

“Ahsante Boss kwa nafasi hii. Hiyo ripoti itakuwa inakusanywa lini”

“ Kila ijumaa jioni. Mtatuma kwenye Email yangu” Wakati Amini anaongea ghafla wafanyakazi wanageuza shingo zao na kutazama kwenye vioo vyenye kingo za Alluminium, anaonekana mdada mweupe mrembo mwenye umbo namba nane akiwa hajui wapi aelekee. Amini naye anatazama upande huo naye akamwona. Alikuwa ni mwanamke mzuri sana. Hapohapo kolowa akamsogelea Amini na kumuuma sikio. Kisha akatoka.

“Naomba utulivu wenu. Turejee kwenye kikao” Amini akasema akiwa anapiga makofi. Utulivu ukarejea.

“ Niwatakie muendelee na majukumu mema. Ahsanteni” Akasema kisha akatoka akiwaacha wafanyakazi nao wakitoka kwenye ule ukumbi wakielekea kila mmoja iliposehemu yake ya kazi.

“Mr. Amini. Kuna mgeni wako hapa” Kolowa alimuita Amini.

“Mgeni wangu?” Amini akawaza huku akiwaogelea Kolowa na yule Mwanamke mweupe mwenye uzuri usioelezeka. Amini hakuwa akifahamiana naye. Sasa ugeni hiyo vipi.

“ Anahitaji kukwona. Nafikiri niwaache”

“ Anahitaji kuniona mimi?”

“Ndio! Nafikiri kuna jukumu moja nilisahau kukueleza. Dada samahani. Unaweza kusubiri pale kwenye kile kiti pale” Kolowa akasema na Yule mwanamke akaondoka akiwaacha pale.

“ Sikiza Amini, kuna kazi nyingine lakini hii itakupasa uianze baada ya kupata uzeofu na kazi ya kwanza niliyokupatia”

“ Kazi gani Boss”

“ Usihofu! Kazi ya nzuri! Inapesa kuliko hii lakini utaifanya hapahapa ofisini” Kolowa akasema huku akimtazama Amini aliyekuwa anajaribu kukisia kazi mpya nyingine.

“ Sikia nenda kaongea naye. Huyu anahitaji kazi kwenye kampuni yetu kwa jinsi nilivyomwona amemaliza chuo hivi karibuni. Atatufaa. Usimfanyie usahili leo. Mpe miadi ya kukutana naye wiki mbili zijazo hapo najua utakuwa umeshazoea kazi. Kisha mengine yataendelea hukohuko”

“Bado sijakuilewa Mr. Kolowa”

“ Kampuni yetu inahitaji wanawake kama yule mrembo. Hii ni nafasi yako kuonyesha unaweza. Unabahati sana” Kolowa alikuwa akizidi kumchanganya sana Amini. Maneno yake yalikuwa kama kitabu cha mafumbo ya wagiriki wa kale ambacho kilikuwa kimeandikwa na wanafalsafa.

“ Unaweza ukaenda sasa” Kolowa akamruhusu.

“Amini! Sorry one thing!” Akamuita kisha akamfuata wakakutana katikati, akamnong’oneza sikioni.

“ Kuwa makini, chunguza maswali yake. Kama yanalingana na jinsi alivyo au huenda ni usalama. Jitahidi kutumia akili katika kazi yako mpya”

Maneno hayo yakamvuruga zaidi Amini. “ Usalama tena! Kwani nini kinaendelea?” akawaza huku akiwa anatazamana na Kolowa. Kisha Kolowa akatabasamu na kumpa saluti kama ishara ya kumtakia kazi njema. Amini naye akainamisha kichwa chake kama jibu la kile alichoambiwa na Kolowa.

“ Nifuate” Amini akasema akimwambia yule Mwanamke mweupe. Wakaelekea ofisini kwake. Muda huo Kolowa alikuwa ameshaondoka.

“Karibu sana mdada. Keti hapo” Amini akasema, huku akikaa kwenye kiti chake kikubwa cha kiofisi, na Yule mrembo akaketi akiwa anashangaa shangaa ofisi ile.

“ Unaitwa nani na unahitaji tukusaidie nini?” Amini alifungua mazungumzo rasmi ya kiofisi.

“ Naitwa Lucy Njama. Ni mhitimu wa sheria” Lucy akasema, ingawaje alikuja kwa mpango wa kukutana na Kalage lakini mazingira ya eneo lile hayakuonyesha uwepo wa Kalage. Sasa alibadili mpango wake kutokana na mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea.

“ Ndio Lucy:”

“Am! Amm! Nimependezwa na kampuni yenu. Nilikuwa nahitaji nishirikiane nanyi katika kuyafikia malengo ya kampuni hii. Kama mwanasheria mahiri na mwenye kipaji kinachotafutwa na wenye ndoto kubwa. Naamini nitakuwa na tija kwenye ofisi yenu hasa nikishirikiana na wafanyakazi wenzangu wenye nia na maarifa kama mimi ya kuisaidia kampuni hii” Lucy alikuwa akiongea kwa utulivu mkubwa.

“ Naweza kuona Wasivu na vyeti vyako au nakala zozote ulizonazo?’

“ Kwa bahati mbaya zipo nazo nakala ngumu, ila nilizonazo ninaweza kukutumia kwenye email au whatsapp. Zaidi naweza kuonyesha uwezo wangu kama nikijaribiwa kwa vitendo. Cheti cha taaluma cha shahada bado hakijatoka lakini hiyo haimaanishi uwezo wangu utashindwa kufanya kazi kwa kutegemea cheti hicho. Nafasi ya cheti ni uthibitisho wa muda tuu kabla ya uthibitisho wa vitendo ambao ndio wa kudumu unaohitaji”

“ Sawasawa! Umejieleza vizuri. Nimevutiwa na jinsi unavyoweza kujieleza. Aaah! Lakini kwa sasa siwezi kusema kitu. Siwezi kukuahidi kama kuna nafasi au hakuna. Ila nimeona umuhimu wa kukupa email yetu ili utume hizo nakala zako. Tutazipitia. Kisha ndani ya wiki mbili tutakupigia simu kwaajili ya kuona nini tutaafikiana. Utachukua hii, ndio namba yangu lakini hii ni emai yetu. Utatuma hapo”

“Nashukuru sana. Hili ndio jina lako”

“Ndio!” Amini akajibu. Lucy mbali na kujieleza sana lakini macho yake hayakuweza kumwangalia Amini. Licha ya kujitahidi lakini alishindwa. Aligundua kuwa macho yake hayakuwahi kuonana na kijana mwenye mvuto kama Amini.Mvuto wa Amini ulimfanya Lucy ashindwe kuyatuliza macho yake katika uso wa kijana huyo.

“Huyu ndiye natakiwa nimuite mpenzi hubby na sio zile takataka zingine” Lucy akawaza huku akiwa anashikashika ile karatasi yenye namba za Amini na jina lake.

“Nafikiri tumeshamaliza” Amini akasema tayari akinyanyuka, kisha wakatoka, akamsindikiza lakini baadhi ya wafanyakazi walikuwa wakichungulia kwenye madirisha ya vioo yenye kingo za alluminium. Wanawake hawakupenda tukio hilo na wengi waliishia kusonya na wengine wakitukana kimoyomoyo. Kila mwanamke alitamani awe na Amini licha ya kuwa ndio ilikuwa siku yao ya kwanza kumwona.

Amini alimsindikiza Lucy mpaka chini kabisa, lakini punde Lucy akamwona mwanaume mmoja mwenye Draid aliyevaa kofia kana kwamba alikuwa akimfananisha. Mwanaume yule alikuwa anaingia kwenye duka kubwa lililokuwa karibu na ile ghorofa.

“Kaka! Kaka!” Lucy akaita Yule mwanaume akageuka.

“ Ndio wewe!” Lucy akasema, Amini akaingiwa na wivu lakini kwa upande wa yule mwanaume alikuwa akamshangaa Lucy.

“ Umenifananisha Dada”

“ Ni wewe mwenyewe”

“ Mimi sikujui! Umenifananisha”

“ Huyu hapa! Huyu hapa!” Lucy akaimba ule wimbo wa uliokuwa ukiimbwa na yule kahaba kwenye jukwaa la burudani kule kwenye ile Casino ya Blackcross.

“Unanipotezea muda wangu samahani” Yule mwanaume akasema kisha akaondoka akiwa ameghairi kuingia kwenye lile duka kubwa. Hakuwa mwingine zaidi ya Peter Mirambo.

“Mbona unaparamia wanaume hovyohvoyo usiwaojua?”

“Hamna namjua huyu Kaka”

“Lakini yeye kasema hakujua na umemfananisha. Wewe unaonekana kulazimisha”

“ Hawezi kunijua lakini mimi namjua”

“Unamaanisha nini?”

“Boss mambo mengine ni Personal. Ila huyu kaka ni mcheza dansi mzuri sana sidhani kama unaelewa maana yake”

“Sasa kama hakujui wewe umemjuaje?”

“Yeye ni mcheza Dansi mimi ni mtazamaji. Hivi Boss wewe unajua kucheza”

“ Mimi! Hahaha! Daaah!”

“ hahahaha” Lucy akacheka akiwa anamtania Amini.

“ Unaonekana wewe sio mtu wa usiku. Ukiwa mtu wa usiku huwezi kushindwa kuwajua watu kama yule mwanaume” hapo alikuwa amefika kwenye gari yake. Amini alishangaa kuona gari ya Lucy ambaye alikuwa binti mdogo tuu tena aliyemaliza chuo juzijuzi lakini alikuwa na gari. Yeye hata baiskel hana licha ya kuwa alikuwa ni Boss.

“ Hii gari ni yako?”

“Kwani unanionaje?” Lucy akajibu kwa madoido huku akibonyeza rimoti ya kufungulia mlango wa gari. Akafungua.

“ Nashukuru Boss kwa kunisindikiza. Nimefurahi sana. Nje ya kazi naweza itumia namba yako?”

“ why not?”

“hayo ndio maneno” Lucy akasema akiwa amefurahia kukutana na Kijana yule ndiye Amini. Wakaachana huku Lucy akiapa moyoni mwake kumteka Amini awe Mpenzi wake.

********************
ITAENDELEA
0693322300
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…