Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 48

Steve aliwasili Samawati
beach Hotel saa mbili na robo za
usiku.Kabla hajashuka garini
akampigia simu Elvis na
kumjulisha kwamba tayari amekwisha fika na anajiandaa
kushuka garini kuingia
hotelini.Taratibu akashuka garini
na kuangaza kila upande kuhakiki
usalama kwake halafu akaanza
kupiga hatua kuelekea ndani
hotelini.Watu walikuwa wengi
kiasi .Alifika mapokezi akawakuta
akina dada wanne wenye sura za
tabasamu ambao walimpokea kwa
uchangamfu
mkubwa.Alijitambulisha kwao
kama Charles Makebu mgeni wa
chumba namba 208.Akahakikiwa
katika kompyuta halafu akapewa
sehemu ya kusaini.Kabla
hajapelekwa chumbani kwake
akawaomba wahudumu
"Kuna wageni wangu
watakuja baadae.Mmoja ni mwanamama anaitwa Vicky.Huyu
nitakuwa naye hapa kwa usiku wa
leo.Wengine ni Erick Mbaga na
Pascal sichoma.Ninaomba
watakapofika wageni hawa
waruhusiwe kuja moja kwa moja
chumbani kwangu bila
kusumbuliwa.Kuna tatizo lolote
Anna? akauliza Steve huku
akilitaja jina la yule mwanadada
lililokuwa katika kitambulisho cha
kazi alichokivaa.Kabla Anna
hajajibu kitu Steve akaingiza
mkono mfukoni akatoa bunda la
noti na kuwapatia kama ahsante.
"Hakikisheni wageni wangu
wanafika chumani kwangu haraka
mara tu watakapofika”akasema
huku akimkonyeza Anna na kuongozana na muongoza wageni
hadi chumbani kwake.
"Chumba kizuri sana
nimekipenda" akasema Steve na
baada ya yule muhudumu kutoka
Steve akachukua simu akampigia
Elvis
"Tayari niko chumbani
namsubiri Vicky ambaye atawasili
hapa muda wowote.Ukifika
mapokezi utajitambulisha kwa
jina la la Erick Mbaga na
utaruhusiwa kuelekea moja kwa
moja chumbani 208 nilipo"
"Sawa Steve.Mimi ninajiandaa
nitoke hapa nyumbani.Nina
uhakika hadi nitakapofika hapo
hotelini tayari Vicky atakuwa
amefika.Kama kutatokea
mabadiliko yoyote naomba unijulishe haraka sana tafadhali"
akasema Elvis
"Sawa Elvis nitakujulisha
"akajibu Steve na kukata simu
Steve akavua koti na shati
akabaki kifua wazi.Alikuwa na
mwili uliojengeka vyema na
uliojaa michoro mingi.Shingoni
alikuwa na mikufu mitatu
mikubwa ya dhahabu.Akafungua
friji na kutoa chupa ya mvinyo
akaketi mezani na kuanza kunywa
Saa tatu na dakika kumi,gari
la kifahari likawasili pale hotelini
na akashuka Vicky mwanamke
mwenye uzuri wa shani japo ana
sifa ya ukahaba.Usiku huu alikuwa
amevaa gauni refu jeupe lenye
mpasuo mrefu hadi pajani.Vidole
vyake vya mikono vilijaa pete za thamani zenye kumemremeta kila
pale zilipopigwa na
mwanga.Vicky alitembea taratibu
kwa madaha kama mtu asiyetaka
kukanyaga ardhi hadi alipofika
mapokezi ambako ghafla kukawa
kimya ,wote waligeuka
kumtazama.Akatabasamu na
kuwatazama kisha akajitambulisa
kwamba ni mgeni wa chumba
208.Bila kupoteza muda
akaongozwa kuelekea chumba
hicho .
Steve akiwa sofani akitazama
muziki huku akiburudika kwa
mvinyo,mara kengele ya mlangoni
ikalia akainuka na kwenda
kuufungua mlango na kujikuta
akiachia tabasamu kubwa kwa
kile alichokiona mlangoni Angel from Mars…..”
akasema Steve kwa furaha kana
kwamba anafahamiana kwa muda
mrefu na Vicky
“Karibu sana malaika wangu"
akasema Steve na kumkumbatia
Vicky kisha akamshika mkono na
kumuongoza hadi sofani.
"How're you Vicky?akauliza
"I'm fine.How're you?
"As you can see ,I'm more
than fine" akasema Steve huku
akitoa kicheko.
"Nimefurahi sana kukutana
nawe Vicky.Unatumia kinywaji
gani?
Vicky akaishika chupa ya
mvinyo aliokuwa anatumia Steve
na kusema
"Nitatumia hii" Steve akammiminia mvinyo
katika glasi
"Sorry I'm late.Foleni ilikuwa
ndefu sana"akasema Vicky baada
ya kunywa funda moja la mvinyo
"Usijali Vick,kwa vile umefika
hakuna kilichoharibika.Serikali
ina mipango gani ya kupunguza
kama si kumaliza kabisa tatizo hili
la msongamano katika jiji hili ?
Kila mara nijapo nakuta hali ni ile
ile.Hawajui kama suala hili lina
athari kubwa kiuchumi kwa watu
kutumia muda mwingi katika
foleni? akauliza Steve
"Juhudi za kila aina
zinafanyika kupunguza
msongamano katika jiji hili lakini
bado hazijaonekana kuzaa
matunda.Bado wanaendelea kubuni njia nyingine mbali mbali
za kukabiliana na tatizo
hili.Umetokea nchi gani?akauliza
Vicky
"Kabla sijajibu swali
lako,ningependa
nijitambulishe.Naitwa
Steve.Napenda tuitane kwa
majina”akasema Steve na kunywa
funda moja la mvinyo
"Ninaishi Texas marekani ila
nina makazi yangu pia Afrika
kusini na London Uingereza.Hizi
zote ni sehemu ninakofanyia
biashara zangu.Nina uraia wa
Marekani lakini nyumbani ni hapa
Tanzania" akasema Steve na
kunywa funda lingine Unajishughulisha na
biashara gani Steve?akauliza
Vicky
"Nina biashara mbali
mbali.Nauza
magari,kompyuta,vipuri mbali
mbali vya magari na mashine,nina
migahawa pia"
"Oh! thats wonderfull.Kijana
mwenye haiba kama yako
nilitegemea angenieleza kwamba
anafanya biashara ya dawa za
kulevya"akasema Vicky na Steve
akaangua kicheko
"Hiyo ni dhana potofu
kwamba vijana wengi wa kutoka
dunia ya tatu wanaokwenda
kufanikiwa ughaibuni wanafanya
biashara ya dawa za kulevya.Mimi
nimefanikiwa bila kujihusisha na biashara hizo haramu.Ninazo
bashara zangu halali ninalipa kodi
na nimeajiri wengine pia kupitia
biashara zangu.Ninapata pesa
nyingi na ndiyo maana ninao
uwezo wa kujivinjari na malaika
kama wewe.Unajishughulisha na
nini hapa Tanzania?
"Ninafanya biashara ya hoteli
na mara moja moja nikiwapata
wanaume wenye pesa zao kama
wewe basi siwezi kuwakataa"
"Good.Nilimtuma binamu
yangu Samira anitafutie mrembo
wa kupitisha naye usiku wa leo na
akaniambia kwamba amekupata
kwa gharama kubwa.Sikujali
gharama kwani pesa kwangu si
tatizo ila nilihitaji sana kumuona
huyo malaika je anafanana na gharama zake.Baada ya kukuona
ninaona hata gharama ile bado
ndogo na nimekata shauri
nitakuongeza
nyingine.Sintautendea haki uzuri
wako bila kuongeza fedha zaidi."
"Steve you are so
sweet.Lakini kiasi kile
nilichopewa kinatosha sana
hakuna haja ya kuongeza tena
fedha nyingine" akasema Vicky
"Nitakuongeza Vicky and
please dont say no" akasema Steve
"Haya ahsante sana kwa
zawadi hiyo"akasema Vicky huku
akianza kumpapasa Steven
maungoni
"Samira aliniomba
nisithubutu kufanya mapenzi na
Vicky lakini sidhani kama nitaweza kwani litakuwa ni kosa
la jinai kumuacha malaika huyu
aende hivi hivi bila kumchezesha
gwaride hata la nusu saa.Gharama
kubwa imetumika kumleta hapa
hivyopesa ile haiwezi kupotea hivi
hivi lazima na mimi leo niingie
katika historia.I have to do it
quick" akawaza Steve
"Steve una kifua kizuri sana
.Nawapenda wanaume
waliojengeka miili kama wewe"
akasema Vicky huku akikipapasa
kifua cha Steve
"Basi leo tumekutana.Kama
wewe unapenda wanaume wenye
miili iliyojengeka mimi ninapenda
nawake wenye haiba kama
yako,mwili mwembamba,kifua
chenye kubeba chuchu ndogo zilizojaa kama zako,kiuno
chembamba lakini kilichobeba
mzigo mkubwa kwa chini na zaidi
sana weupe.Naamini usiku wa leo
utakuwa maridhawa kwetu”
akasema Steve naye akianza
kumfanyia Vicky
utundu.Haikuchukua muda mrefu
wakajikuta watupu na mtanange
ukaanza.
Ulikuwa ni mtanange mkali
uliodumu kwa dakika ishirini
.Wote walikuwa ni mafundi katika
mchezo huu na kila mmoja
alijaribu kumuonyesha mwenzake
ujuzi alionao.Kisha maliza
mzunguko huo Steve akaomba
waelekee bafuni kuoga kabla ya
kujiandaa na mtanange mwingineSteve you are amazing.Una
ujuzi wa kiwango cha juu
sana.Huwa ninafurahi
ninapokutana na mwanaume
kama wewe mwenye ujuzi wa
mambo haya inakuwa ni raha
tupu.Wanaume wengine hata
kama amekulipa anataka
akutumie atakavyo lakini wewe
unanifanya nijisikie starehe
kubwa.Ninajihisi kufanya mapenzi
na si biashara.Ningejua kama uko
hivi hata malipo yako
nisingeyapokea" akasema Vicky
"Wanaume wengine akimpata
mwanamke ni kwa ajili ya
kutimiza haja zake akisahau
kwamba ili yeye astarehe vizuri
anapaswa kumfanya mwanamke
afurahie kitendo lakini ukifanya kwa pupa kwa vile umelipa fedha
hakuna starehe yoyote
utakayoipata" akasema Steve na
kumbusu Vicky ambaye tayari
alikwisha onyesha kuvutiwa sana
na Steve
"Vicky nimesahau kuchukua
mvinyo.Tunapopumzika katika
jakuzi lazima tuwe na mvinyo
pembeni.Ngoja nikaulete"
akasema Steve na kutoka mle
bafuni na haraka haraka
akachukua simu yake na
kumuandikia ujumbe Elvis
"It’s time"
Akautuma ujumbe ule na
kuchukua chupa ya mvinyo
akarejea bafuni wakaendelea
kuoga.
***************

Brigedia Frank aliwasili
katika makazi ya waziri mkuu
mstaafu David Sichoma kwa ajili
ya kikao muhimu kama
alivyotakiwa.Akapokewa na
muhudumu na kumkaribisha
sebuleni na baada ya dakika
chache David akatokea.Uso wake
haukuwa katika ile hali yake ya
kawaida.Akamsalimia Frank na
kumtaka waelekee katika chumba
cha mazungumzo ya faragha
"Frank kwanza kabisa
samahani sana kwa usumbufu
mkubwa niliokupa.Nimelazimika
kukuita usiku huu kwa ajili ya
kuzungumza mambo machache muhimu"akasema David na
kunyamaza
"Usijali David hujanisumbua
kabisa"
"Jambo la kwanza ambalo
nimekuitia hapa Frank ni kwamba
nimekutana na Makwa Tusangira
leo asubuhi alikuja kunitaarifu
kuhusu maendeleo ya ule mpango
wetu.Amenieleza kwamba kila
kitu kinakwenda vyema na kesho
ijumaa watatangaza mkutano wa
hadhara siku ya jumapili na
kuwataka wafuasi wao wafike
kwa wingi bila kukosa.Bado
hawajapata kibali kutoka jeshi la
polisi cha kufanya mkutano lakini
kwa kuwa lengo ni kuanzisha
vurugu basi mkutano utafanyika
na hapo ndipo vurugu ztakapoanzia.Wanachokihitaji ni
kupata fedha za awali ili
ziwasaidie katika maandalizi
hivyo kesho shughulikia suala la
fedha waipate.Tutazungumza na
Makwa asubuhi kuhusu fedha hizi
ziingie katika akaunti gani.Hilo ni
la kwanza"
"Naona mambo yanazidi
kupamba moto."akasema Frank
"Mambo yanazidi kukolea
Frank.Kila kitu kitakwenda kama
tulivyokipanga.Palipo na fedha
hakuna
kinachoshindikana"akasema
David na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
"Jambo la pili,Makwa
aliniletea malalamiko kwamba
Pascal amemfuata ofisini kwake asubuhi ya leo na kumtaka ampe
ufafanuzi kuhusiana na kiwango
kile cha fedha ambacho
wanakihitaji kugharamia
operesheni mafuta yetu.Kama
utakumbuka jana tukiwa katika
kikao alihoji kuhusiana na kiasi
cha fedha walizozihitaji akina
Makwa na hakuridhika na leo
amemfuata kutaka ufafanuzi
kuhusiana na fedha hizo.Makwa
hajakifurahia kitendo
alichokifanya Pascal na ndiyo
maana akaja kuniletea
malalamiko.Hata mimi
sijakifurahia kitendo hicho kwani
kinaonyesha wazi kwamba
hatuaminiani na hii ni mbaya
kama tutashindwa
kuaminiana.Fedha hizi ni nyingi sana kama nilivyokueleza
jana.Zitatumika,zitabaki na sote
tutafaidika." akasema David
"Dah ! Nimestuka sana kwa
hili alilolifanya Pascal.Kwa nini
afanye jambo kama hili? Halafu
amefanya kimya kimya bila hata
kunishirikisha kwani katika
mambo yake mengi huwa
ananishirikisha lakini nashangaa
katika hili
hajanihusisha.Ninavyomuelewa
Pascal bado ana wasi wasi nawe
kwani hajawahi kufanya kazi
nawe na ndiyo maana ameamua
kwenda kwa Makwa kujiridhisha
kuhusu kiwango kile cha fedha”
akasema Frank
"Kwa nini awe na wasi wasi
na mimi wakati wewe uliyenishirikisha katika mpango
huu hauna hata chembe ya wasi
wasi nami?
"David suala hili naamini
limekukera sana lakini nakuahidi
kwamba nitazungumza naye na
kumuelewesha kwamba
anapaswa akuamini kwani wewe
ni mtu mwenye mchango mkubwa
sana katika operesheni
yetu.Nitamkanya asifanye jambo
lolote la kijinga linaloweza
kuharibu operesheni yetu"
akasema Frank
“Itakuwa vyema kama
utazungumza naye kwani sote
tunapawa kuwa katika ukurasa
mmoja.Tukianza kutofautiana
tutashindwa kufikia
malengo.Mwambie asiwe na wasiwasi na mimi hata kidogo na
kama kuna kitu kina mashaka
anifuate na nitampa ufafanuzi
kuliko kufanya kama hivi
alivyofanya leo.Wanasiasa wale
tunawategemea sana kwani bila
wao kuanzisha vurugu mpango
wetu hautafanikiwa.Kutokana na
kile alichokifanya Pascal walikuwa
wameweka azimio la kuachana na
operesheni hii lakini
nimemuomba Makwa wasifanye
hivyo.Kwa sababu ananiheshimu
amekubali kuendelea na mipango
yetu lakini Pascal lazima aonywe
ama sivyo anaweza akaharibu kila
kitu" akasema David
"Nimekuelewa David niachie
suala hilo,nitakaa na Pascal nitamuonya na kumkanya
asirudie tena"
"Good” akasema David na
baada ya sekunde chache akasema
"Suala la tatu nataka
kufahamu jambo moja"
"jambo gani David?
"Tafadhali naomba unijibu
bila kunidanganya.Unamfahamu
Elizabeth?
"Elizabeth yupi?Kuna
Elizabeth wengi sana
ninaofahamiana nao"
"Madam Elizabeth mke wa
Deusdedith"
Frank akawa kimya
akitafakari kisha akasema
"Hapana simfahamu huyo
Elizabeth wala huyu mume wake
Deusdedith.Ni akina nani hao? David akashusha pumzi na
kumtazama Frank halafu akasema
"Are you sure?
"Yes I'm sure.Siwafahamu
watu hao kabisa.Kwa nini
umeuliza? Ni akina nani
hao?akauliza Frank
"It's nothing.Nilitaka tu kuwa
na uhakika kama unawafahamu"
"Hapana siwafahamu”
akasema Frank
"Ok sawa.Nashukuru Frank
kwa kufika kwako.Sina
mazungumzo mengi usiku wa leo
kwani ninategemea wageni fulani
wa familia usiku wa leo hivyo
tutazungumza kwa kirefu zaidi
siku ya kesho kwani tutakuwa na
kikao jioni.Naomba uyafanyie kazi
hayo niliyokueleza" akasema David na kuagana na Frank
akaondoka
"Siamini kama safari hii
nimekutana na watu wanafiki
kiasi hiki.Frank anakana kabisa
kumfahamu Elizabeth wakati
mwenyewe amekiri kuwa Frank
ni mtu wake na anasimamia
biashara yao ya silaha.Ameona
ugumu gani kunieleza kuwa
anamfahamu Elizabeth?Hii tayari
inanipa picha kwamba watu hawa
si wazuri hata kidogo.Huku
nilikoingia safari hii nimekosea
sana.Hawa si watu wazuri kufanya
nao jambo kubwa kama hili la
mapinduzi.Napaswa kuwa makini
mno katika suala hili kwani kuna
kila dalili mambo yanaweza
yasiende kama tulivyopanga na heshima yangu
ikashuka.Nimegundua timu hii
imejaa wanafiki na watu wenye
tamaa.Lazima nianze kuchukua
tahadhari mapema" akawaza
David
"Nimekasirishwa sana na
kitendo cha Frank kukana
kumfahamu Elizabeth hadi
nimesahau kumuuliza kuhusu
Vicky.Laiti ningekuwa na njia ya
kujinasua kutoka katika mpango
huu ningefanya hivyo lakini siwezi
kujiondoa na kuyaacha mamilioni
yale hivi hivi.Lazima nihakikishe
nimechota kiasi cha kutosha ndipo
nifikirie namna ya
kujiondoa"akawaza David
"David amefahamu vipi kama
ninafahamina na Elizabeth?akajiuliza Frank akiwa
garini baada ya kuondoka
nyumbani kwa David
"Lazima wanafahamiana na
ndiyo maana Elizabeth akanitaka
nimjumuishe David katika
mpango huu wa mapinduzi na
akapendekeza yeye ndiye awe rais
baada ya mapinduzi
kufanyika.Kwa nini alitaka kujua
kama ninamfahamu
Elizabeth?Ingemsaidia nini akiju
akama mimi tunafahamiana?
Frank akaendelea kujiuliza
" Elizabeth na mumewe Deus
ni wakuu wangu katika biashara
kubwa ya silaha ambayo ni ya siri
sana na David hapaswi kufahamu
chochote kuhusu biashara
hii.Sifahamu yeye na Elizabeth wana mahusiano gani lakini ni
wajibu wangu kumlinda madam
Eliza kwa kila namna
ninavyoweza.Hadi akauliza swali
lile kama ninamfahamu Elizabeth
lazima kuna kitu amekifahamu
kuhusu mimi na Elizabeth. "
akawaza Frank


****************

Steven na Vicky walitoka
bafuni wakaenda kitandani wote
wakiwa watupu.Waliendelea
kunywa mvinyo huku
wakichezeana kimahaba
wakijiandaa kwa ajili ya raundi ya
pili. Vicky unaonaje endapo mimi
na wewe tukaanzisha mahusiano
ya kudumu?Una kila kitu
ninachokihitaji kwa mwanamke
na hali kadhalika wewe pia
umeonyesha kuvutiwa
nami.Ninaamini tukiwa wapenzi
tutakuwa na furaha sana.Hebu
tazama hatujawahi kuonana
tumekutana kwa muda mfupi tu
uliopita lakini tumezoeana kama
vile ni watu tunaofahamiana kwa
miaka mingi.Unasemaje kuhusu
wazo langu? akauliza Steve huku
akitabasamu na kunywa funda la
mvinyo.
"Steve wewe si mwanaume
wa kwanza kuniambia jambo
kama hilo.Nimekutana na
wanaume wengi ambao wametakakuanzisha mahusiano ya kudumu
nami.Kwa bahati mbaya I'm not
looking for a serious relationship.
Nina kila kitu ninachokihitaji
katika maisha.Nina fedha,nina
mali nina uwezo wa kufanya
chochte mahala kokote ili mradi si
kuvunja sheria.I want to enjoy
life.Sitaki kuwa chini ya
mwanaume yeyote yule.Starehe
yangu ni kuwa na wanaume
tofauti tofauti.."
"Mpaka lini utaishi maisha
hayo Vicky?
"Steve umenileta hapa kwa
gharama kubwa kwa ajili ya
kustarehe nami.Naomba
tusipoteze muda kuyachunguza
maisha yangu.Tufanye kile
ambacho kimetukutanisha hapa ambacho ni starehe.I'm all yours
tonight.Nitumie utakavyo na si
kutaka kunifahamu kuhusu
maisha yangu ambayo
hayatakusaidia kitu” akasema
Vicky akionekana kutopendezwa
na kitendo cha Steve kuanza
kuyachunguza maisha yake
"I'm sorry Vicky sikutaka
kukukera lakini tuna usiku mrefu
sana hivyo si vibaya kuwa na
mazungumzo mengine mbali
mbali kuhusu maisha na mambo
mengi tunayokutana nayo katika
harakati zetu za maisha" akasema
Steve huku akimpapasa Vicky
pajani.
"Usijali.Mimi ni wako kwa
usiku wa leo umenilipa
nikustareheshe kwa hiyo tulia nikuonyeshe raha za dunia"
akasema Vicky huku akiinuka na
kuanza kupiga magoti kisha kwa
kutumia mdomo wake akaanza
utundu katika ikulu ya Steve
ambaye alifumba macho kutokana
na raha aliyoipata.Ghafla Vicky
akageuza shingo na kutazama
mlangoni
"Steve nasikia kama mlango
unachokonolewa" akasema
"Usihofu Vicky hakuna
chochote .Tuendelee na starehe
zetu" akasema Steve huku
akizichezea nywele za Vicky
ambaye aliendelea na utundu
wake ikulu kwa Steve.Wakiwa
wamezama katika mahaba mazito
ghafla mlango ukafunguliwa na
mtu mmoja akaingia mle chumbani.Alikuwa amevaa suti
nyeusi na kofia pana ya mduara na
macho yake aliyafunika kwa
miwani myeusi.Kidevuni alikuwa
na ndevu za
kadiri.Mkononialikuwa na
sanduku dogo.Vicky akageuka
ghafla na kuruka akataka kuiwahi
pochi yake lakini akajikuta
akitazama na mdomo wa bastora
akataka kupiga kelele yule jamaa
akamfanyia ishara asithubutu
kufanya vile
"Nataka muwe kimya .Yeyote
atakayethubutu kupiga kelele
nitamfumua kichwa kwa risasi"
akasema yule jamaa
"Vaeni nguo zenu haraka"
akaamuru .Steve na Vicky
wakavaa huku yule jamaa akiwatazama kwa tahadhari
kubwa huku amewaelekezea
bastora.Mara tu walipovaa nguo
yule jamaa akamrushia Steve
bastora na kutoa nyingine katika
koti kitendo kilichomshangaza
mno Vicky akawatazama kwa
zamu asiamini alichokiona
"Whats the meanng of this?
Are you two together? akauliza
Vicky kwa mshangao.Yule jamaa
aliyevamia mle chumbani akavua
kofia,akavua miwani na kuvua
ndevu bandia alizokuwa ameweka
kidevuni.Vicky akatamani ageuke
hewa na kutoweka
"You ?!! akasema kwa
mshangao
"You are dead !! You are
supposed to be dead !! akasema I'm back from hell." akasema
Elvis.
"Steve why you are doing this
to me?Who are you?
"Quiety !!! akafoka Steve
" Good Job Steve” akasema
Elvis na kumsogelea Vicky
aliyekuwa anatetemeka kwa woga
"My name is Elvis.Ninafanya
kazi katika idara ya ujasusi
Tanzania.Kwa hivi sasa
ninafahamika kama marehemu
but I'm not dead.Vicky sina haja
na wewe na wala hatutaki
kukuumiza ila kuna jambo ambalo
tunalitaka toka kwako na endapo
utatutimizia basi tutakuacha
uende zako.Tafadhali naomba
utupe ushirikiano ili tupate
tunachohitaji toka kwako nawewe uende zako hatuna shida
nawe"
"What do you want? akauliza
Vicky
"Nataka uchukue simu yako
na umpigie mtu anaitwa Pascal
Situmwa na umtake afike hapa
hotelini haraka sana mweleze
kuna jambo la muhimu unataka
kuzungumza naye.Ukifanya hivyo
tutakuacha uende zako" akasema
Elvis
"Pascal?! akauliza Vicky
"Kwa nini mnamtaka Pascal?
Amefanya nini? akauliza Vicky
"Are you going to do it or not?
akauliza Elvis kwa ukali
"I'll do it.Ila nawaomba
nitakapokamilisha kile mnachokihitaji mniruhusu niende
zangu" akasema Vicky
"Fanya kama ulivyoamriwa"
akasema Steve na Vicky akaenda
katika mkoba wake akachukua
simu na kuzitafuta namba za
Pascal akapiga
"Weka sauti kubwa tusikie
sote" akasema Elvis na Vicky
akabonyeza kitufe cha sauti
kubwa na wote wakaisikia simu
ikiita
"Hallow Vicky" ikasema sauti
ya kiume upande wa pili
"Pascal habari yako"
"Nzuri Vicky habari za usiku
huu"
"Nzuri kabisa.Uko wapi mida
hii? Kwa hivi sasa niko njiani
naelekea nyumbani kwa Frank
nina mazungumzo naye
kidogo.Unasemaje Vicky?
"Pascal nina shida ya dharura
ndiyo maana
nimekupigia.Ninaomba kabla
hujafika kwa Frank tuonane nina
mazungumzo nawe ya faragha"
"Una tatizo gani Vicky?
akauliza Pascal
"Ni jambo la binafsi na la
faragha kidogo siwezi
kuzungumza simuni hivyo
naomba ufanye juu chini tuonane
sasa hivi.Ahirisha kwanza safari
ya kuelekea kwa Frank na uje
tuonane"
Pascal akafikiri kwa muda na
kuuliza Uko wapi sasa hivi?
"Niko hapa Samawati beach
hotel chumba namba 208"
"Unafanya nini hapo? Are you
alone?
"Nilikuwa na miadi na mtu
lakini ameahirisha miadi yake
hadi siku nyingine hivyo niko
peke yangu hapa..Dont you like to
see me naked? akauliza Vicky
"Oh Vicky,umeanza mambo
yako" akasema Pascal na kutoa
kicheko kidogo
"Ninakuja hapo sasa hivi"
akasema Pascal
"Tafadhali usimweleze Frank
kama unakuja kukutana nami.Ana
wivu sana"
"Sawa nitafanya hivyo.Baada
ya dakika chache nitakuwa hapo hotelini" akasema Pascal na
kukata simu.Vicky akamgeukia
Elvis
"I've done what you asked me
to do.Can you let me go now ?
akauliza Vicky
"Not so fast pretty lady.kaa
pale!! akasema Steve
"Please I have nothing to do
with you.Let me go now" akasema
Vicky
"Utaondoka pale Pascal
atakapokuja humu ndani!
akasema Elvis
"Kwa nini mnamuhitaji
Pascal?Amewafanya nini?
Akauliza Vicky lakini hakuna
aliyemjibu Tafadhalini naomba mnijibu
kwa nini mnamtaka Pascal na si
mtu mwingine?
"Vicky naomba ukae kimya
tafadhali"akasema Steve
"Ninahitaji maelezo kwa
sababu endapo kuna jambo lolote
likimtokea Pascal mimi ndiye
nitakayekuwa matatizoni kwani
ndiye niliyempigia simu na
kumtaka aje hapa.Kwa nini
mmenitumia mimi? Kwa nini
mmeshindwa kumtafuta kwa njia
nyingine?
"Vicky this is the last
warning.Keep quiety!! akasema
Steve
"I didnt know you are a
monster !! akasema Vicky"Later I'll show you I'm a real
monster!! Akawaza Steve
Chumba kilikuwa kimya
kabisa na baada ya dakika ishirini
kupita kengele ya mlango
ikalia.Elvis akamfuata Vicky na
kumnong'oneza
"Huyo lazima atakuwa ni
Pascal.Nenda kafungue mlango na
umkaribishe ndani na
tukishampata sisi na wewe
tutakuwa tumemalizana
tutakuacha uondoke lakini
ukithubutu kufanya jambo lolote
la kipuuzi nitakifumua kichwa
chako kwa risasi.Umenielewa
Vicky? akauliza Elvis huku
akimuwekea Vicky bastora
kichwani Nimekuelewa" akasema na
kuinuka akaenda mlangoni.Steve
akajibanza pembeni ya kabati na
Elvis akajificha nyuma ya friji
wote wakiwa na bastora
walizozielekeza mlangoni.Vicky
akafungua mlango na kukutana na
Pascal
"Pascal karibu
sana.Sikutegemea kama ungefika
mapema namna hii"
"Sikuwa mbali sana na hapa
na hata hivyo barabara ya kuja
huku haina magari mengi usiku
huu.akasema Pascal
" Karibu ndani" akasema
Vicky na Pascal akaingia ndani na
kabla hajaketi sofani ghafla watu
wawili wakajitokeza wote wakiwa na bastora zilizofungwa viwambo
vya kuzuia sauti.Alistuka sana.
"Taratibu sana inua mikono
yako juu na uiweke kichwani"
Elvis akamuamuru na bila ubishi
akainua mikono na kuiweka
kichwani.Elvis akamrushia Steve
pingu na kumtaka
amfunge.Haraka haraka Steve
akaikamata mikono ya Pascal na
kumfunga kwa nyuma kisha
akamsachi na kumkuta na bastora
ndogo mbili zote zikiwa
zimefungwa vifaa vya kuzuia sauti
akaziweka mezani na kumuamuru
aketi sofani.Elvis akavua kofia
aliyokuwa ameivaa
"Hallow Pascal" akasema
Elvis na sura ya Pascal
ikaonyesha mstuko mkubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kudadeki.....patamu hapo Pascal na Vicky wanakuwa wakwanza kukutana na mtu alikufa na kuzikwa.....nasubiri kuona Frank pia akikutana na Elvis pamoja mkurugezi wa ujasusi...atakapo sema good job vijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko nzuri sana, Vicky hajui kuwa ukiona mzimu lazima ufe, hawezi kwenda mtaani kusimulia mzimu wa Elvis. Lazima watapike yote.

Mtihani hapo ni namna ya kutoka nao nje ya hoteli.
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 49

No !! this is not true.You?!!
akasema Pascal kwa mshangao
midomo ikimtetemeka
"It's true Pascal.It’s me
Elvis.Mimi ni halisi na wala si
mzimu kwa hiyo usiifanye akili
yako ione kama vile uko ndotoni"
akasema Elvis na kuinua glasi ya
mvinyo iliyokuwa mezani
akanywa
"Nadhani sasa hauna wasi
wasi tena.Mimi ni halisi kwani
mzimu hauli wala kunywa lakini
mimi nimekunywa mvinyo mbele
yako"
“You are dead !! akasema
Pascal
"No I'm not." akasema Elvis
na uso wa Pascal ukaonekana kuloa jasho.Ghafla macho yake
akayaelekeza mlangoni
"Vic........" kabla hajamaliza
sentensi yake mara risasi
mfululilzo kutoka katika bastora
iliyofungwa kiwambo cha sauti
zikamiminika kichwani kwa
Pascal na kumuodoa uhai pale
pale.Elvis na Steve kila mmoja
akaruka upande wake
kujinusuru.Vicky alisimama akiwa
na bastora mkononi ikifuka
moshi.Kwa haraka na kwa
shabaha ya aina yake Elvis
akaulenga mkono wa Vicky
uliokuwa na bastora ikaanguka
chini.Wakati Vicky akiwa chini
akigugumia kwa maumvi makali
Steve akaruka na kumuwahi
akamnyooshea bastora .Elvis akaenda kumtazama Pascal tayari
hakuwa na uhai.Kichwa chake
kilifumuliwa kwa risasi.
"Can he make it? Steve
akauliza
"No he's gone" akasema Elvis
na kumfuata Vicky pale chini
"What have you done?!!
akauliza lakini Vicky hakujibu
kitu.Alikuwa anagugumia kwa
maumivu makali ya risasi
"Kill me you bastard!!
akasema kwa ukali.
"We cant kill you.We need
you” akasema Elvis na kwa haraka
akalifungua sanduku alilokuja
nalo lililokuwa na vifaa mbali
mbali akachukua dawa na kuivuta
katika bomba la sindano kisha
akamchoma Vicky karibu na mahala alipopigwa risasi na
kumfanya asihisi maumivu makali
pamoja na kuzuia damu isiendelee
kutoka.
“Steve kila kitu kimeharibika
we have to get out of here now
lakini kabla hatujaondoka lazima
tuhakikishe tumepaacha salama
mahala hapa. Mlaze Pascal hapa
mahala damu ya Vicky
ilipomwagika ili zichanganyike
halafu hakikisha hakuna mahala
ulikoacha alama zako za
vidole.Pangusa kila sehemu
haraka haraka" akasema Elvis na
kumuinua Vicky akampeleka
bafuni akamuamuru aoage aondoe
damu iliyotapakaa mwilini.Wakati
Elvis na Vicky wakiwa bafuni
Steve akaanza kufuta alama za vidole katika sehemu zote ambazo
aliamini amezishika kwani
hakuwa amevaa kitu chochte
mkononi tofauti na Elvis
aliyekuwa amevaa glovu.Baada ya
kuoga na kujifuta damu Elvis
akalifunga jeraha la Vicky halafu
akamtaka avae koti la Steve ili
jeraha lile la risasi lisionekane
"We're going out.Utakuwa
kimya na kufuata maelekezo
yetu.You'll smile like nothing
happened.Ukienda kinyume na
sisi kwa namna yoyote ile you are
finished.Kichwa chako
nitakifumua kwa risasi kama
ulivyomuua Pascal.Umenielewa !!
akauliza Elvis kwa ukali
"Nimekuelewa lakini
naombeni mnipeleke hospitali " akasema Vicky.Elvis na Steve
wakatazamana
"Everything ok? Can we go
now? Elvis akauliza
"Tunaweza kuondoka.Kila
kitu kiko sawa." akasema Steve
wakazima taa na kutoka mle
chumbani.Elvis alikuwa
amemshika kiuno Vicky
wakionekana kama wapenzi.Steve
alikuwa nyuma yao hatua kadhaa
akiangalia kwa makini kama kuna
hatari yoyote nyuma
yao.Walishuka kwa kutumia lifti
halafu wakaingia katika ukumbi
wa chakula na kutoka wakaelekea
maegesho ya magari.Hakuna
yeyote aliyewatilia shaka au kuwa
na wasi wasi nao.Kwa upande wa
Elvis ilikuwa vigumu kutambulikahasa kutokana na vitu bandia
alivyokuwa amevaa na kuubadili
kabisa mwonekano wake.
Vicky akaingizwa katika gari
la Elvis na kukaa kiti cha pembeni
na kwa tahadhari mikono yake
ikafungwa pingu zile alizokuwa
amefungwa Pascal na kuondoka
mahala pale huku Steve akiwa
nyuma yao kuhakikisha
wanakuwa salama.Baada ya
kuingia barabarani Elvis
akampigia simu Dr Philip na
kumtaka wakutane nyumbani
kwake haraka sana usiku ule kuna
dharura imetokea halafu
akampigia simu Meshack Jumbo
na kumtaka pia afike nyumbani
kwake usiku ule kuna jambo
limetokea. Elvis akageuza shingo na
kumtazama Vicky ambaye uso
wake ulikuwa mkavu sana na
hakuonyesha hata chembe ya wasi
wasi kana kwamba hakuna
kilichokuwa kimetokea muda
mfupi uliopita
"Who is this woman? Siamini
kama ni kahaba kwa namna
alivyoweza kuitumia silaha kwa
wepesi ule.Hakuna kati yetu
aliyekuwa na mawazo kama
angeweza kufanya kitu kama kile
na akaitumia fursa wakati sisi
tukiwa tumeelekeza akili zetu kwa
Pasal akachukua bastora na
kumuua.Bastora ile aliitoa wapi?
Ni ya kwake? Kwa nini akamuua
Pascal? akajiuliza Elvis huku
akiongeza mwendo wa gari Ukimtazama alivyo na
kitendo alichokifanya hawaendani
kabisa.Hakuna atakayeamini
akiambiwa kwamba mwanamke
huyu ametoka kutoa uhai wa mtu
kikatili muda mfupi uliopita.Huyu
ni mwanamke hatari na kuna
mambo mengi tutayafahamu
kupitia kwake.Lazima ipo sababu
iliyopelekea akamuua Pascal.Huu
ni mwanzo tutafahamu mambo
mengi yaliyojificha.Nimekwisha
weka ahadi kwamba hakuna jiwe
litakalosalia juu ya
jiwe.Tutawaangusha wote
waliomo katika mtandao haramu
wa kuuza silaha kwa waasi wa
Congo DRC.Je na huyu mwanamke
naye ni mmoja wa watu waliomo
katika mtandao huo? akajiuliza Elvis na kulipita gari lililokuwa
mbele yake
"Ninahisi hata huyu naye ni
moja wao kwa sababu kwa mujibu
wa barua pepe nilizozikuta katika
kompyuta ya Frank,mtu anayejiita
Deusdedith MM alitoa maelekezo
kwamba kahaba huyu atumike
katika mauaji ya kanali
Norman.Kuna uwezekano
mkubwa mwanamke huyu naye
akawa ni mmoja wao au akawa ni
muuaji anayetumiwa na watu
hawa kuua kimya
kimya.Inashangaza sana kahaba
kuwa na utajiri mkubwa kama
alionao huyu Vicky.Atatueleza kila
kitu" akawaza Elvis na kujitazama
tena Vicky ambaye alikuwa ameegemea kitini akionekana
kupitiwa na kijiusingizi.
Waliwasili katika makazi yao
na Graca akawafungulia geti.Vicky
akashushwa na kuingizwa katika
moja wapo ya chumba
kilichokuwa kimeandaliwa
akalazwa kitandani na kufungwa
pingu mkono wake wa kushoto na
miguuni katika kitanda cha
chuma.
"Please take me to hospital"
akasema Vicky
"Hapa uko hospitali usihofu"
akasema Elvis na kutoka mle
chumbani akaufunga mlango
"Elvis nimefurahi umerejea
salama.Kila kitu kimekwenda
vizuri? akauliza Graca Kila kitu kiko sawa
Graca.Nenda chumbani
ukapumzike sisi bado tunaendelea
na kazi" akasema Elvis na Graca
akaenda kupumzika chumbani
kwake
"Good job Steve" akasema
Elvis huku akichukua glasi ya maji
"Elvis kilichotokea pale
ninaona kama filamu.Bado
najaribu kutafakari lakini inaniwia
vigumu kuamini kama kweli Vicky
ndiye aliyefanya kitendo kile na
kwa wepesi ule" akasema Steve
"Ni kweli ni kitu ambacho
kinashangaza sana.Hatukuwa
tumetegemea kama Vicky
angeweza kufanya kitendo cha
namna ile na ndiyo maana
hatukuwa tumeelekeza macho yetu kwake na akatumia mwanya
huo kufanya alichokifanya.Swali
ambalo tunapaswa tulitafutie jibu
ni kwa nini amemuua
Pascal?lazima ipo sababu
iliyomfanya akamuua
Pascal.Alifahamu kuwa
tutamfanyia mahojiano Pascal na
kuna mambo tutayafahamu hivyo
akaamua kumuua ili tusiweze
kumuhoji.Tumemkosa Pascal
lakini tumempata mtu ambaye
naamini ni muhimu sana
atakayetusaidia kupata majibu ya
maswali yetu"akasema Elvis
"Mwanamke yule ni hatari
sana.Angeweza hata kutumaliza
sote" akasema Steve
"Nahisi lengo lake lilikuwa
hilo kutumaliza sote kwani bastora yake bado ilikuwa na
risasi za kutosha na kama
tusingekuwa makini angeweza
kutumaliza na kutokomea
zake.Siku zote nimekuwa
nikikufundisha Steve usiwaamni
sana wanawake hasa hawa wenye
uzuri wa kimalaika.Wanaweza
kuwa hatari kuliko hata
shetani.Mtazame Vicky huwezi
hata kuhisi kama amewahi
kuigusa hata silaha lakini ndani ya
sekunde chache ameweza kuutoa
uhai wa mtu kikatili.Anaonekana
ni mzoefu sana katika mambo……"
Elvis akanyamaza baada ya
kengele ya getini kulia Steve
akaenda kwa tahadhari kubwa na
kumkuta ni Dr Philip karibu sana Dr Philip"
akasema Steve baada ya Philip
kushuka garini
"Nimeitika wito kwa haraka
Elvis.Is everything ok here?
akauliza Dr Philip baada ya
kuingia ndani
"Kazi imeanza Dr Philip na
kuna mtu anahitaji huduma yako
ya haraka amepigwa risasi
mkononi" akasema Elvis na
kumsimulia Dr Philip
kilichotokea.Bila kupoteza muda
Philip na Elvis wakaenda katika
chumba alimo Vicky.Dr Philip
akalitazama jeraha la Vicky kisha
akaelekeza afunguliwe na baadhi
ya vitu viandaliwe ili aweze
kumfanyia upasuaji wa
mkono.Meza kubwa ya chakula ikaletwa mle chumbani na
kuwekwa godoro juu yake Vicky
akalazwa na kuchomwa sindano
ya kuondoa maumivu kisha Dr
Philip akaanza kuufanyia upasuaji
mkono ule kuondoa
risasi.Lilikuwa ni zoezi la dakika
thelathini halafu akashona jeraha
na kumchoma Vicky Sindano
nyingine.Wakiwa katika hatua za
mwisho mlango ukafunguliwa na
Meshack Jumbo akiwa na Steve
wakaingia
"Karibu sana mzee"akasema
Elvis na kumuacha Dr Pilip na
Steve mle chumbani akaongozana
na Meshack kuelekea sebuleni
"Elvis habari za hapa? mambo
yanakwendaje? Nilikuwa na siku
ndefu iliyokabiliwa na mambo mengi na ndiyo maana sikuweza
tena kurejea hapa.Ila nilihudhuria
kikao cha mwisho cha kuhitimisha
msiba na..."
"Tayarini ninafahamu kila
kitu kilichotokea mzee.Doreen
naye alikuwepo na amenieleza
kila kitu"akasema Elvis
"Vizuri kama tayari unazo
taarifa.Alichokifanya Patricia
kimesikitisha wengi.Inaonekana
kuna mambo mengi aliyokuwa
anafanyiwa na ndugu zako hadi
akaamua kuchukua uamuzi ule
mgumu .Tuachane na hayo
ninataka kufahamu
kinachoendelea hapa.Yule
mwanamke mle ndani ni nani na
kafanya nini? akauliza Meshack na Elvis akamsimulia kila kitu
kilichotokea usiku ule.
"Elvis nimesisimkwa mwili
kusikia kitu alichokifanya yule
mwanamama.Mmekwisha
mfahamu ni nani?
"Hapana bado.kwanza
tunamtibu kumuondoa risasi
halafu tutamfanyia mahojiano
tumfahamu ni nani ila lazima ni
mtu hatari na ni mzoefu wa silaha
kwa namna alivyoweza kumuua
Pascal.Alimlenga risasi za kichwa
na lengo likiwa ni kumuua kwa
haraka ili tusiweze kupata
chochote kutoka kwake"
"Kwa mtazamo wangu
mtandao wa hili genge ni mkubwa
na kuna uwezekano hata huyu mwanamke naye akawa ni mmoja
wao." akasema Meshack
"Kwa mujibu wa barua pepe
nilizozipata kutoka katika
kompyuta ya Frank iliyoibwa na
Graca,mtu anayeitwa Deusdedith
MM anaonekana kutoa maelekezo
mengi kwa Frank na ambaye
anaonekana ndiye kiongozi wao
alimuelekeza Frank amtumie
Vicky katika mauaji ya kanali
Norman kwa hiyo basi huyu
mwanamke ni muhimu sana
kwetu kwani anafahamu mambo
mengi kuhusiana na mtandao huu
.Ni yeye ambaye anamfahamu
Deusdedith MM na atatuongoza
kujua mahala alipo.Kuna
uwezekano pia mwanamke huyu
akawa ni muuaji anayetumiwa na akina Frank kuua watu kimya
kimya kwa kutumia uzuri
wake.Tutayafahamu haya yote
ndani ya kipindi kifupi.Zama zake
tayari zimekwisha" akasema Elvis
"Mimi ngoja niwasiliane na
makamu wa rais nimjulishe
kwamba tayari Pascal ameuawa
kama alivyoagiza" akasema
Meshack na kumpigia simu
makamu wa rais akamjulisha
kwamba tayari Pascal ameuawa.
"Kazi nzuri sana Meshack
.Hizi ni taarifa njema kabisa.Kesho
ule mzigo niliokuahidi utaletwa
ofisini kwako" akasema makamu
wa rais Dr Shafi na kuagana na
Meshack
"kwa nini makamu wa rais
atake Pascal auawe? Elvis akaulizaHilo ni swali ambalo
tunapaswa kulitafutia
majibu.Alitaka wewe uuawe kwa
sababu tayari ulikwishaingia
katika anga za vigogo lakini huyu
Pascal sijafahamu yeye alifanya
nini hadi ikaamriwa auawe"
akasema Meshack
"Pascal na Frank ni marafiki
wakubwa na bishara ya silaha
wanaifanya kwa
pamoja.Inawezekana makamu wa
rais ni mmoja wa washirika wa
mtandao huu na ndiyo maana kila
pale maslahi yao yanapoguswa
anatumia nguvu yake kuondoa
vikwazo.Kama ni hivyo kwa nini
Pascal atakiwe kuuawa wakati ni
mwenzao. Je Frank anaweza
kumtoa kafara swahiba wake mkubwa kama Pascal? kama jibu
ni ndiyo basi lazima kuna jambo
kuwa limetokea kati yao kwa
maana hiyo lazima kumchunguza
pia Frank kujua kama kuna jambo
lolote limetokea kati yake na
Pascal lakini kabla ya hayo yote
lazima kwanza tuufahamu
ukubwa wa mtandao huu na
tuwajue wahusika wote kisha
tuanze kuubomoa hatua kwa
hatua.Hakuna atakayesalia hata
mmoja" akasema Elvis.
"Mara nyingi viongozi
wakubwa kama hawa
wanaposhiriki katika magenge
kama haya yenye kufanya
biashara haramu huwa
hawajihusishi moja kwa moja bali
uhusika wao huwa wa siri na inawezekana kukawa na ugumu
wa kuthibitisha kama makamu wa
rais ni mmoja wa
wahusika.Inawezekana akawa si
mmoja wao ila kuna kitu
anakipata kutoka kwa wakuu wa
mtandao huu na akawa
akiwasaidia kutekeleza maagizo
yao mbali mbali.Haya yote
yanawezekana na yanatakiwa
yachunguzwe."
"Usemayo ni ya kweli kabisa
mzee na tutayafanyia kazi ili
kuufahamu ukweli.Ahadi yangu ni
ile ile siku zote kwamba kaika
suala hili hakuna jiwe litasalia juu
ya jiwe.Yeyote anayehusika katika
biashara hii akiwa hapa nchini
lazima atajulikana na hatua stahiki zitachukuliwa" akasema
Elvis.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 49

No !! this is not true.You?!!
akasema Pascal kwa mshangao
midomo ikimtetemeka
"It's true Pascal.It’s me
Elvis.Mimi ni halisi na wala si
mzimu kwa hiyo usiifanye akili
yako ione kama vile uko ndotoni"
akasema Elvis na kuinua glasi ya
mvinyo iliyokuwa mezani
akanywa
"Nadhani sasa hauna wasi
wasi tena.Mimi ni halisi kwani
mzimu hauli wala kunywa lakini
mimi nimekunywa mvinyo mbele
yako"
“You are dead !! akasema
Pascal
"No I'm not." akasema Elvis
na uso wa Pascal ukaonekana kuloa jasho.Ghafla macho yake
akayaelekeza mlangoni
"Vic........" kabla hajamaliza
sentensi yake mara risasi
mfululilzo kutoka katika bastora
iliyofungwa kiwambo cha sauti
zikamiminika kichwani kwa
Pascal na kumuodoa uhai pale
pale.Elvis na Steve kila mmoja
akaruka upande wake
kujinusuru.Vicky alisimama akiwa
na bastora mkononi ikifuka
moshi.Kwa haraka na kwa
shabaha ya aina yake Elvis
akaulenga mkono wa Vicky
uliokuwa na bastora ikaanguka
chini.Wakati Vicky akiwa chini
akigugumia kwa maumvi makali
Steve akaruka na kumuwahi
akamnyooshea bastora .Elvis akaenda kumtazama Pascal tayari
hakuwa na uhai.Kichwa chake
kilifumuliwa kwa risasi.
"Can he make it? Steve
akauliza
"No he's gone" akasema Elvis
na kumfuata Vicky pale chini
"What have you done?!!
akauliza lakini Vicky hakujibu
kitu.Alikuwa anagugumia kwa
maumivu makali ya risasi
"Kill me you bastard!!
akasema kwa ukali.
"We cant kill you.We need
you” akasema Elvis na kwa haraka
akalifungua sanduku alilokuja
nalo lililokuwa na vifaa mbali
mbali akachukua dawa na kuivuta
katika bomba la sindano kisha
akamchoma Vicky karibu na mahala alipopigwa risasi na
kumfanya asihisi maumivu makali
pamoja na kuzuia damu isiendelee
kutoka.
“Steve kila kitu kimeharibika
we have to get out of here now
lakini kabla hatujaondoka lazima
tuhakikishe tumepaacha salama
mahala hapa. Mlaze Pascal hapa
mahala damu ya Vicky
ilipomwagika ili zichanganyike
halafu hakikisha hakuna mahala
ulikoacha alama zako za
vidole.Pangusa kila sehemu
haraka haraka" akasema Elvis na
kumuinua Vicky akampeleka
bafuni akamuamuru aoage aondoe
damu iliyotapakaa mwilini.Wakati
Elvis na Vicky wakiwa bafuni
Steve akaanza kufuta alama za vidole katika sehemu zote ambazo
aliamini amezishika kwani
hakuwa amevaa kitu chochte
mkononi tofauti na Elvis
aliyekuwa amevaa glovu.Baada ya
kuoga na kujifuta damu Elvis
akalifunga jeraha la Vicky halafu
akamtaka avae koti la Steve ili
jeraha lile la risasi lisionekane
"We're going out.Utakuwa
kimya na kufuata maelekezo
yetu.You'll smile like nothing
happened.Ukienda kinyume na
sisi kwa namna yoyote ile you are
finished.Kichwa chako
nitakifumua kwa risasi kama
ulivyomuua Pascal.Umenielewa !!
akauliza Elvis kwa ukali
"Nimekuelewa lakini
naombeni mnipeleke hospitali " akasema Vicky.Elvis na Steve
wakatazamana
"Everything ok? Can we go
now? Elvis akauliza
"Tunaweza kuondoka.Kila
kitu kiko sawa." akasema Steve
wakazima taa na kutoka mle
chumbani.Elvis alikuwa
amemshika kiuno Vicky
wakionekana kama wapenzi.Steve
alikuwa nyuma yao hatua kadhaa
akiangalia kwa makini kama kuna
hatari yoyote nyuma
yao.Walishuka kwa kutumia lifti
halafu wakaingia katika ukumbi
wa chakula na kutoka wakaelekea
maegesho ya magari.Hakuna
yeyote aliyewatilia shaka au kuwa
na wasi wasi nao.Kwa upande wa
Elvis ilikuwa vigumu kutambulikahasa kutokana na vitu bandia
alivyokuwa amevaa na kuubadili
kabisa mwonekano wake.
Vicky akaingizwa katika gari
la Elvis na kukaa kiti cha pembeni
na kwa tahadhari mikono yake
ikafungwa pingu zile alizokuwa
amefungwa Pascal na kuondoka
mahala pale huku Steve akiwa
nyuma yao kuhakikisha
wanakuwa salama.Baada ya
kuingia barabarani Elvis
akampigia simu Dr Philip na
kumtaka wakutane nyumbani
kwake haraka sana usiku ule kuna
dharura imetokea halafu
akampigia simu Meshack Jumbo
na kumtaka pia afike nyumbani
kwake usiku ule kuna jambo
limetokea. Elvis akageuza shingo na
kumtazama Vicky ambaye uso
wake ulikuwa mkavu sana na
hakuonyesha hata chembe ya wasi
wasi kana kwamba hakuna
kilichokuwa kimetokea muda
mfupi uliopita
"Who is this woman? Siamini
kama ni kahaba kwa namna
alivyoweza kuitumia silaha kwa
wepesi ule.Hakuna kati yetu
aliyekuwa na mawazo kama
angeweza kufanya kitu kama kile
na akaitumia fursa wakati sisi
tukiwa tumeelekeza akili zetu kwa
Pasal akachukua bastora na
kumuua.Bastora ile aliitoa wapi?
Ni ya kwake? Kwa nini akamuua
Pascal? akajiuliza Elvis huku
akiongeza mwendo wa gari Ukimtazama alivyo na
kitendo alichokifanya hawaendani
kabisa.Hakuna atakayeamini
akiambiwa kwamba mwanamke
huyu ametoka kutoa uhai wa mtu
kikatili muda mfupi uliopita.Huyu
ni mwanamke hatari na kuna
mambo mengi tutayafahamu
kupitia kwake.Lazima ipo sababu
iliyopelekea akamuua Pascal.Huu
ni mwanzo tutafahamu mambo
mengi yaliyojificha.Nimekwisha
weka ahadi kwamba hakuna jiwe
litakalosalia juu ya
jiwe.Tutawaangusha wote
waliomo katika mtandao haramu
wa kuuza silaha kwa waasi wa
Congo DRC.Je na huyu mwanamke
naye ni mmoja wa watu waliomo
katika mtandao huo? akajiuliza Elvis na kulipita gari lililokuwa
mbele yake
"Ninahisi hata huyu naye ni
moja wao kwa sababu kwa mujibu
wa barua pepe nilizozikuta katika
kompyuta ya Frank,mtu anayejiita
Deusdedith MM alitoa maelekezo
kwamba kahaba huyu atumike
katika mauaji ya kanali
Norman.Kuna uwezekano
mkubwa mwanamke huyu naye
akawa ni mmoja wao au akawa ni
muuaji anayetumiwa na watu
hawa kuua kimya
kimya.Inashangaza sana kahaba
kuwa na utajiri mkubwa kama
alionao huyu Vicky.Atatueleza kila
kitu" akawaza Elvis na kujitazama
tena Vicky ambaye alikuwa ameegemea kitini akionekana
kupitiwa na kijiusingizi.
Waliwasili katika makazi yao
na Graca akawafungulia geti.Vicky
akashushwa na kuingizwa katika
moja wapo ya chumba
kilichokuwa kimeandaliwa
akalazwa kitandani na kufungwa
pingu mkono wake wa kushoto na
miguuni katika kitanda cha
chuma.
"Please take me to hospital"
akasema Vicky
"Hapa uko hospitali usihofu"
akasema Elvis na kutoka mle
chumbani akaufunga mlango
"Elvis nimefurahi umerejea
salama.Kila kitu kimekwenda
vizuri? akauliza Graca Kila kitu kiko sawa
Graca.Nenda chumbani
ukapumzike sisi bado tunaendelea
na kazi" akasema Elvis na Graca
akaenda kupumzika chumbani
kwake
"Good job Steve" akasema
Elvis huku akichukua glasi ya maji
"Elvis kilichotokea pale
ninaona kama filamu.Bado
najaribu kutafakari lakini inaniwia
vigumu kuamini kama kweli Vicky
ndiye aliyefanya kitendo kile na
kwa wepesi ule" akasema Steve
"Ni kweli ni kitu ambacho
kinashangaza sana.Hatukuwa
tumetegemea kama Vicky
angeweza kufanya kitendo cha
namna ile na ndiyo maana
hatukuwa tumeelekeza macho yetu kwake na akatumia mwanya
huo kufanya alichokifanya.Swali
ambalo tunapaswa tulitafutie jibu
ni kwa nini amemuua
Pascal?lazima ipo sababu
iliyomfanya akamuua
Pascal.Alifahamu kuwa
tutamfanyia mahojiano Pascal na
kuna mambo tutayafahamu hivyo
akaamua kumuua ili tusiweze
kumuhoji.Tumemkosa Pascal
lakini tumempata mtu ambaye
naamini ni muhimu sana
atakayetusaidia kupata majibu ya
maswali yetu"akasema Elvis
"Mwanamke yule ni hatari
sana.Angeweza hata kutumaliza
sote" akasema Steve
"Nahisi lengo lake lilikuwa
hilo kutumaliza sote kwani bastora yake bado ilikuwa na
risasi za kutosha na kama
tusingekuwa makini angeweza
kutumaliza na kutokomea
zake.Siku zote nimekuwa
nikikufundisha Steve usiwaamni
sana wanawake hasa hawa wenye
uzuri wa kimalaika.Wanaweza
kuwa hatari kuliko hata
shetani.Mtazame Vicky huwezi
hata kuhisi kama amewahi
kuigusa hata silaha lakini ndani ya
sekunde chache ameweza kuutoa
uhai wa mtu kikatili.Anaonekana
ni mzoefu sana katika mambo……"
Elvis akanyamaza baada ya
kengele ya getini kulia Steve
akaenda kwa tahadhari kubwa na
kumkuta ni Dr Philip karibu sana Dr Philip"
akasema Steve baada ya Philip
kushuka garini
"Nimeitika wito kwa haraka
Elvis.Is everything ok here?
akauliza Dr Philip baada ya
kuingia ndani
"Kazi imeanza Dr Philip na
kuna mtu anahitaji huduma yako
ya haraka amepigwa risasi
mkononi" akasema Elvis na
kumsimulia Dr Philip
kilichotokea.Bila kupoteza muda
Philip na Elvis wakaenda katika
chumba alimo Vicky.Dr Philip
akalitazama jeraha la Vicky kisha
akaelekeza afunguliwe na baadhi
ya vitu viandaliwe ili aweze
kumfanyia upasuaji wa
mkono.Meza kubwa ya chakula ikaletwa mle chumbani na
kuwekwa godoro juu yake Vicky
akalazwa na kuchomwa sindano
ya kuondoa maumivu kisha Dr
Philip akaanza kuufanyia upasuaji
mkono ule kuondoa
risasi.Lilikuwa ni zoezi la dakika
thelathini halafu akashona jeraha
na kumchoma Vicky Sindano
nyingine.Wakiwa katika hatua za
mwisho mlango ukafunguliwa na
Meshack Jumbo akiwa na Steve
wakaingia
"Karibu sana mzee"akasema
Elvis na kumuacha Dr Pilip na
Steve mle chumbani akaongozana
na Meshack kuelekea sebuleni
"Elvis habari za hapa? mambo
yanakwendaje? Nilikuwa na siku
ndefu iliyokabiliwa na mambo mengi na ndiyo maana sikuweza
tena kurejea hapa.Ila nilihudhuria
kikao cha mwisho cha kuhitimisha
msiba na..."
"Tayarini ninafahamu kila
kitu kilichotokea mzee.Doreen
naye alikuwepo na amenieleza
kila kitu"akasema Elvis
"Vizuri kama tayari unazo
taarifa.Alichokifanya Patricia
kimesikitisha wengi.Inaonekana
kuna mambo mengi aliyokuwa
anafanyiwa na ndugu zako hadi
akaamua kuchukua uamuzi ule
mgumu .Tuachane na hayo
ninataka kufahamu
kinachoendelea hapa.Yule
mwanamke mle ndani ni nani na
kafanya nini? akauliza Meshack na Elvis akamsimulia kila kitu
kilichotokea usiku ule.
"Elvis nimesisimkwa mwili
kusikia kitu alichokifanya yule
mwanamama.Mmekwisha
mfahamu ni nani?
"Hapana bado.kwanza
tunamtibu kumuondoa risasi
halafu tutamfanyia mahojiano
tumfahamu ni nani ila lazima ni
mtu hatari na ni mzoefu wa silaha
kwa namna alivyoweza kumuua
Pascal.Alimlenga risasi za kichwa
na lengo likiwa ni kumuua kwa
haraka ili tusiweze kupata
chochote kutoka kwake"
"Kwa mtazamo wangu
mtandao wa hili genge ni mkubwa
na kuna uwezekano hata huyu mwanamke naye akawa ni mmoja
wao." akasema Meshack
"Kwa mujibu wa barua pepe
nilizozipata kutoka katika
kompyuta ya Frank iliyoibwa na
Graca,mtu anayeitwa Deusdedith
MM anaonekana kutoa maelekezo
mengi kwa Frank na ambaye
anaonekana ndiye kiongozi wao
alimuelekeza Frank amtumie
Vicky katika mauaji ya kanali
Norman kwa hiyo basi huyu
mwanamke ni muhimu sana
kwetu kwani anafahamu mambo
mengi kuhusiana na mtandao huu
.Ni yeye ambaye anamfahamu
Deusdedith MM na atatuongoza
kujua mahala alipo.Kuna
uwezekano pia mwanamke huyu
akawa ni muuaji anayetumiwa na akina Frank kuua watu kimya
kimya kwa kutumia uzuri
wake.Tutayafahamu haya yote
ndani ya kipindi kifupi.Zama zake
tayari zimekwisha" akasema Elvis
"Mimi ngoja niwasiliane na
makamu wa rais nimjulishe
kwamba tayari Pascal ameuawa
kama alivyoagiza" akasema
Meshack na kumpigia simu
makamu wa rais akamjulisha
kwamba tayari Pascal ameuawa.
"Kazi nzuri sana Meshack
.Hizi ni taarifa njema kabisa.Kesho
ule mzigo niliokuahidi utaletwa
ofisini kwako" akasema makamu
wa rais Dr Shafi na kuagana na
Meshack
"kwa nini makamu wa rais
atake Pascal auawe? Elvis akaulizaHilo ni swali ambalo
tunapaswa kulitafutia
majibu.Alitaka wewe uuawe kwa
sababu tayari ulikwishaingia
katika anga za vigogo lakini huyu
Pascal sijafahamu yeye alifanya
nini hadi ikaamriwa auawe"
akasema Meshack
"Pascal na Frank ni marafiki
wakubwa na bishara ya silaha
wanaifanya kwa
pamoja.Inawezekana makamu wa
rais ni mmoja wa washirika wa
mtandao huu na ndiyo maana kila
pale maslahi yao yanapoguswa
anatumia nguvu yake kuondoa
vikwazo.Kama ni hivyo kwa nini
Pascal atakiwe kuuawa wakati ni
mwenzao. Je Frank anaweza
kumtoa kafara swahiba wake mkubwa kama Pascal? kama jibu
ni ndiyo basi lazima kuna jambo
kuwa limetokea kati yao kwa
maana hiyo lazima kumchunguza
pia Frank kujua kama kuna jambo
lolote limetokea kati yake na
Pascal lakini kabla ya hayo yote
lazima kwanza tuufahamu
ukubwa wa mtandao huu na
tuwajue wahusika wote kisha
tuanze kuubomoa hatua kwa
hatua.Hakuna atakayesalia hata
mmoja" akasema Elvis.
"Mara nyingi viongozi
wakubwa kama hawa
wanaposhiriki katika magenge
kama haya yenye kufanya
biashara haramu huwa
hawajihusishi moja kwa moja bali
uhusika wao huwa wa siri na inawezekana kukawa na ugumu
wa kuthibitisha kama makamu wa
rais ni mmoja wa
wahusika.Inawezekana akawa si
mmoja wao ila kuna kitu
anakipata kutoka kwa wakuu wa
mtandao huu na akawa
akiwasaidia kutekeleza maagizo
yao mbali mbali.Haya yote
yanawezekana na yanatakiwa
yachunguzwe."
"Usemayo ni ya kweli kabisa
mzee na tutayafanyia kazi ili
kuufahamu ukweli.Ahadi yangu ni
ile ile siku zote kwamba kaika
suala hili hakuna jiwe litasalia juu
ya jiwe.Yeyote anayehusika katika
biashara hii akiwa hapa nchini
lazima atajulikana na hatua stahiki zitachukuliwa" akasema
Elvis.

Sent using Jamii Forums mobile app
Picha linazidi kunoga [emoji39] [emoji39] [emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom