Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED To SAVE PRESIDANT

Sehemu 46


*********************

Saa saba na dakika nane gari
la waziri mkuu mstaafu wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania David Sichoma likawasili
katika kasri moja kubwa lililoko
pembezoni mwa bahari ya Hindi.Lilikuwa ni jumba kubwa
ambalo wengi hudhani labda ni
hoteli lakini kumbe ni makazi ya
Elizabeth.Geti likafunguliwa
akaingia ndani na kuelekezwa
sehemu ya kuegesha.Mlinzi wake
akashuka na kumfungulia
mlango,David akashuka garini na
akatokea jamaa mmoja aliyevalia
suti nadhifu ya rangi ya bluu
akamsalimu na kumtaka
amfuate.David akamuelekeza
mlinzi wake amsubiri pale pale
garini.
Aliingia ndani ya kasri lile
kubwa lililosheheni samani nzuri
za kupendeza na kukaribishwa katika sebule iliyokuwepo ghorofa
ya tatu.Muhudumu akafika na
kumuhudumia kinywaji
alichohitaji
“Mheshimiwa David,Madam
atakuwa hapa ndani ya dakika
tano zijazo hivyo endelea
kumsubiri” yule jamaa
aliyempokea David
akamfahamisha na David akaitika
kwa kichwa huku akiendelea
kupata kinywaji chake.Kichwa
chake kilijaa mawazo mengi sana
kuhusiana na mwaliko ule
alioupata kutoka kwa Elizabeth
Dakika kumi toka awasili pale
katika kasri la madam Elizabeth msafara wa gari tatu za kifahari
ukawasili na kwenda kusimama
karibu na mlango wa kuingilia
ndani.Mlango wa gari la kati kati
ukafunguliwa na akashuka
mwanamama mmoja mwenye
umbo la wastani aliyevalia suti
nyeusi na kichwani akiwa na kofia
nyeusi.Licha ya kuwa tayari ni
mtu mzima lakini kutokana na
matunzo mazuri ya mwili wake
bado alionekana ni mwanamke wa
makamo mwenye mvuto.Akiwa
ameambatana na mwanamke
mmoja aliyeonekana kama
msaidizi wake wakaingia ndani na
moja kwa moja akaelekea katika chumba chake akabadili mavazi
halafu akaenda sebuleni aliko
David
“David” akasema Elizabeth
akiwa na uso uliojaa tabasamu
“madam Elizabeth” akasema
David na kusimama
akakumbatiana na Elizabeth
“Karibu sana David.Samahani
kwa kuchelewa kidogo”
“Usijali madam.Habari za siku
nyingi?
“Nashukuru ninaendelea
vyema japo changamoto zinakuwa
nyingi lakini tunakabiliana
nazo.Unazidi kuzeeka David
hufanyi mazoezi?Mimi na wewe tuna umri unaolingana lakini
niangalie mimi bado naonekana
kijana lakini wewe unazidi kuwa
babu.What’s wrong with you
David? Akauliza Elizabeth
“Madam Elizabeth,umri
huwezi kufukuzana
nao.Utajitahidi lakini utafika
mahala utashindwa.Huu ni
uumbaji wa Mungu hivyo lazima
tukubaliane nao ingawa kwa
wewe mwenzetu mambo yako ni
tofauti.Inabidi tuitafute siri hii
kwa nini huzeeki?akauliza David
na Elizabeth akatoa kicheko
“Siri pekee ni
kuupenda,kuujali na kuuthamini mwili.Vipi maisha ya hapa
yanakwendaje?
“Maisha yanakwenda vizuri
Madam”
“Good to hear
that.Nimefurahi sana kukuona
David.Ni muda mrefu umepita
hatujaonana”
“Ni muda mrefu hatujaonana
ndiyo maana nilistuka nilipoona
simu yako jana usiku”
“Tena umenikumbusha kitu
David.Nilipanga nikueleze hili
jambo tutakapokutana.”
“Jambo gani madam?
“Achana na hawa wanawake
ambao lengo lao ni kuogelea katika utajiri wako.Hawajui ni
wapi utajiri huo
umetoka.Kumbuka hukuupata
utajiri huo kirahisi David.Umetoa
jasho na damu na mkeo Flaviana
ndiye pekee aliyesimama nawe
wakati wa kuusaka utajiri huu
hivyo nakushauri usimfanyie hivi
leo.Tulia naye na mfurahie maisha
yenu ya uzee” akasema Elizabeth
na David akainamisha kichwa
kidogo halafu akasema
“Madam Elizabeth mara moja
moja si vibaya kubadilisha ladha
na kupata joto toka kwa hawa
dogo dogo” akasema David na
wote wakacheka David tuachane na hayo.Kwa
upande wangu sikuwa nimetarajia
kuja Tanzania hivi karibuni ila
imenilazimu kuja kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya mazishi ya
mume wangu Deus.”
“Deus amefariki?!! Akauliza
David kwa mshangao
“Ndiyo .Amefariki kwa ajali ya
ndege”
“Dah ! pole sana
Madam.Mazishi yanafanyika lini?
“Hilo hasa ndilo lililonileta
hapa.Deus aliondoka hapa nchini
miaka mingi iliyopita na hadi
mauti yanamkuta tayari alikuwa
amekorofishana na ndugu zake wote.Hata hivyo nimeona nije
mwenyewe niwajulishe kuwa
ndugu yao amefariki .Ningeweza
kuzika mwenyewe bila
kuwajulisha lakini yule si mnyama
anao ndugu zake na wanastahili
kufahamu kuhusu kifo cha ndugu
yao.Tumekuwa na mfululizo wa
vikao toka nilipofika lakini mpaka
sasa bado hakuna muafaka
wowote uliopatikana kuhusiana
na mazishi ya Deus.Wenyewe kwa
wenyewe wanavutana.Nimewapa
hadi usiku wa leo niwe nimepata
jibu lao ama sivyo nitazika bila
kuwashirikisha.Nimewaacha wakiendelea na kikao nikaja
kuonana nawe ”
“Pole sana madam .Deus
alikuwa ni mtu mzuri sana.Mungu
amrehemu”
“Yeah” akajibu Elizabeth na
muhudumu akafika akawaeleza
kwamba tayari chakula
kimekwisha andaliwa.Elizabeth
akamtakla David waelekee katika
chumba cha chakula
“Madam kwa nini
hukunijulisha kuhusu jambo hili
toka ulipokuja ili na mimi
nishiriki?Sina umuhimu tena
kwako? Akauliza David wakati
wakiendelea kupata chakula David mimi ndiye
niliyepaswa kukuuliza swali hilo
kwa nini umenitenga siku
hizi?Mimi si muhimu tena kwako?
“Sijakutenga Madam na
siwezi kufanya hivyo.Wewe ni
mtu muhimu sana kwangu na
hakuna wa kulibadilisha
hilo.Nimefika hapa nilipofika
kutokana na msaada wako hivyo
utabaki kuwa mtu muhimu sana
katika maisha yangu” akasema
David na Elizabeth akatabasamu
“Kama unalifahamu hilo kwa
nini basi hukutaka kunishirikisha
katika mpango wa mapinduzi?
Akauliza Elizabeth na mara kijiko alichokishika David
kikamponyoka na
kuanguka.Alistuka sana na kwa
sekunde kadhaa akabaki
ametumbua macho akimtazama
Elizabeth
“Rleax David.Take a deep
breath” akasema Elizabeth huku
akitabasamu
“madam..uhhmm……” David
akababaika alikosa cha kusema
‘Relax David.hapa si
mahakamani.You don’t have to
explain”
“Madam how….!
umefahamuje kuhusu jambo hili?C’mon David hilo si swali la
kuniuliza mtu kama mimi.Au
umenisahau mimi ni nani?
“Nimeshangaa sana kwa
sababu jambo hili ni la siri kubwa
na tunaolifahamu ni watu
wachache sana”
“David,Tanzania ni nchi
ndogo na ninaifahamu kama
alama za kiganja cha mkono
wangu.Ninafahamu mambo yote
ya wazi na ya siri yanayoendelea
hapa nchini hivyo kufahamu
jambo kama hili ni kitu kidogo
sana kwangu.Swali langu ni kwa
nini hukutaka
kunishirikisha?Unadhani siwezi kuwa na msaada wowote
kwako?kama niliweza kukufikisha
katika nafasi ya uwaziri mkuu
unadhani ningeshindwa
kukufikisha ikulu ukakalia kiti cha
rais?Dont you trust me
anymore?Dont you trust my
power? David I’m very powerfull
woman na hata wenzangu
wanalifahamu hilo na
wananiogopa.Makundi yote ya
kimafia wananiogopa kwani ninao
uwezo wa kufanya chochote
mahala kokote.Nakushangaa kwa
kushindwa kunishirikisha katika
jambo hili.I’m so dissapointed”
akasema ElizabethMadam Elizabeth …”
akasema David
“Suala hili hata mimi limenijia
ghafla bila kutegemea na wala
sikuwa nimelipanga.Nilialikwa
katika kikao na rafiki zangu
,sikujua kama wanakwenda
kuongelea kuhusu suala
hili.Walinishawishi nikakubali
kushirikiana nao kwa
makubaliano kwamba mapinduzi
hayo yakifanikiwa mimi niwe
rais.Toka hapo ndipo mchakato
ulipoanza na sikuweza hata
kukumbuka
kukujulisha.Utanisamehe sana
kwa hilo madam Elizabeth” David hilo ni kosa
ulilifanya.Ulipopata jambo kubwa
kama hili ulipaswa kuinua simu na
kunijulisha.Hiki kilikuwa kipimo
cha uaminifu na umeshindwa
kufaulu”
“Sijakuelewa madam “
“This was a test and you
failed”
“A test? How? Who tested
me?
“I did! Akajibu Elizabeth
“You? Akauliza David kwa
mshangao
“Yes me.Mpango huu wote
mimi ndiye niliyeuandaa hivyo nafahamu kila kitu
kinachoendelea”
David hakuweza tena
kuendelea kula kwa mshangao
alioupata
“I’m sorry Madam Elizabeth
bado sijakuelewa”
“Ni hivi” akasema Elizabeth
na kunywa funda la kinywaji
“Wale jamaa wawili waliokuja
kuzungumza nanyi kuhusiana na
mpango wa mapinduzi walianzia
kwetu.Walitueleza tatizo lao na
sisi ndiyo tuliotoa wazo la
kufanyika kwa
mapinduzi.Mipango yote
inayofanyika huku tunaifuatilia kwa karibu sana.Mimi ndiye
niliyetoa wazo la wewe
ushirikishwe katika mpango huu .I
wanted to make you president but
I don’t think you deserve that
position” akasema Elizabeth
“Madam Elizabeth nimekosa
neno la kusema.Sikutegemea
kama uko nyuma ya mpango
huu.Hata hivyo madam mimi bado
ni mwaminifu kwako na
nitaendelea kuwa mwaminifu siku
zote .Ninaihitaji sana nafsi hii
ambayo nimeiota kwa muda
mrefu”
“David nilitaka nikupime
kama bado u mtiifu kwangu lakini ukweli ni kwamba tayari katika
akili yako sina umuhimu wowote
kwako tena.Hukumbuki fadhila
wala ulikotoka.Hustahili kupewa
nafasi kubwa kama hii”
“Madam Elizabeth mimi bado
ni mtiifu kwako na katu siwezi
kukusahau.Sikujua kama nawe
upo katika mpango huu”
“Ulikuwa unawasiliana nami
na kunishirikisha katika mambo
mengi na ulipopata mpango
wenye maslahi makubwa kama
huu ulipaswa kunijulisha na hicho
ndicho nilichokuwa
nakihitaji.Tuachane na hayo
nilitaka tu nikufahamishe ujue ni nani walio nyuma ya mpango huu
na nimekupendekeza ushike
nafasi ya juu kabisa endapo
mapinduzi haya yakifanikiwa kwa
sababu kuna mambo nayahitaji
uyafanye mara tu upatapo
urais.You’ll be doing everything I
tell you to do.Umenielewa David”
“Nimekuelewa madam”
akajibu David
“Good.Kitu cha kwanza
ninachotaka ukifanye mara tu
utakapofanikiwa kuingia ikulu
baada ya mapinduzi ambayo
naamini yatafanikiwa ni kumteua
mwanangu kuwa waziri wa
madini. Nchi hii ina madini mengi mno ambayo yanachotwa tu na
wageni.Ni wakati wetu na sisi
kuanza kufaidika na rasilimali
hii.Hilo litakuwa ni jambo la
kwanza ambalo nitakutaka
ulifanye pale utakapokuwa
umeingia ikulu.Mambo mengine
tutaendelea kuelekezana ila hilo ni
la kwanza ambalo ni muhimu
kulifanya.Umenielewa David?
“Nimekuelewa madam
Elizabeth lakini ….”
“David hakuna lakini.This is
an order from me!! Kama unaona
ugumu kulitekeleza hilo sahau
kabisa suala la kuwa
rais”Akasema Elizabeth Madam Elizabeth
nitalitekeleza hilo jambo kama
unavyotaka” akasema David
“Good..” Elizabeth
akatabasamu na kuyaelekeza
macho yake mlangoni,watu wawili
waliingia mle ndani.
“Juliana karibuni” akasema
Elizabeth
“Ahsante mama” akajibu
Juliana na kumsalimu David
“Juliana huyu anaitwa David
Sichoma ni waziri mkuu mstaafu
na ni rafiki yangu wa siku
nyingi.Amekuja kunitembelea
alipopata habari kuwa niko hapanchini” akasema Elizabeth na
kuyaelekeza macho kwa David
“David huyu ndiye mwanangu
Juliana.Nafurahi leo mmekutana”
“Ninamfahamu mheshimiwa
David japo yeye bado
hanifahamu.Huyu ni mtu maarufu
ambaye hakuna asiyemfahamu
hapa nchini.Hata hivyo nafurahi
kwa leo tumekutana ana kwa
ana.Ni mmoja wa wanasiasa
niliokuwa napenda kusikiliza
hotuba zao” akasema Juliana na
David akatabasamu
“Juliana nimefurahi pia
kukutana nawe.U mrembo kama mama yako” akasema David na
wote wakacheka
“Juliana hujatutambulisha
mgeni wetu anaitwa nani?
Elizabeth
“Anaitwa Patricia.Niliwahi
kukupa habari zake”
“Oh ! kumbe ndiyo
huyu.karibu sana Patricia.Juliana
aliwahi kunipa habari
zako.Nafurahi leo nimekuona”
“Nashukuru mama.Juliana ni
mtu wa karibu sana kwangu na
ana mchango mkubwa katika
maisha yangu” akasema Patricia
“Mama tutazungumza
baadae,Patricia anahitaji kupumzika.Hapa alipo yupo katika
majonzi bado.Ni jana tu mumewe
amezikwa.Nimeamua kumchukua
aje hapa nyumbani kupumzika”
akasema Juliana
“Oh jamani,pole sana
Patricia.Kufiwa ni jambo gumu na
ninayafahamu machungu
uliyonayo kwani hata mimi
nimempoteza mume wangu
kipenzi na hivi sasa tuko katika
maandalizi ya mazishi.Sote
tumekutana katika kipindi kigumu
.Nenda kapumzike tutaonana
baadae” akasema Elizabeth na
Juliana akaondoka na Patricia Ama kweli dunia imekuwa
kijiji.Sikutegemea kama
ningeweza kukutana na huyu
mwanamama”
“Patricia?Do you know her?
Elizabeth akauliza
“ Mume wake ambaye
amezikwa jana sisi ndiyo
tuliomzimisha.He was a threat to
us”akasema David
“A threat? Elizabeth akauliza
“Ndiyo.Anaitwa Elvis.Ni
mmoja wa wapelelezi hatari hapa
nchini alikuwa anafanya kazi
katika idara ya ujasusi iliyo chini
ya ofisi ya makamu wa rais.Elvis
alifanikiwa kugundua mambo kadhaa kuhusiana na sisi na ndipo
nilipolazimika kuagiza akatwe
pumzi”
Elizabeth akavuta pumzi
ndefu akamtazama David na
kuuliza
“Ni mambo gani
aliyoyagundua kuhusu sisi?
Yanahusiana na mpango wa
mapinduzi?
“Uhhm…!! Akasema David na
kunyamaza kidogo na baada ya
sekunde chache akasema
“Ninaye rafiki yangu anaitwa
Brigedia Frank Kwaju ambaye
ndiye aliyenishirikisha katika
mpango huu wa mapinduzi.Kwa maelezo aliyoniupa ni kwamba
anaye mtoto wake wa kike
ambaye aliwahi kuiba kompyuta
yenye siri zake nyingi na baadae
binti huyo akapelekwa katika
hospitali ya magonjwa ya akili
iliyoko afrika kusini.Mpaka sasa
haelewi Elvis aligunduaje mahala
mwanae alipo na akamfuata afrika
ya kusini akamtorosha na mpaka
sasa haijulikani huyo mwanae
yuko wapi.Ni wazi kuna jambo
Elvis amekwisha lifahamu kuhusu
sisi na ndiyo maana Frank
akaelekeza kwamba aondolewe
haraka sana” akasema David.Ukimya ukapita kwa muda
Elizabeth akauliza
“Was he
alone?Hamjachunguza kama kuna
wenzake alioshirikiana nao? Kwa
sababu kama alikuwa na wenzake
anashirikiana nao na mkamuua
yeye peke yake bado haitasaidia
kwani wenzake waliobaki
watahakikisha wanaendelea
kuchunguza hadi wahakikishe
wamefanikisha jambo
wanalolichuguza kwenu.Kuna
utafiti wowote mlioufanya kuhusu
hilo? Akauliza Elizabeth
“Nilipokea maelekezo toka
kwa Frank na sifahamu kama alifanya utafiti wa kubaini kuhusu
hilo unalolisema.Inawezekana
labda alifanya utafiti na
kujiridhisha kuwa Elvis alikuwa
peke yake”
“Hilo ni kosa kubwa
mmelifanya.David umekuwa
waziri mkuu kwa miaka kumi na
unaelewa namna upelelezi
unavyofanyika kwa
mashirikiano.Nina uhakika
mkubwa kwamba huyo mpelelezi
aliyeuawa hakuwa peke
yake.Lazima alikuwa na wenzake
na kama mmewaacha hai
watafanya kila wawezalo hadi
wahakikishe wanawafahamu waliomuua mwenzao.Mlijiridhisha
kuwa Elvis hakuwa na wenzake?
Akauliza
“Madam nina uhakika Frank
alifanya uchunguzi wa kutosha
ndiyo maana akaelekeza auawe
Elvis peke yake”
“No ! that’s not true” akasema
Elizabeth na kusimama
akatoka.Baada ya dakika tano
akarejea akiwa na mkebe
akaufungua na kutoa sigara
kubwa akawasha na kuvuta
mikupuo kadhaa akapuliza moshi
na kumtazama David “Nisikilize vizuri David”
akanyamaza na kuvuta tena
mkupuo mwingine mkubwa
“Sikuwa nimepanga
kuzungumza nawe suala hili
kwani sikujua kama nawe
unahusika lakini kuna jambo
ambalo unapaswa kulifahamu”
akanyamaza kidogo na kuendelea
“Nimekuwa katika genge la
kimafia kwa muda mrefu na sasa
baada ya Deus kufariki dunia
mimi ndiye kiongozi wa genge hilo
la watu matajiri,wenye nguvu na
uwezo wa kufanya chochote
mahala kokote.Umepata bahati ya
kushirikishwa katika baadhi ya mambo ya genge letu na hadi
ukafikia hatua ya waziri mkuu wa
jamhuri ya muunganowa Tanzania
lakini kuna mambo mengi
huyafahamu bado kuhusiana na
genge letu na hata mimi
mwenyewe kuna wengine
siwafahamu bado.Nimetoa
machozi na damu kufika hapa
nilipofika leo,kwa ujumla
nimepitia mambo
mengi.Tuachane na hayo ni
mambo yangu binafsi wewe bado
ni mtu mdogo sana kuyafahamu”
akanyamaza akavuta mkupuo
mkubwa na kupuliza moshi
mwingi kisha akasema Mimi na Deus tunafanya
biashara ya silaha na baadhi ya
makundi ya waasi hapa barani
Afrika.Tunafanya biashara na
kundi makundi ya waasi katika
nchi za Libya,Sudan,Somalia
lakini biashara kubwa sana
tunaifanya na waasi wanaopigana
na serikali ya jamhuri
kidemokrasia ya Congo.Brigedia
Frank Kwaju ndiye msimamizi
mkuu katika biashara na waasi wa
Mashariki ya Congo”
“Unamfahamu Frank? Mbona
hajawahi kunieleza chochote
kuhusiana na biashara hiyo ya
silaha? That’s the top secret.Wewe
mwenyewe nimekushirikisha
katika mipango mbali mbali ya siri
na unafahamu namna
tunavyoendesha mambo yetu kwa
usiri mkubwa.Itoshe tu kufahamu
kwamba Brigedia Frank ni mtu
wangu pia.Haya yote unayonieleza
tayari ninayafahamu.Amekwisha
nieleza
kila kitu kuhusu kupotea kwa
kompyuta yake na hata
kutoroshwa kwa mwanae
aliyekuwa anatibiwa katika
hospitali ya wagonjwa wa akili
afrika kusini"akanyamaza akavuta
tena mkupuo mkubwa akapuliza
moshi na kuendelea.
"Kwa bahati mbaya naweza
kusema katika kompyuta hiyoiliyoibwa kulikuwa na
mawasiliano kati ya Deus na
Frank na hofu ikajitokeza kuwa
huyo aliyechukua kompyuta hiyo
kuna kitu anakitafuta na anaweza
kuanza kumchunguza Deus kwani
Frank hakufuta mawasiliano yake
na Deus katika h iyo
kompyuta.Kitu kingne kuna
mwanamke anaitwa Vicky .Huyu
aliwahi kuwa na mawasiliano na
Deus.Huyu ni kahaba na kuna kazi
ambazo Deus alimtumia
kuzifanya.Kwa taarifa ambazo
nimezipata toka kwa Frank ni
kwamba tayari Elvis amekwisha
mfahamu huyo mwanamke na
ameanza kumfuatilia na hii
inaonyesha wazi kwamba kuna
kitu anakitafuta kwake.Endapo angefanikiwa kumpata ingekuwa
hatari sana kwa Deus. Baada ya
kupata taarifa hizo sikuwa na njia
nyingine zaidi ya kumuua Deus"
Mstuko mkubwa ukaonekana
machoni pa David
"You killed him? Akauliza
kwa wasi wasi
"Yes I did.I had no
choice.Tayari Deus alikuwa katika
hatari ya kujulikana.Huu ni
mpango wa siri uliotengenezwa
kitaalamu mno.Endapo Deus
angejulikana basi mimi pia
ningejulikana jambo ambalo
sikuwa tayari litokee.David
ninakueleza haya yote ili upate
picha namna mambo
yanavyotakiwa
kufanywa.Nilimuelekeza Frank ahakikishe anafagia uchafu
wote kwa kuwaondoa Elvis na
Vicky.Je amefanya hivyo au
amekurupuka na kumuua Elvis
peke yake?Je amechunguza na
kujiridhisha kwamba Elvis
hakuwa na mtu mwingine
aliyekuwa anashirikiana naye
katika uchunguzi?akauliza
Elizabeth.David akatoa kitambaa
na kufuta jasho
"Madam nadhani swali hilo
angefaa alijibu Frank
mwenyewe.Mimi aliniomba
nimsaidie kumuondoa Elvis na
nikafanya hivyo.Kuhusu Vicky
sifahamu chochote na wala
simfahamu huyo
mwanamke.Umekwisha muuliza Frank kama ametekeleza maagizo
uliyompa?
“Bado sijapata nafasi ya
kukaa na kuzungumza na
Frank.Nategemea nikishamaliza
masuala ya msiba nitazungumza
naye na atanieleza namna
alivyotekeleza maagizo
yangu.Nimekueleza haya ili upate
picha kwamba uzembe mdogo tu
unaweza ukasababisha madhara
makuwa.Suala hili la Elvis
mnaweza mkalichukulia kirahisi
lakini ni suala kubwa.Kama
huniamini utaona
kitakachotokea.These people will
never stop haunting us na hii ni
mbaya sana kwa sababu inaweza
kusababisha mipango yetu
ikashindikana.Nilitegemea Frank angeweza kushughulikia vyema
kila kitu lakini kwa maelezo haya
mafupi uliyonipa tayari kuna
uzembe nimeuona na bila
kuchukuahatu aza haraka kuna
hati hati mpango huu wa
mapinduzi ukashindwa
kufanikiwa .Kwa sasa naliweka
kando suala hili hadi hapo
nitakapomaliza kumzika mume
wangu ila nataka unisadie kufanya
uchunguzi kuhusu huyu
mwanamke Vicky kama
amekwisha uawa au bado.Huyu ni
mtu hatarisi kwetu kwani endapo
wakimpata anaweza akawaeleza
mambo mengi kuhusiana na
Deus.Kama bado yuko hai nataka
uhakikishe anaondolewa haraka
sana.Can you do that for me? akauliza Elizabeth.Bila hata
kupepesa macho David akajibu
"Nitafanya hivyo madam
Elizabeth."
"Good" akasema Elizabet na
kumalizia sigara yake
"Madam Elizabet huyu mke
wa Elvis hudhani kuwa anaweza
kuwa anafahamu
chochote?Yawezekana labda
mume wake kabla hajafariki kuna
mambo alimueleza.Unaonaje
endapo tutamchunguza pia ili
kuona kama anafahamu chochote?
Akauliza David
"Hilo unalolisema David ni
jambo muhimu sana.Niachie mimi
suala hilo nitalishughulikia baada
ya kumaliza mazishi ya Deusakasema Elizabeth n kunyamaza
baada ya Juliana kutokea
"David nimefurahi kuonana
nawe.Tutaendelea kuonana zaidi.
Nitakujulisha siku ya mazishi"
akasema Elizabeth huku
akimfanyia ishara David ya
kuondoka.Davd akaielewa ishara
ile na kusimama.
"Hata mimi nimefurahi sana
kuonana nawe madam
Elizabeth.Pole sana kwa msiba
huu mkubwa na ninapenda
kukuhakikishia tena kwamba
msiba huu ni wetu sote na
tutashirikiana katika kila hatua
hadi tutakapomsitiri Deus katika
nyumba yake ya milele"akasema
David na kumgeukia Juliana
aliyekuwa amewakaribia Juliana nafurahi leo
nimekufahamu japo tumekutana
katika kipindi hiki cha majonzi
lakini bado tutaendelea
kuonana.Ninamuomba Mungu
awape uvumilivu mkubwa na
nguvu ya kuweza kuhimili kipindi
hiki kigumu sana cha kuondokewa
na mzee wenu"
"Ahsante sana kwa
kutututembelea na
kutufariji.Mungu akubariki sana
Uncle David" akasema Juliana na
kupeana mkono na David
wakaagana .Elizabeth
akamsindikiza hadi garini
"David samahani
nimekuondoa haraka
haraka.Sikutaka Juliana asikie
maongezi yetu.Bado hafahamu chochote kuhusu
sisi.Anachofahamu ni kwamba sisi
ni wafanya biashara na hajui
mambo mengine tunayoyafanya
nyuma ya biashara"
“Lakini Juliana tayari ni mtu
mzima.Kwa nini usimfahamishe
ajue mambo yako hasa kwa
wakati huu ambao umebaki peke
yako?Anaweza akawa ni msaada
kwako”
"No ! I dont want to involve
my children in my dirty business.I
want them to enjoy life.Kwa heri
David tutaendelea kuwasiliana ila
yafanyie kazi hayo niliyokutuma"
akasema Elizabeth na David
akaondoka
"Haya ni maajabu ya
Musa.Hapa nilipo mwili wote unanitetemeka.Sikujua kama
Elizabet naye yupo katika
mpango huu wa mapinduzi.Laiti
kama ningejua huyu shetani yuko
pia katika jambo hili nisingekubali
kujiunga nao kabisa.Sikutaka
ukaribu naye na ndiyo maana
kwa muda nimekuwa nikijaribu
kujiweka mbali naye lakini kwa
bahati mbaya nimejikuta tena
nikirejea katika himaya yake na
siwezi kumkimbia tena.Sikatai ni
mtu mwenye msaada mkubwa
kwangu na ndiye aliyenisaidia
hadi nikafanikiwa kufikia hatua ya
kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania lakini
hakuna anayejua adha niliyokuwa
ninaipata nikiwa waziri mkuu
toka kwa Elizabeth.Aliitumia nafasi yangu katika kufanikisha
mambo yake mengi na sikuwa na
uwezo wa kumzuia na ndiyo
maana sikutaka afahamu chochote
kuhusiana na mpango wa
mapinduzi.Hata kabla mapinduzi
hayajafanikiwa tayari anataka
mwanae awe waziri .Vijana wanao
msemo wao wanasema nimeingia
choo cha kike" akawaza David
“Kingine kilichonistua kumbe
Frank naye ni mtu wake na
anasimamia biashara yake ya
silaha.Kwa nini sikulifahamu hili
toka awali?Nimeingizwa mtegoni
bila kujua na mimi nikanasa
kumbe lengo lao ni kunitaka niwe
rais ili wanitumie katika mambo
yao.Nilifurahi na kuamini ndoto
yangu ya siku nyingi ya kushika wadhifa mkubwa wa rais
inakwenda kutimia lakini baada
ya kuonana na Elizabeth na
kufahamu kuwa naye yupo katika
mpango huu sina hamu tena na
nafasi hiyo lakini siwezi kusema
hapana kwani lazima
watanimaliza.Watu hawa ni hatari
sana na mtandao wao ni mkubwa
pia.Sitakiwi kufanya nao mchezo
hata kidogo.Kwa vile nimekubali
kushirikiana nao ngoja tu
niendelee nao ila napaswa kuwa
makini sana.Halafu kuna huyo
mwanamke Vicky ambaye
Elizabeth anataka
auawe.Nitafuatilia nijue kama
tayari amekwisha uawa au bado"
akawaza David na kuchukua simu
akazitafuta namba za Frank akampigia na kumtaka wakutane
jioni nyumbani kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana...

Sijui itakuaje pale Patricia atakapokuja kugundua kumbe Juliana, mama yake ana chain ya issue haramu mpaka kupelekea mume wake kughushi kifo...

Kweli dunia ni kama kijiji...


Cc: mahondaw
 
Asante sana Kulubule, hii story njema sana, na unatiririsha vizuri.
 
I just knew it, that somehow, somewhere, Elvis, Godson and Juliana will meet at an intertwined fate!

Mkuu kulubule leo ni sikukuu tafadhali ikikupendeza na kupata kibali machoni pako leo shusha hata episode 10.

Leo ni Eid mkuu hii harufu ya pilau inapotezwa na Riwaya tu
 
Mkuu kulubule wakati wengine wakienda kupata furaha na wapendwa wao tushushie angalau vigongo viwili ili tuende nao sambamba....natanguliza shukran zangu za dhati kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 47

Baada ya David
kuondoka,Elizabeth akarejea
ndani na kumkuta Juliana katika
chumba cha chakula
"Rafiki yako anaendeleaje?
"Anaendelea vyema.Kwa sasa
amepumzika" akajibu Juliana
"Japokuwa na sisi pia
tumefiwa kama yeye lakini
namuonea huruma sana
Patricia.Amepoteza mume katika
umri mdogo.Dunia hii imejaa watu
makatili sana" akasema Elizabeth
"Hata mimi nimesikitika mno
na kinachoniuma zaidi ni kwambaPatricia na huyu marehemu
mumewe hawajabahatika kupata
mtoto hata mmoja. Hilo
limemfanya Patricia anyanyasike
mno kutoka kwa ndugu za mume
wake.Leo hii katika kikao cha
kumaliza msiba imemlazimu
kuzikabidhi mali zote alichuma na
marehemu mume wake kwa
mama mkwe wake.Amefanya hivi
ili aweze kuishi kwa amani
.Amechoshwa na manyanyaso"
"Kwa nini amefanya hivyo?
hakutakiwa kufanya hivyo.Zile ni
mali zake za halali alichochuma na
mume wake hivyo hakuna ambaye
angetaka kumdhulumu" akasema
Elizabeth
"Mimi namuunga mkono kwa
alichokifanya .Hata ningekuwa mimi mahala pake ningefanya
kama alivyofanya.Siwezi kukubali
kunyanyasika kwa sababu ya
mali.Amefanya kitu sahihi kabisa
kuwaachia kila kitu na ndiyo
maana nimeamua kumchukua ili
aje aishi nasi hapa nyumbani
wakati akijipanga kuytaanza upya
maisha upya maisha yake.Hapa
nyumbani tunayo nafasi ya
kutosha na ninatumai hakutakuwa
na tatizo lolote kwako" akasema
Juliana
"C'mon Juliana hakuna tatizo
lolote lile.Kwanza kwa nini niwe
na tatizo?Jumba hili ni kubwa na
linahitaji watu wa kuishi,sisi peke
yetu hatutoshi.Ni jambo zuri kama
Patricia akija kuishi nasi hapa
nyumabni.Anafanya kazi gani? Ni daktari bingwa wa
mishipa ya fahamu"
"Oh ! kumbe ni msomi mzuri"
"Hukumbuki niliwahi
kukueleza kwamba alishika nafasi
ya kwanza kitaifa katika mtihani
wa kidato cha nne na nafasi ya pili
kitaifa katika mtihani wa kidato
cha sita.Ni mwanamke mwenye
akili nyingi"
"Nafurahi kusikia
hivyo.Tumuache kwanza
apumzike.Nimetoka katika kikao
bado hakuna muafaka na ndugu za
baba yako.Nimewapa hadi usiku
wa leo hii wawe wamefanya
maamuzi ama sivyo nitafanya
maamuzi yangu mwenyewe na
kumzika mume wangu bila
kuwashirikisha.Nimewaacha wanaendelea kujadiliana na
watakapokuwa tayari
watanijulisha .Nilifahamu mambo
haya yatatokea na ndiyo maana
sikutaka kuuleta msiba huu hapa
Tanzania.Wewe ndiye uliyesisitiza
kwamba tuje kumzika baba yako
Tanzania"
“Yalikuwa ni maamuzi sahihi
kuja kumzika baba nyumbani
alikozaliwa.Huku anao ndugu zake
na ambao wana haki ya kushiriki
mazishi yake.Tungemzika nje ya
nchi wasingepata nafasi
hiyo.Tuwavumilie wamalize
tofauti zao ili waje pamoja na
tushirikiane kumzika baba kwa
heshima zote"
"Hakuna tatizo lakini
sintaendelea kuwavumilia kama hawatakubaliana kukaa pamoja na
kupata suluhu ya matatizo yao ili
tumzike baba yako"
"Sawa mama" akasema
Juliana na kuendelea kula kimya
kimya.

*****************

Steve alifika haraka sana
nyumbani kwa Samira baada ya
kumtaka afike mara moja.
"Summer baby" akasema
Steve baada ya kuingia chumbani
kwa Samira na kumbusu
"Steve sijui mikono yako ina
nini kwa sababu kila unaponigusa
mwili wangu wote husisimka
kama vile nimepitiwa na umeme"akasema Samira.Steve
akatasamu na kumbusu tena
"Niambie malaika wangu
huko ulikotoka mambo
yamekwendaje?Umefanikiwa?aka
uliza Steve
“Kila kitu kimekwenda
vizuri.Samira hashindwi na jambo
lolote"akasema Samira na
tabasamu likaonekana usoni pa
Steve
"Nimefanikiwa kuonana na
Vicky.haikuwa rahisi lakini
nimefanikiwa kumshawishi hadi
amekubali kuonana nawe"
"Ahsante sana Samira kwa
kulifanikisha jambo hili.Anahitaji
shilingi ngapi?
"Masuala ya gharama yote
niachie mimi.Nitashughulikia kila kitu na kuhakikisha unafanikiwa
kukutana naye kama
ulivyoomba.Nimemweleza
kwamba wewe ni mfanya biashara
tajiri unaishi nje ya nchi japokuwa
nyumbani ni hapa Tanzania na
kwa hivi sasa umekuja kwa
mapumziko.Vicky ni kahaba ghali
sana na ametaka makutano yenu
yawe katika hoteli kubwa ya nyota
tano na tayari nimekwisha weka
oda ya chumba katika hoteli ya
Samawati beach ambayo ni hoteli
yenye hadhi kubwa hapa nchini
.Chumba chako ni namba 208.Kwa
sasa nataka nikupeleke kwenda
kukufanyia
maandalizi,kukubadilisha
mwonekano wako ili uendane na
ubilionea ili hata Vickyatakapokuona aamini kweli leo
amekutana na Bilionea.Usihofu
kuhusu gharama zote ni juu
yangu" akasema Samira na Steven
akabaki anamtazama asijue la
kusema
"You want to say something
Steve" akauliza
"I have nothing to say .Sina
neno la kusema kwa haya
uliyoyafanya .Hili ni deni kubwa
ambalo sujui nitalilipaje"
"C'mon Steven huu si mkopo
na usiwaze kuhusu kunilipa.Ni
wajibu wangu kukusaidia pale
unapohitaji msaada.Ninakupenda
sana Steve na niko tayari kufanya
chochote kwa ajili yako.Hizi
gharama zote nilizotumia
haziwezi kufikia thamani yako kwangu.Hakuna mwanamke
katika hii dunia anayeweza
kutumia gharama kubwa ili
mpenzi wake akalale na kahaba
lakini mimi nimelifanikisha
hilo.Nimefanya hivyo kwa maenzi
makubwa niliyonayo kwako na
nikiamini kwamba suala ili ni la
muhimu sana
kwako.Ninachohitaji kutoka
kwako ni mambo matatu
tu.kwanza uniamini.Niamini
kwamba ninakupenda toka katika
sakafu ya moyo wangu na niko
tayari kufanya lolote kwa ajili
yako.Pili naomba univumilie kila
pale ninapokuwa na yule
mzee.Kuna mipango mingi
mikubwa anayo juu yangu na
ambayo itakuwa na faida kwetu sote pia.Nitaachana naye ila
ninaomba muda ili niweze
kuchuma utajiri ambao
utatusaidia sote katika maisha
yetu.Steve sitaki uendelee kufanya
hizi kazi.Nataka pindi
nitakapoachana na yule mzee
tuingie katika biashara na tuishi
maisha ya furaha yasiyo na shida
yoyote."akanyamaza na
kumtazama Steve akaupeleka
mkono wake kifuani na kukisugua
taratibu kifua cha Steve.
"Jambo la tatu,nimekubali
kwa moyo wote ukaonane na
Vicky ila nakuomba mpenzi
wangu fanya kila linalowezekana
kuhakikisha haufanyi naye
mapenzi.Yule ni kahaba na hatuna
uhakika kama yuko salama au la,hivyo nakuomba mpenzi wangu
fanya kila linalowezekana upate
taarifa unayoihitaji bila kufanya
naye mapenzi.Mashine hii ni
yangu peke yangu na sitaki
kuchangia na mwanamke
mwingine yeyote"akasema Samira
huku akiupeleka mkono maeneo
ya ikulu ambako tayari kulianza
kuchachamaa.Wakatazama na
macho yao yalionyesha wazi kuna
kitu wanakihitaji na bila hiyana
kila mmoja akawa tayari kumpatia
mwenzake kile
anachokitaka.Wakaingia katika
mtanange mkali wa dakika ishirini
halafu wakaingia bafuni kujiweka
safi
"Steve wewe ni wa kipekee
sana.Unanifikisha mahali ambalo hakuna mwanaume aliyewahi
kunifikisha"akasema Samira
wakati wakioga
"Samira ulinipa kazi ya
kumfahamu mke wa David"
akasema Steve
"Enhee! umegundua nini?
"Mke wa David anaitwa
Veronika na si Elizabeth" akasema
Steven na mshangao ukaonekana
usoni kwa Samira
"Who is Elizabeth?akauliza na
wote wakabaki
wanatazamana,baada ya muda
akasema
"Anyway ,tuachane naye na
mambo yake lakini mstuko
alioupata David baada ya
kupigiwa simu na Elizabeth ni
mkubwa na ndiyo maana nikataka nimfahamu ni nani huyo Elizabeth
aliyemstua David kiasi kile"
akasema Samira.Wakamaliza
kuoga wakajiandaa na kuondoka

***************

Saa kumi na moja kasoro
dakika nane ,Steve akarejea katika
makazi yao.Graca ambaye ndiye
aliyemfungulia geti akapatwa na
mshangao baada ya Steve kushuka
garini
"Steve is that you?!!akauliza
kwa mshangao
"Yeah its me”akajbu Steve
huku akitabasamu
"Ama kweli dunia ina
maajabu.Uliondoka mwingine na
umerejea mwingine kabisa.Steve wa asubuhi ni tofauti na Steve wa
jioni hii" akasema Graca na Steve
akamsogelea karibu
"No body is ugly.Kila kitu
kinawezekana Graca.Hebu
jitazame ,Graca wa jana si Graca
wa leo.Umependeza kumzidi hata
binti mfalme.Graca u mzuri
mno.Unao uzuri ambazo si rahisi
kuuelezea.Kila nikuonapo mwili
wangu wote hunisisimka .Niahidi
kwamba tutapata nafasi ya
kuzungumza "akasema Steve
akiwa katika hali ya utani
"Go to hell...!! akasema Graca
na kuingia ndani Steve akamfuata
.Graca akaenda kuufungua mlango
wa chumba cha Elvis akaingia
ndani Elvis we have a visitor from
Hollywood"
"From Hollywood? Elvis
akashangaa na mara Steve
akaingia mle ndani
"Wow !akasema Elvis
akimshangaa Steve kwa namna
alivyobadilika.Steve akamuomba
Graca awapishe kwa ajili ya
maongezi muhimu
"Elvis kazi imeanza" akasema
Steve
"Kila kitu kimekwenda vizuri
na jioni ya leo ninakwenda
kuonana na Vicky na ndiyo maana
nimefanya maandalizi haya ili
niweze kuendana na Steve yule
ambaye Vicky ameelezwa kuwa ni
bilionea." kazi nzuri sana
Steve.Sikufanya kosa
kukushirikisha katika mpango
huu. Kila kitu kitakwenda kama
tulivyokipanga hakuna
mabadiliko.Utaingia hotelini
utakutana na Vicky na utakapoona
n wakati muafaka kwa mimi
kuingia utanijulisha halafu
nitaingia kama mzimu humo
chumbani na shuguli itaanzia
hapo.Umekumbuka kununua simu
mpya pamoja na kusajili laini za
simu kwa ajili ya mawasiliano?
“Kila nitu nimekifanikisha
usihofu Elvis"
"Good"akasema Elvis na
ukimya mfupi ukapita,Steve
akauliza Elvis are you sure you want
to do this?
"Yes I want.This is what I died
for.Pascal ni mmoja wa watu
wanaojihusisha na mtandao huu
ambao tunakwenda kuufyeka kwa
hiyo tukimpata utakuwa ni
mwanzo mzuri wa kuufahamu
mtandao wote.Usiwe na wasi wasi
Steve siwezi kugundulika”
"Okay then,let's do
this”.Tukifanikiwa kumpata Pascal
tutamuhifadhi wapi? na vipi
kuhusu Vicky tutaondoka naye au
tutamuacha aende zake?akauliza
Steve
"Vicky hatuwezi
kumuacha,tutaondoka
naye.Tunayo nafasi ya kutosha
hapa kwa ajili yao ,tutatengeneza chumba maalum kwa ajili ya
mahojiano.This house will be like
hell.Tayari ninaanza kuvuta
harufu ya damu.Damu yote
iliyomwagika toka kwa watu
wasio na hatia kwa sababu ya
silaha zinazouzwa na genge hili
itawarudia .Its time to make them
pay" akasema Elvis
"Yeah,let's make them pay !!
akasema Steve

*****************

Tayari jua limekwisha zama
na taratibu kiza kimeanza
kuchukua nafasi.Sauti ya mlio wa
kengele ya mlango ilimstua
Patricia toka usingizini ,akajizoa
zoa hapo kitandani na kwenda kuufungua akakutana na Juliana
akiwa na sinia lenye matunda
'Juliana karibu dada yangu"
"Ahsante sana .Unaendeleaje
Patricia?
"Ninaendelea vyema.lazima
nijikaze nikubaliane na hali
halisi.Elvis is gone and will never
come back.Hata kama nikiendelea
kulia machozi usiku na mchana
haitanisaidia.I must find strength
to move one.Vipi wewe
unaendeleaje na maandalizi ya
mazishi ya baba yako?
"Kwa sasa kinachoendelea ni
vikao vya ndugu.Baba na ndugu
zake walikuwa na ugomvi wa
muda mrefu na hakukuwa na
maelewano baina yao.Mama
anaufahamu mgogoro huo na hakutaka baba azikwe hapa
Tanzania ni mimi niliyeshinikiza
tuje kumzika baba mahala
alikozaliwa hivyo ikatulazimu kuja
kwanza kuonana na ndugu zake ili
tuweze kushirikiana katika
mazishi.Hii ni njia moja wapo ya
kuzimaliza tofauti zao na kuwaleta
pamoja kama ndugu.Tuachane na
hayo pole sana kwanza kwa
kuondokewa na mama.Sikujua
kama mama yako naye alikwisha
fariki hadi nilipoelezwa na watu
wanaokaa katika ile nyumba yenu
ya zamani nilipokwenda
kukuulizia leo asubuhi" akasema
Juliana
"Mama alifariki kitambo
sana.Alipata ajali ya gari.Mpaka
leo ninajuta kwa nini nilimnunulia gari.kama nisingefanya hivyo
pengine mpaka leo angekuwa
bado hai" akasema Patricia na
kunyamaza akainamisha kichwa
"Pole sana Patricia"
"Ahsante sana dada
Juliana.Nilipotoka masomoni nje
ya nchi nilimletea mama gari kwa
ajili ya shughuli zake za kilimo na
biashara .Nilimwekea dereva wa
kumuendesha na kumpeleka
kokote anakotaka kwenda.Kwa
bahati mbaya walipata ajali na
wote wakafariki"
"Mwenyezi Mungu mwingi
wa rehema ampumzishe sehemu
salama.Samahani sana Patricia
sikuwepo karibu nawe wakati
huo"akasema Juliana Ni kweli Juliana nilikuwa na
wakati mgumu mno.Hata hivyo
ninamshukuru Elvis ambaye
alisimama nami wakati ule.Nini
hasa kilitokea dada Juliana hadi
ukaondoka nchini ghafla bila hata
kuniaga mdogo wako?
Juliana akainamisha kichwa
kwa swali lile la Patricia
"Kuna mambo makubwa
yalinipata mdogo wangu na
kunifanya niondoke nchini kimya
kimya na bila hata kuwaaga watu
wangu wa muhimu kama
wewe.Nitakueleza siku nyingine
nini hasa kilitokea lakini fahamu
tu kuwa yalinipata mambo
makubwa.Nisingeweza kuondoka
bila kukuaga mdogo wangu lakini
ilinilazimu kufanya hivyo.Utanisamehe sana kwa
hilo.Vipi kuhusu maisha yako toka
tulipoonana mara ya
mwisho?Nakumbuka ulikuwa
bado shuleni Tanga"akauliza
Juliana
“Nimepitia mengi
dada.Nimekutana na mengi
magumu lakini nashukuru
sikuacha kumtegemea Mungu
ambaye alinipa nguvu za
kuyakabili yote niliyokutana
nayo"akasema Patricia na kuanza
kumsimulia Juliana maisha yake
tangu alipokuwa shuleni mkoani
Tanga.

***************** Elvis ni wakati wa mimi
kuanza kujisogeza eneo la
tukio.Unaniruhusu niondoke? Vipi
kuhus muonekano wangu
naonekana kama mfanya biashara
bilionea?akauliza Steve
"Uko sawa kabisa supa
bilionea Steve.Unaweza kuondoka
ila nakukumbusha umakini
mkubwa sana unatakiwa
hatutakiwi kuharibu operesheni
hii muhimu mno kwetu"
"Usihofu Steve.Kila kitu
kitakwenda kama kilivyopangwa"
akasema Steve kisha wakaagana
akaingia katika gari na
kuondoka.Baada ya Steve
kuondoka Elvis akamfata Graca
jikoni alikokuwa akiandaa chakulana kumtaka wakazungumze.Graca
akaacha kazi zote akamfuata Elvis
"Graca nimekuita kukueleza
kwamba ile kazi ambayo
ilinilazimu nife ili niifanye
inakwenda kuanza usiku wa leo"
akanyamaza na kumtazama Graca
ambaye uso wake ulionyesha wasi
wasi
"Nimeona nikujulishe
mapema ili uelewe kwamba
mambo yanaanza .It’s going to be
taugh but you dont have to worry
,you are well
protected"akanyamaza tena
kidogo halafu akaendelea
"Baadae usiku wa
leo,tunategemea kuwaleta hapa
ndani watu wawili kwa ajili ya
mahojiano hivyo usistuke.Kwa kawaida tunapomfanyia mtu
mahojiano huwa tunabadilika
kidogo na kuwa wakali ili tuweze
kupata taarifa
tunazozihitaji.Wengine huwa
wabishi wa kutupa taarifa hivyo
hulazimika kutumia nguvu na
mbinu mbalimbali za kuhoji ili
kuweza kuipata taarifa
hiyo.Utakaposikia mtu akipiga
ukelele mkubwa usiogope ujue
tuko kazini.Ntakuomba pia wakati
haya yote yakifanyika ujifungie
chumbani kwako.Umenielewa
Graca?
"Nimekuelewa Elvis ila sina
cha kusema.This is what you died
for so you have to do it.Kwa
upande wangu usiwe na wasi wasi
kabisa na kama utakumbukaniliwahi kukueleza kuwa napenda
sana kuwa mpelelezi siku moja"
akasema Graca na Elvis
akatabasamu
"Good to hearthat.Napenda
ujasiri wako.Kuhusu kazi hii
nakuomba itoe kabisa
mawazoni.Ni kazi iliyojaa hatari
nyingi"akasema Elvis na kwenda
kumuelekeza vyumba viwili
ambavyo wangevitumia kwa usiku
ule ili aanze kuviandaa
"Elvis"akaita Graca
" Unasemaje Graca?akauliza
"Una uhakika huko unakotaka
kwenda hakutakuwa na tatizo
lolote?Hakuna anayeweza
kukutambua? Usihofu Graca.Hakuna
kitakachoharibika"akasema Elvis
na kuingia chumbani kujiandaa


*****************

Juliana alihisi kutetemeka
kwa ndani baada ya Patricia
kumaliza kumsimulia hadithi ya
maisha yake katika kipindi
ambacho hakuwepo
nchini.Akashusha pumzi halafu
akainuka akatoka mle chumbani
baada ya dakika tano akarejea
akiwa na chupa ya mvinyo
"Unatumia
mvinyo?akamuuliza Patricia
"Ndiyo ninatumia tena
nahitaji mvinyo mkali" This is Martina 76.Moja kati
ya mvinyo mkali kabisa”akasema
Juliana na kummiminia Patricia
katika glasi wakaanza kunywa
.Ilimlazimu Patricia afumbe
macho kutokana na ukali wa
mvinyo ule.Baada ya muda macho
ya Juliana yakajaa machozi
"Patricia nashindwa nianzie
wapi.Sijui niseme kitu gani.Haya
yote uliyonieleza ni ya
kweli?akauliza Juliana huku
akifuta machozi
"Yote ni kweli tupu
Juliana.Hayo ndiyo maisha
niliyoyapitia toka wakati ule hadi
hii leo"
"How the world could be so
cruel?akasema Juliana Dunia si mbaya dada
Juliana,walimwengu ndiyo
wanaoifanya dunia ionekane
mbaya na kuwafanya wengine
wakate tamaa hata ya kuendelea
kuishi.Mungu alimpa mwanadamu
dunia yenye uzuri usioelezeka
lakini tumeiharibu sisi
wenyewe"akasema Patricia
"Patricia imeniumiza sana
kusikia kwamba mdogo wangu
Godson ndiye chanzo cha haya
yote yaliyokupata.Kama
asingekurubuni na kukupa
ujauzito haya
yasingekukuta.Imeniumiza mno
na ninatamani angekuwepo leo hii
ashuhudie kitu alichokufanyia"
akasema Juliana kwa masikitiko
makubwa Yuko wapi Godson?akauliza
Patricia.Juliana akafuta machozi
na kusema
"He's dead "
"Dah ! pole sana Juliana .Nini
kilimuua?
"Ni hadithi ndefu Patricia ila
kwa ufupi tu ni kwamba Godson
aliuawa"
"Pamoja na yote
aliyonitendea lakini alikuwa ni
kijana mwenye roho
nzuri.Naamini waliofanya ukatili
huu kwa sasa wanaozea gerezani"
Juliana akainamisha kichwa
akaonekana kuwa na mawazo
mengi
"Godson was a good
boy.Hakustahili kudhulumiwa
uhai wake kikatili namna ileDada Juliana nini hasa
kilitokea na kusababisha hao watu
wamuue?Aliwafanya nini?Who
killed him?akauliza
Patricia.Ilimchukua Juliana muda
kidogo kujibu swali lile
" He was shot fifty
times.Mwili wake wote ulijaa
matundu ya risasi.Alikatishwa
uhai kikatili mno.Hakustahili
unyama ule mkubwa"
"Oh my God! akasema Patricia
kwa masikitiko
"Waliofanya unyama huo ni
akina nani?naamini watakuwa
tayari wanaozea gerezani"
Juliana akafuta machozi na
kusema Its commplicated
Patricia.Let's not talk about that
unsolved case"
"Dada Juliana unaonekana na
wewe pia umepitia mambo
magumu sana"
"Nimepitia kupindi kigumu
sana Patricia.Nitakueleza mambo
niliyopitia wakati mwingine lakini
naomba ufahamu kwamba sina
cha kufanya kukutibu kidonda
chako ambacho chanzo chake ni
ndugu yangu .Nimeumizwa mno
na sij..........."
"Dada Juliana"Patricia
akamkatisha
"Usikwazwe na mambo haya
yaliyotokea ambayo tayari
yamekwisha kuwa
historia.Matatizo ni sehemu ya maisha yangu na nimekwisha
zoea.Ninashukuru hata hivyo
nimepitia magumu hayo na
nimeimarika japo kwa hili la
kuondokewa na Elvis limenifanya
niwe dhaifu sana.He was
everything to me" akasema
Patricia
"Ninatamani ningepata bahati
ya kuonana na Elvis ana kwa ana
.Wanaume kama yeye
hawapatikani tena katika sayari
yetu hii.Patricia pamoja na huzuni
ulizonazo lakini unapaswa
kumshukuru sana Mungu kwa
kukupatia mwanaume kama Elvis
japo umeishi naye kwa kipindi
kifupi.Inanishangaza sana kwa
nini aliamua kufanya kazi hii ya upelelezi?Hukuwahi kumshauri
atafute kazi nyingine?
"Nilianza kumshauri toka
tukiwa shuleni lakini inaonekana
kazi hii ilikuwa damuni mwake na
hakutaka kusikia ushauri wa mtu
yeyote."akasema Patricia na
ukimya ukatawala mle
chumbani.Baada ya muda Juliana
akasema
"Laiti angekuwa hai
ningeweza kumuomba anisaidie
kutafuta watu waliomuua Godson"
"Elvis alikuwa mahiri sana
katika kazi yake na angeweza
kuwapata.Mpaka leo wauaji wa
Godson hawajulikani?
Kabla Juliana hajajibu swali
lile ujumbe mfupi ukaingia katikasimu yake akausoma kisha
akasema
"Patricia tutazungumza
wakati mwingine,tunatakiwa
kwenda kuonana na ndugu za
baba usiku huu kwa ajili ya kujua
wamefikia maamuzi yapi katika
kikao chao.Nakuomba usihisi
upweke humu ndani kuna
wahudumu ambao
watakuhudumia kwa kila
ukitakacho.Jisikie
nyumbani"akasema Juliana
"Usihofu Juliana hapa ni
nyumbani.Kabla hujaondoka
nahitaji simu kuna mtu nataka
kuwasiliana naye.Simu yangu
haina chaji hata kidogo"
“Simu utapata
usijali.Nitakaporejea nitakuja kukufahamisha nini
kimeafikiwa"akasema Juliana na
kutoka.Baada ya dakika tano
akafika mtumishi wa ndani akiwa
na simu akampatia Patricia
akaweka laini yake na kuzitafuta
namba za Dr Steven washington
akampigia
"Dr Patricia" akasema Dr
Steven akionekana
kustuka.Hakuwa ametegemea
kupigiwa simu na Patricia
"Dr Washington habari
yako?Unaendeleaje?
“Mimi ndiye ninayepaswa
kukuuliza unaendeleaje?
"Ninaendelea vyema .Si rahisi
ila ninajitahidi kukubaliana na
kilichotokea na kuilazimisha akili
yangu izoee ili maisha yaendelee"akasema Patricia na ukimya
ukapita
"Patricia pole sana.Sifahamu
niseme neno gani zaidi ya hilo
ambalo linaweza likakupa faraja
kwa wakati huu mgumu.Lakini
naomba utambue kwamba msiba
huu ni wetu sote.Tumeumia kama
ulivyoumizwa wewe.Muda
wowote utakaohitaji rafiki,mtu wa
kuzungumza naye,mtu wa kulia
naye,mimi nipo hapa" akasema Dr
washington kwa sauti ya upole
"Nashukuru sana Dr
Washington.Nimekupigia tu
kukufahamisha kwamba
ninaendelea vyema"
"Nimefurahi sana kuisikia
tena sauti yako Patricia.Uko wap........"Kabla Dr Washington
hajamaliza kuuliza simu ikakatwa.
"I don’t know why I called
him but I need some one to
comfort me,to tell me it'll be ok.I
need to be in strong hands right
now,I need...."
Patricia akaondolewa
mawazoni baada ya siku yake
kuita .Mpigaji alikuwa ni mke wa
rais.Haraka haraka akaipokea
"Shikamoo mama"akasema
"Marahaba Patricia
unaendeleaje?
"Ninaendelea vizuri
mama.Vipi wewe unaendeleaje?
"Ninaendelea vyema pia.Hofu
yetu ni juu yako”
"Msihofu mama.Suala hili
litapita na nitakuwa salama" .Nimekutafuta kuanzia
asubuhi bila mafanikio,simu yako
haikuwa ikipatikana.Nilitaka
nikufahamishe kwamba
tumejadiliana mimi na rais na
tumeona kwamba itakuwa vyema
kwa wakati huu ambao bado
unaomboleza kifo cha mumeo basi
uje ukae nasi ikulu.Patricia wewe
ni daktari wangu,ni mwanangu na
tunakuchukulia ni sehemu ya
familia yetu kwa hiyo tunataka
uishi nasi hapa japo kwa muda
hadi hapo utakapokuwa umerejea
katika hali ya kawaida.Uliwahi
kunieleza kwamba wazazi wako
wote wamekwisha fariki na sasa
baada ya kuondokewa na
mume,unahitaji kuwa karibu na
watu ambao watakufariji na kukusaidia kukivuka kipindi hiki
kigumu.Ninakuomba ukubali kuja
kuishi nasi hapa na tutafanya kila
lililo ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha kwamba unakuwa na
furaha na amani..unasemaje
kuhusu ombi letu hilo? akauliza
mke wa rais
Patricia akashusha pumzi na
kujibu
"Mama ninawashukuru sana
wewe na mheshimiwa rais kwa
kuwa nami katika kipindi hiki
kigumu.Sina cha kuwapa zaidi ya
kuwaombea kwa Mungu awajalie
baraka nyingi na maisha marefu
yenye furaha na amani.Kuhusu
ombi lako siwezi kulikataa mama
kwani kwa hivi sasa nahitaji mno
faraja.Nimelipokea kwa mikono miwili.Niko tayari kuja kuishi
nanyi ila ninaomba muda kidogo
ili niweke sawa mambo yangu"
"Patricia ahsante sana kwa
kukubali ombi letu.Muda wowote
utakapokuwa tayari unitaarifu ili
nitume watu waje kukuchukua "
"Nashukuru sana
mama.Nifikishie shukrani zangu
kwa mheshimiwa rais”
"Nitazifikisha .Ila nakuomba
muda wowote ukihitaji kitu
chochoe nipigie simu.Wewe ni
mwanetu na tutakufanyia
chochote utakachokitaka"
"Ubarikiwe sana mama"
"Haya kwa heri Patricia.Uwe
na siku njema" akasema mke wa
rais na kukata simu ."Inanipa faraja sana kuona
bado wapo watu wema ambao
wamesimama nami kwa kila hali
ninayopitia na wako tayari
kufanya lolote lililo ndani ya
uwezo wao kuhakikisha kwamba
ninakuwa na furaha tena.Nina
jiona ni mwenye bahati sana kuwa
na watu hawa wachache ambao
hawaniachi na katika gumu lolote
ninalopitia tunafumba macho na
kuomba pamoja"akawaza Patricia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom