Riwaya: From Isra to Isra (Kutoka Isra kwenda Isra)

Riwaya: From Isra to Isra (Kutoka Isra kwenda Isra)

KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............24
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Mafisa wapelelezi kutoka jeshi la polisi Inspekta Brandina na Inspekta Masoud wanapanga mikakati ya kuhakikisha wanamkamata Felix moja kati ya wahusika wa matukio ya utekaji. Upande wa pili katika bonde la Magnus, Dayana anamganda David akihitaji penzi kutoka kwake.

Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
[emoji294][emoji294][emoji294]
Dayana alizidi kumsogelea David.
"Kasema anarudi baada ya dakika 10, Davii..zinatosha sana please nisaidie mwenzio nateseka" Alisema Dayana huku akianza kuushika shika mwili wa David. Ilikuwa ni rahisi kwa sababu pia wote walivaa nguo za ndani pekee

"Da...ya...naaa!!" David aliita kwa taabu kidogo lakini Dayana hakuacha, alidhamiria.

Punde Dayana alianza kummwagia David mvua ya mabusu shingoni kwa kasi na mwisho akahamia mdomoni huku taratibu akiupeleka mkono wake ndani ya boksa ya David. Hali hii ilizidi kumuweka David katika wakati mgumu, alijitahidi kumsukuma Dayana lakini tayari Dayana alishaingiza mkono hadi ndani kabisa ya boksa yake.

David akajikuta mwili wake unapata ganzi ya ghafula mithiri ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Wakati huo huo David alisikia vishindo vya miguu ya Zungu akirudi, lakini Dayana yeye hakuwa akisikia kitu aliyafumba macho yake huku akiwa amezama mazima na kuelea kwenye ulimwengu wa huba.

David hakutaka kuendelea kusubiri haraka alimsukuma Dayana kwa nguvu kubwa, Dayana alirudi nyuma na kuanguka chini.

"Oii! Twendeni basi kuposhwari hu....." Alisema Zungu lakini akashindwa kumalizia sentesi yake akabaki ameduwaa akishangazwa na mazingira aliyowakuta David na Dayana.
Dayana alikuwa amekaa chini huku David naye akizuga na kugeuka akawa anatazamana na ukuta wa bonde hilo.

"Nyie vipi kuna nini? Dayana mbona umekaa chini kwamba umeshachoka tayari?" Aliuliza Zungu akiwatazama David na Dayana kwa zamu.

Hakuna aliyejibu wote wakawa kimya.

"Aah! Dayana anasema anahisi kizunguzungu" Mwisho David alidanganya huku akiwa bado amegeukia kule ukutani. Hakuwa na jeuri ya kugeuka atazamane na Zungu kwani tayari hata yeye mwanajeshi wake alishasimama imara tayari kwa mapambano mara baada ya kushikwa na Dayana, mbaya zaidi alikuwa amevaa boksa pekee, ilikuwa ni rahisi mno kwa Zungu kumshtukia.

"Nilisema lakini usitufuate, si unaona sasa mambo ya kung'ang'ania mishe za kiume" Alisema Zungu huku akisogea hadi pale alipo Dayana.

"Vipi tukurudishe au?" Aliuliza Zungu.
"No! Nendeni nitarudi mwenyewe" Alijibu Dayana huku akisimama ghafula. Alionekana kuwa na hasira sana, Zungu akawa anashangaa mtu aliyeambiwa anahisi kizunguzungu kasimama kwa kasi bila tabu yoyote.

Mwisho walikubaliana hivyo, Dayana akawa anarudi, David na Zungu wao wakaendelea kusonga mbele. Lakini kabla hawajafika mbali mara walisikia kelele za Dayana akilia kwa nguvu.

"Mamaaa...nakufa!"

David na Zungu walisimama ghafula na kutazamana, wote walisikia kelele hizo kutoka kwa Dayana, wakawa wanasikilizia kwa mara ya pili lakini kukawa kimya.

"Oya turudi kuna shida mwanangu" Alisema Zungu na bila kujiuliza mara mbili mbili aligeuka haraka na kuanza kurudi, David naye akawa anamfuata nyuma kwa kasi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati huo upande wa pili Magnus alikuwa akiendelea kuongea na watu aliowaita wanafunzi wake kutoka ISRA, wale aliowateka kwa nyakati tofauti tofuauti akawaleta katika kisiwa hicho.
Sasa walikuwa darasani...

"Leo tunao wageni wawili ambao ni wenzetu kutoka ISRA, Zucc na Femi kule nyuma. Karibuni sana" Magnus aliongea kwa sauti nzito yenye kukoroma huku akinyoosha kidole chake kuwaelekea Zucc na Femi ambao walikaa nyuma kabisa ya darasa hilo.
Macho ya Magnus yalizidi kuwa mekundu kutokana na ule moshi uliokuwa ukitoka kwenye vile visahani mezani lakini yeye wala hakujali. Aliendelea kuifurahia harufu ya moshi huo, kwake ikiwa ni burudani kubwa.
Nywele zake ndefu, ndevu zake nyingi na nyeupe vilizidi kumfanya mzee huyo awe na muonekano wa kutisha mno. Aliendelea kuzungumza...

"Kule ISRA wananiita mimi muasi, lakini sio kweli. Mimi Magnus sio muasi bali ni mtu ambaye nilifanikiwa kuzijua siri nyingi za ISRA zilizofichwa kwa muda mrefu, siri ambazo zimefichwa kwa makusudi ili kuinyima uhuru ISRA na watu wake. Ni siri hizo ambazo zilinifanya mimi kutamani kufanya mabadiliko lakini watu wenye roho mbaya, watu wanaong'ang'ania madaraka wakaniita muasi, wakanishambulia wakaninyang'anya nguvu zangu na baadae wakanitupa nje ya ISRA" Magnus aliongea kwa masikitiko makubwa. Akatulia kwa muda kisha akaendelea...

"Hata baada ya kuwa nje ya ISRA sikuwahi kukata tamaa bado nimeendelea kupambana kuhakikisha haki ya ISRA inapatikana. Unaweza ukashangaa kwa nini na uzee wangu huu bado nataka sana kurudi ISRA, si kwa ajili yangu. Ni kwa ajili yenu ninyi na vizazi vyenu, ni lazima Mapinduzi yafanyike ili wajukuu zangu na watoto wenu wasije kuishi gizani kama sisi tulivyoishi. Nataka tutengeneze historia mpya ndani ya ISRA, mimi nikishirikiana na ninyi kwa pamoja tutamtoa Gu Gamilo na watu wake kwenye kiti kisha tutaweka watu watakaofuata haki na misingi ya ISRA iliyokuwepo tangu enzi za mababu zetu. Leo kwa mara ya kwanza nitaziweka wazi baadhi ya siri zilizofichwa ili na ninyi muone kama ni sahihi Magnus kuitwa muasi au alaa! MAPINDUZI YAFANYIKEEEE....."

"KWA AJILI YA MAISHA BORA YA ISRA NA WATU WAKE" Walijibu wanafunzi wa Magnus.

"Sisi leo tunaitwa WALINZI WA NAFSI tena nafsi za wanadamu, la hasha hilo sio jina letu tulipewa tu ili kutupotosha. Ukweli tunatofauti kubwa sana na Binadamu wala hatuhusiani kwa lolote ndio maana Mungu alituumba sisi akatupa nguvu na uwezo kuliko binadamu akatuweka ndani ya ISRA na binadamu akawaweka kwenye hii Dunia. Sisi kupewa nguvu zaidi yao ni kwamba tunaruhusiwa kuwatawala na si kulinda nafsi zao kama tunavyo danganywa siku zote. Sisi ni watawala na wao ni watawaliwa. Kama ni ulinzi wa nafsi zao kuna malaika ambao wanafanya kazi hiyo na sio sisi. Kuna malaika Gabriel, Michael, Israel na wengi wengi, sisi hatuhusiani na kazi zao KABISA, Ndugu zangu WAISRA tunahitaji kuungana na kwenda kuchukua kile kilichochetu kutoka kwa Gu Gamilo kule ISRA hatutaki tena kufanya mambo yasiyotuhusu Sijui kukusanya machozi, kuzuia ajali, kuua au kulinda binadamu zote hizo sio kazi zetu" Magnus aliongea kwa kumaanisha, sauti yake iliyojaa mamlaka na ushawishi mkubwa iliweza kuwaingia asilimia kubwa ya wanafunzi wake.

"Anaongea nini huyu?" Femi alimuuliza Zucc aliyekaa pembeni yake kwa sauti ya chini, wakawa wananong'ona.

"Hata sielewi lakini maneno yake ni kama yana ukweli Femi"

"Hapana, ni muongo anadanganya. Magnus ni mtu mwenye tamaa kama tulivyoambiwa, muangalie hata machoni, hafanani kabisa na mambo anayoongea. Anajaribu kutushawishi ili tuwe upande wake, anataka tufanye kazi badala yake kwa sababu hana nguvu tena za kuingia ISRA" Alisema Zucc.

"Lakini sisi tayari ni mateka wake, hatuwezi kutoka hapa kama tusipokuwa upande wake" Alijibu Zucc.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili Baada ya Zungu na David kusikia kelele za Dayana walirudi haraka na baada ya hatua kadhaa walimuona Dayana akiwa ametereza na kuangukia kwenye kichaka kilichokuwa na miiba.

"Dayana shida nini" Aliuliza Zungu huku akikimbia kumuwahi Dayana pale chini.
Dayana aliumia sana ukizingatia mwili wake ulikuwa wazi akajikuta anachomwa vibaya na miiba ile.

"Uko sawa Dayana" Aliuliza David huku naye akiwahiwa na kumshika mgongoni, akawa anasaidia kumuinua lakini Dayana akautoa mkono wake hakutaka kabisa David amguse.
Bado Dayana alikuwa amekasirishwa mno na kitendo alichokifanya David, kama mwanamke alikuwa amejizalilisha vya kutosha akiamini David angemsikiliza na kumtimizia haja yake lakini David hakufanya hivyo, badala yake alimsukuma.

David alijikuta anaumizwa pia na hali aliyokuwa nayo Dayana licha ya kutambua kwamba hana kosa lolote lakini bado alimuonea huruma mwanamke huyo.
Walisaidiana kumuinua Dayana kutoka pale chini kwenye miiba, wakati wanasimama mara ghafula mwanga mkali wa tochi ulipita mbele yao kwa kasi.

"Chuchumaeni chini" Alisema Zungu haraka wote wakafanya hivyo.

"Ni tochi za walinzi, bila sasha wamesikia kelele za Dayana" Alisema Zungu.

"Hapa mambo yameshaharibika, turudi tu hili zoezi tutalifanya kesho mshikaji wangu" Zungu alitoa wazo.

Mwisho Zungu, David na Dayana walirudi kule walipokaa mateka wengine, wakachagua sehemu nzuri pembeni ya kuta za bonde hilo wakawasha moto na kulala.
Ilikuwa ni ngumu sana kwa David kupata usingizi, hakuwa amezoea kuishi kwenye mazingira magumu kama hayo. Alikaa na kuegemea ukuta huku akitafakari hatima ya maisha yake itakuwa ni nini. Aliwaza pia kuhusu mdogo wake Tatu pamoja na mama yake ambaye kwa mara ya mwisho alimuacha akiwa ni mgonjwa amelazwa hospitali. Hadi inafika saa 11 alfajiri bado David hakuwa amepata usingizi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

ASUBUHI SIKU INAYOFUATA.....ISRA.

Ilikuwa ni asubuhi na mapema siku inayofuata katika mji wa ISRA, tayari viongozi mbalimbali wa ISRA walishafika ndani ya jengo la Ikulu na moja kwa moja walielekea kwenye jengo ambalo hutumika kujadili na kutoa hukumu mbalimbali za kisheria ndani ya ISRA.

Sasha, Handan pamoja na wale wanawake wawili wakiongozwa na askari wa ulinzi waliletwa na kuingizwa ndani ya chumba hicho. Sasa alikuwa anasubiriwa mkuu wa ISRA Gu Gamilo ambaye pia ni baba yake Sasha.
Haukupita muda Gu Gamilo aliingia akiwa ameongoza na askari wawili nyuma yake. Sura yake ilionekana kujaa simanzi kubwa.
Gu Gamilo alikumbuka siku kama hiyo iliwahi kutokea miaka mingi iliyopita, siku ambayo alisimama mbele katika chumba hicho hicho akamuhukumu kaka yake Magnus na kumfukuza ISRA. Leo hii tukio kama lile lile linajirudia tena lakini safari hii si kaka yake bali ni mtoto wake SASHA.

Je, nini kitafuata?
Hii ni SASHA MLINZI WA NAFSI sehemu ya 24, tukutane sehemu ya 25.
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

.Simulizi hii inapatikana yote hadi episode ya 125 kwa Tsh 1400/= tu lipa kwa namba M-PESA ~ 0756862047
AIRTEL MONEY~ 0788967317
JINA-SAUL MWANAWIMA
UKILIPIA TUMA SCREENSHOT AU SMS YA MALIPO kwa namba hizo hizo WhatsApp au kawaida, kama huna WhatsApp piga namba hizo juu nitakupa utaratibu wa kupata simulizi hii.
 
Kwani nini kilitokea hii simulizi inaridiwa maana ililetwa humu na mtunzi akapotea naona sasa inarudiwa tena
 
KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............25
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Gu Gamilo alikumbuka siku kama hiyo iliwahi kutokea miaka mingi iliyopita, siku ambayo alisimama mbele katika chumba hicho hicho akamuhukumu kaka yake Magnus na kumfukuza ISRA. Leo hii tukio kama lile lile linajirudia tena lakini safari hii si kaka yake bali ni mtoto wake SASHA.

SASA ENDELEA...
Majadiliano mazito yalinza huku Sasha akihusishwa moja kwa moja kwamba yeye ndiye sababu ya kutoweka kwa msitu wa Bi Noha. Sasa akawa anaonekana ni mtu mwenye makosa mawili, kwanza ni kuingia ndani ya msitu huo pasipo ruksa na pili ni kusababisha kutoweka kwa msitu huo na kuacha shimo kubwa jambo ambalo viongozi wote walilitafsiri kama ni laana nzito ndani ya ISRA.

Mwisho ukafika wakati wa kutoa adhabu anayostahili Sasha pamoja na walinzi wake ambao wao walishtakiwa kwa kosa la kushindwa kutimiza wajibu yao wakamuacha Sasha aingie ndani ya msitu wa Bi Noha.

Sasa kila mmoja akawa kimya kusubiri ni hukumu gani itatolewa na mkuu wa ISRA Gu Gamilo.

Jasho jembamba likawa linamtoka Gu Gamilo, kila akimtazama binti yake Sasha usoni alijikuta anakosa ujasiri kabisa. Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa asijue aseme nini, mikononi mwake alikuwa ameshikilia kitabu chao tukufu cha sheria za ISRA, kila mmoja akawa kimya anamtazama Gu Gamilo.

Dumayo ambaye ni mjomba wa Sasha baada ya kuona Gu Gamilo amekaa kimya kwa muda mrefu, alimtazama kwa macho yaliyojaa dharau kisha bila kusita akapiga hatua kadhaa kusogea mbele kule aliko Gu Gamilo kisha akawageukia viongozi.

"Hakuna asiyejua hapa kuwa Sasha ni mtoto kipenzi wa Gu Gamilo, ni ngumu sana kutoa hukumu kwa mtoto wako umpendae, naomba kwa niaba yake nisaidie kurahisisha hukumu hii kwa sababu kosa liko wazi na hukumu zake zinajulikana. Kuna muda maamuzi sahihi yanahitaji roho ngumu Mheshimiwa Gu Gamilo. Tafadhali tuambie ni hukumu gani unatoa kwa Sasha katika ya hizi mbili, moja ku......"

"Simama kwenye nafasi yako Dumayo" Gu Gamilo alifoka na kusogea mbele, akawa anamtazama Dumayo kwa macho makali.
Huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini Dumayo alirudi kwenye nafasi yake taratibu.

"Kwa kuheshimu sheria na mamlaka niliyopewa kuiongoza ISRA, nawahukumu walinzi wa Sasha Handan, Emine na Froza miezi tisa gerezani kwa kosa la kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo. Sambamba na hilo, kwa kosa kubwa alilolifanya SASHA, kuingia katika msitu wa Bi Noha pasipo ruksa na mwisho kusababisha maafa makubwa ndani ya ISRA leo hii namuhukumu kifungo cha kukaa nje ya ISRA daima, atanyang'anywa nguvu zake zote kama SASHA MLINZI WA NAFSI na mwisho atatupwa nje ya ISRA na hatorudi milele" Gu Gamilo alikaza roho na kutoa hukumu kwa Sasha na walinzi wake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Saa moja baadae Sasha akiwa amefungwa minyororo mikono na miguu yake alibebwa kwenye farasi na askari mmoja kuelekea lilipo jengo moja kubwa lilokuwa nyuma ya Ikulu ya ISRA, huko waliishi watu maarufu kama watakatifu wa ISRA. Walikuwa ni wanaume 12 pekee. Kichwani walinyoa vipara huku wakivaa mashuka yenye rangi ya kahawia, bega moja wakiliacha wazi. Walifanana kabisa na wale watu wafuasi wa dini ya imani ya Buda.

Askari aliyembeba Sasha alifika na kumtupa chini mahali penye uwanja mpana nje ya jengo hilo.

Haukupita muda walitokea wanaume watano kutoka ndani ya ile nyumba takatifu. Mikononi mwao walikuwa wamebeba vioo virefu na vipana. Walitembea taratibu hadi walipomfikia Sasha. Taratibu walivipanga vile vioo kumzunguuka Sasha, wakatengeneza kitu kama boksi la vioo Sasha akiwa ndani yake. Mara akatokea mwanaume mwingine kutoka ndani ya jengo lile, alionekana ndiye kiongozi wa wenzake, sasa wakaongezaka na kuwa sita.
Walitengeneza duara kuzunguuka lile boksi la vioo kisha wakakaa na kukunja miguu yao kama vile wafanyavyo mabuda.
Baadae waliunganisha mikono yao wakawa wanasali kwa namna ambayo waliijua wao.

Wakati haya yakiendelea. Gu Gamilo, Dumayo pamoja na viongozi wengine wa ISRA walikuwa wakishuhudia kwa mbali zoezi hili la kuondoa nguvu za Sasha kabla ya kumfukuzwa ISRA.

Ilikuwa ni tukio lenye kuuumiza vikali moyo wa Gu Gamilo lakini hakuwa na chaguo, binti yake Sasha alikosea na alistahili adhabu. Yeye kama mkuu wa ISRA hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuacha sheria ifuate mkondo wake.

Kila tukio lililokuwa kilifanywa na wale wanaume lilimkumbusha Gu Gamilo yale yaliyotokea miaka mingi iliyopita baada ya kaka yake MAGNUS kugeuka muasi. Naye pia aliadhibiwa kama anavyoadhibiwa Sasha hii leo.

Wakati wale wanaume wakifanya Sala zao, mara ghafula Sasha alianza kupiga kelele na kugaa gaa ndani ya lile boski la vioo, kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo Sasha alizidi kulalamika mithiri ya mtu anayepitia maumivu makali yasiyo na mfano. Mara ghafula vilionekana vitu kama radi za moto kutoka kwenye mwili wa Sasha, radi ambazo zilitoka na kupiga pande zote za vile vioo. Wale wanaume wakadizisha sala yao na safari hii walianza kuongea kwa sauti kubwa kwa lugha wanayoielewa wao.

Sasha aliendelea kupiga kelele na mwisho amini usiamini aliweza kuikata ile minyororo ya chuma aliyokuwa amefungwa nayo. Akasimama ghafula huku akipiga kelele akawa anahangaika huku na kule ndani ya lile boski akijaribu kutoka lakini hakuweza. Radi za ajabu zikaendelea kutoka kwenye mwili wake na taratibu zikaanza kutengeneza mipasuko kwenye vile vioo.
Baada ya muda Sasha alianza kuhisi kuishiwa nguvu, hata kelele zake zikapungua pia. Mwisho alianza kuyumba yumba kama mlevi hatimae akaanguka chini.
Akiwa pale chini Sasha aliiona sura ya yule bibi kizee aliyekutana naye kule msituni, Bi Noha akiongea...

"Jikaze binti yangu, njia unayoipitia ni njia sahihi kuielekea hatima yako, usikate tamaa SASHA"

Alisema Bi Noha na wakati huo huo akapotea kwenye macho ya Sasha na hapo ikamuijia taswira nyingine ya binadamu aitwae David.
Sasha alimuona David akiwa ndani ya shimo moja kubwa akihangaika namna ya kutoka, lakini mara juu ya shimo hilo akamuona mzee mmoja mwenye sura ya kutisha sana alikuwa ni Magnus baba yake mkubwa.
Mzee huyo alikuwa na watu wengine wengi nyuma yake, wakaanza kutupia shimoni vitu kama kuni na mwisho wakamalizia kwa kumwagia mafuta.

Magnus alitoa kiberiti akawa anataka kukiwasha, lakini mara ghafula katika shimo lile akatokea Sasha mwenyewe akiwa na mnyororo mrefu mkononi mwake akampa David. David aliurushwa ule mnyororo kuelekea juu ukamnasa Magnus kisha akamvuta kwa nguvu. Haraka David akamshika Sasha kiunoni, wakati Magnus akiangukia ndani ya shimo lile bàada ya kuvutwa na mnyororo David na Sasha wakawa wanavutwa na mnyororo huo huo kuelekea juu.

Hii ilikuwa ni kama ndoto iliyokuwa ikipita kwenye akili ya Sasha na muda huo huo Sasha akapoteza fahamu (akazimia).
Baada ya Sasha kuzimia mara ghafula kile kioo kikapasuka kwa nguvu vipande vipande.
Vile vipande viliruka na kuwajeruhi wale wanaume lakini hawakujali, wakaendelea na sala yao hadi walipofika mwisho.

Baada ya hapo wakatokea wanaume wengine tena wanne wakiwa wamebeba sanduku la mbao mikononi mwao.
Walifika na kuvikusanya vile vipande vya vioo wakaviweka katika sanduku hilo kisha wakalifunga kwa kulipiga misumali wakaondoka nalo kurudi ndani.

Baada ya hapo yule mwanaume kiongozi akatoa ishara fulani kule alipokuwepo Mkuu wa ISRA Gu Gamilo na viongozi wengine. Naye Gu Gamilo akatoa ishara kwa askari wake mwenye farasi akasogea na kwenda kumchukua Sasha ambaye bado alikuwa hajitambui akaondoka naye.
Yule mwanaume alifuata nyuma taratibu alipofika karibu na Gu Gamilo pamoja na viongozi wengine akasimama. Wote wakainamisha vichwa vyao chini kuonyesha heshima kubwa kwa mtu huyo. Akaongea...

"Huyu binti atolewe haraka nje ya ISRA kabla hajalejewa na fahamu zake. Nimefanya kazi hii kwa muda mrefu mpaka sasa lakini leo nimeshuhudia kitu cha tofauti sana. Huyu binti anayo nguvu kubwa mno ndani yake. Sijui ametenda kosa gani hadi mkampa hukumu kama hii, lakini basi niseme tu sisi tumefanya kazi yetu, niwatakie kila la kheri" Alisema yule mwanaume, kauli iliyowafanya Dumayo na Gu Gamilo watazamane.

ITAENDELEA...
Simulizi hii inapatikana yote hadi episode ya 125 kwa Tsh 1400/= tu lipa kwa namba M-PESA ~ 0756862047
AIRTEL MONEY~ 0788967317
JINA-SAUL MWANAWIMA
UKILIPIA TUMA SCREENSHOT AU SMS YA MALIPO kwa namba hizo hizo WhatsApp au sms ya kawaida.
 
KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............26
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"......Sijui ametenda kosa gani hadi mkampa hukumu kama hii, lakini basi niseme tu sisi tumefanya kazi yetu, niwatakie kila la kheri" Alisema yule mwanaume, kauli iliyowafanya Dumayo na Gu Gamilo watazamane.

SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]

Ilikuwa ni majira ya saa nane mchana Inspekta Brandina alitoka ofisini akawa anaelekea katika hoteli moja jirani na ofisi kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.
Akiwa ndio kwanza anashuka tayari kuingia ndani ya hoteli hiyo mara simu yake iliita, akatazama namba ya mpigaji ilikuwa ni namba ngeni, akapokea.

"Hallo"

"Hallo bila shaka nazungumza na Inspekta Brandina"sauti nzito ya kiume ilisikika simuni.

"Yes ndio mimi, nani mwenzangu?"

"Unaongea na Jacob kutoka idara ya usalama wa taifa, tulipokea ripoti yenu asubuhi ya leo na tayari tumeanza kuifanyia kazi tafadhali umaweza kufika zilipo ofisi zetu sasa hivi?"

"Sawa, bila shaka, nakuja sasa hivi. Samahani nije mwenyewe au na wenzangu tunaoshiriki kufuatilia kesi hii?"

"Njoo mwenyewe tayari tumewapigia wenzako wawili Inspekta Masoud na Inspekta Shamsa wapo njiani, nafikiri mnatosha"

" Haswaa, Asante nipo njiani nitafika ndani ya dakika kumi" Alisema Inspekta Brandina huku akitabasamu na kukata simu. Tayari matunda ya kile alichokifanya yalianza kuonekana. Kama walivyodhania kuwa kitendo cha kuiona picha ya Felix nyumbani kwa Tesha na kisha kupata mawili matatu kumuhusu ilikuwa ni hatua kubwa, na kweli.

Brandina alifungua mlango wa gari ili aianze safari kuelekea zilipo ofisi za Idara ya usalama wa Taifa, lakini kabla hajaingia mara alisikia sauti ya kike ikiita kutokea nyuma yake.

"Afandee..Afande...madam B"

Brandina aligeuka kutazama, mara uso kwa uso anakutana na mtu ambaye hakuwa ametegemea kukutana naye, alikuwa ni Tesha.

"Teshaa...!!" Aliita Brandina sauti yake ikiambatana na mshangao mkubwa.

"Yes! Its me..."Alisema Tesha huku akihema kwa nguvu, alikuwa akikimbia hadi pale alipomfikia Inspekta Brandina.

"Kwa nini uko hapa?"

"Aah! Actually nilikuwa napita tu naelekea hospitali mara moja, kwa bahati nikakuona hapa unaongea na simu nikamuomba dereva wangu asimamishe gari nikusalimu" Alieleza Tesha huku akiachia tabasamu ang'avu lililozidi kuipamba sura yake nzuri ya kuvutia.

"Hospitali nani anaumwa?" Aliuliza Brandina huku akiitazama saa yake ya mkononi. Tayari zilikuwa zimekatika dakika mbili tangu alipomaliza kuzungumza na Jacob kutoka ofisi za Idara ya usalama wa Taifa.

"Ni mama wa yule kijana aliyetekwa jana, aah! Unajua David kapatwa na matatizo mbaya zaidia alimuacha mama yake hospitali ni mgonjwa nikapata wazo la kwenda kumuona..."

"Ooh! That's good Tesha, kuna mahali nawahi please naomba nikuache au una jambo muhimu unahitaji kunieleza" Alisema Brandina, Tesha akaikunja sura yake akionekana kutofurahishwa na kauli hiyo ya Inspekta.

"Hapana, sina jambo la muhimu sana ila nilitaka kujua maendeleo ya lile tukio la jana vipi kuna dalili zozote za David kupatikana?"

"Aaa.. ukweli mambo yanaenda vizuri tumefanikiwa ku...." Alisema Brandina huku akitaka kueleza hatua waliyofikia lakini mara akakumbuka kuwa Felix ambaye ni target yao namba moja ni mpenzi wa Tesha hivyo kama ataweka wazi jambo hilo itakuwa ni sawa na kuvuruga mipango yao.

"...tunafanya jitihada kubwa kuhakikisha David na wengine wote waliotekwa wanapatiakana haraka iwezekanavyo" Brandina akapindisha maelezo.

"Sawa basi nashukuru sana, nitafurahi kama David atapatikana akiwa hai"

"Usijali, tutaendelea kuonana chukua namba yangu kwa kaka yako Godfrey" Alisema Inspekta Brandina haraka akaingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi hata bila kusema kwa kheri.

Tesha naye alirudi ndani ya gari yake safari ya kuelekea hospitali kumuona mama yake David ikaanza.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Kutokana na mwendo aliokuwa nao, dakika 7 pekee zilimtosha Brandina kufika zilipo ofisi za Idara ya usalama wa Taifa. Haraka alishuka kutoka garini akaanza kupiga hatua ndefu ndefu kuingia ndani ya jengo kubwa lilokuwa na maandishi makubwa getini yaliyosomeka 'TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE (TISS). Baada ya kufuata taratibu zote za kiusalama Inspekta Brandina aliruhusiwa kuingia ndani.

Aliingia katika chumba alichoelekezwa akawakuta tayari wenzake wawili walishafika wanamsubiri. Alikuwepo Inspekta Masoud Inspekta Samsha pamoja na sura nyingine ngeni za watu wawili ambao hakuwafahamu. Brandina alikaa kitini mbele ya meza moja ya duara.

Bila kupoteza muda mmoja kati ya zile sura ngeni alisimama na kusogea mbele kulipokuwa na screen moja kubwa ukutani, akaiwasha.

"Tuko nje ya muda, naomba tuanze moja kwa moja. Nitafanya utambulisho wa haraka kwa sisi wawili ambao hamtufahamu. Mimi niite Jajusi Jacob, na mwenzangu muite Jajusi Mwaseba. Tumepewa jukumu la kushirikiana na ninyi baada ya kuipitia ripoti yenu asubuhi ya leo hivyo kuanzia sasa tutakuwa wote katika jukumu la kuifuatilia kesi hii ya utekaji mpaka mwisho.
Kwanza kabisa nitoe pongezi kwa hatua kubwa mliyofikia kuweza kumbaini moja kati ya watu wanaohusika na utekaji huu." Alieleza Jajusi Jacob kisha akachukua rimoti ndogo mezani akaibinya. Picha ya kijana Felix ikaonekana kwenye uso wa screen ile huku pembeni yake ile video ya kamera za CCTV zilizomnasa Felix siku ya utekaji ikionekana pia.
Jacob akaendelea kutoa maelezo ya kina...

"Tuliweza kuwasiliana na shirika la Ujasusi nchini Marekani CIA watusaidie kumpata huyu mtu, kwa bahati nzuri wametupa ushirikiano wa kutosha. Ni kweli huyu mtu ameonekana nchini Marekani na anatumia jina Tofauti na lile mliloandika kwenye ripoti yenu, haitwi Felix. Jambo muhimu zaidi ambalo nataka kuwaeleza ni kwamba leo hii huyu mtu ameonekana majira ya saa sita mchana katika uwanja wa ndege wa JK Kennedy jijini New York huko Marekani. Hizi ni picha zinaonyesha wakati akipanda ndege ya BOENG 707 AIRWAY , ndege hii inakuja nchini Tanzania na hivi tunavyoongea tayari imeisharuka hivyo tutalajie majira ya saa moja asubuhi siku ya kesho itawasili nchini. " Alieleza Jacob

Hizi zilikuwa ni taarifa njema sana kwa Brandina na wenzake, sasa walikuwa wanaukaribia ushindi mkubwa.
Kilichoendelea baada ya hapo yalikuwa ni majadiliano ya kina kuhusu namna watanavyoweza kumkamata Felix mara tu Ndege itakapotua uwanja wa Ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili tayari Tesha alishafika hospitali, akafanya taratibu zote muhimu kuhakikisha mama yake David anapata matibabu yote muhimu ikiwa ni pamoja na kulipia ghalama zote za matibabu.

"Mwanangu..." Aliita mama David wakati akiwa pamoja na Tesha eneo la mapumziko katika bustani nzuri nje ya hospitali hiyo.

"Nashukuru kwa kila kitu ulichofanya, japo umesema ni David kakutuma lakini asante. Hata wewe unaonekana mkarimu sana" Alisema Mama David wakati huo Tesha hakuwa amemweleza lolote kuhusu tukio la kutekwa kwa mwanae David, hakutaka mama ajue kwa sababu kwanza alikuwa ni mgonjwa.

"Asante mama, mimi na David ni marafiki wakubwa. Kwa hiyo sioni shida kufanya hivi. Familia yake ni familia yangu pia" Alieleza Tesha huku akimshika Mama David mikono yake yote miwili.

"Marafiki ee!...."

"Ndiyo mama sisi ni marafiki wakubwa sana"

"Aah! Sawa kwa hiyo nyinyi ni marafiki eti?" Mama David alirudia tena swali lilelile kiasi cha kumfanya Tesha amtazame kwa mshangao lakini mwisho akatabasamu.

"Yah! Sisi ni mara..." Alijibu Tesha lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara akakatishwa na mlio wa simu yake iliyokuwa ikiita, haraka akaichukua kutoka kwenye mkoba wake akapokea.

"Eenhe! Shoga angu skendo skendooo... nilikwambia kuwa super star' kazi ingia WhatsApp basi fastaaaa..." Ilisikika sauti hiyo kutoka upande wa pili wa simu na mwisho ikakatwa.

"Khaa! huyu naye" Aliwaza Tesha akiwa katika hali ya kuduwaa lakini mwisho akafungua data na kuingia kwenye mtandao wa kijamii WhatsApp kama alivyoelezwa.

Aliiacha simu yake kwa muda akisubiri kwanza ziingie meseji zote kwani hakuwa ameifungua programu ya WhatsApp tangu asubuhi ya saa nne.
Baada ya kusubiri Tesha akaanza kufungua ujumbe mmoja baada ya mwingine huku akianza na watu wa muhimu kwanza kabla hata ya yule aliyempigia simu, alijua hana lolote zaidi ya umbeya.

Wakati akifanya hivyo Mama David akawa anamtazama huku akionekana kuwa na tabasamu usoni, tayari alishampenda Tesha, akawa anatamani pengine David amuoe na kumfanya mkwe wake.

Mara ghafula Tesha alionyesha mshtuko wa ajabu, almanusra simu yake idondoke.

"Vipi mwanangu kuna tatizo?" Aliuliza mama David huku naye akionekana kushtuka.

Tesha hakujibu kitu badala yake akawa anaangalia picha moja aliyotumiwa na rafiki yake kipenzi anaitwa Mina. Picha hiyo ilimuonyesha Mina akiwa ndani ya ndege lakini siti kadhaa pembeni yake alimuona mwanaume mmoja amevalia jeans na shati jeupe la mikono mifupi, usoni alivaa miwani mikubwa myeusi, huyu hakuwa mwingine bali Kipenzi chake Felix.
Picha hiyo iliambatana na maelezo haya chini yake.

,,,,,,,, Bestie nko Marekan now napanda ndege kurud tz c nmekutana na shemela yle uliwah nitambulisha mwaka jna ofcn kwko, nakwambia nimejikausha kma vle cmjui maana na ww mahusiano yko hata cyaelewag mpo kama hampo, hebu mchek shem mwenyew alivyonuna [emoji12],,,,,,,,,,

Tesha alimaliza kuusoma ujumbe huu huku mikono yake ikitetemeka, akaitazama vizuri ile picha kwa mara nyingine ni kweli alikuwa ni Felix mwenyewe.

,,,,,Ndege gani mmepanda?,,,,,,,,
,,,,,,Inaondoka saa ngapi,,,,,,,,,,,
,,,,,,Mina nambie plz,,,,,,,,,,,,

Tesha alituma ujumbe mfululizo akisahau kwamba kama wameshaanza safari basi Mina hawezi kuwa hewani wakati huo.

"Mwanangu nini shida? Uko sawa kweli?" Mama David alirudia tena swali lake.

"Ukweli siko sawa mama" Alijibu Tesha.

Wakati huo upande wa pili ndani ya ofisi za Idara ya usalama wa Taifa (TISS) kikao cha maafisa upelelezi kutoka jeshi la polisi na wale majasusi kilimalizaka, sasa mikakati yote ilikuwa imekaa sawa, wakaingia kwenye utekelezaji.

Je nini kitafuata?
Je mtoto wa Magnus -Felix atakamatwa?
Je Tesha atafanya nini?
Vipi kuhusu hukumu ya Sasha kule ISRA?
Nini maendeleo ya David, Dayana na Zungu kule bondeni"

ITAENDELEA....
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Simulizi hii inapatikana yote hadi episode ya 125 kwa Tsh 1400/= tu lipa kwa namba M-PESA ~ 0756862047
AIRTEL MONEY~ 0788967317
JINA-SAUL MWANAWIMA
UKILIPIA TUMA SCREENSHOT AU SMS YA MALIPO kwa namba hizo hizo WhatsApp au sms ya kawaida.
 
KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............27
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Wakati huo upande wa pili ndani ya ofisi za Idara ya usalama wa Taifa (TISS) kikao cha maafisa upelelezi kutoka jeshi la polisi na wale majasusi kilimalizaka, sasa mikakati yote ilikuwa imekaa sawa, wakaingia kwenye utekelezaji.

SASA ENDELEA...
Majira hayo ya mchana ilikuwa ni wakati wa mateka wa Magnus walio hifadhiwa ndani ya bonde lile la ajabu kupata chakula cha mchana.
Tofauti na siku nyingine, leo zilikuja gari tatu ambazo zote zilikuwa zimesheheni chakula ambacho ni makopo ya juisi na maji pamoja na vipande vya keki vilivyofungwa vizuri ndani ya mifuko ya laironi.

Kama kawaida yale magari yalianza kumwaga vyakula bondeni na wale mateka walikimbizana na kung'ang'ania chakula kile. Hakuna aliyejua sababu hasa ya kubadilishwa kwa chakula siku ya leo kwani siku zote walizoea kupewa mikate na maji. Ilikuwa ni siku njema sana kwao isitoshe chakula kilikuwa kingi mno tofauti na siku nyingine. Kila mmoja alipata.

David akiwa amejikunyata kwenye kona moja ya bonde hilo yeye hakwenda kung'ang'ania chakula na wenzake, alikuwa hajiskii kabisa kufanya hivyo. Bado alikuwa hajazoea.

Mara kwa mbali alimuona Dayana anakuja. Mikononi mwake amebeba mifuko mitatu ya keki maji makopo wawili na juisi kopo moja. Alitembea taratibu akielekea pale David alipo.

David alikuwa akimtazama Dayana tangu akiwa mbali. Dayana alikuwa ni mwanamke mzuri wa sura na umbo pia, licha ya kuwa na maisha magumu bondeni lakini bado mwili wake ulionekana kunawili na kupendeza, Ile taiti aliyovaa ilimkaa vilivyo ikimbana kiono chake na kulifanya umbo lake namba nane lionekane dhahiri shahiri.
David hakuacha kumkodolea macho Dayana hadi alipofika pale alipo.

"Kwa hiyo utakuwa unafanya hivyo mpaka lini?" Aliuliza Dayana akiwa amesimama mbele ya David na kushika kiuno chake.

David alimtazama Dayana kuanzia juu hadi chini.

"Ni mzuri!!" Aliwaza David kisha naye akauliza...

"Kufanyaje..?"

"Kwa nini huendi kuchukua chakula? Utaishije humu bondeni bila kupambania chakula au na wewe unampango wa kufa kama wengine?" Aliuliza Dayana, sasa hakuwa na kinyongo tena na kijana David kuhusiana na lile tukio la jana usiku.

"Nitakufaje na njaa na wewe upo..." David aliongea huku akitabasamu, Dayana naye akatabasamu.

"Una masihara wewe haya shika, jioni ni zamu yako kwenda ku-fight, ole wako urudi mikono mitupu" Alisema Dayana huku akimrushia David mfuko mmoja wa keki na lile kopo la juisi.

Wakati Dayana akiwa anajiandaa kukaa mara ghafula kuna mtu alimvuta kutokea nyuma yake kwa nguvu na kumtupa chini. Dayana alianguka vibaya huku akitonesha majeraha kidogo aliyoyapata usiku wa jana.
Kufumba na kufumbua aliona kundi la wanawake nane wakiwa wamesimama mbele yake, nao pia walikuwa ni mateka wa mle bondeni.

"Unajifanya mjanja eti wewe mwanamke, ujue huwa tunakuangalia sana namna unavyojishaua humu bondeni kwamba unahisi wewe ndio mwenye haki kuliko wengine eti..?" Aliongea mmoja kati ya wale wanawake ambaye yeye alivaa chupi pekee, hata sidiria hakuwa nayo matiti yake yote yalikuwa wazi.
Dayana akiwa pale chini hakuelewa ni kosa gani hasa amewatendea wanawake hao ambao ni wazi walikuwa na hasira kali dhidi yake.
David pia alibaki katika hali ya kuduwaa asielewe ni nini kinaendelea. Alitulia pale pale chini akishuhudia vita hiyo ya wanawake huku akiwaza nini afanye kumsaidia Dayana. Ukweli hakuwa na nguvu za kupambana na wale wanawake wote.

"Shida nini jamani mbona siwaelewi..?" Aliuliza Dayana.

"Shida nini inamaana hujui? Hiyo nguo uliyovaa ni ya kwako? Eti we kahaba? Hiyo taiti ni yako nakuuliza? Kwa hiyo wewe unatuibia nguo zetu alafu sisi tubaki uchi si ndio...!? unaona raha wenzio viungo vyetu vya mwili vikiwa wazi kama hivi ila wewe vya kwako vinathamani sana ndio maana unachukua nguo zetu... Sasa leo tutakuonyesha, tunakuacha uchi mshezi mmoja wewe..." Alisema yule mwanamke kwa sauti ya juu akipayuka kisha akapiga hatua kumfuata Dayana pale chini, wenzake nao wakamfuata nyuma.

"Nyieeeeh..." Mara David aliita kwa sauti kubwa akiwa bado amekaa pale chini.
Wale wanawake wakasitisha kufanya kile walichokusudia kufanya wakageuka kumtazama David.
Ajabu David hakuwa hata anajali, alikuwa akitafuna keki na kisha akanywa juisi.

"Yani asithubutu mtu yeyote kumgusa huyo mwanamke hapo chini. Kama unajipenda ondoka mwenyewe taratibu kabla sijainuka hapa. Nikisimama na wewe ukawepo, kitakacho kupata utamsimulia kila mtu anaeingia kwenye hili bonde" David alitoa mkwara mzito.

Wale wanawake waliogopa licha ya kwamba David hakuwa mtu wa kutishika kiivo lakini maneno yake yalikuwa ni mazito mno, taratibu walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine huku wakisonya, mwisho wakaondoka wote.

Dayana alisimama taratibu akajifuta vumbi. Akamtazama David, akaona yuko bize na keki zake. Dayana akatabasamu na kumuuliza swali...

"Kwa hiyo ungewafanya nini, kama wangesogea kunipiga?"

"Waambie warudi uone ningefanya nini"
Alijibu David kisha wote wakacheka kwa nguvu.

"Dah! Huyu Zungu kanipoza kweli, kumbe aliiba nguo ya watu" Alisema Dayana.

Mara ghafula walisikia sauti kubwa ikitokea kwenye vipaza sauti vilivyofungwa juu kabisa ya jengo hilo.

"Tafadhali tunaomba msogee karibu mkuu anataka kuzungumza na ninyi...." Ilisikika sauti ya mtu mmoja akiongea kupitia kipaza sauti.

Taratibu wale mateka walisimama wakawa wanasogea upande ule alipo yule mtu anayezungumza.
Haukupita muda wakamuona Mzee mmoja mweusi mwenye nywele ndefu nyeupe zinazofika mabegani mwake. Alikuwa amefuga ndevu nyingi nyeupe pia. Pembeni yake aliongozana na wanawake wanne waliobeba visahani vinavyotoa moshi. Huku nyuma alikuwa na walinzi zaidi ya watano, huyu alikuwa si mwingine bali Magnus mwenyewe.

"Ni yeye! Huyu ndiyo Magnus" Dayana aliongea kwa sauti ya chini akimwambia David aliyesimama pembeni yake.

Kwa mara ya kwanza David anamtia machoni Magnus ambaye kwa mujibu wa maelezo ya Bi Noha kule ISRA ataingia kwenye vita kubwa na mtu huyu hapo baadae. David alitumia zaidi ya sekunde 120 pasipo kupepesa macho akawa ameinua uso wake juu na kukaza macho kumtazama Magnus.

"Kwa hiyo huyu ndiyo kiongozi wa hili eneo, yeye ndiye ametuteka na kutuleta hapa?"

"Yes! Ndiyo huyu" Alijibu Dayana, akageuka na kumtazama David akaona jinsi alivyokunja sura yake kwa hasira huku mishipa ya shingo ikiwa imemsimama.

"Usijaribu kufanya ujinga wowote David utapigwa risasi utakufa na habari yako itaishia hapa" Dayana alimtahadharisha David baada ya kuona hayupo sawa hata kidogo.

Magnus alisogea hadi kwenye ukingo wa bonde lile, akasimama na kutanua mikono yake kama mtu anayetaka kupaa kisha akapaza sauti na kusema.

"Habari za mchana huu Funguo zanguu...."
Akiwa amevaa kinasa sauti Magnus alisikika vizuri kupitia vile vipaza sauti na kusikika kwenye masikio ya mateka wake wote waliokuwa bondeni lakini hakuna hata mmoja aliyeitikia salama hiyo. Kila mmoja akionekana kumchukia Magnus.

"Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu, Ndiyo maana nimetoa ofa na bila shaka mmefurahia chakula cha leo. Nimekuja hapa kutoa ofa nyingine ya ninyi kuuliza maswali, nitawajibu kwa usahihi bila shida yoyote karibuni, mwenye swali anyooshe mkono" Alisema Magnus.

Minong'ono ya hapa na pale ilisikika mle bondeni kila mmoja akiogopa kuuliza swali. Magnus alitisha, alitisha mno. Lakini baada ya muda kidogo kuna mmoja akajitoa ufahamu na kunyoosha mkono.

Wakati haya yakiendelea Femi, Zucc pamoja na wanafunzi wengine wa Magnus walikuwa wakichungulia kupitia dirishani juu ya ghorofa moja kubwa kisiwani hapo.

"Eeh! Karibu mama" Magnus alimkaribisha yule aliyenyoosha mkono.
Yule mama akaanza kuongea kwa sauti yenye lafudhi ya kisukuma.

"Sisi tunataka kujua kwa nini tuko hapa? Kwa nini mmetuteka na kutuleta humu? Kwa nini unatwita funguo? Kwa nini umetuweka humu bila nguo? Ni lini tutabaki huru na kurudi makwetu, tunaomba utuweke wazi kama tunafia humu useme kama utatuacha useme, sisi ni wakazi gani kwako!?" Aliuliza yule mama msukuma. Hapo minong'ono ikaanza tena kwa mara nyingine huku wengi wakiunga mkono swali hilo la msingi kwa Magnus.

Wakati Magnus akijiandaa kujibu mara alimuona mfanyakazi wake mmoja wa karibu sana akija pale alipo. Kwa namna alivyokuwa anapiga hatua ndefu ndefu kusogea Magnus akajua wazi kuna taarifa isiyo njema inaletwa. Alichokifanya kwanza akazima kile kinasa sauti kisha akawa tayari kumsikiliza mtu wake ambaye mara baada ya kufika akamnong'oneza.

"Bosi kuna tatizo tena tatizo kubwa, nimepewa taarifa na shushushu wetu kutoka ofisi za usalama wa Taifa kuwa wanampango wa kumkamata Felix mara tu Ndege aliyopanda itakapotua kesho asubuhi..."
Magnus alitoa macho mara baada ya kuipokea taarifa hiyo, kisha akaikunja sura yake mithiri ya mtu aliyeramba limao.

Je, nini kitafuata?
Magnus atakubali Mwanae Felix akamatwe?
Vipi kuhusu Tesha atachukua hatua gani baada ya kujua Felix anakuja Tanzania?
Nini kinaendelea kule ISRA?

makorere Queen Kan JAGGER JR Trimmer
 
Simulizi za SAUL DAVID zilizopo sokoni

[emoji117] STAY WITH ME (Baki na mimi).

[emoji117] FROM ISRA TO ISRA

[emoji117] MODERN WAR(Vita ya kisasa)
 
Asante mkuu, nasubiri muendelezo
 
FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya............28
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Bosi kuna tatizo tena tatizo kubwa, nimepewa taarifa na shushushu wetu kutoka ofisi za usalama wa Taifa kuwa wanampango wa kumkamata Felix mara tu Ndege aliyopanda itakapotua kesho asubuhi..."
Magnus alitoa macho mara baada ya kuipokea taarifa hiyo, kisha akaikunja sura yake mithiri ya mtu aliyeramba limao.

SASA ENDELEA...
Magnus alihisi kuchanganyikiwa, hakuwa na nguvu tena za kuendelea kuzungumza na mateka wake, akageuka haraka na kuondoka, wale wanawake pembeni yake,walinzi na yule msaidizi wake wa kazi wakamfuata nyuma.

"Mkuu atajibu maswali yenu kwa wakati mwingine, kwa sasa amepata dharula ndogo" Alisema yule mtangazaji ambaye awali ndio aliwaambia mateka wale wasogee.

Dayana, David pamoja na mateka wengine walirudi kwenye nafasi zao huku baadhi yao wakilalamika. Maswali aliyouliza yule mama msukuma yalikuwa ya muhimu mno. Kila mmoja alitamani kujua kwa nini ametekwa? Kwanini yuko ndani ya bonde lile? Nini hatima yake?. Lakini kwa bahati mbaya mambo yanaingiliana na kumfanya Magnus kushindwa kujibu maswali hayo.

Wakati huo mvua ilianza kunyesha, mateka hawakuwa na mahali pa kujificha zaidi ya kujibana kwenye kuta za bonde hilo. Hii ndiyo ilikuwa hali halisi ya maisha ya mateka wale mle bondeni. Mvua na jua vyote vilikuwa vyao.

"Felix ameanza safari saa ngapi kutoka Marekani?" Aliuliza Magnus wakati akipiga hatua kuingia ndani ya jengo moja kubwa.

"Kaanza safari leo saa kumi na moja alfajiri ambayo ni sawa na saa sita mchana huku kwetu" Alijibu yule msaidizi wake.

Baada ya kuingia ndani Magnus alikaa juu ya kiti chake kilichotengenezwa mithiri ya viti wanavyokaa wafalme.

"Katika vitu sipendi ni kapambana na Binadamu. Sipendi na sitaki, bado nini safari ndefu. Nahangaika usiku na mchana kutafuta namna ya kurudi ISRA alafu kirahisi tu mtu anafanya uzembe kunivurugia mipango yangu. Hebu kwanza niambie imekuwaje hadi Felix anatafutwa na polisi?"

"Mkuu kama utakumbuka miaka kadhaa iliyopita ulikuwa ukimfundisha Felix kuwa jasiri. Alikuwa akitoka mara kwa mara kwenda kuwaleta mateka kwa bahati mbaya alirekodiwa na kamera za CCTV" Yule msaidizi alieleza kwa ufupi.

"Ona, ni upuuzi mtupu. Inakuwaje arekodiwe na kamera? Hakuvaa helmet?. Mtoto mjinga sana huyu kwanza alivunja utaratibu akaanza kutafuta wanawake, akawa na mahusiano sijui na nani yule wanamwita, kile kisichana kinaitwa nani...!!"

"Tesha"

"Eeh! Huyu Tesa sijui Tesha. Bado najiuliza hizo kamera zilimnasa vipi, na mbona nizamani sana kwa nini iwe sasa?"

"Alivaa, lakini aliivua kabla ya kuingia ndani ya gari. Askari walianza kumtafuta kwa siri tangu kipindi hicho. Hadi leo ndio wamefanikiwa kujua alipo kwa bahati nzuri shushushu wetu akapata taarifa pia"

"Shezi kabisa, Naomba waite MG Family sasa hivi wambie nawahitaji" Magnus alitoa agizo

"Sawa napiga simu sasa hivi"

"Waambie wafanye haraka"

"Sawa mkuu".
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili hospitali kule alipo Tesha na Mama yake David.
Tesha alionyesha kuchanganyikiwa mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mina kuwa yupo pamoja na Kipenzi chake Felix ndani ya Ndege moja inayotoka nchini Marekani kuja Tanzania.

"Mwanangu nini shida? Uko sawa kweli?" Mama David alirudia tena swali lake.

"Ukweli siko sawa mama" Alijibu Tesha.

"Nini tatizo mwanangu?"

"Nitakweleza mama" Alijibu Tesha akihangaika kupiga simu kwa kaka yake Godfrey, simu iliita mara kadhaa ikapokelewa.

"Nambie Tesha, uko home?" Sauti ya Godfrey Ilisikika simuni akiuliza swali

"Sikia kaka nina shida kubwa hapa"

"Shida gani?"

"Ni kuhusu Felix...!"

"Ooh! Ushaanza na huyo Felix wako, haya kimetokea nini"

"Nitakweleza, kwa sasa naomba unisaidie kitu kimoja wasiliana na yule dada wa airport mulize ni ndege gani imeondoka majira ya saa sita kutoka Marekani, inakuja moja kwa moja Tanzania. Mulize pia itafika saa ngapi?"

"Dada gani huyo unamuongelea?"

"Si yule mpenzi wako anafanya kazi airport kaka jamani"

"Unaamanisha Khadija, mbona nilishaachana naye mda sana"

"Sasa kaka si unamuliza tu jamani kwani akiwa X wako tayari ni adui"

"Aah! Usirahisishe basi huwezi kujua mazingira gani tuliachana, anyway dakika kumi nakupa jibu"

"Kumi?"

"Eh! Tano basi" Alijibu Godfrey akakata simu.

Wakati huo pale walipo aliwafuata nesi mmoja akampa taarifa mama David kuwa daktari anataka kumuona.
Baadae alipewa ruhusu ya kutoka hospitali huku Tesha akiwa ndio msimamizi wa kila kitu. Tesha alikuwa anasubiri simu kwa hamu kutoka kwa kaka yake Godfrey, lakini hadi dakika 10 zinakwisha bado alikuwa hajampigia.

"Lakini mwanangu kwani David yeye yuko wapi?" Hatimae mama David aliuliza swali wakati wanatoka hospitali.

Tesha aliwaza haraka haraka amjibu nini, ilikuwa sio rahisi kumwambia moja kwa moja kuwa David ametekwa na watu wasiojulikana siku ya jana. Isitoshe hata polisi nao walifanya siri.

"Aah! David kuna kazi nimempatia Mama, amesafiri ameenda nje ya Dar, usijali nitakupeleka mwenyewe hadi nyumbani kwako" Tesha alidanganya.
Waliingia ndani ya gari la Tesha yeye pamoja na mdogo wake David yaani Tatu, safari kuelekea nyumbani kwa mama David ikaanza. Wakati huo Tesha alikuwa akiitazama simu yake mara kwa mara kuangalia kama kaka yake kamtumia hata ujumbe wa maandishi lakini bado Godfrey alikuwa kimya.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili ndani ya lile bonde, Dayana na David walionekana wamekaa na kujikunyata ukutani, wakati huo mvua ilipungua na sasa yalibaki manyunyu pekee ingawa baridi ilikuwa ni kali mno eneo hilo.

David alionekana kuwa na mawazo sana, aligeuka pembeni yake akamtazama Dayana akamuona anatetemeka mno kutoka na baridi kali.
David alimuonea huruma mno. Akamsogelea karibu kisha akazunguusha mkono wake nyuma ya mgongo wa Dayana akamlaza kifuani pake. Aliweza kuuhisi mwili wa Dayana namna ulivyokuwa ukitetemeka.
Kimya kilitawala kwa muda, mwisho Dayana akauvunja ukimya huo.

"Unawaza nini David? haupo sawa kabisa"

"Nawezaje kuwa sawa Dayana..."

"Ni sahihi lakini kuna wakati lazima ukubali matokeo"

"Sio kwamba sijakubali Dayana, lakini siwezi kuvumilia kuendelea kuwepo hapa. Siwezi kabisa, nakuapia sito maliza wiki humu ndani" Alisema David akimaanisha, Dayana akatabasamu huku akijiweka vizuri kwenye kifua cha David.

"Unajua nini Davi..."

"Nambie..."

"Sahau"

"Nisahau nini?"

"Namaanisha sahau kutoka humu huwezi David, na ukitaka kulazimisha sana utaishia kupoteza maisha. Naomba usifanye hivyo tafadhali sitaki nikupoteze na wewe" Alisema Dayana.

"Kwani nini cha ajabu cha kunizuia kutoka Dayana, kila tatizo lina ufumbuzi wake. Umemuona hata huyo mnaemwita Magnus anamapungufu kibao ndio maana ameondoka ghafula bila kusema kitu, inamaanisha hata yeye mnaemuona Mungu mtu kuna mambo yake hayaendi sawa, na nikwambie kitu Dayana... Ukitaka kumshinda adui yako tafuta udhaifu wake. Magnus anao udhaifu lazima anao" Alieleza David.

"Sasa huo udhaifu wa Magnus wewe utaujuaje, sikia David. Hata ukifanikiwa kutoka kwenye hili bonde bado huko nje tumezunguukwa na msitu wenye walinzi kibao hadi ufike ufukweni, na bado hata ukifika ufukweni utapata wapi usafiri wa majini kukutoa kwenye hichi kisiwa. David futa hilo wazo"

"Siwezi kufuta Dayana, mimi sio kama ninyi mnaokaa hapa na kusubiri miujiza ya Mwenyezi Mungu, hata maandiko yanasema jisaidie na mimi nitakusaidia" Alisema David.

Mara wote walishtushwa na sauti ya Zungu akifoka.

"Inamaana ninyi mmekaa mmekumbatiana hapo mmeacha kuni zimelowana tutaota moto gani usiku.."

Dayana na David walikurupuka na kugeuka.

"Kwa hiyo tungefanyaje sasa, tuzikumbatie hizo kuni zisilowane?" Dayana alijibu swali kwa swali. Wakawa wanatazamana na Zungu kwa macho makali yaliyojaa hasira lakini hawakuweza kustahimiri mwisho wote wakaangua kicheko.
Zungu alikimbia akitaka kumvaa Dayana, Dayana naye akainuka haraka na kuanza kukimbia. Wakaanza kukimbizana huku wakicheka kwa furaha, hawakujali tena yale manyunyu ya mvua.

Dayana hakufika mbali akateleza na kuanguka chini kwenye tope, Zungu alimfikia na kulala juu yake.

"Wewe ni wakunikazia macho mimi!!" Alisema Zungu huku akicheka.

"Sasa kama unauliza maswali ya hovyo nifanyaje" Dayana alijibu huku naye akicheka.

Sasa wote wakawa wamelala chali na kutazama juu angani huku wakionekana kuwa na furaha moyoni.
David aliwatazama naye akajikuta anatabasamu. Si David tu hata mateka wengine waliowaona Dayana na Zungu walijikuta wakitabasamu pia. Tabasamu lenye uchungu ndani yake.
Licha ya kuwa kwenye mazingira magumu lakini bado waliitafuta furaha na kuipa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Haukupita muda mara walisikia muungurumo wa helikopta iliyokuwa angani ikiwasili kisiwani hapo.
Naam, walikuwa ni GM Family wakiwasili.

Je nini kitafuata?

GM Family ni watu gani?
Harakati za kumkamata Felix zinakwendaje?
Magnus na GM Family watafanya nini?

ITAENDELEA...
 
FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya............29
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Haukupita muda mara walisikia muungurumo wa helikopta iliyokuwa angani ikiwasili kisiwani hapo.
Naam, walikuwa ni MG Family wakiwasili.

SASA ENDELEA...
Mwisho helikopta hiyo ilitua na kugusa ardhi katika kisiwa cha Magnus. Watu wanne walionekana wakishuka mmoja baada ya mwingi. Wanaume watatu na mwanamke mmoja.
Wanaume hawa walivalia suti nadhifu za bei ghali zenye rangi nyeusi na tai nyekundu. Yule wa kike yeye alivaa baibui la njano hijabu nyekundu na miwani mikubwa ya jua. Walishuka na kuanza kutembea kwa madaha wakiingia ndani ya jumba kuu la Magnus kisiwani hapo. Hawa ndio GM Family wenyewe majina yao waliitwa Kareem, Noel, Yuda na Madam Husnata.

IKO HIVI...
Ni miaka mingi imepita tangu siku Magnus alivyofukuzwa na kutupwa nje ya ISRA. Magnus hakutaka kukubali kushindwa aliendelea kupambana kujipanga upya kuhakikisha anarudi ISRA kwa mara nyingine kuendelea pale alipoishia.
Akiwa nje ya ISRA Magnus aliyaanza upya maisha yake, mambo mengi yanatokea hapa katikati na baada ya kipindi kirefu kupita Magnus anaibuka tena akiwa ni mtu mkubwa anayeishi katika kisiwa kimoja mbali na makazi ya wanadamu. Akiwa huko anaendelea jitihada zake akiamini ipo siku lazima atarudi tena ISRA, wala hakujali kuhusu umri wake ambao tayari ulikuwa umemtupa mkono mno.

Moja kati ya mafanikio makubwa aliyoyapata Magnus katika kipindi chote akiwa nje ya ISRA ni kuunda kundi moja kubwa la kigaidi tena lenye nguvu ambalo alilibatiza jina akaliita MG Family yaani familia ya Magnus, MG ikiwa ni kifupisho cha jina lake.

Kwa msaada mkubwa wa Magnus MG Family ikawa ni mtandao mkubwa na maarufu wa kigaidi Afrika mashariki na hata Afrika kwa ujumla. Ukiacha Boko haram ya Nigeria, Al-Shabab ya Somalia, Ansar-al-sharia ya Tunisia MG Family nayo ikawa ni moja ya kundi tishio la kigaidi nchini likajipatia umaarufu ingawa si kwa ukubwa sana.

Hakuna jambo gumu lililopita kwenye mikono ya MG Family likashindwa kupatiwa ufumbuzi. Walikuwa wamejikamilisha kwa kila idara. si kiuchumi wala si kisiasa kote walikuwa vizuri mno. Tayari walishaingiza mikono yao na kuwashika masikio hadi baadhi ya viongozi wakubwa serikalini. Tofauti na makundi mengine ya kigaidi, MG Family wao walifanya matukio yale tu ambayo yanafaida au ni agizo la kiongozi wao mkubwa yaani Magnus. Mfano wale watu wanaovaa helmet zenye vioo vya rangi nyekundu wanaofanya kazi ya kuwateka watu na kuwapeleka katika kisiwa cha Magnus walikuwa wapo chini ya mtandao huo wa MG Family. Ni mara chache sana MG Family walifanya vitu tofauti, na walifanya kwa siri bila Magnus mwenyewe kujua. Katu hakuwaruhusu kuanza kujihusisha na mambo ya kisiasa kama ilivyo ada kwa makundi mengi ya kigaidi.

Jambo ambalo liliendelea kuwa siri na hakuna aliyejua ni kuhusu kiongozi mkuu wa kundi hilo la kigaidi yaani Magnus mwenyewe.
Hawakujua Magnus ni nani anaishi wapi anafanya nini. Siku zote watu waliokuwa chini ya mtandao wa MG Family waliamini viongozi wakubwa ni watu wanne waliokuwa wakiratibu kila kinachoendelea yaani Kareem, Noel, Yuda na Madam Husnata. Hawa walikuwa ni viongozi wakubwa waliowekwa na Magnus, lakini wengi waliamini hawa ndio wamiliki wakuu wa mtandao wa kigaidi MG Family.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Baada ya helikopta kutuwa Kareem, Noel, Yuda na Madam Husnata walishuka na kuanza kutembea kwa madaha kuingia ndani ya jumba kuu la Magnus kisiwani hapo.

Walimkuta Magnus amekaa kwenye kiti chake cha heshima akiwasubiri kwa hamu.
Walisimama mbele yake na kuinamisha vichwa vyao kwa heshima kubwa. Magnus aliwatazama kwa zamu mmoja baada ya mwingine kisha akaongea.

"Nafikiri kila mmoja anataarifa ya kile kinachoendelea wakati huu, nataka kujua wakati mwanangu anaingia kwenye vitabu vya polisi wapelelezi na kuanza kutafutwa ninyi mlikuwa wapi?" Hili lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa Magnus.

Kimya kilitawala kila mmoja akimtegea mwenzake ajibu, walimuogopa mno Magnus.

"Mkuu, ukweli hatukujua lolote na hata watu wetu hawamfahamu Felix kama...." Noel alijitoa muhanga na kujibu

"Hamkujua lolote?" Magnus alifoka na kusimama. Kareem, Yuda, Noel na Husnata wote wakapiga magoti na kuinamisha vichwa vyao chini, hawakutakiwa kusimama pindi ambapo mkubwa wao Magnus amesimama.

Magnus aliwatazama tena kwa zamu akionekana kuwa na hasira sana.

"Niangalieni" alitoa amri. Wote wakatii na kuinua nyuso zao.

"Mwanangu anafika Tanzania kesho asubuhi, sitaki aguswe hata unywele wake. Sitaki awe na kesi ya aina yoyote, aachwe huru na asifuatiliwe tena"

"Sawa mkuuu.." Waliitikia kwa pamoja.

"Sitovumilia uzembe wa aina yoyote utakao jitokeza" Magnus alisisitiza.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Dakika tano baadae vigogo wa MG Family walitoka nje ya jumba la Magnus, kila mmoja akionekana kuwa bize na simu yake, tayari taratibu za kutimiza jukumu walilopewa zilianza papo hapo.
Mwisho waliingia ndani ya helikopta na baadae helikopta hiyo ikaacha ardhi na kupaa angani.
[emoji294][emoji294][emoji294]

David, Zungu na Dayana wakiwa bondeni waliisindikiza helikopta hiyo kwa macho hadi pale ilipopotelea juu mawinguni.

"Next time hii helikopta ndiyo itakayotubeba na kututoa hapa" Aliongea David. Dayana na Zungu wakageuka kwa pamoja kumtazama.

"Unaota au?" Aliuliza Dayana.

"Nimepata wazo" Alisema David

"Kabla hujatuambia hilo wazo lako kuna kitu nataka kuwaeleza" Zungu alidakia.

"Nini?" David na Dayana wakauliza kwa pamoja.

"Nimepata njia ya kutoka hapa moja kwa moja hadi ufukweni mwa bahari"

"Nini? Acha masihara Zungu" Alisema Dayana

"Unamaanisha kweli jamaangu?" David naye kaongeza swali. Zungu alitikisa kichwa akiashiria kumaanisha kile alichokisema kisha kaongea...

"Wakati mvua imeanza kunyesha mimi nilitoka hapa, kawaida kukiwa na mvua walinzi huwa wanatoka na kukaa kwenye vibanda vyao hivyo niliweza kupenya vikwazo vyao vyote kwa urahisi, kwa bahati nzuri leo nimefanikiwa kuona njia ya pango linalopita chini kwa chini na kutokea kwenye ile barabara iliyopita mlimani chini ya ardhi"

"Unamaanishe ile barabara tuliyopita wakati tunaletwa hapa"

"Ndiyo David" Zungu aliitika.

Zilikuwa ni habari njema mno kwa wote watatu, mwisho walikaa na kukubaliana usiku watoke kwa mara nyingine kwenda kuhakiki njia hiyo.
Taratibu matumaini ya kutoka kwenye mateso hayo yalianza kujionyesha japo si kwa asilimia kubwa sana.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili...
Dakika 17 pekee baada ya kutoka hospitali zilitosha kabisa kufika nyumbani kwa Mama David. Nyumba ilikuwa imejitenga peke yake maeneo ya uswahilini hatua kama 50 kutoka barabarani. Ilikuwa ni nyumba ya kawaida yenye bati lililochakaa.

"Asante mwanangu, tutashuka tu hapa hapa haina shida..." Alisema Mama David huku akimuomba Tesha amsaidie kufungua mlango wa gari.

Kwa sababu Tesha naye alikuwa na haraka hakutaka kubishana na Mama David aliona ni heri ashukie hapo ili yeye na dereva wake warudi haraka mjini aendelee kufuatilia habari za Ndege aliyopanda mpenzi wake Felix kutoka Marekani.

"Usijali mama, muhimu nimepajua nyumbani nitakuwa nakuja mara kwa mara kukutembelea. Naomba usisahau maelezo ya daktari mama yangu, punguza mawazo, kula chakula kwa wakati na usiache kutumia dawa pia"

"Nashukuru sana mwanangu. Kwa hiyo David atarudi lini?" Aliuliza Mama David mara baada ya kushuka garini pamoja na mwanae tatu.

"David mmm! Nafikiri baada ya siku nne hivi atakuwa amekamilisha kazi yake, ila tutawasiliana kama kukiwa na mabadiliko nitakwambia" Tesha alidanganya mwisho wakaagana na mama David. Lakini kabla Dereva hajaondosha gari Tesha alitupa macho kwa mara nyingine kutazama nyumbani kwa mama David akaona gari tatu za kifahari aina ya Benz-Mercedes zikiwa zimepaki nje ya nyumba hiyo tena zote zilikuwa nyeusi zinafanana.
Hali hii ilimshangaza sana Tesha lakini kwa kuwa alikuwa na haraka hakutaka kulizingatia sana hilo, akamtaka Dereva aondoshe gari, wakaondoka.

Si kwamba hali hiyo ilimshangaza Tesha pekee, hata Mama David naye alibaki kinywa wazi mara baada ya kuziona gari hizo nyumbani kwake. Haikuwa kawaida na vilevile haikuwahi kutokea tangu ahamie kwenye nyumba. Alijipa moyo akawa anapiga hatua kusogea, mkono wake wa kulia alishika mkoba wake mkubwa na mkono wa kushoto alimshika mwanae tatu.
Akiwa amebakiza hatua kama kumi kufika nyumbani kwake mara ghafula mlango wa gari moja ulifunguliwa akashuka mwanaume wa miraba minne aliyepigilia suti nadhifu nyeusi. Mwanaume huyo alisogea nyuma akafungua mlango wa gari kwa heshima kubwa mara akashuka mwanamke mmoja maji ya kunde, mrefu na mnene kiasi. Alivaa baibui la njano hijabu nyekundu na miwani mikubwa ya jua.
Huyu alikuwa ni Madam Husnata kigogo mmoja wapo kutoka kundi la MG Family linalomilikiwa na Magnus.
Ndiyo ni Madam Husnata yule yule ambaye muda mfupi uliopita alikuwa katika kisiwa cha Magnus akiwa na wenzake Kareem Noel na Yuda.

Kwa nini mwanamke huyu yupo nyumbani kwa mama David? Kuna mahusiano gani? Kafuata nini? Kivipi?

Haya ni maswali ambayo hata mimi mtunzi wako yananiacha kinywa wazi.

Usijali majibu ya maswali haya utayapata kwenye mfululizo wa episode zinazofuata KAA MKAO.

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
Back
Top Bottom