Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 43

Toka ilipogonga saa kumi na
moja za alfajiri,Graca tayari
alikwisha amka na kuanzashughuli za usafi wa nyumba.Siku
hii alikuwa mchangamfu na hata
usoni pake palijaa
tabasamu.Alisafisha nyumba yote
na alipomaliza akaanza kuandaa
kifungua kinywa.Hadi jua
lilipoanza kuchomoza tayari
alikwisha maliza kazi zote akaenda
kuoga.Alitumia zaidi ya saa moja
akiwa katika meza ya Doreen
iliyosheheni vipodozi vya kila
aina.Siku hii ya leo alitaka
aonekane tofauti
“Naamini wote
watakaponiona watashangaa kwa
namna watakavyonikuta asubuhi
ya leo.Mimi ni mzuri sana,ni
maisha yale magumu niliyoyapitia
ndiyo yaliyouficha uzuri
wangu.Kuanzia sasa sitaki tena
kuendelea kuuficha uzuri wangu
kwani hakuna tena sababu ya kufanya hivyo.Niko katika mikono
salama na muda si mrefu
nitayaanza maisha mapya tena
mbali na hapa hivyo ni fursa
kwangu kuishi yale maisha ya
ndoto zangu” akawaza na
kutabasamu alipojitazama namna
alivyopendeza lakini ghafla wazo
moja likamjia
“Sifahamu kama ninafanya
kitu sahihi kutaka kumvutia mume
wa mtu lakini tayari imekwisha
nitokea na sina namna nyingine ya
kufanya.Kikohozi kimenikamata
na muda wowote itanilazimu
kukohoa.Siwezi kuvumilia
zaidi.Ninampenda sana
Elvis.Kiumri mimi na yeye hatuko
sawa yeye ni mkubwa zaidi yangu
lakini hicho si kigezo.Kadiri siku
zinavyozidi kwenda ndivyo
ninavyojikuta nikimpenda zaidi na zaidi na ninaanza kushindwa
kujizuia kuonyesha
ninavyompenda.Elvis ananipenda
na kunijali kama mdogo wake
lakini mimi nataka iwe zaidi ya
hapo.Nataka awe mpenzi wangu.Ni
mwanaume mzuri wa sura na
roho.Ana utu,mkarimu na zaidi ya
yote nitakuwa salama zaidi nikiwa
naye.Katika wanaume wote
duniani ni yeye pekee aliyeweza
kunifuta machozi na kunifanya
nitabasamu tena jambo ambalo
niliamini halitawezekana kamwe
katika maisha yangu.Mtu kama
huyu siwezi kumuacha na
ninaomba asirejeane na mke wake
tena.Nadra sana kuwapata
wanaume wa aina hii katika dunia
ya leo” akawaza Graca
“Nilionja kidogo ladha ya
penzi wakati nilipozama mapenzini na Davis wakati ule
nikiwa mwanafunzi wa kidato cha
tano lakini baba kwa ukatili
alonifanyia alinifanya niwachukie
wanaume wote na niliapa
kutokujihusisha na mwanaume
katika mahusiano yoyote lakini
baada ya kukutana na Elvis mambo
yamebadilika na ghafla nimejikuta
nikimpenda.Ninajifahamu mimi ni
mdhaifu mno nikipenda na pale
ninapozama mapenzini huwa sioni
wala sisikii la mtu.Nimempenda
mume wa mtu lazima nihakikishe
ninampa…….” Graca akatolewa
mwazoni baada ya kusikia mlango
wa mojawapo ya vyumba
ukifunguliwa ikamlazimu kutoka
mle chumbani kwa Doreen.Mtu wa
kwanza kuonana naye alikuwa ni
Dr Philip Graca!! Dr Philip akasema
kwa mshangao huku
akitabasamu.Aliustaajabia uzuri
wa Graca.
“Dr Philip vipi maendeleo ya
Elvis? Akauliza Graca
“Nilimtazama saa kumi za
usiku na alikuwa anaendelea
vyema”
“Naweza kuruhusiwa
kumuona?
“Bila shaka” akasema Dr
Philip wakaongozana kuelekea
katika chumba cha Elvis.Dr Philip
akagonga kidogo mlango na sauti
toka ndani ikamruhusu
aingie.Elvis alikuwa amekwisha
amka amekaa kitandani.Mara tu
Graca na Dr Philip walipoingia
ndani Elvis akabaki mdomo wazi.
“Wow !akasema Elvis huku
akitabasamu Dr Philip ninachokishuhudia
ni kitu cha kweli au bado niko
katika usingizi? Akauliza Elvis
“Hata mimi nilistuka sana
nilipomuona nikaogopa labda
tumetembelewa na kiumbe
mwingine lakini baada ya kusikia
sauti ndipo nikagundua ni Graca”
akasema Dr Philip na kumfanya
Graca aangue kicheko
“Kumbe Tanzania tunao
uwezo wa kuchukua taji la
mrembo wa dunia.Tuna hazina
kubwa ya
warembo.Ninakuhakikishia Graca
ukiamua kushiriki katika
mashindano ya urembo utaondoka
na taji.Huu si uzuri wa
kawaida.Kwa nini siku hizi zote
umekuwa unauficha uzuri huu?
Akauliza Elvis Nimejaribu kujiremba kidogo
leo nione kama nitapendeza”
akasema Graca
“C’mon Graca.hata bila ya
vipodozi wewe bado ni mrembo
sana.Tuachane na hayo vipi hali
zenu?
“Sisi tuko vizuri sijui
wewe.Vipi maendeleo
yako?Unajisikiaje sasa hivi? Dr
Philip akauliza
“kwa ujumla ninaendelea
vizuri sana.Mwili uko vizuri
isipokuwa kuna maumivu
nayasikia katika baadhi ya
sehemu” akasema Elvis na Dr
Philip akaanza kumpima.Wakati
Dr Philip akimpima Elvis ili
kujiridhisha kuhusu maendeleo
yake Graca alikuwa anaandaa
kifungua kinywa.Akiwa jikoni
akahisi kuna mtu mlangoni akageuka na kukutanisha macho
na Steven
“This is unbeliavable!! Is that
you Graca? Akauliza Steven
“Kwani nikoje Steven?
“Nafahamu wewe ni mrembo
lakini sikutegemea kama unaweza
kuwa mrembo kiasi hiki.This is
amazing!! Akasema Steven na
kumkonyeza halafu akaelekea
katika chumba cha Elvis
“Itanilazimu nijiweke mbali
sana na huyu Steven anaonekana
ni mpenda wnawake.Nimeona
namna alivyonikonyeza”akawaza
Graca akiendelea kuandaa
kifungua kinywa.
Meshack Jumbo naye aliwasili
asubuhi ile ili kujua maendeleo ya
Elvis.Uso wake ulijawa tabasamu
pale alipokuta Elvis anaendelea
vyema.Wote walipokuwa tayari wakajumuika mezani kupata
kifungua kinywa.Ilikuwa ni
asubuhi ya furaha sana.Kila moja
alionyesha tabasamu usoni
pake.maongezi yalitawaliwa na
vicheko na utani wa hapa na pale
“Ndugu zangu,napenda
nichukue nafasi hii kuwashukuru
sana kwa namna tulivyoshirikiana
katika shughuli hii nzito na
kuifanikisha kwa ufanisi
mkubwa.Haikuwa rahisi lakini
tumefanikiwa.Baada ya zoezi
kumalizika ninapenda kuwajulisha
kwamba mimi nitalazimika
kuwaacha na kwenda kuendelea
na majukumu mengine na muda
wowote mtakaonihitaji nitafika
kwa haraka sana.Elvis tayari
anaendelea vyema na kazi yangu
nadhani nimeimaliza” akasema Dr Philip na ukimya mfupi ukapita
kisha Meshack akasema
“Binafsi sipati neno zuri la
kukushukuru Dr Philip kwa kazi
kubwa uliyoifanya ila naomba
ufahamu kwamba operesheni hii
haijaishia hapa.Bado inaendelea
na muda wowote unaweza
ukahitajika hivyo ujiweke tayari
muda wowote ukihitajika uitike
kwa haraka”
“Mimi niko tayari mzee muda
wowote” akajibu Dr Philip.
“Elvis utaendelea kupumzika
kwa siku ya leo ili mwili uweze
kurejea katika hali yake ndipo
tuanze kushughulika na
operesheni yetu.Leo shughuli za
msiba zinahitimishwa na
niliombwa nihudhurie hivyo
nikitoka hapa nitakwenda huko
kujua nini kinachoendelea.Hapa nitakuja usiku ili tuweze
kujadiliana namna tutakavyoweza
kuifanikisha operesheni yetu”
akasema Meshack
“Mzee jana kuna kitu
ulinieleza lakini ukasema kwamba
utanieleza kwa kirefu leo”
akasema Steven
“Ouh samahani nilikwisha
sahau.Tutazungumza baada ya
kumaliza kupata kifungua kinywa”
akasema meshack Jumbo
Walipomaliza kupata
kifungua kinywa Dr Philip
akaondoka zake.Elvis,Steven na
Meshack wakaenda kuketi nje
katika sehemu ya kupumzikia na
ndipo Meshack alipowaeleza
kuhusiana na agizo alilopewa na
makamu wa rais la kumuua Pascal
Situmwa Pascal Situmwa?!! Elvis
akashangaa
“Ndiyo”
“Hii inashangaza sana.Pascal
ndiye mshirika mkubwa wa
brigedia Frank na hata katika ile
biashara ya silaha wako
pamoja.Iweje leo Pascal atakiwe
kuuawa? Elvis akahoji
“Sasa nimepata jibu.Nilikuwa
najiuliza sana kuhusiana na hili
jina la Pascal Situmwa kwamba
nimewahi kulisikia wapi? Kumbe
uliwahi kunieleza kwamba ndiye
mshirika wa brigedia Frank.Kama
ni hivyo basi tuna sehemu nzuri ya
kuanzia.Huyu Pascal hatakiwi
kuuawa.Tunapaswa kumteka na
kumuhoji na anaweza akatusaidia
kupata taarifa za kutosha
kuhusiana na mtandao wao.Huyu ni mtu muhimu sana kwetu”
akasema Meshack Jumbo
“Hilo ni wazo zuri mzee.Huyu
Pascal anaweza kuwa ni mtu
muhimu sana kwetu.Tufanye kama
ulivyoshauri.Tumteke na
kumfanyia mahojiano.Kupitia
kwake tunaweza kufahamu
mambo mengi na ya muhimu
yatakayotuwezesha kufanikisha
operesheni yetu ya kuufyeka
mtandao huu wa kuuza silaha”
akasema Elvis.
“Kinachotakiwa ni kupanga
mikakati ya namna ya
kumpata.Nitawaachia zoezi hilo la
kupanga mikakati namna
tutakavyoweza kumpata huyo
Pascal.Hadi usiku wa leo tuwe
tayari tumepata jibu namna
tutakavyoweza kumpata” akasema
Meshack Jumbo kisha akaondoka kuelekea nyumbani kwa mama
yake Elvis kwa ajili ya shughuli za
kuhitimisha msiba
“Nashindwa kuelewa kwa nini
pascal atakiwe kuuawa wakati ni
mwenzao na wanashirikiana wote
katika biashara zao haramu?
Akauliza Elvis
“Elvis jibu la swali hili
tutalipata kama tukifanikiwa
kumpata Pascal tujue ni kwa nini
wanataka kumuua? Kitu cha
msingi kwa sasa ni kutafuta namna
ya kuweza kumpata pascal”
akasema Steven
“Kuna mwanamke mmoja
anaitwa Victoria.Huyu ni kahaba
lakini mwenye utajiri
mkubwa.Amekuwa akitembea na
vigogo wakubwa ambao humlipa
pesa nyingi sana.Anamiliki hoteli
kubwa ya Angel Vicky.Huyu mwanamke anatumiwa na
mtandao wa akina Frank katika
kufanikisha shughuli zao mbali
mbali.Nilipata namba zake za simu
katika kompyuta ya brigedia Frank
na tayari nilianza kumchunguza
ndipo mambo haya
yalipotokea.Tukifanikiwa kumpata
huyu mwanamke anaweza
akatusaidia sana kumpata
Pascal”akasema Elvis
“Tayari nimemfahamu huyo
mwanamke.Jina lake maarufu
anaitwa Vicky Mapenzi.Ni
mwanamke mwenye pesa nyingi
na ana uzuri wa kipekee”
“Dah ! sikuwezi
Steven.Wanawake wote wazuri wa
jiji hili unawafahamu” akasema
Elvis na wote wakacheka Kama ni Vicky tunaweza
kumpata.Kuna mtu anayeweza
kuniunganisha naye”
“Nani huyo anayeweza
kukuunganisha na Vicky?
“Ni Samira”
“Samira? Elvis akashangaa
“Elvis samahani sikuwa
nimekujulisha kwamba juzi
sikulala hapa nilikuwa kwa
Samira.Yule mwanamke sijui
amenipa nini kwani kila dakika
namuwaza hivyo ikanilazimu
kumtafuta”
“Hayo ni mambo yako binafsi
Steven mimi hayanihusu ila
nakuomba uwe mwangalifu sana
kwani ni huyo ndiye aliyekuwepa
katika matatizo”
“Usijali nitakuwa mwangalifu
sana safari hii” Una hakika anaweza
akakuunganisha na Vicky?
Wanafahamiana? Akauliza Elvis
“Sina hakika kama
wanafahamiana lakini Samira ni
mwanamke ambaye hashindwi
kuingia sehemu yoyote.Nikimtaka
aniunganishe na Vicky atafanya
hivyo.Kama tukikubaliana
kwamba Samira aniunganishe na
Vicky tusipoteze muda mimi
nimfuate Samira” akasema
Steven.Elvis akafikiri kidogo na
kusema
“Mpano uwe hivi.Samira
akuunganishe na Vicky kwamba
unamtaka kimapenzi na utamlipa
pesa nyingi na ukifanikiwa
kupanga naye sehemu ya kukutana
utanijulisha ili nami nifike hapo na
Samira atafuata maelekezo yetu na
tutampata Pascal” Elvis !! You are
dead.Hutakiwi kuonekana huko
nje.Ni vipi endapo mtu
anayekufahamu
akikuona?Utaharibu kila
kitu.Isitoshe bado unahitaji
kupumzika”
“Usihofu Steven.Nilikufa kwa
ajili ya operesheni hii sasa kazi
ndo imeanza.Fanya mipango ya
kuonana na Vicky halafu
utanijulisha” akasema Elvis na
Steven hakupoteza muda
akampigia simu Samira na
kumjulisha kwamba anakwenda
kwake ana mazungumzo naye
hivyo asitoke amsubiri
“Lazima ipo sababu kubwa
iliyopelekea itolewe amri ya
kumuua Pascal ambaye ni
mshirika mkubwa sana katika
mtandao huu wa kuuza silaha.Tutaifahamu sababu hiyo
baada ya kumpata Pascal.Vicky
naye ni mtu muhimu sana kwetu
kwani yeye atatusaidia
kumfahamu mtu anayeitwa
Deusdedith m.m ambaye kwa
mujibu wa mawasiliano
niliyoyakuta katika kompyuta ya
Frank ndiye ambaye amekuwa
akitoa maelekezo mbali mbali na
ndiye aliyemuunganisha Frank na
Vicky ambaye alitumwa kwenda
kumuua kanali Norman.Walitaka
nife na sasa nimekufa ila
hawatalala usingizi.Nitahakikisha
ninawafyeka mmoja baada ya
mwingine” akawaza Elvis na
kutolewa mwazoni baada ya Graca
kutokea akiwa na sinia lenye
vinywaji akaweka mezani na
kumpatia Elvis glasi yenye juisi Naweza kuketi hapa?
Akauliza Graca akiomba kuketi
katika kiti kilichokuwa pembeni
ya Elvis
“Usiogope Graca.karibu”
akasema Elvis na Graca akaketi
“Vipi maendeleo yako Graca?
Naona leo umeamka na furaha
kubwa” akasema Elvis.Graca
akatabasamu na vishimo
vikaonekna katika mashavu yake
kisha akajibu
“Ni kweli leo nimeamka na
furaha ya ajabu sana.Yote hii ni
kwa sababu ya mambo yote
kwenda vizuri.Najiona kama mtu
mpya kwani nafahamu mipango
yangu yote inakwenda kufanikiwa
kwa uwepo wako” akasema Graca
na Elvis akatabsamu
“Nina furaha pia kukuona
ukiwa katika hali hii.Nakuona kama Graca mpya.Usihofu kila kitu
nilichokuahidi
nitakutimizia.Mipango inafanyika
hivi sasa ili uelekee nje ya nchi
ukaanze maisha mapya mbali na
hapa”
“Vipi kuhusu
wewe.Unaendeleaje?
“Kama unavyoniona.I’m
ok.Nimekwisha rejea katika hali ya
kawaida”
“Namshukuru sana Mungu
kwani hali niliyokuwa nayo jana ni
yeye tu anayeifahamu.Nilihisi
kama vile sintakuona tena,niliona
kama vile maisha yangu
yanakwenda kufika ukingoni bila
wewe.Kwa ujumla nilikuwa na hali
mbaya na sikuweza kutia kitu
tumboni kwa siku nzima hadi pale
ulipozinduka” Pole sana Graca.Nilifahamu
jambo kama hilo lingetokea lakini
nilikuwa na uhakika mkubwa
kwamba jambo hili litafanikiwa
kwani tayari majaribio yalikwisha
fanyika na tukajiridhisha kwamba
kila kitu kimekwenda sawa”
akasema Elvis na Graca akashusha
pumzi
“Elvis tafadhali usijaribu tena
kufanya kitu kama kile.Ulitupa
wakati mgumu sana sisi watu
tunaokupenda na kukutegemea”
akasema Graca Elvis akatabasamu
“Pole sana.Jambo kama lile
halitajirudia tena.Naomba
nikuweke wazi kwamba haikuwa
rahisi hata kwangu pia lakini
nililazimika kulifanya kwa kuwa
hakuna njia nyingine ya kuweza
kuusafisha mtandao wa baba yakozaidi ya kuwaaminisha kwamba
nimekufa”
“Kwa sasa wanaamini tayari
umekufa.Nini kinafuata?
“Kinachofuata kwa sasa ni
kuanza kuusambaratisha mtandao
wote unaojihusisha na biashara
haramu ya silaha.Nakuhakikishia
kwamba hakuna hata mmoja
anayejihusisha na mtandao huu
atabaki salama.Hakuna jiwe
litasalia juu ya jiwe.Wote lazima
wafikishwe mbele ya sheria”
“Operesheni itakapomalizika
na ukafanikiwa kuwafikisha wote
mbele ya sheria nini
kitafuata.Utarudi kwa mke wako?
Ilimchukua Elvis muda kidogo
kujibu swali lile
“Swali lako ni gumu na hata
mimi mwenyewe nimekuwa
najiuliza sana swali hili na bado sijapata majibu mpaka leo hii
kwamba nini kitafuata baada ya
operesheni kumalizika.Ni jambo
gumu sana kurejea kwa watu
waliomwaga machozi yao
wakanishuhudia ndani ya jeneza
hadi nikiingizwa kaburini na
wakamwaga udongo juu yake
kunizika halafu nikawaambia
kwamba sikuwa nimekufa.Ni
vigumu sana kueleweka.” akasema
Elvis
Graca akampiga piga
mgongoni na kusema
“Mimi na wewe sote tuko
katika hali sawa.Mimi ninatafutwa
niuawe na wewe tayari
unajulikana umekwisha kufa na
ukazikwa.Sote hatutakiwi
kuendelea kuonekana
hapa.Twende mbali tukaanze
maisha mapya mahala ambako hakuna anayetufahamu” akasema
Graca na Elvis akageuka
akamtazama halafu akasema
“Nitalitafakari hilo lakini hata
kama nikuondoka hapa Tanzania
lazima niondoke na mke wangu
Patricia.Ninampenda mno na
siwezi kuondoka na kumuacha
hapa akiteseka”
Jibu lile likamnyong’onyeza
Graca.Baada ya muda akauliza
“Vipi kuusu Doreen.Will she
come back?
“Doreen atarejea.kwa sasa
yuko karibu na Patricia
akimfariji.Doreen na Patricia ni
marafiki wakubwa sana”
“Samahani kwa kuuliza swali
hili Elvis.kama Doreen na Patricia
ni marafiki wakubwa iweje Doreen
awepo hapa na wewe badala ya
mke wako Patricia? Halafu mbona wewe na Doreen mna mahusiano
ya kimapenzi?
Swali lile likamstua Elvis
“Mahusiano? Mimi na Doreen
hatua mahusiano ya
kimapenzi.Yule ni shemeji yangu
na katu siwezi kuwa na mahusiano
naye ya kimapenzi”
“Elvis sijauliza kwa ubaya
kwani nafahamu mambo kama
haya yanatokea ila wewe na
Doreen mmekuwa mnakutana na
kufanya mapenzi na hata kulala
pamoja jambo ambalo haliwezi
kutokea kwa mtu na shemeji yake”
akasema Graca na Elvis
akashindwa kukataa akabaki
kimya
“Do you love her? Graca
akauliza
“Nani?
“Doreen” Elvis akafikiri kwa dakika
mbili kisha akasema
“Sikiliza Graca wewe si mtoto
mdogo na kuna mambo tayari
umeyashuhudia kuhusu mimi na
Doreen.Ni historia ndefu kidogo
hadi imekuwa hivi lakini
nitakueleza kwa kuwa nataka
uelewe ili usijenge picha mbaya
kwangu na kwa Doreen” akasema
Elvis na kuanza kumsimulia Graca
kila kitu kuhusu maisha yake na
Patricia toka walipokutana shuleni
hadi walipokuwa wapenzi.Ni
historia ambayo ilimsisimua mno
Graca.
“Pole sana Elvis sikujua kama
historia yako na Patricia iko hivi.Ni
historia yenye kusisimua
mno.Anakupenda sana na hadi
akaamua kutumia njia ya
kukutaka ulale na rafiki yake ili uweze kupata mtoto.Anakujali na
anataka uwe na furaha ndiyo
maana anajaribu kufanya kila njia
ili upate mtoto.Huyu ni mwanamke
mwenye mapenzi ya ajabu sana na
sipati picha ni uchungu gani alio
nao baada ya kuamini kwamba
umefariki dunia”akasema Graca
“Nimemsababishia kidonda
ambacho hakitapona.Ninaapa wale
wote ambao wamesababisha
nikafanya hivi na kuwaumiza watu
niwapendao watalipa uovu wao
kwa gharama kubwa sana.Siku zao
zinahesabika” akasema
Elvis.Baada ya muda Graca
akauliza
“Umefikia maamuzi gani
kuhusu kuzaa na Doreen?
Ilimlazimu Elvis atoe kicheko
kidogo baada ya kuulizwa swali
lile Hilo ni jambo ambalo katu
haliwezi kutokea.Siko tayari kuzaa
na Doreen”
“Tayari mmekwisha kutana
kimwili utakataa endapo
atakwambia kwamba tayari ana
mimba yako?
“Naomba jambo hilo
lisitokee.Zaidi ya yote sitaki tena
kuendeleza mchezo huu na
Doreen.Atakaporejea sitaki
aendele tena kushi hapa kwani
kwa sasa nina majukumu mazito
sana.Halafu mbona leo umeniuliza
maswali mengi sana kuhusu mimi
vipi kuhusu wewe?Una mpango
wowote wa kwenda kumtembelea
Davis gerezani?
“Mimi na Davis mapenzi yetu
yalikwisha muda mrefu
sana.Ninachomuombea ni atoke
aendelee na maisha yake lakini sitaki tena kurejeana naye katika
mahusiano.Kwa sasa nina mambo
mengi ya kufanya kuhusu maisha
yangu” akajibu Graca
*******************
Steven aliwasili nyumbnai
kwa Samira na kumkuta
akimsubiri.Mara tu aliposhuka
garini akalakiwa kwa mabusu
mazito mazito na kukaribishwa
ndani
“Karibu sana mpenzi
wangu.Nikuandalie nini?
“Usisumbuke baby summer
mimi nikikuona tu ninaridhika na
sihitaji tena kitu kingine chochote”
akasema Steven na Samira
akamfuata sofani akabusu ksha akanza kumchezea kifua na
kufungua vifungo vya shati
“Habari za toka jana?
“Pole sana mpenzi wangu
najua jana ulichukia nilipokueleza
kwamba usije yule mzee atakuwa
hapa”
“Ni kweli niliumia lakini hizo
ndizo changamoto ambazo lazima
nikubaliane nazo.Sina wasi wasi
kwa kuwa tayari umeniahidi
kwamba utalifanyia kazi jambo
hilo na ninakuamini kwamba kweli
utalifanyia kazi”
“Ahsante sana Steven.Wewe ni
mwanaume mwenye uelewa
mkubwa sana” akasema Samira na
kumbusu kisha akaanza uchokozi
wake
“Mzee hajakuchosha jana
usiku hadi unataka tena kipute
muda huu? Akauliza Steven Jana kuna mambo yalitokea
hapa na yule mzee hakunifikisha
kokote zaidi ya kunisugua na
kuniacha njia panda.Nikate
kwanza kiu yangu halafu
tutazugumza” akasema Samira na
bila kupoteza muda Steven
akamuinua wakaelekea chumbani
na shughuli ikaanza.Kilikuwa ni
kipute kikali cha dakika zaidi ya
arobaini kisha wote wakajilaza
wakiwa hoi
“Dah ! haya ndiyo mambo
ninayoyataka na siyo kuchezewa
na kuachwa nikitaabika usiku
kucha” akasema Samira
“Uliniambia kuna jambo
lilitokea jana.Nini kilitokea?
akauliza Steven
“Jana wakati tukifanya
mapenzi yule mzee akapigiwa
simu na mtu anaitwa Elizabeth.Alistuka sana alipoliona
jina hilo na muda huo huo ikulu
kukapoa.Akatoka akaenda
kuzungumza na simu nje na
aliporejea ndani hakutaka kukaa
tena akaondoka.Nimejiuliza sana
huyu Elizabeth ni nani hadi
akamuogopesha David kiasi
kile?Ninahisi anaweza kuwa ni
mke wake na ndiyo maana
akastuka baada ya kuona simu
yake.Kama ni mke wake basi kuna
uwezekano akaa ni mwanamke
mshari sana hivyo nataka nikupe
kazi moja unisaidie kuifanya.Kabla
ya hayo kuna jambo nilizugumza
na David jana.Nilimwambia
kwamba ninaye binamu yangu
anahitaji msaada wa kuanzisha
biashara akaniahidi kwamba
atakupa mtaji wa kufungua duka
kubwa la kuuza piki piki na baadae kuuza magari mapya.Sina hakika
kama utapendezwa na hili lakini ni
katika kujaribu kuyajenga upya
maisha yako.Naomba usinipe jibu
sasa hivi bali nenda katakari
kwanza.Tukirudi katika lile suala
nililokueleza mwanzo ninataka
unisaidie kufanya uchunguzi
kumfahamu huyu Elizabeth kama
ndiye mke wake David.Nataka
nianze kujihadhari ili nisije
vamiwa siku moja kwa kuiba
mume wa mtu.Hawa wake wa
viongozi wanaweza wakakufanyia
kitu kibaya”
Steven akamvuta Samira
kwake akambusu na kusema
“Usihofu baby
Summer.Nitalifanyia uchunguzi
jambo hilo na hadi kufikia jioni ya
leo nitakuwa na jibu”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…