RIWAYA: Hukumu Nzito

RIWAYA: Hukumu Nzito

McCollum

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2023
Posts
384
Reaction score
684
SIMULIZI: HUKUMU NZITO
GENRE: THRILLER
MWANDISHI: YI BANG JI

“Nataka tuimalize kazi kwa haraka,” aliongea Julius Fungo, huyu alikuwa kiongozi wa kikundi
cha majambazi ambao walikuwa wakifanya matukio mazito ya uhalifu jijini Mbeya, kwa muda
huu alikuwa akitweta na alikuwa analisogelea dirisha la nyumba ambayo walikuwamo ndani.

Yalikuwa majira ya usiku lakini ndani ya chumba walichokuwamo yeye na wenzake kilikuwa na
taa ya chemli pekee.

Taa hii iliwekwa juu ya meza, meza ya mbao ambayo ilisogezwa karibu na kiti cha chuma ambacho kilitumika kumfungia kijana mdogo ambaye alikuwa ametekwa na kundi la Julius Fungo, kijana aliyetekwa alifungwa kitambaa kilichozunguka mpaka nyuma ya kichwa chake na kupita sehemu ya mdomo kwa kujaa na kuziba nafasi kiasi cha kutoruhusu meno kuonekana.

Mikono ya kijana ilifungwa sehemu ya nyuma na ilitengeneza umbo V kwani ilifungwa kwenye sehemu ya viganda kwa kutumia kamba ngumu, miguuni kamba nzitoilitumika kufunga mguu mmoja mmoja kwenye vyuma viwili ambavyo vilikuwa kama miguu ya kiti.

“Bado hautaki kuongea?,” aliuliza Daniel ambaye mara nyingi alifahamika kwa jina la Dan, huyu alikuwa mnyama, katili na mara nyingi ndiye aliyekuwa akiwaua watu ambao walitakiwa kuuawa baada ya kuona umuhimu wa hao watu haupo, baada ya kuuliza swali hilo alitoweka mahali hapo na baada ya dakika chache alirejea akiwa na chuma chembamba mithili ya fimbo, chuma hiki kilikuwa kina ncha kali, baada ya kukiweka kile chuma sakafuni alimfuata Julius na kuteta naye jambo fulani.

“Deal naye, ikishindikana muue” hili ndilo lililokuwa jibu la mwisho la Julius ambaye baada yahapo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokea sehemu ya sebule ya nyumba hiyo na baada ya kupapasa ukuta kwa muda hatimaye aliifikia swichi na kuwasha taa, baada ya hapo aliiwasha televisheni ambayo ilikuwa imewekwa sehemu ya ukutani.

“I say don’t worry about a thing..
Don’t worry about a thing...”

Huu ulikuwa wimbo wa Bob Marley uliokuwa ukisikika kupitia spika kubwa zilizowekwa chini ya televisheni ile, muda huu Julius alikuwa akivuta sigara na kuubana mdomo wake alipokuwa akiutoa moshi ambao ulinyoka kama mstari uliochorwa na rula.

“Atasema tu..” kabla Julius hajamalizia kauli yake simu yake ndogo aina ya Nokia kitochi iliunguruma kwa sekunde kadhaa na akaipokea baada ya kugundua alikuwa akipigiwa simu na bosi aliyemtuma kumkamata yule kijana.

“Kazi inaendeleaje? Huyo kijana ameongea jambo lolote?” Bosi yule aliuliza maswali mawili kwa mfululizo bila kuruhusu kupoteza muda kwa kuanza na salamu, kwa muda huo salamuhazikuwa na maana yoyote
“Tupo nae, tutakupa mrejesho ndani ya nusu saa” alijibu Julius kwa sauti ya kikakamavu kamakomando wa vita aliyekuwa akiongea na mkuu wake wa kazi, muda huu Julius alikuwa akijua kwamba kama angeongea hovyo hovyo basi hasingeweza kupata kazi yoyote kutoka kwa huyo aliyempigia ambaye yeye alimsevu kwa jina la Bosi Kidevu.

“Ataongea saa ngapi? Mbona mnaongea naye kama ndugu yenu shida ni nini?” aliuliza yule bosi kwa jazba na kukata simu. Julius alijua majibu yalihitajika ndani ya muda mchache na hakuwa tayari kupoteza sifa zake kutoka kwa bosi wake huyo.

“Huyu mjinga anacheza na mimi, nitamuonesha maana ya maumivu” aliongea Julius kwa hasira akiwa anayasugua meno yake ya juu kwa kutumia yale ya chini, muda huu hata uso wake ule ambao punde ulikuwa ukifurahia sigara uligeuka na kujaa mikunjo juu ya ngozi iliyo juu yamacho yake, hata mapigo ya moyo ya Julius yaligeuka alijikuta akiwa anapumua kama duma ambaye alikuwa akikimbia kulifuata windo lake kwenye pori.

“Sogea, nitaendelea naye” aliongea Julius akiwa anaufungua mlango wa kile chumba alichomuacha Daniel na vijana wengine wawili. Baada ya hapo aliifuata swichi na kuiwasha, chumba kile kikatawala mwanga mkali ambao ulikuwa ukimmulika yule kijana ambaye alifungwa kwenye kiti.

“Naomba hilo begi” aliamuru Julius na baada ya sekunde kadhaa begi moja jekundu lililetwa sehemu ya karibu yake na hapo alilifungua kwa haraka na kutoa vifaa mbalimbali vya chuma.

“Unaitwa John Shayo, ila umegoma kutaja hata jina lako. Umetembea na mke wa mshua na bado haujataka kukubali kuwa ulifanya hivyo. Nimependa ujasiri wako na unafaa kuitwa mwanaume ila si mbele yangu, usithubutu kucheza na mimi utapotea” aliongea Julius na baada ya hapo alikitoa kisu kilichokuwa na makali yaliyochongeka sana, baada ya hapo alikita kile kisu kwenyemguu wa yule kijana na kisu kilitokea mpaka sehemu ya unyayo, muda huu yule kijana alikuwa akijaribu kufurukuta kutoka kwenye kiti kile lakini wala haikusaidia kwani vijana wengine watatu walimshikilia kwa nguvu ili asijitikise na kuharibu “mchakato” wa kumtaka aseme alichokosea.

Kisu kilichomolewa kwenye le mguu na kukitwa kwenye mguu mwingine kwa nguvu, maumivu aliyoyapata yule kijana yalimfanya atoe macho na muda huu machozi yalikuwa yakimtoka na alikuwa akipumua kwa kasi.

“Bado sijaanza, utaongea nikiamua uongee na sio kunisumbua kama ulivyofanya” aliongea Julius ambaye sura yake ilikuwa haina hata chembe ya ubinadamu. Muda huu yule kijana alibanwa vilivyo na alishindwa kujitikisa na kila alipojaribu aliishia kubamizwa vibao vizito ambavyo mara nyingi vilikuwa vinalenga sehemu ya jicho lake la kushoto. Muda huu Julius aliamua kukaa chini ya sakafu na alikuwa akifuta uso wake na mkono na alikuwa akitukana matusi mazito ya nguoni.

“Nataka nikuue ukiwa unashuhudia” aliongea na kukichomoa kile kisu kwenye mguu, muda huu kijana yule hata macho yake yaligeuka rangi nakuwa mekundu kama nyanya ya sokoni iliyokuwa ikisubiri mnumnuzi. Hata Daniel alijua kabisa kwamba kijana yule asingeweza kupona kwani alikuwa akimfahamu Julius kwa muda mrefu na alijua kwamba hasira yake haikuwa ikipoa kwa haraka. Baada ya hapo Julius alitumia kile kile kisu kuchimba sehemu ya ngozi ya mguu katika eneo la paja, damu nzito ilikuwa ikivuja kutoka kwenye lile jeraha ambalo lilisababishwa na Julius.

“Mkuu, tumuache aongee” aliongea Daniel akiwa anamtazama Julius ambaye ndo kwanza alikuwa hana hata muda wa kusikiliza maongezi ya Daniel, kisu kile kile kilitumika kuchimba sehemu ya paja la mguu mwingine wa yule kijana. Wale vijana wengine walijua hapo kazi ilikuwa imeanza na kama wangejaribu kuongea zaidi hata wao kingewatokea kilichomtokea yule kijana.

Julius alimfungua yule kijana kitambaa cha mdomoni na baada ya hapo alitoka ndani ya kile chumba akienda mahali kuchukua kitu fulani, baada ya muda alirejea akiwa na stendi ya kamera ambayo ilikuwa imeungaanishwa na kamera ya kurekodia video. Baada ya muda alirejea akiwa na reflector ya mwanga na taa kubwa ambayo aliielekeza sehemu ya ile reflector.

“Muda huu nataka majibu yaliyonyooka sawa” aliongea Julius kwa sauti nzito zaidi ya zile sauti za waimbaji wa mziki aina ya Country kutokea huko Marekani ya Kaskazini. Julius alikuwa akimtazama yule kijana aliona kabisa adhabu yake ilikuwa haijatosha ila aliona ingekuwa vyema kama angemaliza mahojiano yake kwa haraka.

Muda huu yule kijana alijibu maswali yote kwa ufasaha tena bila kusumbua. Baada ya kupata yale mahojiano aliizima kamera na kumfuata, kijana yule alipatwa na wasiwasi mno, kamwe hakujua kwamba angeweza kufa kifo cha haraka na kikatili kama kile ambacho kilikuwa kinamfuata, ndio! Julius ndiye aliyekuwa kifo mwenyewe na alikuwa akiogofya kwa kila hatua aliyokuwa akiipiga kuusogelea mwili wa yule kijana ambao ulikuwa kwenye maumivu.

“Ungeongea tusingefika hapa” aliongea Julius na muda huu alikitumia kile kisu kukata Paja la kushoto akizungusha kijiduara kidogo na kuikwangua nyama ile kwa nguvu, maumivu yalikuwa makali na hata kijana alipojaribu kulia aliwaiwa na kubanwa mdomo na Daniel. Baada ya hapo Julius alikichukua kile kisu na kumchoma nacho yule kijana sehemu ya tumbo na alikuwa anatoboatoboa kila sehemu ambazo alipata upenyo, damu ilimrukia usoni lakini wala hakujali alichomachoma ule mwili mpaka alipojisikia ametosheka na muda huu yule kijana alikata roho kabisa.

“Dogo njoo hapa, fungua mwili wa huyu dogo na uulaze hapa chini” aliamuru Julius na baada ya hapo alitumia kile kile kisu kuchana sehemu ya tumbo la yule kijana, alitoa utumbo, figo na moyo tena akiwa na mikono mitupu. Vijana waliokuwa na Julius walipatwa na mshangao ambao uliwahakikishia walikuwa wakifanya kazi na mtu wa hatari ambaye alikuwa radhi kufanya chochote.

“Tupa huu mwili kwenye pipa na uuchome kabisa” aliamuru Julius na muda wale vijana watatu waliubeba ule mwili na kuutupa kwenye pipa na baada ya hapo waliuchoma moto. Baada ya kurejea ndani wote wanne walishirikiana kusafisha kile chumba na kilirejea katika usafi isipokuwa roho ya John Shayo ambayo ilibaki ikimtazama Julius kwa kisasi lakini haikuwa na namna ya kumdhuru.

Je, nini kitaendelea?

Itaendelea siku ya Jumatano.
 
Back
Top Bottom