I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 47
Baada ya David
kuondoka,Elizabeth akarejea
ndani na kumkuta Juliana katika
chumba cha chakula
"Rafiki yako anaendeleaje?
"Anaendelea vyema.Kwa sasa
amepumzika" akajibu Juliana
"Japokuwa na sisi pia
tumefiwa kama yeye lakini
namuonea huruma sana
Patricia.Amepoteza mume katika
umri mdogo.Dunia hii imejaa watu
makatili sana" akasema Elizabeth
"Hata mimi nimesikitika mno
na kinachoniuma zaidi ni kwambaPatricia na huyu marehemu
mumewe hawajabahatika kupata
mtoto hata mmoja. Hilo
limemfanya Patricia anyanyasike
mno kutoka kwa ndugu za mume
wake.Leo hii katika kikao cha
kumaliza msiba imemlazimu
kuzikabidhi mali zote alichuma na
marehemu mume wake kwa
mama mkwe wake.Amefanya hivi
ili aweze kuishi kwa amani
.Amechoshwa na manyanyaso"
"Kwa nini amefanya hivyo?
hakutakiwa kufanya hivyo.Zile ni
mali zake za halali alichochuma na
mume wake hivyo hakuna ambaye
angetaka kumdhulumu" akasema
Elizabeth
"Mimi namuunga mkono kwa
alichokifanya .Hata ningekuwa mimi mahala pake ningefanya
kama alivyofanya.Siwezi kukubali
kunyanyasika kwa sababu ya
mali.Amefanya kitu sahihi kabisa
kuwaachia kila kitu na ndiyo
maana nimeamua kumchukua ili
aje aishi nasi hapa nyumbani
wakati akijipanga kuytaanza upya
maisha upya maisha yake.Hapa
nyumbani tunayo nafasi ya
kutosha na ninatumai hakutakuwa
na tatizo lolote kwako" akasema
Juliana
"C'mon Juliana hakuna tatizo
lolote lile.Kwanza kwa nini niwe
na tatizo?Jumba hili ni kubwa na
linahitaji watu wa kuishi,sisi peke
yetu hatutoshi.Ni jambo zuri kama
Patricia akija kuishi nasi hapa
nyumabni.Anafanya kazi gani? Ni daktari bingwa wa
mishipa ya fahamu"
"Oh ! kumbe ni msomi mzuri"
"Hukumbuki niliwahi
kukueleza kwamba alishika nafasi
ya kwanza kitaifa katika mtihani
wa kidato cha nne na nafasi ya pili
kitaifa katika mtihani wa kidato
cha sita.Ni mwanamke mwenye
akili nyingi"
"Nafurahi kusikia
hivyo.Tumuache kwanza
apumzike.Nimetoka katika kikao
bado hakuna muafaka na ndugu za
baba yako.Nimewapa hadi usiku
wa leo hii wawe wamefanya
maamuzi ama sivyo nitafanya
maamuzi yangu mwenyewe na
kumzika mume wangu bila
kuwashirikisha.Nimewaacha wanaendelea kujadiliana na
watakapokuwa tayari
watanijulisha .Nilifahamu mambo
haya yatatokea na ndiyo maana
sikutaka kuuleta msiba huu hapa
Tanzania.Wewe ndiye uliyesisitiza
kwamba tuje kumzika baba yako
Tanzania"
“Yalikuwa ni maamuzi sahihi
kuja kumzika baba nyumbani
alikozaliwa.Huku anao ndugu zake
na ambao wana haki ya kushiriki
mazishi yake.Tungemzika nje ya
nchi wasingepata nafasi
hiyo.Tuwavumilie wamalize
tofauti zao ili waje pamoja na
tushirikiane kumzika baba kwa
heshima zote"
"Hakuna tatizo lakini
sintaendelea kuwavumilia kama hawatakubaliana kukaa pamoja na
kupata suluhu ya matatizo yao ili
tumzike baba yako"
"Sawa mama" akasema
Juliana na kuendelea kula kimya
kimya.
*****************
Steve alifika haraka sana
nyumbani kwa Samira baada ya
kumtaka afike mara moja.
"Summer baby" akasema
Steve baada ya kuingia chumbani
kwa Samira na kumbusu
"Steve sijui mikono yako ina
nini kwa sababu kila unaponigusa
mwili wangu wote husisimka
kama vile nimepitiwa na umeme"akasema Samira.Steve
akatasamu na kumbusu tena
"Niambie malaika wangu
huko ulikotoka mambo
yamekwendaje?Umefanikiwa?aka
uliza Steve
“Kila kitu kimekwenda
vizuri.Samira hashindwi na jambo
lolote"akasema Samira na
tabasamu likaonekana usoni pa
Steve
"Nimefanikiwa kuonana na
Vicky.haikuwa rahisi lakini
nimefanikiwa kumshawishi hadi
amekubali kuonana nawe"
"Ahsante sana Samira kwa
kulifanikisha jambo hili.Anahitaji
shilingi ngapi?
"Masuala ya gharama yote
niachie mimi.Nitashughulikia kila kitu na kuhakikisha unafanikiwa
kukutana naye kama
ulivyoomba.Nimemweleza
kwamba wewe ni mfanya biashara
tajiri unaishi nje ya nchi japokuwa
nyumbani ni hapa Tanzania na
kwa hivi sasa umekuja kwa
mapumziko.Vicky ni kahaba ghali
sana na ametaka makutano yenu
yawe katika hoteli kubwa ya nyota
tano na tayari nimekwisha weka
oda ya chumba katika hoteli ya
Samawati beach ambayo ni hoteli
yenye hadhi kubwa hapa nchini
.Chumba chako ni namba 208.Kwa
sasa nataka nikupeleke kwenda
kukufanyia
maandalizi,kukubadilisha
mwonekano wako ili uendane na
ubilionea ili hata Vickyatakapokuona aamini kweli leo
amekutana na Bilionea.Usihofu
kuhusu gharama zote ni juu
yangu" akasema Samira na Steven
akabaki anamtazama asijue la
kusema
"You want to say something
Steve" akauliza
"I have nothing to say .Sina
neno la kusema kwa haya
uliyoyafanya .Hili ni deni kubwa
ambalo sujui nitalilipaje"
"C'mon Steven huu si mkopo
na usiwaze kuhusu kunilipa.Ni
wajibu wangu kukusaidia pale
unapohitaji msaada.Ninakupenda
sana Steve na niko tayari kufanya
chochote kwa ajili yako.Hizi
gharama zote nilizotumia
haziwezi kufikia thamani yako kwangu.Hakuna mwanamke
katika hii dunia anayeweza
kutumia gharama kubwa ili
mpenzi wake akalale na kahaba
lakini mimi nimelifanikisha
hilo.Nimefanya hivyo kwa maenzi
makubwa niliyonayo kwako na
nikiamini kwamba suala ili ni la
muhimu sana
kwako.Ninachohitaji kutoka
kwako ni mambo matatu
tu.kwanza uniamini.Niamini
kwamba ninakupenda toka katika
sakafu ya moyo wangu na niko
tayari kufanya lolote kwa ajili
yako.Pili naomba univumilie kila
pale ninapokuwa na yule
mzee.Kuna mipango mingi
mikubwa anayo juu yangu na
ambayo itakuwa na faida kwetu sote pia.Nitaachana naye ila
ninaomba muda ili niweze
kuchuma utajiri ambao
utatusaidia sote katika maisha
yetu.Steve sitaki uendelee kufanya
hizi kazi.Nataka pindi
nitakapoachana na yule mzee
tuingie katika biashara na tuishi
maisha ya furaha yasiyo na shida
yoyote."akanyamaza na
kumtazama Steve akaupeleka
mkono wake kifuani na kukisugua
taratibu kifua cha Steve.
"Jambo la tatu,nimekubali
kwa moyo wote ukaonane na
Vicky ila nakuomba mpenzi
wangu fanya kila linalowezekana
kuhakikisha haufanyi naye
mapenzi.Yule ni kahaba na hatuna
uhakika kama yuko salama au la,hivyo nakuomba mpenzi wangu
fanya kila linalowezekana upate
taarifa unayoihitaji bila kufanya
naye mapenzi.Mashine hii ni
yangu peke yangu na sitaki
kuchangia na mwanamke
mwingine yeyote"akasema Samira
huku akiupeleka mkono maeneo
ya ikulu ambako tayari kulianza
kuchachamaa.Wakatazama na
macho yao yalionyesha wazi kuna
kitu wanakihitaji na bila hiyana
kila mmoja akawa tayari kumpatia
mwenzake kile
anachokitaka.Wakaingia katika
mtanange mkali wa dakika ishirini
halafu wakaingia bafuni kujiweka
safi
"Steve wewe ni wa kipekee
sana.Unanifikisha mahali ambalo hakuna mwanaume aliyewahi
kunifikisha"akasema Samira
wakati wakioga
"Samira ulinipa kazi ya
kumfahamu mke wa David"
akasema Steve
"Enhee! umegundua nini?
"Mke wa David anaitwa
Veronika na si Elizabeth" akasema
Steven na mshangao ukaonekana
usoni kwa Samira
"Who is Elizabeth?akauliza na
wote wakabaki
wanatazamana,baada ya muda
akasema
"Anyway ,tuachane naye na
mambo yake lakini mstuko
alioupata David baada ya
kupigiwa simu na Elizabeth ni
mkubwa na ndiyo maana nikataka nimfahamu ni nani huyo Elizabeth
aliyemstua David kiasi kile"
akasema Samira.Wakamaliza
kuoga wakajiandaa na kuondoka
***************
Saa kumi na moja kasoro
dakika nane ,Steve akarejea katika
makazi yao.Graca ambaye ndiye
aliyemfungulia geti akapatwa na
mshangao baada ya Steve kushuka
garini
"Steve is that you?!!akauliza
kwa mshangao
"Yeah its me”akajbu Steve
huku akitabasamu
"Ama kweli dunia ina
maajabu.Uliondoka mwingine na
umerejea mwingine kabisa.Steve wa asubuhi ni tofauti na Steve wa
jioni hii" akasema Graca na Steve
akamsogelea karibu
"No body is ugly.Kila kitu
kinawezekana Graca.Hebu
jitazame ,Graca wa jana si Graca
wa leo.Umependeza kumzidi hata
binti mfalme.Graca u mzuri
mno.Unao uzuri ambazo si rahisi
kuuelezea.Kila nikuonapo mwili
wangu wote hunisisimka .Niahidi
kwamba tutapata nafasi ya
kuzungumza "akasema Steve
akiwa katika hali ya utani
"Go to hell...!! akasema Graca
na kuingia ndani Steve akamfuata
.Graca akaenda kuufungua mlango
wa chumba cha Elvis akaingia
ndani Elvis we have a visitor from
Hollywood"
"From Hollywood? Elvis
akashangaa na mara Steve
akaingia mle ndani
"Wow !akasema Elvis
akimshangaa Steve kwa namna
alivyobadilika.Steve akamuomba
Graca awapishe kwa ajili ya
maongezi muhimu
"Elvis kazi imeanza" akasema
Steve
"Kila kitu kimekwenda vizuri
na jioni ya leo ninakwenda
kuonana na Vicky na ndiyo maana
nimefanya maandalizi haya ili
niweze kuendana na Steve yule
ambaye Vicky ameelezwa kuwa ni
bilionea." kazi nzuri sana
Steve.Sikufanya kosa
kukushirikisha katika mpango
huu. Kila kitu kitakwenda kama
tulivyokipanga hakuna
mabadiliko.Utaingia hotelini
utakutana na Vicky na utakapoona
n wakati muafaka kwa mimi
kuingia utanijulisha halafu
nitaingia kama mzimu humo
chumbani na shuguli itaanzia
hapo.Umekumbuka kununua simu
mpya pamoja na kusajili laini za
simu kwa ajili ya mawasiliano?
“Kila nitu nimekifanikisha
usihofu Elvis"
"Good"akasema Elvis na
ukimya mfupi ukapita,Steve
akauliza Elvis are you sure you want
to do this?
"Yes I want.This is what I died
for.Pascal ni mmoja wa watu
wanaojihusisha na mtandao huu
ambao tunakwenda kuufyeka kwa
hiyo tukimpata utakuwa ni
mwanzo mzuri wa kuufahamu
mtandao wote.Usiwe na wasi wasi
Steve siwezi kugundulika”
"Okay then,let's do
this”.Tukifanikiwa kumpata Pascal
tutamuhifadhi wapi? na vipi
kuhusu Vicky tutaondoka naye au
tutamuacha aende zake?akauliza
Steve
"Vicky hatuwezi
kumuacha,tutaondoka
naye.Tunayo nafasi ya kutosha
hapa kwa ajili yao ,tutatengeneza chumba maalum kwa ajili ya
mahojiano.This house will be like
hell.Tayari ninaanza kuvuta
harufu ya damu.Damu yote
iliyomwagika toka kwa watu
wasio na hatia kwa sababu ya
silaha zinazouzwa na genge hili
itawarudia .Its time to make them
pay" akasema Elvis
"Yeah,let's make them pay !!
akasema Steve
*****************
Tayari jua limekwisha zama
na taratibu kiza kimeanza
kuchukua nafasi.Sauti ya mlio wa
kengele ya mlango ilimstua
Patricia toka usingizini ,akajizoa
zoa hapo kitandani na kwenda kuufungua akakutana na Juliana
akiwa na sinia lenye matunda
'Juliana karibu dada yangu"
"Ahsante sana .Unaendeleaje
Patricia?
"Ninaendelea vyema.lazima
nijikaze nikubaliane na hali
halisi.Elvis is gone and will never
come back.Hata kama nikiendelea
kulia machozi usiku na mchana
haitanisaidia.I must find strength
to move one.Vipi wewe
unaendeleaje na maandalizi ya
mazishi ya baba yako?
"Kwa sasa kinachoendelea ni
vikao vya ndugu.Baba na ndugu
zake walikuwa na ugomvi wa
muda mrefu na hakukuwa na
maelewano baina yao.Mama
anaufahamu mgogoro huo na hakutaka baba azikwe hapa
Tanzania ni mimi niliyeshinikiza
tuje kumzika baba mahala
alikozaliwa hivyo ikatulazimu kuja
kwanza kuonana na ndugu zake ili
tuweze kushirikiana katika
mazishi.Hii ni njia moja wapo ya
kuzimaliza tofauti zao na kuwaleta
pamoja kama ndugu.Tuachane na
hayo pole sana kwanza kwa
kuondokewa na mama.Sikujua
kama mama yako naye alikwisha
fariki hadi nilipoelezwa na watu
wanaokaa katika ile nyumba yenu
ya zamani nilipokwenda
kukuulizia leo asubuhi" akasema
Juliana
"Mama alifariki kitambo
sana.Alipata ajali ya gari.Mpaka
leo ninajuta kwa nini nilimnunulia gari.kama nisingefanya hivyo
pengine mpaka leo angekuwa
bado hai" akasema Patricia na
kunyamaza akainamisha kichwa
"Pole sana Patricia"
"Ahsante sana dada
Juliana.Nilipotoka masomoni nje
ya nchi nilimletea mama gari kwa
ajili ya shughuli zake za kilimo na
biashara .Nilimwekea dereva wa
kumuendesha na kumpeleka
kokote anakotaka kwenda.Kwa
bahati mbaya walipata ajali na
wote wakafariki"
"Mwenyezi Mungu mwingi
wa rehema ampumzishe sehemu
salama.Samahani sana Patricia
sikuwepo karibu nawe wakati
huo"akasema Juliana Ni kweli Juliana nilikuwa na
wakati mgumu mno.Hata hivyo
ninamshukuru Elvis ambaye
alisimama nami wakati ule.Nini
hasa kilitokea dada Juliana hadi
ukaondoka nchini ghafla bila hata
kuniaga mdogo wako?
Juliana akainamisha kichwa
kwa swali lile la Patricia
"Kuna mambo makubwa
yalinipata mdogo wangu na
kunifanya niondoke nchini kimya
kimya na bila hata kuwaaga watu
wangu wa muhimu kama
wewe.Nitakueleza siku nyingine
nini hasa kilitokea lakini fahamu
tu kuwa yalinipata mambo
makubwa.Nisingeweza kuondoka
bila kukuaga mdogo wangu lakini
ilinilazimu kufanya hivyo.Utanisamehe sana kwa
hilo.Vipi kuhusu maisha yako toka
tulipoonana mara ya
mwisho?Nakumbuka ulikuwa
bado shuleni Tanga"akauliza
Juliana
“Nimepitia mengi
dada.Nimekutana na mengi
magumu lakini nashukuru
sikuacha kumtegemea Mungu
ambaye alinipa nguvu za
kuyakabili yote niliyokutana
nayo"akasema Patricia na kuanza
kumsimulia Juliana maisha yake
tangu alipokuwa shuleni mkoani
Tanga.
***************** Elvis ni wakati wa mimi
kuanza kujisogeza eneo la
tukio.Unaniruhusu niondoke? Vipi
kuhus muonekano wangu
naonekana kama mfanya biashara
bilionea?akauliza Steve
"Uko sawa kabisa supa
bilionea Steve.Unaweza kuondoka
ila nakukumbusha umakini
mkubwa sana unatakiwa
hatutakiwi kuharibu operesheni
hii muhimu mno kwetu"
"Usihofu Steve.Kila kitu
kitakwenda kama kilivyopangwa"
akasema Steve kisha wakaagana
akaingia katika gari na
kuondoka.Baada ya Steve
kuondoka Elvis akamfata Graca
jikoni alikokuwa akiandaa chakulana kumtaka wakazungumze.Graca
akaacha kazi zote akamfuata Elvis
"Graca nimekuita kukueleza
kwamba ile kazi ambayo
ilinilazimu nife ili niifanye
inakwenda kuanza usiku wa leo"
akanyamaza na kumtazama Graca
ambaye uso wake ulionyesha wasi
wasi
"Nimeona nikujulishe
mapema ili uelewe kwamba
mambo yanaanza .It’s going to be
taugh but you dont have to worry
,you are well
protected"akanyamaza tena
kidogo halafu akaendelea
"Baadae usiku wa
leo,tunategemea kuwaleta hapa
ndani watu wawili kwa ajili ya
mahojiano hivyo usistuke.Kwa kawaida tunapomfanyia mtu
mahojiano huwa tunabadilika
kidogo na kuwa wakali ili tuweze
kupata taarifa
tunazozihitaji.Wengine huwa
wabishi wa kutupa taarifa hivyo
hulazimika kutumia nguvu na
mbinu mbalimbali za kuhoji ili
kuweza kuipata taarifa
hiyo.Utakaposikia mtu akipiga
ukelele mkubwa usiogope ujue
tuko kazini.Ntakuomba pia wakati
haya yote yakifanyika ujifungie
chumbani kwako.Umenielewa
Graca?
"Nimekuelewa Elvis ila sina
cha kusema.This is what you died
for so you have to do it.Kwa
upande wangu usiwe na wasi wasi
kabisa na kama utakumbukaniliwahi kukueleza kuwa napenda
sana kuwa mpelelezi siku moja"
akasema Graca na Elvis
akatabasamu
"Good to hearthat.Napenda
ujasiri wako.Kuhusu kazi hii
nakuomba itoe kabisa
mawazoni.Ni kazi iliyojaa hatari
nyingi"akasema Elvis na kwenda
kumuelekeza vyumba viwili
ambavyo wangevitumia kwa usiku
ule ili aanze kuviandaa
"Elvis"akaita Graca
" Unasemaje Graca?akauliza
"Una uhakika huko unakotaka
kwenda hakutakuwa na tatizo
lolote?Hakuna anayeweza
kukutambua? Usihofu Graca.Hakuna
kitakachoharibika"akasema Elvis
na kuingia chumbani kujiandaa
*****************
Juliana alihisi kutetemeka
kwa ndani baada ya Patricia
kumaliza kumsimulia hadithi ya
maisha yake katika kipindi
ambacho hakuwepo
nchini.Akashusha pumzi halafu
akainuka akatoka mle chumbani
baada ya dakika tano akarejea
akiwa na chupa ya mvinyo
"Unatumia
mvinyo?akamuuliza Patricia
"Ndiyo ninatumia tena
nahitaji mvinyo mkali" This is Martina 76.Moja kati
ya mvinyo mkali kabisa”akasema
Juliana na kummiminia Patricia
katika glasi wakaanza kunywa
.Ilimlazimu Patricia afumbe
macho kutokana na ukali wa
mvinyo ule.Baada ya muda macho
ya Juliana yakajaa machozi
"Patricia nashindwa nianzie
wapi.Sijui niseme kitu gani.Haya
yote uliyonieleza ni ya
kweli?akauliza Juliana huku
akifuta machozi
"Yote ni kweli tupu
Juliana.Hayo ndiyo maisha
niliyoyapitia toka wakati ule hadi
hii leo"
"How the world could be so
cruel?akasema Juliana Dunia si mbaya dada
Juliana,walimwengu ndiyo
wanaoifanya dunia ionekane
mbaya na kuwafanya wengine
wakate tamaa hata ya kuendelea
kuishi.Mungu alimpa mwanadamu
dunia yenye uzuri usioelezeka
lakini tumeiharibu sisi
wenyewe"akasema Patricia
"Patricia imeniumiza sana
kusikia kwamba mdogo wangu
Godson ndiye chanzo cha haya
yote yaliyokupata.Kama
asingekurubuni na kukupa
ujauzito haya
yasingekukuta.Imeniumiza mno
na ninatamani angekuwepo leo hii
ashuhudie kitu alichokufanyia"
akasema Juliana kwa masikitiko
makubwa Yuko wapi Godson?akauliza
Patricia.Juliana akafuta machozi
na kusema
"He's dead "
"Dah ! pole sana Juliana .Nini
kilimuua?
"Ni hadithi ndefu Patricia ila
kwa ufupi tu ni kwamba Godson
aliuawa"
"Pamoja na yote
aliyonitendea lakini alikuwa ni
kijana mwenye roho
nzuri.Naamini waliofanya ukatili
huu kwa sasa wanaozea gerezani"
Juliana akainamisha kichwa
akaonekana kuwa na mawazo
mengi
"Godson was a good
boy.Hakustahili kudhulumiwa
uhai wake kikatili namna ileDada Juliana nini hasa
kilitokea na kusababisha hao watu
wamuue?Aliwafanya nini?Who
killed him?akauliza
Patricia.Ilimchukua Juliana muda
kidogo kujibu swali lile
" He was shot fifty
times.Mwili wake wote ulijaa
matundu ya risasi.Alikatishwa
uhai kikatili mno.Hakustahili
unyama ule mkubwa"
"Oh my God! akasema Patricia
kwa masikitiko
"Waliofanya unyama huo ni
akina nani?naamini watakuwa
tayari wanaozea gerezani"
Juliana akafuta machozi na
kusema Its commplicated
Patricia.Let's not talk about that
unsolved case"
"Dada Juliana unaonekana na
wewe pia umepitia mambo
magumu sana"
"Nimepitia kupindi kigumu
sana Patricia.Nitakueleza mambo
niliyopitia wakati mwingine lakini
naomba ufahamu kwamba sina
cha kufanya kukutibu kidonda
chako ambacho chanzo chake ni
ndugu yangu .Nimeumizwa mno
na sij..........."
"Dada Juliana"Patricia
akamkatisha
"Usikwazwe na mambo haya
yaliyotokea ambayo tayari
yamekwisha kuwa
historia.Matatizo ni sehemu ya maisha yangu na nimekwisha
zoea.Ninashukuru hata hivyo
nimepitia magumu hayo na
nimeimarika japo kwa hili la
kuondokewa na Elvis limenifanya
niwe dhaifu sana.He was
everything to me" akasema
Patricia
"Ninatamani ningepata bahati
ya kuonana na Elvis ana kwa ana
.Wanaume kama yeye
hawapatikani tena katika sayari
yetu hii.Patricia pamoja na huzuni
ulizonazo lakini unapaswa
kumshukuru sana Mungu kwa
kukupatia mwanaume kama Elvis
japo umeishi naye kwa kipindi
kifupi.Inanishangaza sana kwa
nini aliamua kufanya kazi hii ya upelelezi?Hukuwahi kumshauri
atafute kazi nyingine?
"Nilianza kumshauri toka
tukiwa shuleni lakini inaonekana
kazi hii ilikuwa damuni mwake na
hakutaka kusikia ushauri wa mtu
yeyote."akasema Patricia na
ukimya ukatawala mle
chumbani.Baada ya muda Juliana
akasema
"Laiti angekuwa hai
ningeweza kumuomba anisaidie
kutafuta watu waliomuua Godson"
"Elvis alikuwa mahiri sana
katika kazi yake na angeweza
kuwapata.Mpaka leo wauaji wa
Godson hawajulikani?
Kabla Juliana hajajibu swali
lile ujumbe mfupi ukaingia katikasimu yake akausoma kisha
akasema
"Patricia tutazungumza
wakati mwingine,tunatakiwa
kwenda kuonana na ndugu za
baba usiku huu kwa ajili ya kujua
wamefikia maamuzi yapi katika
kikao chao.Nakuomba usihisi
upweke humu ndani kuna
wahudumu ambao
watakuhudumia kwa kila
ukitakacho.Jisikie
nyumbani"akasema Juliana
"Usihofu Juliana hapa ni
nyumbani.Kabla hujaondoka
nahitaji simu kuna mtu nataka
kuwasiliana naye.Simu yangu
haina chaji hata kidogo"
“Simu utapata
usijali.Nitakaporejea nitakuja kukufahamisha nini
kimeafikiwa"akasema Juliana na
kutoka.Baada ya dakika tano
akafika mtumishi wa ndani akiwa
na simu akampatia Patricia
akaweka laini yake na kuzitafuta
namba za Dr Steven washington
akampigia
"Dr Patricia" akasema Dr
Steven akionekana
kustuka.Hakuwa ametegemea
kupigiwa simu na Patricia
"Dr Washington habari
yako?Unaendeleaje?
“Mimi ndiye ninayepaswa
kukuuliza unaendeleaje?
"Ninaendelea vyema .Si rahisi
ila ninajitahidi kukubaliana na
kilichotokea na kuilazimisha akili
yangu izoee ili maisha yaendelee"akasema Patricia na ukimya
ukapita
"Patricia pole sana.Sifahamu
niseme neno gani zaidi ya hilo
ambalo linaweza likakupa faraja
kwa wakati huu mgumu.Lakini
naomba utambue kwamba msiba
huu ni wetu sote.Tumeumia kama
ulivyoumizwa wewe.Muda
wowote utakaohitaji rafiki,mtu wa
kuzungumza naye,mtu wa kulia
naye,mimi nipo hapa" akasema Dr
washington kwa sauti ya upole
"Nashukuru sana Dr
Washington.Nimekupigia tu
kukufahamisha kwamba
ninaendelea vyema"
"Nimefurahi sana kuisikia
tena sauti yako Patricia.Uko wap........"Kabla Dr Washington
hajamaliza kuuliza simu ikakatwa.
"I don’t know why I called
him but I need some one to
comfort me,to tell me it'll be ok.I
need to be in strong hands right
now,I need...."
Patricia akaondolewa
mawazoni baada ya siku yake
kuita .Mpigaji alikuwa ni mke wa
rais.Haraka haraka akaipokea
"Shikamoo mama"akasema
"Marahaba Patricia
unaendeleaje?
"Ninaendelea vizuri
mama.Vipi wewe unaendeleaje?
"Ninaendelea vyema pia.Hofu
yetu ni juu yako”
"Msihofu mama.Suala hili
litapita na nitakuwa salama" .Nimekutafuta kuanzia
asubuhi bila mafanikio,simu yako
haikuwa ikipatikana.Nilitaka
nikufahamishe kwamba
tumejadiliana mimi na rais na
tumeona kwamba itakuwa vyema
kwa wakati huu ambao bado
unaomboleza kifo cha mumeo basi
uje ukae nasi ikulu.Patricia wewe
ni daktari wangu,ni mwanangu na
tunakuchukulia ni sehemu ya
familia yetu kwa hiyo tunataka
uishi nasi hapa japo kwa muda
hadi hapo utakapokuwa umerejea
katika hali ya kawaida.Uliwahi
kunieleza kwamba wazazi wako
wote wamekwisha fariki na sasa
baada ya kuondokewa na
mume,unahitaji kuwa karibu na
watu ambao watakufariji na kukusaidia kukivuka kipindi hiki
kigumu.Ninakuomba ukubali kuja
kuishi nasi hapa na tutafanya kila
lililo ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha kwamba unakuwa na
furaha na amani..unasemaje
kuhusu ombi letu hilo? akauliza
mke wa rais
Patricia akashusha pumzi na
kujibu
"Mama ninawashukuru sana
wewe na mheshimiwa rais kwa
kuwa nami katika kipindi hiki
kigumu.Sina cha kuwapa zaidi ya
kuwaombea kwa Mungu awajalie
baraka nyingi na maisha marefu
yenye furaha na amani.Kuhusu
ombi lako siwezi kulikataa mama
kwani kwa hivi sasa nahitaji mno
faraja.Nimelipokea kwa mikono miwili.Niko tayari kuja kuishi
nanyi ila ninaomba muda kidogo
ili niweke sawa mambo yangu"
"Patricia ahsante sana kwa
kukubali ombi letu.Muda wowote
utakapokuwa tayari unitaarifu ili
nitume watu waje kukuchukua "
"Nashukuru sana
mama.Nifikishie shukrani zangu
kwa mheshimiwa rais”
"Nitazifikisha .Ila nakuomba
muda wowote ukihitaji kitu
chochoe nipigie simu.Wewe ni
mwanetu na tutakufanyia
chochote utakachokitaka"
"Ubarikiwe sana mama"
"Haya kwa heri Patricia.Uwe
na siku njema" akasema mke wa
rais na kukata simu ."Inanipa faraja sana kuona
bado wapo watu wema ambao
wamesimama nami kwa kila hali
ninayopitia na wako tayari
kufanya lolote lililo ndani ya
uwezo wao kuhakikisha kwamba
ninakuwa na furaha tena.Nina
jiona ni mwenye bahati sana kuwa
na watu hawa wachache ambao
hawaniachi na katika gumu lolote
ninalopitia tunafumba macho na
kuomba pamoja"akawaza Patricia
Sent using
Jamii Forums mobile app